KAIMI MKUU WA MKOA WA TANGA AIPONGEZA TAYODEA KWA KUSAIDIA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

February 22, 2017
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa akibadhi vifaa vya vijana wa mradi wa WEKEZA (Wezesha Ustawi Endelevu kiwango cha Elimu Kuzuia Ajira kwa watoto) kulia ni Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyegea na kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga,Faidha Salim
 Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyege akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza.
Mwenyekiti wa Tayodea Stephen Kiama Mwaimu akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza akizungumza kwenye halfa hiyo

 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza kushoto akionyeshwa baadhi ya vifaa vya ushonaji waliokabidhiwa vijana kupitia mradi wa WEKEZA
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza kushoto akionyeshwa kitu na Meneja wa Mradi wa WEKEZA wa Tayodea Michael Mchomvu wakati wa halfa hiyo
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza akitazama vifaa mbalimbali vya ushonaji wa kwanza kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Tayodea ,David Chanyegea
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza akimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi wa Tayodea,David Chanyegea kulia wakati wa halfa ya kukabidhiwa vifaa vya ushonaji kwa vijana kupitia mradi wa WEKEZA.

 Meneja wa Mradi wa WEKEZA wa Tayodea Michael Mchomvuwa kwanza kulia akifuatilia hotuba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa kukabidhiwa vifaa kwa vijana.

DKT. KALEMANI AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI JIMBONI KWAKE

February 22, 2017

Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (aliyevaa miwani) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyakayondo kuhusiana na utekelezaji wa miradi mbalimbali kijijini humo na jimboni kwa ujumla.
Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa kisima (kilichofunikwa kwa nyasi) kilichochimbwa katika kijiji cha Nyakayondo. Jumla ya visima virefu 30 vinatarajiwa kuchimbwa jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi ya Nyarututu, iliyopo Kata ya Bwanga. Jumla ya vyumba vya madarasa vitano na matundu 30 ya vyoo vinatarajiwa kujengwa katika shule hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiongozana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chato, Ibrahim Bagula (kushoto) na Diwani wa Kata ya Bwanga, Nuhu Mahmoud (kulia) wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa Jimboni humo.

Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shaban Ntalambe (kulia) na Diwani wa kata ya Bwanga, Nuhu Mahmoud (katikati) wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi ya walimu katika shule ya Msingi ya Bwanga B. Mradi huo unahusisha ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa, ofisi ya walimu na matundu 30 ya vyoo.
Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kushoto) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali jimboni humo. Kulia ni Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Mali Misango. Nyuma ya Dkt. Kalemani ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato, Christian Manunga.

MKUU WA MKOA WA ARUSHA ASHIRIKIANA NA WANANCHI KATIKA KAZI ZA MAENDELEO MONDULI

February 22, 2017
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(kushoto)akipokea kutoka kwa Mhandisi Shin Pil Soo sehemu ya msaada mabati 300 na mifuko ya Sementi 500 iliyotolewa na Kampuni ya ujenzi ya Hanil Jiangsu Joint Venture Ltd inayojenga barabara ya Sakina hadi Tengeru yenye urefu wa kilometa 14.1 ,kulia ni Meneja wa Tanrods mkoa wa Arusha,Mhandisi John Kalupale,msaada huo umetolewa kwa Mkuu wa mkoa ili umwezeshe kusaidia shughuli za maendeleo zilizoanzishwa na wananchi na alikabidhi ili utumike kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Makuyuni wilayani Monduli. 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akishirikiana na askari wa JKT kambi ya Makuyuni na wananchi wa Kata ya makuyuni katika ujenzi wa Kituo cha Afya katika ziara yake wilayani Monduli. 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(katikati) akilakiwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rifit Valley Kata ya Majengo wilaya ya Monduli,kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Idd Kimanta na kulia ni Mkuu wa Shule,Julius Maghembe. 
Mkuu wa Shule ya Sekondari Rift Valley ,Julius Maghembe akiinua Sh 500,000 zilizotolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho gambo kwaajili ya kununua viti vitano vya walimu. 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(kushoto) akiwa na viongozi wa wilaya ya Monduli ndani ya moja vya vyumba viwili madarasa vilivyozinduliwa baada ya ujenzi wake kukamilika katika Shule ya Sekondari Rifit Valley. 
Wananchi wakichangia nguvu zao katika ujenzi wa jengo la Upasuaji kwenye Kituo cha Afya Mto wa Mbu 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akishiriki kazi za mikono pamoja na wananchi katika ujenzi wa jengo la Uapsuaji katika Kituo cha Afya Mto wa Mbu aliahidi kutoa mifuko 100 ya Sementi na Mabati 100.
Dk. Kigwangalla afunguka Maandhimisho ya Miaka 25 ya Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii

Dk. Kigwangalla afunguka Maandhimisho ya Miaka 25 ya Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii

February 22, 2017
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, ameungana na Wadau wa Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC) katika kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Tume hiyo. Akizungumza katika ufunguzi, Dkt. Kigwangala amesema kuwa katika kipindi cha miaka 25, Tume hii imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali na Wadau wengine katika kuhakikisha huduma za Jamii zinatolewa kwa kuzingatia ubora na uwiano mzuri.
Rais wa Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC), Askofu Dkt. Alex Malasusa, akizungumza na Wajumbe na wageni mbalimbali waliohudhuria katika kumbukumbu ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Tume hiyo. Kumbukumbu hizo zinafanyika tarehe 21/02/2017 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
“Kulingana na taarifa nilizopewa, kwa sasa Tume ina taasisi za elimu zaidi ya 1000. Hizi zinajumuisha shule na vituo vya kutolea Elimu ya awali, shule za Elimu ya Msingi na Sekondari, Vyuo vya ualimu, vituo vya mafunzo ya ufundi stadi na Vyuo vya Elimu ya Juu. Kwa upande wa Sekta ya Afya, nimeambiwa mna vituo vya afya vipatavyo 900. Hii ni pamoja na hospitali 102, vituo vya afya 102 na zahanati zipatazo 696. "Vilevile kuna takribani taasisi zipatazo 58 za kutolea mafunzo ya wataalamu wa Afya na pia kuna Vyuo Vikuu. Ni dhahiri kabisa, taasisi zote hizi zinatoa mchango mkubwa katika nchi yetu na pia zimeiwezesha jamii yetu kupata huduma za elimu na afya zilizo bora,” alisema Dkt. Kigwangala.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala, akitoa hotuba ya ufunguzi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC), yanayofanyika tarehe 21/02/2017 katika ukumbi wa Diamond Jubilee , jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yanapambwa kwa kauli mbiu isemayo “Wito wa Kuelimisha na Kuponya Jamii: Changamoto na Mafanikio ya utoaji wa huduma za jamii Tanzania”, yamehudhuriwa na Mh. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu Tanzania, Waheshimiwa Maaskofu, akiwemo Rais wa Tume hiyo Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, Makamu wa Rais wake, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Mganga Mkuu wa Serikali, pamoja na Wadau mbalimbali wa Tume hiyo. Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kigwangala, pia alitoa rai kwa Wadau wa Tume hiyo hususan kwa Taasisi zote za Afya zilizo chini ya CSSC, kuwa na uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali fedha ili kuhakikisha kuwa hudum a za afya zinamfikia kila mlengwa. Na pia aliongeza kwamba uendeshwaji wa vituo hivi vya afya uende sambamba na sera ya afya ya nchi.
Baadhi ya Washiriki wanaohudhuria katika maadhimisho ya miaka 25 ya Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC), wakimsikiliza ,Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala wakati akitoa hotuba ya ufunguzi . Maadhimisho hayo yanafanyika tarehe 21/02/2017 katika ukumbi wa Diamond Jubilee , jijini Dar es Salaam.
Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) ni chombo kilichoundwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) mwaka 1992 kwa dhumuni la kuratibu na kusimamia huduma za kijamii zitolewazo na Taasisi za Makanisa husika za Elimu na Afya nchini.
Baadhi ya Maaskofu waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 25 ya Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (Hayupo pichani). Kutoka kulia ni Askofu Severine Niwemugizi ( Jimbo Katoliki la Rulenge), Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Judah Thadei Rwaichi, akifuatiwa na Askofu Telesphor Mkude wa Jimbo Katoliki la Mororogoro.
Makamu wa Rais wa Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa (Jimbo la Iringa), akimpongeza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala mara baada ya kutoa hotuba fupi ya ufunguzi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Tume hiyo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC, Bw. Peter Maduki, na kulia kwake ni Rais wa Tume hiyo, Askofu Dkt. Alex Malasusa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala wa pili kutoka kushoto akiwa pamoja na Rais wa Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC), Askofu Dkt. Alex Malasusa (katikati), pamoja na Makamu wa Rais wa Tume hiyo, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa (kushoto). Wengine ni Mganga Mkuu wa Serikali, Prof Mohamed Bakari na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa CSSC, Bw. Peter Maduki. Hii ni katika maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa, Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii, yanayofanyika tarehe 21/02/2017 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR

February 22, 2017
Pichani Mpendwa wetu Jennifer Livigha aliyekuwa Mmiliki wa Libeneke la Chinga One na Mwanachama wa TBN Enzi za uhai wake. Marehemu alizaliwa 25.01.1979 Nachingwea, alifariki nyumbani kwake kinyerezi 18.02.2017 Jijini Dar es salaam. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ini. Atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao Nachingwea.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Jennifer Livigha aliyekuwa mmiriki wa Blog ya Chinga One katika Hospitali ya Amana.
 Waongozaji wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jennifer
 Waombolezaji wakiwemo baadhi ya wana Tanzania Bloggers Network (TBN) ambapo Marehemu Jennifer alikuwa mwanachama
 Mmoja ya waombolezaji akitoa historia fupi ya Marehemu
Mmoja wa wanafamilia akitoa utaratibu kabla ya kuanza kutoa heshima za Mwisho kwa mpendwa wetu Jennifer
 Baadhi ya wanachama wa Tanzania Bloggers Network (TBN) wakiwa wanaaga mwili wa aliyekuwa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer 'Chinga One'
Baadhi ya ndugu wa karibu, Jamaa na Marafiki wakiwa wanaaga Mwili wa Marehemu Jennifer
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wanaimba nyimbo za maombolezo 
Baadhi ya wanachama wa TBN , ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wanapeleka mwili wa Marehemu Jennifer katika Gari tayari kwa safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi
Baadhi ya wanafunzi wakilia kwa uchungu 
Baadhi ya ndugu, jamaa na mafafiki pamoja na wanachama wa TBN wakiwa wanawaaga wanaosafiri na mwili kuelekea Nachingwea
 Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi (Aliyevaa T-Shirt ya Mistari) akiongea jambo kabla ya safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi.
Baadhi ya wana TBN wakiwa katika Msiba wa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer
 Safari ya kuelekea Nachingwea ikiwa imeanza ..
Picha zote  na Fredy Njeje wa TBN