MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma,
unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma Ally akizungumza wakati wa Uzinduzi
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma,
unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Abdul
Kitula ambaye ni mtaalam wa fedha wa mradi wa PS3 akizungumza kwa niaba
ya Mkurugenzi wa Mradi huo wakati wa uzinduzi hii leo mjini Mtwara.
Mwakilishi
wa USAID, Laura Kikuli alikuwepo na kutoa salamu zake katika uzinduzi
huo a,mbao ulishirikisha watendaji wa Halamashauri zote za Mkoa wa
Mtwara.
Baadhi ya viongozi wa meza kuu wakifuatilia hotuba za ufunguzi
Washiriki mbalimbali ambao ni watendaji kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mtwara wakifuatilia mada katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Msaidizi Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga akisema neno.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu pamoja na wakuu wa Wilaya za Mkoa huo
wakifuatilia mawasilisho kutoka kwa maafisa Mradi wa PS3.
Afisa Rasilimali watu wa mradi wa PS3, Godfrey Nyombi akitoa mada.
Uzinduzi
wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma,
unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID),
umefanyika mjini Mtwara siku ya Jumatano na Alhamisi, Aprili 27-28, 2016.
Mradi
huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening
(PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na
Halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.
PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.
Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una
nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa
jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.
Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, na uzinduzi ulihudhuriwa pia na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Dodoma ambaye amehamishiwa mkoa wa
Songwe, Chiku Galawa. Watu takribani 180 walihudhuria. Washiriki wa
uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya
za Dodoma, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe
wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka
kwenye Halmashauri.
Mkoa
wa Dodoma una Halmashauri nane, ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya
Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya
Bahi, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa,
Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, na
Halmashauri ya Mji wa Kondoa.
PS3
ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na
Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID. Unatekelezwa na
mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni: Abt
Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao
ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya
Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health
International, na Urban Institute.
Mikoa
13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma,
Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe,
Rukwa, na Shinyanga.
PS3
itaimarisha mifumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri. Mradi
utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa
kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa
utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania. Mafanikio yanayotarajiwa ni
pamoja na:
· Utawala
Bora na Ushirikishwaji wa Raia: Uimarishaji wa utawala katika ngazi ya
kitaifa na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili kuweza kutumia
rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga,
kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta.
· Rasilimali
Watu: Kuongezeka kwa usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili
ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi. Kuimarisha
mfumo wa ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini.
· Fedha:
Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza
ufanisi katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati
ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.
· Mifumo ya Mawasiliano: Kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini, pamoja na matumizi ya takwimu kwa wadau.
Utafiti Tendaji: Tafiti Tendaji muhimu zitakazosaidia mradi kujua changamoto na mikakati
ya kuzishughulikia changamoto hizo. Tafiti hizi zitasaidia kugundua
fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa. Pia
tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini.
Mtaalam wa Mawasiliano na Takwimu wa Mradi wa PS3, Desideri Wengaa akitoa mada juu ya mawasiliano na utoaji takwimu sahihi.
Washiriki wakifuatilia kwa makini.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akisisitiza jambo
Wakuu wa Wilaya wakifuatilia mada
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akimpa mkono wa shukrani Afisa wa
Mradi wa PS3, Abdul Kitula baada ya uzinduzi. Kushoto ni Mwakilishi wa
USAID, Laura Kikuli.
Wakuu wa Wilaya wakijadiliana jambo
Picha mbalimbali za makundi tofauti zilipigwa baada ya uzinduzi huo.