Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf)
akishirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Msongela Palela na Katibu
Tawala wa wilaya hiyo,Edward Mpogolo (kulia) wakifanya usafi katika maeneo ya
buguruni kwa malapa kutimiza kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi
kila mwisho wa wiki ya mwezi jijini Dar es Salaam juzi. (PICHA NA ELISA SHUNDA)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Msongela Palela akizungumza na wananchi wa eneo la Buguruni kwa Malapa na Darajani kuhusu kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka ili kujikinga na kujiepusha na magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu baada ya kufanya usafi kutekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila mwisho wa wiki ya mwezi jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) na Katibu tawala wa wilaya hiyo,Edward Mpogolo.
NA EMERISIANA ATHANAS
DIWANI wa Kata ya
Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Adam Fugame ameagiza
viongozi wa kata akiwemo Ofisa Afya, kuwakamata na kuwachukulia hatua
watu wasiofanya usafi au kuchangia kwaajili yakuzolewa uchafu.
Akizungumza
jijini hapa jana, wakati wa zoezi la ufanyaji usafi ulioshirikisha
viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Ilala akiwemo Mkurugenzi Msongela
Palela, alisema ni vema viongozi wakafanya kazi kwa mujibu wa sheria ili
kuwashughulikia watu hao.
"Suala hili sio rai
bali tufanye kama sheria ili kufanikisha zoezi la kuimarisha usafi
katika maeneo yetu, kwani tusipofanya hivi hakuna litakalotekelezwa,
watu hawafanyi usafi," alisema.
Kutokana na
umuhimu wa kufanya usafi alisema ni vema watakaokutwa hawachangii wala
kujishughulisha na kufanya usafi wakachukuliwa hatua na kutozwa fedha.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Palale alisema kuwa katika
kata tisa zilizoko katika manispaa hiyo kata ya Buguruni ndiyo imekuwa
na ugonjwa wa kipindu pindu ambacho husababishwa na hali ya uchafu.
Alitumia
nafasi hiyo kuwataka wakazi wa kata ya Buguruni kuhakikisha wanafanya
usafi na kuwa walinzi katika kuhakikisha wanalinda mazingira na
kuimarisha usafi kwenye maeneo yao.
Imeandaliwa na Mtandao wa WWW.ELISASHUNDA.BLOGSPOT.COM/0 719976633
Elisa Shunda
Photographer-Raia Tanzania Newspaper