WANAWAKE WAJASIRIAMALI 450 WAPEWA BURE MITUNGI YA GESI YA ORYX,MAJIKO JIJINI TANGA

September 09, 2023



Na Mwandishi Wetu, Tanga


WAZIRI wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu amekabidhi mitungi mikubwa ya gesi ya Oryx 150 pamoja na majiko yake bure kwa wanawake wajasiriamali 450 wa Jiji la Jiji la Tanga.

Akizungumza leo jijini Tanga wakati akikabidhi mitungi hiyo iliyotolewa na Kampuni ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Cocacola Waziri Ummy amewapongeza wadau hao kwa kutoa vifaa hivyo kwa wajasiriamali wanawake wa jiji hilo.

Ametumia nafasi hiyo kueleza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuthamini na kutambua mchango wa wanawake pamoja na kuwashirikisha katika ngazi za maamuzi.

“Tunawashuku wadau wote kwa kutuunga mkono kwa kutupatia bure mitungi ya gesi Oryx na majiko yake,meza pamoja na kreti 150 za Cocacola kwa ajili ya wanawake wajasiriamali wa Tanga.

“Tunaamini matumizi ya nishati ya gesi yatakwenda kumaliza matumizi ya kuni na mkaa katika kupikia.Nitoe rai kwa wanawake hiki ambacho tumekipata leo iwe ni chachu ya kuboresha biashara zetu,”amesema .

Aidha amewataka wajasiriamali hao wasijione wanyonge kwani wanaweza kufanya vizuri zaidi ya wanavyofanya sasa huku akifafanua kwa sasaa kuna watoto wengi wanamaliza vyuo na vyuo vikuu nafasi ya kuajiriwa ni chache.

“Kwa hiyo lazima tujiajiri na tuchukulie ujasiriamali kama ofisi rasmi, hivyo niendelee kuwaomba wanawake wajiamini na wajithamini katika kuimarisha biashara zenu.

“Serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan itaendelea kutambua na kuthamini mchango wa wanawake pamoja na kuwashirikisha wanawake katika nafasi za maamuzi.”

Awali akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Benoit Araman , Meneja Masoko wa kampuni hiyo Kanda ya Mashariki Shaban Fundi amesema lengo la kutoa mitungi ya gesi ni kuendeleza kampeni yake ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia huku ikisisitiza pia Oryx gas imekua ikiyaishi maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kwamba ifikapo 2032 asilimia ya 80 ya watanzania watumie nishati safi ya kupikia.

Shaban amesema matumizi ya gas yamekua yakiongezeka kwa kasi nchini kutokana na juhudi kubwa ya kuhamasisha inayofanywa na Oryx Gas kwa kushirikiana na wadau ikiwemo Serikali inayoongozwa na Rais Samia.

"Kwa ushirikiano mkubwa uliopo kati ya OryxGas na Cocacola, tumeendelea kuwezesha makundi mbalimbali ya wajasiriamali hususani wanawake maeneo mbalimbali nchini katika kuhamasisha watanzania wengi watumie nishati safi ya kupikia, " amesema.

Amefafanua kupika kwa Gas ya Oryx kunaimarisha afya kwa kuepuka kuvuta moshi mbaya wa kuni na mkaa,kupika kwa umaridadi na kwa wakati, hivyo kuongeza mapato mengi huku akikisitiza kwa ujumla ni pamoja na kulinda mazingira kwa kuzuia kukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Ameongeza hivyo Oryx imeendelea kuwekeza kuhakikisha nishati hiyo inapatikana nchini kote lakini zaidi wanawekeza katika kutoa elimu kupitia makundi mbalimbali kuhusu matumizi sahihi ya Gas

Pamoja na hayo amesema kwa ushirikiano na Cocacola hadi sasa wamefanikiwa kutoa mitungi ya gesi ya Oryx zaidi ya 2000 na kuwafikia wajasiriamali 5000 na wataendelea na ushirikiano kwa ajili ya kuyafikia makundi mengi zaidi ili kutimiza ndoto ya Rais Samia.

TPA YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA MILIONI 10 KOROGWE

September 09, 2023

MKUU wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo kushoto akipokea msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha kwa ajili ya Hospitali ya wilaya ya Korogwe ikiwa leo ni siku yao ya kusheherekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bandari nchini.
MKUU wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo kushoto akipokea msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha kwa ajili ya Hospitali ya wilaya ya Korogwe ikiwa leo ni siku yao ya kusheherekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bandari nchini.
MKUU wa wilaya ya Korogwe  Jokate Mwegelo  kushoto akipokea msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha kwa ajili ya Hospitali ya wilaya ya Korogwe ikiwa leo ni siku yao ya kusheherekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bandari nchini.
MKUU wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo kushoto akipokea msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha kwa ajili ya Hospitali ya wilaya ya Korogwe ikiwa leo ni siku yao ya kusheherekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bandari nchini.
MKUU wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo  kushoto katikati akimkabidhi  msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya Milioni 10 Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Korogwe Miriam Cheche mara baada ya kuvipokea kutoka kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha kulia  kwa ajili ya Hospitali ya wilaya ya Korogwe ikiwa leo ni siku yao ya kusheherekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bandari nchini.
MKUU wa wilaya ya Korogwe     Jokate Mwegelo  kushoto akiwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Mrisha Masoud wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo
MKUU wa wilaya ya Korogwe   Jokate Mwegelo    kushoto akiwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Mrisha Masoud wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo



Sehemu ya vifaa hivyo





Na Oscar Assenga,KOROGWE

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wamekabidhi msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Milioni 10 katika Hospitali ya wilaya ya Korogwe  ikiwa kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu za kuondoa changamoto kwenye sekta ya afya, elimu na mambo mengine kwenye jamii.


Vifaa vilivyotolewa ni viti mwendo 10 vyenye thamani ya milioni 4 na ya mashine ya ECG kwa ajili ya matibabu ya moyo ambavyo vitakwenda kuwasaidia wananchi wanapata huduma kwenye Hospitali hiyo kutoka maeneo vijiji mbalimbali wilayani humo ikiwa  ni kurudisha kwa jamii

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa wilaya ya Korogwe  Jokate Mwegelo , Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha alisema kwamba wameamua kutoa msaada huo ikiwa leo ni siku yao ya kusheherekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bandari nchini.

Alisema wao wametoa kwa jamii walichokipata mwaka huu na wameamua kupeleka msaada huo kwenye Hospitali hiyo ili kuweza kuwasaidia kuwapunguzia baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili kwenye Hospitali ya Korogwe.

“Licha ya kutoa msaada huu hapa lakini tutaendelea kusaidia kitakachpatikana ili kuweza kutatua changamoto kwenye hospitali ili kuhakikisha wananchi wanaondokana na vikwazo mbalimbali katika kupata huduma za matibabu”Alisema

Awali akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa wilaya ya Korogwe  Jokate Mwegelo   aliishukuru Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa msaada huo mkubwa ambao wamewapatia kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Korogwe ambao ni vitindi mwendo ambavyo uhitaji wake ulikuwepo.

Alisema pia msaada huo mashine ya  ECG   kwa ajili ya matibabu ya moyo utawasaidia wananchi katika wilaya hiyo kutokana na idadi ya watu wenye matatizo ya moyo inaongezeka vijijini kutokana na matumizi ya chumvi kuongezeka.

Alisema pia matumizi ya mafuta vinachangia pia na mtindo ya maisha huku akieleza kifaa hicho kitakwenda kuwatibu wananchi na hivyo kuwasaidia kuwa na afya bora kutokana na kwamba Taifa lenye nguvu lazima wananchi wake wawe na afya bila afya hawaweze kufanya kazi na kuweza kushiriki shughuli za kijamii ili kuweza kukuza uchumi.

Naye kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Korogwe Miriam Cheche aliishukuru TPA kwa kugawawia msaada wa vifaa hivyo ikiwemo kifaa cha kisasa ambacho kinagundua matatizo ya moyo kwa mtu anayeugua kabla ya kupelekwa kwenye Hospitali za Rufaa.

“Kwa kweli tunawashukuru sana TPA kwa msaada huu kwa sababu wananchi watafaidika na mashine hii lakini tunamshukuru DC kwa hamasa zake na hivyo kupelekea wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia pia Rais Dkt Samia Suluhu kuendelea kutupatia fedha kuendeleza hospitali yetu ya Makuyuni”Alisema