*RAIS KIKWETE AWASILISHA RIPOTI YA KAMATI YA VIONGOZI YA JUU YA MABADILIKO YA TABIANCHI

February 01, 2015
 Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Juu ya mabadiliko ya Tabia nchi(The Committee of African Heads of State and governments on Climate change) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimakabidhi  nakala ya Ripoti ya utendaji mwenyekiti mpya wa kamati hiyo Rais wa Misri Abdel Fattah el Sisi wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa Ethiopia.Rais Kikwete alipongezwa kwa kuiwezesha kamati hiyo kupata mafanikio makubwa.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn muda mfupi kabla ya kumalizika kwa mkutano wa 23 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika ulifanyika katika mji Mkuu wa Ethiopia Addis Ababa. .Picha na Freddy Maro

*RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA SWEDEN 

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Waziri Mkuu wa Sweden Stefan Lofven jijini Addis Ababa Ethiopia jana.Tayari Rais Kikwete amerejea nchini baada ya kumaklizika mkutano wa wakuu wa nchi za umoja wa Afrika AU jijini Addis Ababa Ethiopia kwa siku mbili.
Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Juu ya mabadiliko ya Tabia nchi Rais ikwete akiwasilisha ripitiDkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasilisha ripoti ya utendaji wakamati hiyo katika mkutano wa Viongozi wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia. Mkutano huo ulimalizika jana.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »