Tigo yafungua duka kubwa, la kisasa Dodoma

August 01, 2017
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akikata utepe kuzindua duka jipya la kisasa lililofunguliwa leo mkoani Dodoma, Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa usimamizi na masuala ya kiserikali wa Tigo,Sylvia Balwire, Meneja usimamizi wa wateja wa Tigo kanda kaskazini, Vitalis Stephen na kushoto ni George Lugata mkurugenzi wa Tigo kanda kaskazini.

Meneja  usimamizi wa wateja wa Tigo kanda kaskazini, Vitalis Stephen akimuonesha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari baadhi ya simu zinazouzwa kwenye duka jipya la kisasa lililozinduliwa leo mkoani Dodoma . Pembeni ni mkuu wa huduma kwa wateja wa Tigo Dodoma,Scolastica Kisori.

VIKOSI VYA MAJESHI YA SADC KUFANYA ZOEZI LA PAMOJA MKOANI TANGA

August 01, 2017
Msimamizi wa Zoezi la pamoja kwa vikosi maalumu vya Majeshi
ya SADC ambalo limepewa jina la  Matumbawe,Meja Generali Harison Msebu katika kupambana na matishio mbalimbali ya usalama kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuanza zoezi hilo ambalo litaanza Agosti 2 hadi Septemba 1 Jijini Tanga,kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
VIKOSI vya Majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwaafrika (SADC SPECIAL FORECES) vimeamua kupambana na ugaidi,Uharamia kwa kushirikiana kufanya zoezi la pamoja lililopewa jina la “EX MATUMBAWE” ikiwa ni mkakati wa kutokomeza vitendo hivyo.
Zoezi hilo litakaloshirikisha vikosi vya Makomandoo, Ndege za
kivita,meli za kivita na makomandoo watakao ruka na miavuli huku wote kwa pamoja kutoka nchi zote shiriki watafanya mazoezi hayo kubadilishana uzoefu litafanyika kuanzia Agosti 2 mpaka Septemba 1 mwaka huu katika maeneo ya Mapango ya Mleni.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga,Msimamizi wa Mazoezi hayo,Meja Generali Harison Msebu alisema kuwa lengo la zoezi hilo ni kufanya mazoezi ya pamoja kwa vikosi maalumu vya Majeshi ya SADC,ili kuviwezesha kuwa na utayari na harakati katika kupambana na matishio mbalimbali ya usalama.

Aidha alisema kuwa kutasaidia kuviwezesha vikosi hivyo kukabiliana na masuala ya Ugaidi,Uharamia na maafa yatokanayo na  mabadiliko ya hali ya hewa na kusaidia vikundi vya kulinda amani kama ilivyoelekezwa na Jumuiya ya SADC pamoja na umoja wa Afrika (AU).

Alisema Nchi za Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Mwaafrika zimejiwekea mikakati ya kuondoa uhasama wao na zaidi kuunganisha mahusiano ikiwa na lengo la kupambana mambo ambayo yanaweza kuleta madhara katika nchi zote za Jumuiya hiyo na Afrika kwa ujumla.

Alisema yapo madhumuni ya kimkakati,utendaji kivita na kimbinu haya yote yakitekelezwa kwa ufanisi zaidi kwa nchi zote upo uwezekano wa hali ya juu katika mafanikio ya mapambano ya kigaidi na kiharamia.
“Tunajenga misingi mizuri kwa majeshi yetu na kuondoa dhana ya kupambana wenyewe kwa wenyewe sasa tunaelekeza nguvu zetu katika mapamabano ya kigaidi na kiharamia zaidi jambo ambalo litasumbu katika nchi hizi za Afrika”Alisema Meja Jenerali Masebu.

Alisema zoezi hilo litashirikisha Nchi saba za Jumuiya hiyo zikiwa Botswana,Lesotho,Malawi,
Jumuiya ya Afrika ya kusini,Zambia, Zimbabwe na Tanzania ambao ndio watakauwa wenyeji katika zoezi hilo ambalo linafanyika hapa kwa mara ya kwanza.

Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigela aliwaomba wananchi wasiwe na wasiwasi pindi watakapokutana na vikosi hivyo vikiwa vinaendelea na majukumu yao huku akiwataka kutoa ushirikiano pindi watakapo hitajika.

Alisema wananchi wasiokote vitu vyovyote wasivyovielewa na watoe taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama kwa kitu ambacho watakiona kinawapa mashaka.

EU injects TZS. 1.4 billion to counter child marriage and FGM

August 01, 2017
The European Union Delegation in Tanzania has funded and launched today a TZS. 1,400,000,000, equivalent to EUR 600,000, three- year project (2017 – 2020) to counter child marriage and female genital mutilation (FGM) that will be implemented by Plan International Tanzania in partnership with Children’s Dignity Forum (CDF) and New Light For Children Organisation (NELICO), Tackle Africa and Tanzania Football Federation (TFF) in Geita and Tarime Districts.

The Head of Delegation of the European Union to Tanzania Ambassador Roeland van de Geer underlined the EU's commitment to acting in genuine partnership with Tanzania, international and regional organizations, and civil society to combat violence and harmful practices against women and girls. "Child marriage and FGM are a violation of girls’ human rights. These harmful practices have a devastating impact on a girl's health, her well-being and personal development but they also have a detrimental ripple effect on the society as a whole. Ending child marriage means a positive effect on the health and education of girls and their children, it contributes to a lower fertility rate and increases women’s expected earnings and household welfare."

Plan International Tanzania Deputy Country Director, Ms. Gwynneth Wong, said that Child Marriage in Tanzania prevails at the rate of 37%, where three out of ten girls enter into marriage before the age of 18 with Mara having the highest rate of 55% and Geita 37%. The Deputy Country Director also revealed that while the national prevalence rate of Female Genital Mutilation is at 10%, Mara is at the rate of 32%, three times the national rate. All these practices deprive the girl child of their potential to contribute to both national and personal developments.

“The girls are deprived of their right to enjoy their childhood and reaching their goals. Subjecting them to early marriages and mutilating their genitals puts them at risk of maternal health complications and even deaths. This fuels the poverty cycle and is against the UN Sustainable Development Goals”, said Gwynneth Wong.

The project targets over 1,500 in-school and out-of-school girls aged between the age of 10 – 24, and aims to prevent the incidences of harmful traditional practices of Child Marriage and FGM through empowering girls and strengthening of community, civil society and government support systems to respond to girls’ rights violation and challenges.

SIMBACHAWENE: SEKTA YA KILIMO BADO NI MUHIMILI WA UCHUMI TANZANIA

August 01, 2017
Na Mathias Canal, Lindi

Sekta ya Kilimo imetajwa kuwa bado ni muhimili wa uchumi wa Tanzania kwa kuwa inatoa ajira kwa asilimia  65.5  ya Watanzania na kuchangia zaidi ya asilimia 100 ya chakula hapa nchi katika miaka yenye mvua ya kutosha. 

Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais,tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, kwa mwaka huu wa 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, tarehe 1/8/2017.

Alisema Kaulimbiu ya Nane Nane mwaka huu inasema “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati”. Kaulimbiu hii inahamasisha Wakulima, Wafugaji na Wafugaji kuongeza uzalishaji na tija katika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Mhe Simbachawene alisema kuwa mwaka 2015, Sekta ya Kilimo ilichangia asilimia 29 ya pato la Taifa, na mwaka 2016 ilichangia asilimia 29.1. Hivyo, ni dhahiri kuwa mchango mkubwa katika pato la Taifa ulitokana na Sekta ya Kilimo ukifuatiwa na Sekta nyingine za kiuchumi. 

Alisema Kutokana na umuhimu huo, Serikali inaeendelea kutekeleza mikakati ya kuongeza kasi ya kukuza kilimo, mifugo na uvuvi ili kuchochea na kufikia uchumi wa viwanda sawasawa na Azma ya Serikali ya Awamu ya Tano. 

Alisema kuwa Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2016 uliongezeka kufikia kiwango cha utoshelevu wa asilimia 123 ikiwa ni zaidi ya kiwango cha asilimia 120 cha mwaka 2015.  

Hali hiyo, imechangiwa na ongezeko la asilimia 6.7 la uzalishaji wa mazao ya nafaka yakiwemo mahindi na mchele. Usalama wa chakula pia unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mazao yasiyo nafaka kama vile mihogo, viazi, ndizi na mazao ya jamii ya mikunde ambayo kwa ujumla kulikuwa na ongezeko la uzalishaji wa asilimia 1.5

Pamoja na kiwango cha kuridhisha cha uzalishaji wa mazao ya chakula, Mhe Simbachawene alisema kuwa hali mbaya ya hewa iliyojitokeza mwisho wa mwaka 2016 na mwanzoni mwa mwaka 2017 ilisababisha kupanda kwa bei za chakula katika maeneo mbalimbali ya nchi. 

Hata hivyo Katika kukabiliana na hali ya ukame uliotokana na uhaba wa mvua za vuli na kuchelewa kuanza kwa mvua za masika katika baadhi ya maeneo, hatua sitahiki zilichukuliwa. 

Amezitaja Baadhi ya hatua hizo kuwa  ni pamoja na kusambaza mbegu bora zinazokomaa kwa muda mfupi, zikiwemo mahindi, mtama na mpunga huku vipando vikiwemo pingili za mihogo na viazi vitamu vilisambazwa.

"Nchi yetu imebahatika kuwa na idadi kubwa ya mifugo ikiwemo ngómbe, kondoo, mbuzi, kuku wa asili na kuku wa kisasa. Pamoja na kuwa na idadi kubwa ya mifugo, viwango vya ulaji wa mazao ya mifugo hususani nyama, maziwa na mayai bado viko chini. Katika mwaka 2016, mifugo inayouzwa katika minada iliongezeka ukilinganisha na mwaka 2015 na hivyo kupata mapato yanayotokana na ng’ombe shilingi trilioni 1.34, mbuzi na kondoo shilingi trilioni 1.02" Alisema Mhe Simbachawene

Aliongeza kuwa Mapato yanayotokana na mauzo ya ngozi yalifikia shilingi bilioni 34.7 kwa ngozi ya ngómbe, shilingi bilioni 6.2 kwa ngozi ya mbuzi na kondoo. Mapato yanayotokana na uzalishaji wa malisho katika mashamba ya Serikali yalifikia shilingi bilioni 1.14. Aidha, mapato yanayotokana na uzalishaji wa mbegu za malisho bora ya nyasi  yalifikia shilingi milioni 55.8 na jamii ya mikunde shilini milioni 11.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) akizungumza na Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.(Picha Zote na Mathias Canal) 
Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB), Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb), na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Halima Dendego wakitazama namna ya uzalishaji samaki katika banda la JKT wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI PIA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO WA MABALOZI WATANO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI PIA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO WA MABALOZI WATANO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

August 01, 2017
1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Benedict Mashiba kuwa Balozi  wa Tanzania nchini Malawi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
3
Balozi wa Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba akila kiapo cha uadilifu kwa Viongozi mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Benedict Mashiba mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
5.v
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn, Ikulu jijini Dar es Salaam.
6.v
Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
7.v
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn mara baada ya kumaliza mazungumzo pamoja na kupokea Hati za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
8.v
Balozi wa Vietnam hapa nchini Nguyeni Kim Doahn katikati akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
9.indo
Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof. Ratlan Pardede(katikati ) akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
10.ind..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof. Ratlan Pardede, Ikulu jijini Dar es Salaam
12-ind
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Indonesia hapa nchini Prof. Ratlan Pardede, Ikulu jijini Dar es Salaam
14
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Vatican hapa nchini Mwadhama Askofu Mkuu Marek Solcynski, Ikulu jijini Dar es Salaam.
15
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Vatican hapa nchini Mwadhama Askofu Mkuu Marek Solcynski mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini.
17.b
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef  Wachter akipigiwa wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kukabidhi Hati zake Utambulisho.
17
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef  Wachter akijitambulisha kabla ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
18
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati za utamblisho kutoka kwa Blozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Detlef  Wachter Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
20
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef  Wachter mara baada ya kupokea hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
21
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Richard Tumisiime Kabonero Ikulu jijini Dar es Salaam.
23
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma ya Brass Bendi ya Jeshi la Polisi ambayo ilifika Ikulu kwa ajili ya mapokezi ya Mabalozi mbalimbali kutoka nje ya nchi.
24
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Brass Bendi ya Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

JESHI LA ZIMAMOTO LAZINDUA KAMPENI YA NAMBA YA DHARURA 114 KUKABILIANA NA MAOKOZI YA MAISHA NA MALI

August 01, 2017
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Wengine ni Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuzuia Uhalifu, ajali (UAC), Elliot Andrew na Naibu Kamishna Rasilimali Watu wa Jeshi hilo, Billy Mwakatage (kulia). Uzinduzi huo umefanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye, akikabidhiwa kipeperushi na Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuzuia Uhalifu, ajali (UAC), Elliot Andrew(kushoto), wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Kulia ni Naibu Kamishna Rasilimali Watu wa Jeshi hilo, Billy Mwakatage. Uzinduzi huo umefanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye, akionyesha kipeperushi   wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Wengine ni Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na kuzuia Uhalifu, ajali S(UAC), Elliot Andrew na Naibu Kamishna Rasilimali Watu wa Jeshi  wa jeshi hilo, Billy Mwakatage(kulia).Uzinduzi huo umefanyika leo Makao Makuu ya Jeshi,jijini Dar es Salaam.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye, akionyesha mfano wa uwekaji stika yenye Namba ya Dharura 114, itakayobandikwa kwenye vyombo vya usafiri na maeneo mengine kwa ajili ya  kutumiwa  na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Uzinduzi huo umefanyika leo, Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
 Maafisa wa Jeshi waliohudhuria Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine, wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye (hayupo pichani) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Vyombo vya Habari. Uzinduzi huo umefanyika leo, Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uokoaji, Thobias Andengenye (watano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo, Viongozi na Wadau walioshirikiana na Jeshi hilo kuwezesha  Uzinduzi wa Kampeni ya Namba ya Dharura 114, itakayotumiwa na wananchi kutoa Taarifa za majanga ya moto, ajali, mafuriko, tetemeko la ardhi na majanga mengine. Uzinduzi huo umefanyika leo, Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, MAKAO MAKUU

SERIKALI YAONGEZA MUDA WA KUNYONYESHA KWA WATUMISHI WA UMMA NA MASHIRIKA NA SEKTA BINAFSI

August 01, 2017
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

SERIKALI imeongeza masaa ya unyonyeshaji kwa watoto kwa watumishi wa serikali, mashirika pamoja sekta binafsi ili kuwezesha watoto kuwa na afya bora inayotokana na maziwa ya mama.

Hayo ameyasema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akifungua Wiki ya Unyonyeshaji, amesema kuwa mama mzazi baada ya kumaliza miezi mitatu ataingia kazini 3:30 na kuondoka saa 7:30 katika kumuwezesha mama kunyonyesha mtoto bila kuingiliwa na majukumu ya kikazi.

Ummy amesema kuwa watendaji wa Umma na mashirika pamoja na taasisi lazima wafanye hivyo katika kutambua umuhimu wa mama mzazi kunyosha kwa muda uliowekwa kwa kipindi cha miezi sita.

Amesema kuwa ni gharama kubwa katika kuhudumia watoto walio na utapiamlo ambao unatokana moja ni kukosa maziwa ya mama kwa muda mrefu hivyo kuepuka ni nyia rahisi ikiwemo kutengwa kwa masaa hayo.

Waziri Ummy amesema kuwa suala la lishe lazima liangaliwe kwa ukaribu na wadau wote katika kuweza kuwaondoa watoto katika utapiamlo ambao unafanya kudumaa kwa akili.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Chakula na Lishe Nchini(TFNC), Joyceline Kaganda amesema jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika juu ya masuala ya lishe na wadau kwa mifumo mbalimbali.

Amesema kuwa wiki ya unyonyeshaji wa kina mama ni muhimu katika katika ukuaji wa mtoto wa kumjenga katika afya bora.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Lishe nchini (Panita), Tumaini Mkindo amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. Pombe Magufuli imwemeka kipaumbele katika ubaoreshaji wa lishe nchini.

Amesema kuwa sera zimeweza kuongezeka katika masuala ya lishe ikiwa eneo la kipaumbele katika mpango wa taifa wa miaka mitano pamoja mikoa na halmashauri kuwa na bajeti ya lishe.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipata maelezo juu masuala ya lishe kutoka kwa mtaalam wa lishe wa Taasisi ya Chakula lishe nchini (TFNC),Neema Joshua wakati maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya unyonyeshaji na uzinduzi usambazaji taarifa kwa njia ya simu leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chakula na Lishe Nchini(TFNC), Joyceline Kaganda akizungumza juu ya mikakati ya lishe na umuhimu wa unonyeshaji leo jijini Dar es Salaam.

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA TFF LEO AGOSTI 1

August 01, 2017
DK. NDUMBARO, MGONGOLWA WATEULIWA TFF
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imeteua Kamati ya Rufaa ya Leseni za Klabu, ikiwa ni maandalizi ya kuanza msimu mpya wa mashindano ya soka yanayosimamiwa na kuendeshwa na TFF.
Viongozi na wajumbe waliteuliwa na kupitishwa Jumapili Julai 30, 2017 katika Mkutano wa Kamati ya Utendaji uliofanyika Ukumbi wa Hosteli za TFF, zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam yaliko Makao Makuu ya shirikisho.
Viongozi na Wajumbe walioteuliwa ni Msomi Wakili Dk. Damas Ndumbaro atayekuwa Mwenyekiti; Msomi Wakili Alex Mngongolwa (Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo) wakati Wajumbe ni Meneja wa zamani wa Uwanja wa Taifa, Charles Matoke, Tumainiel Mlango na Ahmed Menye.
Viongozi wa Kamati hiyo watakuwa na majukumu ya kusililiza rufaa kutokana na uamuzi wa Kamati ya Leseni za Klabu inayoongozwa na Msomi Wakili Lloyd Nchunga ambayo inasimamia utekelezaji wa Kanuni ya 11 ya Ligi Kuu.
Kwa mujibu wa kanuni hiyo ya 11, Klabu za Ligi Kuu zinawajibika na kutakiwa kuwasilisha maombi ya kupatiwa Leseni ya Klabu kwa TFF katika muda utakaotangazwa na Kamati ya Utendaji ya TFF na kuhakikisha zinakidhi masharti na vigezo vyote vya msingi kupatiwa leseni ili kuweza kushiriki Ligi Kuu.
Kanuni hiyo ya 11 inasema kwamba Klabu itakayoshindwa kukidhi kiasi cha kukosa Leseni haitashiriki Ligi Kuu kwa msimu husika. Vigezo hitajika kwenye kupata leseni ya klabu ni kuwa na Uwanja wa nyumbani wa mechi, uwanja wa mazoezi, umiliki wa klabu moja, kuwa na timu ya vijana, uwepo wa ofisi rasmi na watendaji wake akiwamo mtendaji mkuu (CEO) na maofisa masoko, habari na mhasibu mwenye taaluma ya uhasibu.
Tayari Klabu zilielekezwa kuwasiliana na Meneja wa Leseni za Klabu, Jemedari Said ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Mpira wa Miguu Tanzania wa TFF kwa ajili ya maelezo ya kuchukua na kurejesha fomu kwa mujibu wa taratibu na kanuni za mashindano kabla ya kuanza rasmi mashindano.

TIGO KUTOA SMARTPHONE ZENYE MUDA WA BURE WA MAONGEZI KILA SAA KWA SAA 24

August 01, 2017
 Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, Wiliam Mpinga, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu promosheni mpya ya Jaza Ujazwe ambapo simu za kisasa 720 zitatolewa kila siku kwa washindi wa promosheni hiyo. Kulia ni  Mtaalamu wa  Bidhaa Mpya za Tigo, Jaqualine Nnunduma
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, Wiliam Mpinga, akionesha moja ya simu aina ya Teco S1 zitakazotolewa katika promosheni hiyo.
Mtaalamu wa  Bidhaa Mpya za Tigo, Jaqualine Nnunduma, akizungumzia promosheni hiyo.

Na Dotto Mwaibale



Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo  Tanzania, bado inawavutia wateja wake tena na prmosheni kubwa ambayo itashuhudia wateja hao  wakiondoka na simu za mkononi za kisasa (Smartphones) kila saa kwa saa 24 kila siku. Simu za mkononi zitatolewa zikiwa na muda wa  bure wa  mawasiliano kwa mwaka mmoja.

 Kwa mujibu wa Tigo, jumla ya simu za kisasa (Smartphones) 720  zipo tayari kuchukuliwa katika kampeni ya promosheni hii mpya.  Wateja wanaweza kushinda simu za mkononi kila saa tu kwa kuzijaza simu zao muda wa maongezi  kwa kukwangua kadi, e-pin au TigoPesa, ambapo namba yao ya simu itaingia kwenye droo kwa ajili ya kushinda  moja ya Smartphones za Tecno S1 ambayo itakuwa tayari kuchukuliwa  kila saa,  kila siku, katika siku saba za wiki.
                                             
Tofauti na promosheni nyingine ambapo ni wateja wachache tu wanapata zawadi chache, promosheni hii ya Tigo imethibitisha kusimama mahali ambapo  kila mteja mmoja anazawadiwa  kila anapojaza. Washindi wa Smartphone ya Tecno S1  watafurahia mawasiliano ya bure kwa mwaka mmoja ambapo zawadi nyingine za kushinda zinajumuisha bonasi ya bure katika  sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno ( SMS) kulingana na muundo wa matumizi wa wateja.

Akitangaza zawadi hizo mpya, Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema kuwa kampuni hiyo kwa mara nyingine tena imefurahishwa na mwitiko chanya wa wateja kwa kampeni maarufu ya  Jaza Ujazwe na ndiyo sababu imewafanya waongeze zawadi za kuvutia zaidi pamoja na bonasi zaidi za kusisimua kama ishara ya shukrani.
  
"Ni sehemu ya utamaduni wa Tigo katika  kutambua kuungwa mkono kusiko na ukomo ambao wateja wetu wametupa. Ndiyo maana, tunaamini kwamba wanastahili kupewa shukrani  kwa kujitoa kwao kwa kwa ajili ya  bidhaa  na huduma zetu. Tuna furaha  mara nyingine tena, kuwapatia  wateja wetu zawadi hizi, zitakazowawezesha kuendelea kufurahia huduma zetu za maisha ya kidijitali ", alisema Mpinga.


Tuzo za kusisimua zinaendana na  kuongezeka kwa miundombinu ya mtandao wa kisasa ya Tigo, aliongeza Mpinga akibainisha kuwa kipaumbele muhimu cha kampuni kilikuwa kikizingatia mahitaji ya wateja na kutoa suluhisho linalofaa kushughulikia mahitaji hayo.

 "Wateja wote wa Tigo wanastahili kupokea tuzo; tunatarajia kukidhi mahitaji ya mteja ya kuwa na uzoefu usio na  dosari kila wakati wanapowasiliana kwa chapa zetu.

Tunaamini kuwa wateja wetu watafurahishwa na zawadi hizi  mpya ikiwa ni pamoja na bonasi kwa dakika, ujumbe mfupi wa maneno (SMS) au data wanazozawadiwa na hivyo  kuimarisha utamaduni wao wa mawasiliano, "alibainisha Mpinga.



MWENYEKITI CHARLES MAKOGA : SHERIA MPYA KUTUMIKA KUKUZA MAPATO YA MJI WA MAFINGA

August 01, 2017
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Mji wa Mafinga wakiwa katika baraza pamoja na wataalamu mbalimbali wa halmashauri hiyo.

Na fredy Mgunda, Mafinga

Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoni Iringa inatarajia kukuza mapato katika mwaka Mpya wa 2017/2018 kutokana na kuanza kuzitumia sheria mpya za ukusanyaji mapato pamoja na kuvijua vyanzo vingine vya mapato ambavyo ndio vitasababisha kukuza uchumi wa halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa baraza la madiwani Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga alisema kuwa sheria mpya walizoletewa toka mwezi wa tano zinawapa nafasi ya kuanza kuzitumia wakati wa kukusanya mapato katika maeneo ambayo walikuwa hawakusanyi.

"Tulikuwa hatukusanyi mapato katika maeneo ya stand,sehemu za maegesho ya magari,sokoni na maeneo mengine kwa kuwa sheria zilikuwa bado si rafiki kwetu kwenda kukusanya mapato ila kwa mwaka unaoanza tutakusanya mapato na kukuza mapato kutoka asilimia 56 hadi kuvuka lengo la serikali la asilimia 80" alisema Makoga

Makoga aliwataka wananchi na viongozi kushiriana kukusanya mapato kulingana vyanzo ambavyo madiwani wameviolozesha kwa manufaa ya halmashauri ya Mafinga Mjini ambavyo vipo kisheria kutoka serikali kuu.

Jamani naombeni mchango wetu kufanikisha swala hili la kukusanya mapato ili tufikie lengo la serikali kwa kuwa mwaka huu hatufikia lengo hilo ni aibu kubwa kwa serikali hii ya awamu ya tank ambayo inaenda kwa kasi kubwa kwa kukuza uchumi wa nchi.

Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji wa mafinga Zacharia Vang'ota wa kata changarawe,Chesco lyuvale wa Kata ya kinyanambo walimtaka Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuzisimamia ipasavyo sheria ambazo zimetungwa na halmashauri pamoja na serikali ya jamhuli ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Dr John pombe Magufuli ili kukuza mapato katika halmashauri hiyo.

"Ukiangalia hapa Mafinga tunavyanzo vingi vya mapato lakini watalaamu wetu hawavifanyii kazi ndio maana sisi madiwani tumeamua kuanzia sasa vyanzo vyote tulivyovibainisha leo kwenye baraza vifanyiwe kazi haraka sana ili kukuza mapato ya halmashauri yetu"walisema madiwani

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Mafinga Mjini walisema kuwa Mji huo una changamoto nyingi hivyo serikali ya mji inatakiwa kuanza kuzitumia hizo sheria Mpya haraka ili hata wananchi wayatambue maeneo yanayopaswa kulipa kodi na kuewezesha halmashauri kukuza mapato na kutatua changamoto za Mji wa Mafinga.

