WAZIRI MPINA AAGIZA MKATABA WA OVENCO KUVUNJWA NA KUUNDWA MKATABA MPYA

December 23, 2017


Katika Picha,  Ng’ombe aina ya Borani inayomilikwa na mwekezaji kampuni ya Overland katika Ranchi ya Mzeri , Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Picha 3
Katikati Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Mhe. Luhaga Mpina akiongea  vyombo vya habari baada ya ziara ya ukaguzi wa  baadhi ya vitalu katika Ranchi ya Mzeri iyopo Wilayani Handeni Mkoani Tanga, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe, na kulia ni mkurugenzi wa kampuni ya Overland Bw. Faizal Edha.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kati kati na Mkuu wa Wilaya ya Handeni kulia Godwin Gondwe pamoja na wataalam kutoka Wizarani na Mkoani Tanga wakiwa katika zoezi la kukagua baadhi ya vitalu  vilivyopo katika Ranchi ya Mzeri Wilayani Handeni.
Picha 5
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akikimkimbiza Ng’ombe aina ya Borani katika Ranchi  ya Mzeri alipokuwa katika zoezi la ukaguzi wa vitalu .

Aliyesimama Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akongea na Uongozi wa Wilaya ya Handeni na wajumbe wa Msafara kabla ya kuanza kwa ziara katika Ranchi ya Mzeri kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe
……………

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ameagiza kuvunjwa kwa mkataba ulioundwa baina ya RANCHI ya Taifa NARCO na kampuni ya Overland  kwa pamoja na kuunda kampuni ya OVENCO uliyokuwa na mapungufu ya kisheria na kiutendaji kufunjwa ifikapo mwisho wa mwezi huu wa December na kutoa mwezi mmoja kwa  NARCO kuunda mkataba mpya wenye mwengozo wa kisheria.
Mpina aliyasema hayo jana alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa Ranchi ya Mzeri iliyopo wilayani Handeni Mkoani Tanga yenye ukubwa kwa Hekta 41,000  ambapo hekta 21,000 zinamililiwa na Muwekezaji kampuni ya Overland muwekezaji ambaye, amekuwa na mgogoro wa muda mrefu na  NARCO ambapo baada ya Waziri Mpina kusililiza pande zote mbili na kujiridhisha  na kumuona muwekezaji kutokuwa na uwezo wa kufikia malengo ya kuendeleza eneo lote la ardhi  ambalo amekuwa akiliendeleza bila makubaliano yoyote ya kisheria, jambo ambalo limempelekea Waziri Mpina kuagiza  NARCO  kuingia katika hatua ya kuunda mkataba mpya baina yake na muwekezaji huyo utakaozingatia masharti mapya ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa muwakilishi wa NARCO Katika kitalu hicho.
Aidha Waziri Mpina ameagiza muwekezaji huyo asihamishwe kwa kuwa ameonyesha nia ya kuendeleza eneo hilo kwa kuwepo kwa ng’ombe wambegu aina ya Borani pamoja na miundombinu mingine
Akizungumzia eneo la hekta 20,000 linalomilikiwa na wawekezaji wengine wadogo, Mpina aliwataka wawekezaji hao kulipa na kumaliza madeni yote ya kodi ya serikali wanayodaiwa  katika vitalu vyao ifikapo January mosi 2018.
“Wawekezaji wengine wengine wanaomiliki vitalu katika ranchi hii ya Mzeri mnatakiwa kulipa madeni yote ya kodi mnayodaiwa na Serikali kodi mnayolipa ya shilingi elfu moja (1000) kwa mwaka ni kidogo sana lakini bado hamlipi, kinyume na hili ni bora muondoke wenyewe au tutawaondosha kwa nguvu muda huo ukifika. “ Alisisitiza Mpina.
“Baada ya kumaliza kulipa nawagiza NARCO kuwapa miezi mitatu wawekezaji hawa kuhakikisha wanaweka miondombinu inayolingana na ukubwa wa eneo na matumizi ya ardhi , tunataka wawekezaji wafikie malengo na mashamba haya yafanye kazi.” Alisema Mpina.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema kuwa, Wiaya ya handeni itaendelea kulinda  mazao na rasilimali za Mifugo kupitia sheria ndogondogo ambazo wilaya hiyo imejiwekea.
Akizungumza kwa namna ambavyo ameyapokea maagizo wa Waziri Mpina , mmiliki wa kampuni ya Overland Bw. Faisal Edha alisema kuwa amekubalina na maagizo ya Mpina na yupo tayari kuendelea na uwekezaji na anaamini kuwa mkataba mpya utanufaisha pande zote mbili.
Awali akipokea taarifa ya Mifugo ya wilaya ya Handeni, Waziri Mpina alimpongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Godwin Gondwe  kwa kuzitambua sheria za usimamizi wa mifugo na kuzitumia jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kutokuwepo kwa uonevu kwa watu wa jamii ya wafugaji na kuzitaka wilaya nyingine nchini kuiga mfano wa wilaya hiyo kwa kuunda sheria ndogo ndogo zitakazowaongoza katika sekta  ya mifugo.

JUMUIYA YA WAZAZI TANZANIA MKOA WA DAR ES SALAAM, WAMPOKEA KWA KISHINDO MWENYEKITI WA TAIFA WA JUMUIYA HIYO DK. EDMUND MNDOLWA

December 23, 2017
Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akisalimia baadhi wa wana CCM waliofurika katika ukumbi wa Tawi la CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambao walifika kumlaki katika mapokezi yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam, jana.
 Gari la Dk. Mndolwa likiwasili lango Kuu la Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mapokezi hayo
 Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar  Abdallah Haj Haidar akimpokea Dk Mndolwa kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Katibu wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba kwenda kusaini vitabu wa wageni na kuzungumza na uongozi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo
 Dk. Mndolwa akisaini kitabu wa wageni katika Ofisi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alipowasili. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa huo, Frank Kalokola Kamngisha
 Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Abdallah Haj Haidar akisaini kitabu cha wageni, huku Dk. Mndolwa akiendelea kufanya hivyo pia.
 Abdallah Haj Haidar akisalimia
 Mama Patricia Rukia Mndolwa akisalimia
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Bara Burhan Rutta akisalimia
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Kusilawe akisalimia
 Kalokola akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, amkaribishe Dk. Mndolwa kuzungumza na Uongozi
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba alizungumza kabla ya kumkaribisha Dk Mndolwa kuzungumza
 Kate Kamba akimkaribisha Dk Mndolwa kuzungumza na uongozi
 Dk. Mndolwa akizungumza na Uongozi
 Mwafongo na Katibu wa CCM Kata ya Ilala Habib Nasser ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, wakitoka nje kumsubiri Dk Mndolwa kutoka nje tayari kwa safari ya kwenye kwenye eneo kuu la mapokezi ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala
 Gari lilobeba Dk Mndolwa likiwasili kwenye Viwanja vya Ofisi ya Tawi la CCM Mwinjuma 
 Kijana wa CCM akimvisha Skafu Dk. Mndolwa baada ya kuwasili CCM Mwinjuma
 Dk. Mndolwa akipokea kwa ukakamavu saluti ya kijana wa CCM baada ya kuvishwa skafu
 Dk Mndolwa akiongozana na baadhi ya viongozi kwenda eneo la tukio
 Dk Mndolwa akisalimia baadhi ya wana CCM wakati akienda ukumbini
 Dk Mndolwa akisalimia baadhi ya viongozi wakati akienda ukumbini  
 TOT wakitumbuiza kumlaki ukumbini Dk. Mndolwa
 Dk. Mndolwa akienda meza kuu
 Dk. Mndolwa na Makamu wake- zanzibar wakiwa tayari meza kuu
 Viongozi wa meza kuu wakiungana na Dk Mndolwa kushangilia baada ya kuwasili eneo hilo
 Mmoja wa viongozi katika Baraza la Wazee wa jumuiya ya Wazazi Mzee Mkali akisalimia
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Mwafongo akifanya utambulisho wa viongozi ndazi ya mkoa
 Viongozi ndazi ya mkoa wakisalimia baada ya kutambulishwa 
 Baadhi ya viongozi waliohudhuria mapokezi hayo wakiwa ukumbini
 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya wazazi Tanzania Ndugu Rutta akitambulisha viongozi ngazi ya taifa  
 Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi tanzania Seif Shaban Mohammed akifafanua maana na umuhimu wa neno 'Mapinduzi'  baada ya kutambulishwa  
 Ndugu Mwafongo akiendeleza ratiba
 Mwenyekiti wa CCM Temeke ndugu Almish akizungumza baada ya kutambulishwa 
 Ndugu Kalokola akizungumza kumtambulisha Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Ndugu Haj
 Kakamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Ndugu Hajj akizungumza
 Shabiki wa CCM akimuombea maisha marefu na uongozi bora Dk. Mndolwa tukio ambalo lilikuwa la ghafla
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba akizungumza kabla ya kumkaribisha Dk. Mndolwa kuzungumza na hadhara 
 Omar Kimbau aliyewahi kuhamia CUF akitangaza kurudi CCM mbele ya Dk. Mndolwa
 Dk. Mndolwa akimpongeza Kimbau kwa kuzinduka na kurejea CCM
 Dk. Mndolwa akihutubia kweye mapokezi hayo

CHAKULA CHA JIONI SERENA HOTEL
 Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Mwafongo akiwakaribisha Dk. Mndolwa na Mkewe walipowasili hoteli ya Serena kwa ajili ya chakula cha jioni
 Mwafongo akiwaongoza kwenda eneo la kuketi 
 Dk. Mndolwa akimsalimia Mwenyekiti  wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Kalokola
 Dk Mndolwa akimsalimia  Ndugu Kizigha
 Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania- Zanzibar Ndugu Hajj akimsalimia Mama Mndolwa
 Dk Mndolwa akizungumza jambo wakati wakisubiri muda wa chakula
 Ndugu Mwafongo akiwa amesimama kuwakaribisha rasmi waalikwa wote 
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Kalokola akizungumza maneno ya ukaribisho kwenye chakula hicho cha jioni
 Dk Mndolwa akiongozana na Ndugu Hajj kuchukua chakula
 Angela Kizigha akimsaidia Dk. Mndolwa kubeba chakula
 Mweneyekiti wa CCM Kinondoni akichukua chakula
 Viongozi mbalimbali wakichukua chakula
 Ndugu Mwafongo akiongoka na chakula chake kwenda sehemu ya kuketi
 Ndugu Hajj akichukua chakula 
 Baadhi ya waandaaji wa nyama choma hotei ya Serena
 Waalikwa wakila chakula 
 Dk Mndolwa na mkewe wakipata chakula na waalikwa wengine  

 Dk Mndolwa akitoa nasaha zake baada ya chakula   
Kisha Dk. Mndolwa akapozi kwa picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali aliopata nao chakula hicho cha jioni. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO