MKUU WA MKOA WA MWANZA AKUTANA NA WAGENI KUTOKA MAREKANI

October 02, 2017
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani ikiongozwa na Mwinjilisti Rojas Matias, walipomtembelea ofisini kwake jana. 

Watumishi hao walikuwa na mkutano mkubwa wa injili tangu Septemba 27 hadi Oktoba Mosi, 2017 katika uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza ulioandaliwa na kanisa la EAGT Lumala Mpya chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola.

Mhe.Mongella aliwahakikishia ushirikiano mwema pindi watakapokuwa tayari kuwekeza katika shughuli mbalimbali ikiwemo za kielimu katika mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani
Wageni kutoka Marekani pamoja na mwenyeji wao Mchungaji Kulola, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia) akizungumza na wageni/ watumishi wa Mungu kutoka taasisi ya More International Ministry ya Marekani. Katikati ni Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani na kushoto ni Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Baada ya mazungumzo, watumishi hao walifanya maombi kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Baada ya mazungumzo, watumishi hao walifanya maombi kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati), Mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani (kushoto) pamoja na Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza (kulia)
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto) akiwa pamoja na Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola kutoka kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza (kulia).
Katibu wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Levi Matia (kushoto), akiwakaribisha wageni kutoka Marekani walipotembelea ofisini hapo jana.

SPANEST BAND YAENDELEA KUHAMASISHA UTALII NA KUPIGA VITA UJANGILI

October 02, 2017
Mratibu wa mradi wa SPANEST na mwenyekiti wa SPANEST Band Godwell Ole Meing’ataki akiwa katika maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.
SPANEST Band wakitumbuiza wakati wa maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

SPANEST Band ya mkoani Iringa yaendelea kutoa elimu ya utalii na kupiga vita ujangili kwa watanzania kupitia nyimbo mbalimbali ambazo zimekuwa zikihamasisha wananchi kuujua utalii,kutunza vivutio vyote vya kitalii na kuacha kuuwa wanyama wanaoendelea kuliingizia taifa pato kupitia utalii.
 
Akizungumza na blog hii mratibu wa mradi wa SPANEST na mwenyekiti wa SPANEST Band Godwell Ole Meing’ataki alisema kuwa wameamua kuanzisha Band hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya utalii na kupiga vita ujangili kwa njia ya sanaa ili kuwafiki wananchi walio wengi.

“Unajua kuwa watu wengi wanapenda kusikiliza nyimbo na kuona maenyesho ya wasanii hivyo uwepo wa SPANEST Band umesaidia kutoa elimu ya utalii ndio maana unaona kwenye maonyesho mengi wakuwa wakitumbuiza na kupendwa na kila mtu anayekuwa katika eneo hilo” alisema Meing’ataki.

 Meing’ataki alisema kuwa nyimbo za SPANEST Band zinatoa elimu mahususi ya maswala ya utalii hivyo imekuwa kazi rahisi kuwafika vijana na watu wengine wa rika mbalimbali ambao wamekuwa wakihudhuria matamasha au maonyesho ya kitalii.

Aidha Meing’ataki alisema kuwa Band hiyo tayari imeshasajili na baraza la Sanaa na michezo (BASATA) hapa nchi ili kupata fursa ya kutumbuiza katika maonyesho yoyote hapa nchini na kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa watanzania na wasio watanzania.

“Usiposajili kazi yako utakuwa unajinyima haki yako ya msingi hivyo band hii ya SPANEST imesajili na BASATA wanaijua hivyo kuifanya kufanya hata kazi za serikali kwa kuwa waandaa nyimbo zao bila kukiuka sheria za nchi” alisema Meing’ataki

Meing’ataki aliwaomba wadau mbalimbali wa utalii na uhifadhi kuendelea kuiunga mkono SPANEST Band ili wapate nafasi ya kuendelea kutoa elimu kwa njia ya Sanaa ya uimbaji ambao kwa kiasi kikubwa kwa sasa vijana wengi wanaitumia.

“Mimi nawapongeza sana wasnii wote wa SPANEST Band kwa kazi wanaifanya kuelimisha jamii kwani wanatunga nyimbo zao vizuri na zinahamasisha wananchi kupembela vivutio vyao na kupiga vita ujangili wa wanayama ambao ndio vituo vikubwa kwenye mbuga zetu hapa nchini” alisema Meing’ataki

Naye katibu wa band hiyo Denis Nyali alisema waliamua kuanza kuandaa nyimbo za kuhamasisha utalii na kuacha kuuwa wanyama kutoka na kufanya utalii katika mbuga mbalimbali na kijionea vitu vingi ya kuvutia.

