JACQUELINE MENGI AFANYA UZINDUZI WA DUKA LA SAMANI “AMORETTE”

JACQUELINE MENGI AFANYA UZINDUZI WA DUKA LA SAMANI “AMORETTE”

September 15, 2016

Alhamisi ya Septemba, 15 inaingia katika historia ya mjasiriamali, Jacqueline Mengi kwa kufanya uzinduzi wa duka la samani za ndani la Molocaho Amorette likiwa na vitu ambavyo ni vya pekee kutokana na aina ya malighafi ambayo wametumia kutengeneza.

Akizungumzia duka hilo, Bi.Mengi alisema kuwa ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu ya kutaka siku moja kuwa na duka kama hilo ambalo litakuwa na samani ambazo ni ngumu kuzipata sehemu nyingine kutokana na kutengenezwa tofauti na samani nyingi ambazo zinapatikana madukani.

"Siamini kama ndoto yangu imetia, kwa kipindi cha miaka iliyopita kuna vitu nilikuwa nikitamani kuwa navyo nyumbani lakini sikuweza kuvipata nilipokuwa nikitafuta na hapo ndipo ndoto za kuwa na duka zilipoanzia,

"Nilikuwa nataka kitu cha tofauti ambacho ni ngumu kukikuta sehemu nyingine kutokana na kuwa na ubunifu wa kipekee ambao utawavutia wateja wa ndani ya nchi na nje ya nchi na ninaamini watafurahia," alisema Bi. Mengi.

Aidha Bi. Mengi alisema kuwa bidhaa ambazo zitakuwa zikipatikana katika duka la Molocaho - Amorette zimetengenezwa na malighafi kutoka Tanzania kama mbao za Mninga na hivyo kuwataka Watanzania kuwa wazalendo kwa kutumia bidaa ambayo imetengenezwa na malighafi za Tanzania.

Mmoja wa wageni waliohudhuria halfa ya uzinduzi, Faraja Nyalandu alisema kuwa kwa kijana kama Jacqueline Mengi kuwa na duka kama hilo ni hatua kubwa ambayo vijana wengi wanatamani kuifikia, kumpongeza kwa juhudi alizozifanya lakini pia kutoa ushauri kwa wengine ambao wanataka kufanikiwa.

"Kwanza nimpongeze Jacqueline amefanya uthubutu na amefanikiwa kuwa na kitu kama hiki, juhudi yake inaonyesha kuwa kila mtu tu anaweza kufanikiwa kama akiongeza juhudi katika jambo analotaka kulifanya," alisema Bi. Nyalandu.

Duka hilo la kisasa na la aina yake linapatikana Masaki karibu na hoteli ya Sea Cliff kwenye jengo la "Village Walk" gorofa ya kwanza.

Mrembo wa taji la Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na wageni walikwa pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa duka lake la samani za ndani "Amorette" lililopo katika jengo la Village Walk gorofa ya kwanza karibu na Sea Cliff Hotel, Masaki jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa nje utaokutambulisha hili ndio duka la "Amorette"
Bi. Jacqueline Mengi akikata utepe kuzindua duka lake hilo.
Ha ha ha ha, sasa mko huru kuingia wageni waalikwa kujionea yaliyomo,.....Bi. Jacqueline Mengi akifurahi jambo mara baada ya kukata utepe.
Bi. Jacqueline Mengi akiongozana na baadhi ya wageni waalikwa kuingia ndani ya duka la "Amorette"
Balozi Juma Mwapachu na baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia moja ya meza ya chakula (dining table) iliyotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga baada ya kuzinduliwa duka hilo lililopo katika jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar.
Wageni waalikwa wakiendelea kukagua samani mbalimbali katika duka hilo.
Bi. Jacqueline Mengi akiwaonyesha mambo mazuri yaliyomo katika duka la Amorette baadhi marafiki waliohudhuria uzinduzi huo.
Bi. Jacqueline Mengi akizungumza jambo na Balozi Juma Mwapachu wakati akiwatembeza wageni waalikwa katika maeneo mbalimbali ndani ya duka lake la Amorette.
Wageni waalika wakiangalia moja ya kitanda cha aina yake kinachouzwa katika duka la Amorette lililopo katika jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar es Salaam.
Sehemu maalum ya kitanda hicho ya kuhifadhia mashuka, Blanket pamoja na mito.
Bi. Jacqueline Mengi akipozi katika moja ya samani ndani ya duka lake la Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi katika pozi matata ndani ya duka lake la Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua duka lake la samani za ndani la Amorette.
Wanahabari na wageni waalikwa wakiwa ndani ya duka la Amorette kujionea bidhaa mbalimbali.
Wageni waalikwa wakiendelea kutazama kitanda hicho cha aina yake.
Sophia Byanaku akijinafasi katika moja ya samani zilizomo kwenye duka la Amorette.
Mmoja wa wageni waalikwa akitazama bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga ndani ya duka la Amorette.
Baadhi ya samani zilizomo ndani ya duka la Amorette.
Balozi Juma Mwapachu (kushoto) akibadilishana mawazo na mwalikwa mwenzake kwenye uzinduzi wa duka la Amorette.
Mwanadada Monica Joseph akipozi kwenye moja ya bidhaa zilizopo ndani ya duka la Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akipozi kwenye samani moja wapo inayopatikana katika duka lake la Amorette.
Warembo wakiwa wamepozi kwenye samani zinazopatikana katika duka la Amorette lililopo ndani ya jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo ndani ya duka la Molocaho-Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akiwa kwenye picha ya pamoja na rafiki zake.
Bi. Jacqueline Mengi akibadilishana mawazo na baadhi ya marafiki zake.
Mkurugenzi wa Dorice Mollel Foundation, Dorice Mollel (kulia) katika picha ya pamoja na Mdau Monica Joseph.
Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na Dorice Mollel.

Vijana nchini wahimizwa kuunga mkono kampeni ya Uchumi wa Kijani.

September 15, 2016
Mkutano Vijana na Uchumi wa Kijani






Baadhi ya picha kutoka katika mkutano huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Raleigh Tanzania, Bw Alistar Mackay akizungumza na washiriki wa mkutano


Washiriki wa mkutano huo
Wawakilishi wa taasisi na ofisi za serikali

Mgeni Rasmi akizungumza na waandishi wa habari
Ms Clara Makenya kutoka United Nations Environment Programme akizungumzia uchumi wa kijani katika mkutano huo.




Vijana nchini Tanzania wahimizwa kujiunga na kampeni ya Vijana kwa Maendeleo ya Kijani ili kulinda mazingira kwa kuyafanya endelevu sambamba na kujiiinua kiuchumi.

Hayo yalibainishwa na Afisa Mawasiliano wa shirika la kimataifa la Raleigh Tanzania Bw. Kennedy Mmari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Uchumi wa Kijani kwa Vijana iliyofanyika kwatika ukumbi wa British Council.

Bwana Mmari alisema kuwa wao kama shirika linalojihusisha na vijana wamekuja na kampeni hii ya kitaifa kwakua wanaamini uwezo walionao vijana katika kuleta mabadiliko endapo watapewa nafasi.

 “Sisi kama vijana tunahitaji sana maendeleo ya kiuchumi ila lazima maendeleo hayo yalinde mazingira yetu hivyo basi tunahitaji uchumi wa kijani, uchumi ambao utazingatia vilivyo shughuli za kiuchumi kwaajili ya kupunguza umasikini lakini ukijikita pia katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo na mazingira endelevu” alielezea Bw. Mmari.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Raisi  Muungano na Mazingira Injinia Ngosi Mwihava alisema wao kama Serikali wametoa Baraka zote kwa kampeni hiyo kwani athari za mabadiliko ya tabia nchi zimedi kuongezeka siku hadi siku.


“Sisi kama serikali ni jukumu letu kuhakikisha wananchi wanayatunza mazingira na kuyafanya yawe endelevu, na ndio maana leo tupo hapa na vijana ili kuhakikisha elimu ya mazingira endelevu inawafikia na wao wanaisambaza” alisema Injinia Mwihava.

Aidha Injinia Mwihava alisema kuwa serikali itahakikisha mazingira yanalindwa na kuwa endelevu hivyo wataanza na kupiga marufku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Januari mwakani kama njia mojawapo wa kuzuia uchafuzi wa mazingira.

“Serikali sasa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tunaandaa kanuni  za kudhibiti mifuko ya plastiki nchini na hata kama mgeni akija nayo toka nje akifika mpakani lazima aambiwe kuwa hatutumii tena mifuko ya plastiki” alisisitiza Injinia Mwihava.

Naye mmoja wa vijana waliohudhuria hafla hiyo Pius Matunge  alisema ni wakati sasa kwa vijana kushika hatamu kwenye kulinda mazingira.
"Kila kijana lazima ajione yuko mbele kwenye kulinda na kuyatetea mazingira ili yaweze kutumika kwenye kuinua uchumi wa nchi yetu" alihitimisha Bw. Pius.


Hafla hiyo iliyoandaliwa na shirika Raleigh Tanzania ilikutanisha pamoja vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini na mashirika mbalimbali na wadau wa mazingira kujadili jinsi gani vijana wanaweza kuwa mawakala wa maendele ya Uchumi wa Kijani.

Kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo yatoa madawati 235 mkoani Dodoma

September 15, 2016


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma, Japhar Mwanyemba akipokea moja kati ya madawati 235 yenye thamani ya milioni 39 toka kwa Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, George Lugata. Katikati ni Diwani  Kikuyu kaskazini, Israel Mwansasu


Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kushoto) Diwani wa Kikuyu kaskazini, Israel Mwansasu na Meya wa Dodoma Mstahiki Japhar Mwanyemba wakiwa wameketi mara baada ya makabidhiano.



Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Patrick Moshi akiongea na  walimu,wanafunzi na wanahabari kwenye hafla ya kukabidhi madawati toka kampuni ya Tigo, wengine pichani Meya Japhar Mwanyemba, George Lugata, Aidan Komba



Meneja wa Tigo kanda ya kaskazini, Aidan Komba akiongea na walimu, wanafunzi na wanahabari wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati viwanja vya shule ya msingi Kikuyu A mkoani Dodoma


Walimu na Wanafunzi wakisheherekea


Mwanafunzi Josephine Mahundi akitoa shukurani




MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI ARUSHA KUSHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA SARPCCO EXTRA ORDINARY MEETING KESHO

September 15, 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  akisalimiana akisalimiana na mmoja wa viongozi wa dini mara baada ya kuwasili jijini Arusha mapema leo,
tayari kwa ufunguzi wa mkutano wa SARPCCO EXTRA ORDINARY MEETING kesho tarehe 16 Septemba 2016 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC.Pichani kulia ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  akilakiwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh.Mrisho Gambo mapema leo mara baada ya kuwasili jijini humo tayari kwa ufunguzi wa mkutano wa SARPCCO EXTRA ORDINARY MEETING kesho tarehe 16 Septemba 2016 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC.

SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA (ATCL) LAPATA MWENYEKITI MPYA WA BODI NA MKURUGENZI MKUU

September 15, 2016

BANK OF AFRICA (BOA) YAZIDUA KADI MBILI AMBAZO NI TOUCAN VISA NA PROXMA VISA JIJINI DAR.

September 15, 2016


Meneja Masoko, Utafiti na Maendeleo wa Bank of Africa (BOA), Bw. Muganyizi Bisheko akionesha card aina ya PROXIMA iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Benki ya Afrika (BOA) imezindua kadi mbili TOUCAN VISA CARD na PROXMA VISA CARD ambazo zinasaidia kulinda usalama wa mteja tofauti na zilizokuwa zimetolewa mwanzo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala za Huduma za Kibenki Kidigital wa Bank of Africa (BOA), Bw. Emmanuel Mshindo. Picha na Emmanuel Massaka wa Blogu ya Jamii.
Mkuu wa Kitengo cha Njia Mbadala za Huduma za Kibenk Kidigital wa Bank of Africa (BOA), Bw. Emmanuel Mshindo akionyesha kadi aina ya TOUCAN iliyotolewa na benki ya Afrika (BOA). Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo, Bw. Kaisha Boge.  Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo, Bw. Kaisha Boge (katikati) akizielezea kadi hizo zilizotolewa nabenki ya Afrika (BOA) mapema leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

UVCCM YATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU VURUGU ZA JIJINI ARUSHA,YAMSIMAMISHA KAZI KATIBU WA UVCCM ARUSHA

September 15, 2016



Jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM imemsimamisha kazi aliyekuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ezekiel Mollel kwa kutotiii agizo la Makao Makuu linalomtaka kuhama na kusibabisha mvutamo na malumbano yasio na tija kwa chama cha Mapinduzi mkoani Arusha.

Pia Jumuiya imewataka vijana wa uvccm kutambua kuwa shughuli za uendeshaji wa umoja huo zinafanyika kwa kufuata taratibu za kikanuni chini ya misingi ya nidhamu na utii.

Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka Hamdu Shaka amewaeleza wandishi wa habari katika ofisi za UVCCM mkoa wa Arusha mara baada ya kumaliza mzozo ulioibuka na kusababisha baadhi ya vijana kufunga ofisi wakimkataa Ezekiel asiendelee kubakia mkoani hapo.

