AZAM FC WAFUNGA 'SOFA ZA HATARI' CHAMAZI, KOMBE LA SHIRIKISHO PALE PALE MWAKANI
Imewekwa Desemba 19 saa 2:23
Siti za kulala |
SASA KESI ZA MAPENZI HADI KWA MADOGO: MWANAFUNZI WA KIKE WA KIDATO CHA TATU ACHOMWA KISU TUMBONI NA MWANAFUNZI MWENZAKE WA KIKE KWA WIVU WA MAPENZI
Na Walter
Mguluchuma
.Mpanda Katavi
Mwanafunzi wa kidato cha
tatu katika shule ya Sekondari
ya Istiqama iliyoko mjini Mpanda Mkoa wa Katavi (17) jinalake limehifadhiwa amejeruhiwa
kwa kuchomwa na kisu mara mbili
tumboni na mwanafunzi mwenzake wa
kike (15) wa kidato cha tatu wa shule hiyo kwa kisa cha kugombea mwanaume.
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi
Kamishina Dhahiri Kidavashari alisema
tukio hilo la mwanafunzi huyo kuchomwa
kisu tumboni mara mbili lilitokea
hapo Desemba 14 mwaka huu majira ya saa
kumi na mbili na nusu jioni katika eneo
la mtaa wa Kashaulili mjini hapa
TASWIRA ZA KIJIJI CHA QUNU ALIKOZIKWA MZEE NELSO MANDELA JUMAPILI DESEMBA 15, 201
IMEWEKWA DESEMBA 19 SAA 01;21MCHANA
Daraja la waendao kwa miguu likipita juu ya barabara mpya ya lami inayojengwa kuelekea kijijini Qunu.
Siku ya mazishi barabara ya kuelekea Qunu ilifungwa na ni magari yaliyokuwa na kibali tu ndiyo yaliyoruhusiwa kupita
Ulinzi ulikuwa mkali kila sehemu kijijini Qunu
Wageni wakiwa katika geti kuu la nyumba ya Mzee Mandela hapo Qunu
MAANDALIZI YA MWILI WA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA YAENDELEA MORTUARY YA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA IRINGA
Mzee Teming'ombe akilia kwa uchungu
kufuatia kifo cha kijana wake aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa
Emanuel Mteming'ombe aliyerafiki usiku wa kuamkia leo katika
Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa alikolazwa kwa zaidi ya siku mbili
waombolezaji wakiwa ktk hospital ya
rufaa ya mkoa wa Iringa katika maandalizi ya mwili wa aliyekuwa katibu
wa CCM mkoa wa Iringa hivi sasa
Waombolezaji wakishusha jeneza la kuuweka mwili wa katibu wa CCM mkoa wa Iringa
BREAKING NEWS.. KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA AFARIKI DUNIA
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Bw. Emanuel Mteming'ombe. Bw. Mteming'ombe
KATIBU
wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Bw Emanuel Mteming'ombe
amefariki dunia katika hospital ya mkoa wa Iringa.
Katibu
huyo alikuwa amelazwa katika Hospital ya mkoa wa Iringa kwa
zaidi ya siku moja akisumbuliwa kwa ugonjwa athima na leo amefariki
dunia.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu amethibitisha juu ya
taarifa hiyo na kuwa taratibu za mazishi zinafanywa .
Habari zaidi juu ya taarifa hii utaendelea kuzipata endelea kutembelea mtandao huu
WATU WANNE WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI MOSHI.
Afisa wa polisi katika ofisi ya kamanda wa polisi akipanga vitu mbalimbali walivyokutwa navyo watu
hao wanaotuhimiwa kuwa majambazi.
Laptop mbili pia zilikuwa ni miongoni mwa vitu walivyokutwa navyo.
Vifaa mbalimbali vya kubomolea.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Koka Moita akionesha Vocha za mitandao mbalimbali walizokutwa nazo watu hao.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Koka Moita akionesha bunduki aina ya Shotgun waliyokutwa nao watu hao.
****************
****************
IMEWEKWA DESEMBA 19 SAA 12:33 MCHANA.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Moshi
JESHI la polisi mkoani Kilimanaro, limewatia mbaroni watu 4 kwa
tuhuma za kushiriki katika matukio mbali mbali ya uhalifu na
unyangaji wakutumia silaha yaliyotokea mkoani hapa.
Kaimu kamanda wa jeshi hilo, Koka Moita, alisema jeshi hilo
lilifanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao baada ya kukamata gari
lenye namba za usajili T564 AUW aina ya Grand Mark 2 wenye rangi ya
siliva, katika maeneo ya Kiusa Manispaa ya Moshi ambalo limesadikika
kushiriki kwenye matukio hayo.
Alisema dereva wa gari hilo ambaye alifahamika kwa jina la Nicksoni
Elias Urio (28) mkaazi wa Majengo Moshi alitoa ushirikiano mkubwa
ambao ulipelekea kuwakamata watu 3 ambao wamesadikika kuwa majambazi
walioshiriki katika baadhi ya mtukio mkoani hapa.
“ Baada ya kuwatia mbaroni watumiwa hao, operatini kali ilifanyika
yakuwapekuwa na kubaini vitu mbali mbali ikiwemo ikiwemo bumbuki
aina ya shotgun ikiwa imekatwa mtutu na kitako cha bunduki hiyo hivyo
hatukupata namba zake”alisema na kuendelea kuwa
“laptop, 2 aina ya dell na hp, Plate namba 3 na funguo za magari,
simu 8 za mkononi , vocha za simu za mitandao yote , ambaye thamani
yake haijatulikana, pamoja na vifaa mbali mbali vya kuvunjia”alisema
Moita.
Moita alisema Vocha za simu bado hazijajulikana thamani yake, na
uchunguzi unaendelea marautakapokamilisha watuhumiwa
watafikshwamahakamani.
Aidha Kamanda Moita aliwataka wananch kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi
la polisi ili kufichua matukio mbali mbali ya uhalifu yanayojitokeza
mkoani hapa.
Kwa Hisani ya Michuzi Blog
MWENYEKITI CCM WILAYA YA TANGA AHAMASISHA MICHEZO KWA VIJANA.
Subscribe to:
Posts (Atom)