“Mimi ni mwandishi wa habari hapa mkoani Iringa tulikuwa tumeenda kutalii katika mbuga ya Ruaha iliyopo mkoani Iringa tukapewa zoezi la kutafuta njia za kutoa elimu ya kupinga ujangili na kutoa elimu ya utalii na ndio ulikuwa mwanzo wa kuanzisha SPANET Band” alisema Nyali

Nyali alimpongeza mratibu wa mradi wa SPANEST Godwell Ole Meing’ataki ambaye pia ni mwenyekiti wa Band hiyo kwa juhudi zake za kuanzisha na kuendeleza kwa kuwaongezea majukumu ya kutumbuiza kwenye matasha mbalimbali ya utalii na kuzifanya nyimbo zake kuwa maarufu.

“Unajua sisi ni wasanii tu hivyo bila kuwa na mtu anayetusaidia hatuwezi kufika popote pale ndio maana kushikwa mkono na mratibu wa mradi wa SPANEST Ole Meng’ataki kumetusaidia kuendelea kutunga nyimbo na kufanya video za nyimbo hizo ambazo zimekuwa na mvuto kwa jamii” alisema Nyali

Nyali alisema kuwa lengo la Band hiyo ni kuendelea kutoa elimu ya kitalii kwa kutumia nyimbo ambazo wanazoziimba kwa njia tofauti tofauti kufikisha ujumbe halisi kwa wanachi waupende utalii na kupiga vita ujangili ambao umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo ya utalii.

“Tunawaomba wananchi wawe na subila hivi karibuni tutawaambia kuwa nyimbo hizi zitapatikana wapi kwa kuwa Band hii ipo chini ya mratibu wa mradi wa SPANEST hivyo tunasubili muungozo wa kutoka kwao kwa kuwa kazi yetu tumeshamaliza ya kurekodi na tunaendelea kutumbuiza katika maonyesho mbalimbali ambayo tunakuwa tunaalikwa” alisema Nyali

DC WA KIBAHA AWAASA WANAWAKE KUTODHARAU KAZI

October 02, 2017
Na.Vero Ignatus ,Mlandizi

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumtha mshana amewaasa wanawake kutokudharau kazi hata kama ni ndogo kwani kwenye hiyo ndogo ndipo nyingine kubwa itafuata.

Ameyasema hayo Katika Kanisa la RGC lililopo Mlandizi ambapo alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la wanawake lililoambatana na Changizo kwa ajili ya kununua eneo la kiwanja cha kujenga kanisa

Mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni mchungaji alipata nafasi ya kuhubiri katika kongamano hilo, ambapo amewataka wanawake kujiamini na kuaajibika kwani hata neno la Mungu linasema asiyefanya kazi na asili.

"Nyumba ambayo mwanamke ni legelege nyumba hiyo haitaendelea kamwe,wanawake changamkeni wajibikeni nyie ndiyo nguzo ya familia hutamchosha mume wako" alisema

Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi Kambi ya Waebrania Mlandizi Mercy Adam Mwakimomyile amesema kuwa Kongamano hilo limebeba kaulibiu isemayo Nguvu ndani ya Mwanamke(Power in Woman)ambapo imewafanya wanawake wajisikie wanaweza

"Kutokana na uwezo uliopo ndani ya mwanamke basi leo tumeamua kuwa tunaweza kumjengea Mungu madhabahu kupitia kongamano hili" alisema

Amesema katika kanisa hilo wato watoto zaidi ya elfu moja ambao wanafundishwa maadili kupitia neno la Mungu kuibua vipawa  mbalimbali vilivyopo ndani yao na kuviibua
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumta Mshama .Picha na Vero Ignatus Blog.
Mkuu wa wilaya akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kanisa la GRC kambi ya Waebrania Mlandizi àliyepo kulia kwake ni mchungaji kiongozi wa kanisa hilo la Mlandizi.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Assumtha Mshama akiwa anaonyeshwa mipaka ya eneo la kiwanja cha Kanisa la GRC Kambi ya Warbrania Mlandizi aliyepo nae ni Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo  Mercy Adam Mwakimomyile.Picha na Vero Igbatus Blog.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe.Assumta Mshama akiwa anaongoza maombi mara baada kuona eneo ambalo linatarajiwa kujengwa kanisa .Picha na Vero Ignatus Blog.Kuna Mama Mtume Deo Rwetaka 

