Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam.
TIMU ya Yanga leo imeshindwa kutamba mbele ya Wanganda baada ya kulazimisha sare ya goli 2-2,katika mchezo wa kirafiki ulifanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ulikuwa wa kusisimua kutokana na timu zote kuonyesha kandanda safi na la kuvutia lililowafanya mashabiki kushangili kila wakati huku Simba wakionekana kuwashangilia URA.
Katika mchezo huo timu zote zilishambuliana kwa zamu huku URA,wakionekana kuutawala mchezo katika kipindi cha kwanza.
Dakika ya 9,Yanga walipata faulo nje kidogo ya 18,baada ya Jerison Tegete kufanyiwa madhambi na kipa wa URA,lakini faulo hiyo haikuzaa matunda.
Katika dakika ya 14 Tegete tena aliunganisha mpira kwa kuachia kiki kali baada ya kupata krosi kutoka kwa Saidi Bahanuzilakini lilipaa juu.
Timu ya URA,ilifanya shambulizi la ngumu mnamo dakika ya 27,baada y mshambuliaji wa timu hiyo Ngawe Emanuel kuachia mkwaju mkali ambao kipa wa Yanga Deogratus Munis 'dida',kudaka shuti hilo ndani ya eneo la hatari.
URA,waliliandama kama nyuki lango la Yanga ambapo katika dakika ya 42,Lutimba Yoyo aliiandikia timu yake goli la kwanza baada ya kuwatoka walinzi wa Yanga na kuachia mkwaju mkali ulimshinda mlinda mlango wa Yanga na kuukwamisha nyavuni.
Kipindi cha pili timu zilianza mchezo kwa kasi kila moja ikitaka kupata ushindi kutokana na maelekezo waliyopata kutoka kwa makocha wao.
Matunda ya mapunziko yalionekana kuwa mazuri kwa URA,ambapo walifanikiwa kushinda goli la pili kupitiakwa mshambuliaji wake aliyefunga goli la kwanza Lutimba Yoyo baada y kupiga faulo na kujaa kimiani huku ikimuacha Dida asijue la kufanya.
Baada ya kuona mambo magumu Yanga walifanya mabadiliko walimtoa Saidi Bahanuzi na nafasi yake ikachukuliwa na Abdalah Mguli.
Mabadiliko hayo yalizaa matunda katika dakika ya 58,Abdalah Mguli aliwainua mashabiki wa Yanga baada ya kufunga goli la kwanza.
Yanga walizi kucharukua wakiliandama lango la URA kama nyuki ambapo dakika ya 66,Didier Kavumbagu anaisawazishia Yanga baada ya kupata krosi safi na kuunganichwa kwa kichwa kutoka kwa Juma Abdul.
Yanga waliendelea kutandaza soka la uhakika huku URA ,wakionekana wamechoka ambapo dakika za lala salama waliandika goli la tatu kupitia kwa Jerison Tegete lakini muamuzi wa mchezo huo Kenedy mapunda alipiga filimbi ya kuotea na mpaka mwisho wa mchezo magoli 2-2.
Kikosi Yanga:
Deogratus Munis,Juma Abdul,Oscal Joshua,Ibrahimu Job Rajabu Zahir,Salum Terela,Said Bahanuzi/ Haruna Niyonzima,Hamisi Thabit/Bakari Masood,Didier Kavumbagu,Jerison Tegete,Shabani Kondo/Abdalah Mguli.