Shaka alisema tokea tarehe 25 August makao makuu ilimuandikia barua Mollel kumuhamishia Makao Makuu Dar Es Salam lakini cha ajabu kwa muda wote amekuwa akikaidi kuhama kwa sababu zake binafsi.

Alisema kikao cha sekreterieti ya Taifa kilichoketi jijijini Dar es salaam 14 September kimeamua kumsimamisha kazi katibu huyo na kumtaka ampishe katibu wa mkoa mpya Said Goha aliyehamia Arusha akitokea lindi

"Mollel amekuwa akidai kuwa Arusha kuna harufu ya ubadhirifu wa mali na miradi ya Jumuiya, Makao makuu haijapinga dai hilo , kuhama kwake si kikwazo cha kuzuia kubaini nani amehusika na tuhuma hizo, amehamishwa kwa sababu za kawaida pia kutokana na sintofahamu iliopo "alisema shaka.

Alipoulizwa iwapo ni mpango wa kukuondoa ili kuficha ukweli wa ufujaji wa miradi alisema kuhama kwake hakuwezi kuzuia ukweli usijukikane, kwani Jumuiya inafanya uchunguzi wa miradi na rasilimali zake pia vyombo vya serikali vimeombwa viingiliie sakata hilo ili kupata ukweli wa mambo.

"Mtumishi unapohamishwa toka kituo kimoja kwenda kingine na kukataa huo ni uvunjaji wa taratibu, ukiukaji wa kanuni na kutoonyesha nidhamu ya kazi, amesimamishwa kazi hadi jambo lake litakapifikishwa katika vikao vya kitaifa vyenye mamlaka ya uteuzi wake wa mwisho kwa mujibu wa kanuni ya UVCCM"alieleza shaka

Akijibu swali la mwandishi kwamba katibu huyo amekuwa akikaidi kuondoka kwa sababu analindwa na baadhi ya wakubwa wa makao Makuu pia makao makuu ikitaka kumlinda kiongozi mmoja wa juu asihusishwe na ubadhirifu huo, shaka alikana na kusema wanaoeneza maneno hayo ni mashabiki wa kisiasa..

"Nasema vijana wenzetu wa Arusha wafahamu uendeshaji wa kazi zetu ni uzingatiaji wa taratibu na kikaanuni, makao makuu haiwezi kumkingia kifua mwizi na kumtetea , kumlinda na kumtetea mvunja taratibu husika "alisema.

Aidha Kaimu huyo Katibu mkuu alisema kazi ya ufuatiliaji miradi, mikataba , mapato na matumizi yake yatafuatiliwa hatua kwa hatua na ukweli wa jambo hilo utaanikwaa bila mtu kulindwa na kuogopwa.

Hata hivyo shaka alipoulizwa kwamba makao makuu imeshindwa kumchukulia hatua za kinidhamu mwenyeikiti wa mkoa huo Lengi Sabaya anayedaiwa kufanya hadaa na kukutwa na vitambulisho feki , alijibu kuwa madai hayo ni binafsi yenye mwekeleo wa jinai na iwapo kweli anakabiliwa na tuhuma hizo vyombo vya dola vipo na vinapaswa kuchukua hatua haraka UVCCM haitamlinda mtu katika jambo lolote lililo kinyume na maadili ya Chama.

Pia akiwataka wana Jumuiya kuacha tabia ya kubuni au kubashiri mambo ambayo mtu hana ushahidi nayo akidai kwamba kiongozi fulani anamlinda mtu fulani wakati hakuna kiongozi makini anayeweza kumlinda mtu anayekiuka kanuni na kuvunja taratibu halali

"chama chetu kina Katiba jumuiya yetu ina kanuni toleo la 2012 tuna kanuni ya utumishi kanuni ya fedha na maadili iyo ndio miongozo yetu katika kutekeleza majukumu ya kila siku hatutafumbia macho mtu yoyote atakaepindisha mstari mmoja wa kanuni au taratibu kwa vile hakuna aliye juu ya miongozo hiyo" alisema shaka

Amewataka vijana wa Arusha kuwa watulivu kwani viongozi wote wako makini katika kila jambo na jumuiya Arusha itaendelea kubaki salama.

Shaka amewasili mkoani arusha jana kufuatia kuibuka kwa mzozo uliosabanisha baadhi ya vijana kumfungia ofisi katibu aliyehamishwa Ezekiel molel ambae anaungwa mkono na Mwenyekiti wa UVCCM wa mkoa huo kwa madai amempa kazi afanye na hajakamilisha.