Mhe.Assumtha Mshama akihubiri neno la Mungu katika kanisa hilo la GRC lililopo Mlandizi.Picha na Vero Ignatus Blog
 Wa kwanza kulia ni Mchungaji Kiongozi wa RGC Kambi ya Waebrania Mercy Adam Mwakimomyile Mama Mtume Deo Rwetaka wa Kwanza kushoto,Mama Askofu Amon Lukama wa RGC Tanzania na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Assumtha mshana
Baadhi ya waumini walioshiriki katika ibada hiyo ya Kongamano la Wanawake RGC Mlandizi.Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya watoto wanaolelewa kanisani hapo wakiimba wimbo maalumu wa kuliombea Taifa la Tanzania pamoja na Rais wa nchi.Picha na Vero Ignatus Blog.
Ibada ya ikiendelra katika kanisa hilo la GRC Kibaha Mlandizi .Picha na Vero Ignatus Blog.
MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BONDE LA NGORONGORO

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BONDE LA NGORONGORO

October 02, 2017

2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia bonde kuu la Ngorongoro mara baada ya kuwasili tayari kwa Uzinduzi wa Makumbusho Mpya ya Olduvai utakaofanyika kesho tarehe 3, oktoba 2017.
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Mhifadhi Dkt. Maurus Msuha mara baada ya kutembelea bonde kuu la Ngorongoro mara baada ya kuwasili tayari kwa Uzinduzi wa Makumbusho Mpya ya Olduvai utakaofanyika kesho tarehe 3, oktoba 2017.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Maandalizi ya Utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika Yaanza

October 02, 2017

Picha Na 1
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha wataalam kutoka Uganda,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) kabla ya kuanza ziara katika Ziwa Eyas Wembere lililopo mkoani  Singida.
Picha Na 2
Wataalam kutoka ,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani).
Picha Na 3
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande (kulia) pamoja na wataalam kutoka Uganda wakifuatilia ufafanuzi  uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani)
Picha Na 4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (kushoto mbele) akieleza jambo katika kikao hicho.
Picha Na 5
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akielezea hali ya utafiti wa mafuta na gesi nchini.
Picha Na 6
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande akifafanua jambo katika kikao hicho.
Picha Na 7
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Nishati na Madini, Asteria Muhozya (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki, Salum Mnuna katika kikao hicho
…………………

Asteria Muhozya na Greyson Mwase.
Timu ya wataalam kutoka Uganda imewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta. Mbali na kubadilishana uzoefu wataalam hao watafanya ziara Ziwa Eyasi Wembere lililopo mkoani  Singida.

Kabla ya kuanza kwa ziara hiyo wataalam hao leo tarehe 2 Oktoba, 2017  wamefanya  kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani na kuwashirikisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kalemani amesema  maandalizi hayo ni  juhudi za Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa  Tanzania, Dkt. John Magufuli za kuhakikisha kuwa rasilimali ya mafuta inagunduliwa na kuanza kuleta manufaa kwa wananchi, ambapo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Ujenzi wa Mradi ya Bomba la Kusafirisha Mafuta  Ghafi la  Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania tarehe 5 Agosti, 2017 alieleza kuwa wataalam waliogundua mafuta katika Ziwa Abert nchini Uganda kushirikiana na wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na  Eyasi nchini Tanzania.

Dkt. Kalemani amesema baada ya Rais wa Uganda kukubali ombi hilo yalianza maandalizi kupitia vikao mbalimbali ambapo hatua iliyofikiwa kwa sasa ni wataalam kukutana na kubadilishana uzoefu kabla ya kuanza kwa shughuli za utafiti katika maziwa husika.

Amesema wataalam wataanza kwa kufanya ziara ya siku mbili katika Ziwa Eyasi Wembere mkoani Singida ili kupata picha halisi kabla ya kuanza kwa majadiliano ya kubadilishana mawazo ya namna bora ya utafiti katika maziwa husika.

“ Sisi kama  Tanzania  tupo  tayari kubadilishana uzoefu na wataalam wa Uganda kwenye utafiti wa mafuta na kuanza kazi mara moja;  hata hivyo pia tupo  tayari kubadilishana nao uzoefu  kwenye masuala ya  gesi kwa kuwa tuna utaalam huo, lengo likiwa ni kuimarisha sekta hizi za mafuta na gesi kwa nchi zote mbili,” amesema  Dkt. Kalemani.

Ameongeza kuwa kwa kuwa Tanzania ina uzoefu mkubwa kwenye utafiti wa gesi asilia, wapo tayari kutuma wataalam nchini Uganda kushirikiana kwenye utafiti wa gesi nchini Uganda.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda na kiongozi  wa ujumbe huo, Robert Kasande amesema kuwa wapo tayari kubalishana uzoefu ambapo watalenga katika kuangalia tafiti zilizowahi kufanyika nyuma, kutembelea maeneo husika na kuweka mikakati ya namna bora ya kufanya utafiti kwa ubora wa hali ya juu kwa kushirikiana na  Tanzania.