"Angalieni nyie waandishi Mafinga maji ni tatizo kubwa,Barbara bado hazijatengenezwa hasa huku mitaani kwetu,Mji bado mchafu kila mtu anatupa takataka anavyotaka kwa kuwa hakuna mtu wa kumkamata ila ukiangalia sheria Mpya zipo lakini hazifanyiwi kazi na Mafinga maeneo ya maegesho ya magari hayalipiwi wakati miji mingine ni moja vya mapato hivyo viongozi wanapaswa kuanza kuzitumia sheria Mpya" walisema wananchi
kawaida:

Mpina awataka wakulima wa pamba Kisesa kuhifadhi chakula

August 01, 2017
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na baadhi ya  wananchi wa kijiji cha  Mwagayi katika kata ya Itinje Mkoani Simiyu wilayani Meatu, Jimboni Kisesa leo kuhusu ongezeko la bei ya pamba ambapo kwa sasa inanunuliwa kwa kiasi cha shilingi 1,200 kwa kilo.
Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akiongena na Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mwagayi kuhusu Ongezeko la bei ya pamba leo wananchi hao walimsimamisha Naibu Waziri Mpina alipokuwa katika ziara yake ya kikazi jimboni Kisesa.

Na Evelyn Mkokoi - Meatu
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina amewataka wananchi wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu mkoani Simiyu kutumia vizuri fedha wanazopata kwa kuuza pamba kununua chakula cha kutosha na kukihifadhi ili kuondokana na uhaba wa chakula.
Akizungumza Leo na wananchi wa Kijiji cha Mwagayi Kata ya Itinje  Wilaya ya Meatu, Mpina alisema uamuzi uliofanywa na Rais Dk John Pombe Magufuli kusimamia ongezeko la bei ya pamba umelenga kuboresha maisha ya wananchi wanyonge waliodhulumiwa kwa miaka mingi hivyo ni muhimu wakulima hao kutumia vizuri ongezeko hilo la bei kuboresha maisha yao ikiwa ni pamoja na kununua ziada ya chakula.
Mpina alisema Rais Magufuli amesimamia na kuweka msimamo usioyumba katika suala la pamba ambapo kwa sasa bei ya pamba imefikia shilingi 1200 kwa kilo tofauti na hapo awali ambapo wakulima walikuwa wakidhulumiwa kwa kulipwa shilingi 600 kwa kilo na kusababisha wananchi kuishi maisha duni na kushindwa kunufaika na zao hilo.
“Rais Magufuli ameweka msimamo kwamba pamba isinunuliwe chini ya shilingi 1000 na kwamba kampuni itakayoshindwa kununua kwa bei hiyo izuiliwe kununua pamba na kufutiwa usajili wa kutonunua tena zao hilo sehemu yoyote nchini”alisema Mpina.
Pia Mpina ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa  (CCM) aliwataka wananchi hao kutumia mabadiliko hayo ya bei ya pamba kama fursa ya kuboresha maisha badala ya kutumia vibaya fedha hizo kwa mambo ya anasa ikiwemo kuongeza idadi ya wake.

Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli imedhamiria kwa dhati kuboresha maisha ya wananchi wanyonge na ndio sababu ya kuwekwa msimamo huo kuhusu bei ya pamba kwani kwa miaka kumekuwa hakuna msimamo wa Serikali kuhusu zao hilo na hivyo kusababisha wanunuzi wa pamba kujipangia bei wenyewe na kuwakandamiza wakulima.
Kuhusu maendeleo ya jimbo hilo, Mpina alisema juhudi zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kumaliza kero ya maji ambapo kila kata ya jimbo hilo itapata visima vinne vya maji ambavyo vitamaliza kero kubwa ya maji kutokana na maeneo mengi ya jimbo hilo kuwa na ukame hasa nyakati za msimu wa kuangazi.
Aidha Mpiana alisema kauli mbiu yake ya ‘Sitapumzika hadi maendeleo ya kweli yapatikane jimbo la Kisesa’ haijabadilika na kuwahakikishia kuwa hajawahi kuchoka,kuogopa wala kushindwa kazi yoyote na kuwasihi kuendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano ili iendelee kuleta mabadiliko ambayo wananchi wameanza kuonja matunda ya utawala wa Rais Magufuli.