MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI (PSSN) WABADILISHA MAISHA YA WANANCHI VIKUGE, KIBAHA

MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI (PSSN) WABADILISHA MAISHA YA WANANCHI VIKUGE, KIBAHA

April 23, 2016
Natalia Kanem -TASAF Beneficiaries Kibaha
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa PSSN wa TASAF. (Picha na Modewjiblog)
Washirika wa maendeleo nchini wametembelea vijiji viwili Vikuge na Mwanabwito vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya kusaidia kaya masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo zinatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambapo washirika hao wamekuwa wakitoa fedha ili kusaidia miradi hiyo.
Washirika hao wa maendeleo kutoka UN Tanzania, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (DFID), Irish Aid, USAID na Shirika la Kimataifa la Misaada la Sweden (SIDA) ambao wamekuwa wakishirikiana na TASAF katika Mpango wa Kusaidia Kaya Masikini (PSSN).
Wakitoa taarifa mbele ya washirika wa maendeleo, wanavikundi kutoka Kijiji cha Vikuge wamesema kuwa kupitia mpango huo wameweza kuboresha maisha yao tofauti na jinsi ilivyokuwa awali.
Walisema kuwa maisha yao ya awali yalikuwa magumu lakini kutokana na msaada walioupata kutoka TASAF wameweza kuanzisha vikundi ambavyo vinawasaidia kuboresha maisha kwa kufanya biashara za mazao, nguo na chakula.
“Kuna mafanikio tumeyapata darasani mahudhurio yameongezeka, klini wamama wanakwenda na hata utapiamlo haupo tena kwa watoto kwa sababu ya TASAF kutusaidia,” alisema mwakilishi wa wanavikundi kutoka Vikuge.
TASAF Kibaha
Mratibu TASAF Kibaha, Goodson Hare, akitoa neno la ukaribisho kwa ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini waliotembelea vijiji viwili Vikuge na Mwanabwito vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya kusaidia kaya masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo zinatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Akizungumzia ziara hiyo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa MATAIFA NCHINI, Alvaro Rodriguez alisema wamefanya ziara hiyo ili kuona ni hatua gani imefikiwa na wanufaikaji na kuona ni changamoto gani bado zinawakabili.
“Tunaangalia changamoto zilizopo ili kuona ni jisni gani tunaweza kuwasaidia kama Mpango wa Kusaidia Kaya masikini ulivyo nab ado kuna wahitaji zaidi licha ya kuwa tumeshasaidia kaya Milioni1.1 kwa nchi nzima,
“Mpango huu ni mzuri na kawa wasaidiwa wakiwa kama wajasiliamali na kutengeneza kipato inaweza kusaidia Tanzania kuondokana na umasikini kuelekea katika uchumi wa kati kama jinsi ilivyojiwekea malengo,” alisema Rodriguez.
UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr. Alvaro Rodriguez
Kiongozi wa msafara wa washirika wa maendeleo nchini, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumzia madhumuni ya ziara yao kwa wanakijiji.
DSC_0311
Mkurugenzi wa Programu Jamii wa TASAF, Amadeus Kamagenge akizungumza jambo wakati wa utambulisho wa ujumbe huo.
DSC_0183
Wanufaikaji wa mpango wa PSSN wakisoma risala kwa wageni.
DSC_0299
Mmoja wa wanufaikaji wa mpango wa PSSN akitoa maoni wakati wa mkutano na washirika wa maendeleo waliotembelea kijiji chao.
DSC_0321
Mwenyekiti kijiji cha Vikuge, Vitus Mchami akitoa salamu kwa niaba ya wanakijiji kwa ugeni huo.
DSC_0173
Baadhi ya wanakijiji cha Vikuge wanaonufaika na mradi wa PSSN waliohudhuria mkutano huo.
DSC_0145
Zoe Glorious (kulia) kutoka ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akifanya mahojiano na Mnufaikaji wa kijiji cha Vikuge, Bi. Halima ambaye aliwezeshwa na mpango wa PSSN na kuanzisha biashara ya kufuga bata ambayo imemuwezesha kuendesha maisha yake na kumuingizia kipato.
DSC_0170
Bi Halima akiwa katika picha ya pamoja na mtoto wake wakati wa ziara ya washirika wa maendeleo nchini walipomtembelea nyumbani kwake.
DSC_0388
Mwakilishi wa Ubalozi wa Finland nchini, Milma Kettunen (kulia) akinunua moja ya bidhaa iliyotengenezwa na ukili kutoka kwa wakinamama wa kijiji cha Vikuge walionufaika na mpango wa PSSN na kujikwamua kiuchumi.
Natalia Kanem -TASAF Beneficiaries Kibaha
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa PSSN wa TASAF.
DSC_0413
Mwakilishi wa USAID, Daniel Moore akinunua kitamba cha Batiki kutoka kwa wanufaikaji wa mpango wa PSSN unaoendeshwa na TASAF wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya TASAF mkoa wa Pwani.
DSC_0375
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Eric Beaume wakimsikiliza mmoja wa wanakijiji cha Vikuge aliwezeshwa na mpango wa PSSN na kufanya biashara ya kilimo cha matunda na mazao mbalimbali. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Vikuge,Vitus Mchami, anayefatia Mratibu TASAF Kibaha, Goodson Hare
DSC_0379
Baadhi ya Biashara za wananchi wa Vikuge walionufaika na mpanngo wa PSSN wa TASAF.
DSC_0717
DSC_0556
Baadhi ya wanakijiji wa Mwanabwito, Kibaha mkoa wa Pwani waliohudhuria mkutano wa washirika wa maendeleo.
DSC_0367
Mratibu TASAF wa wilaya ya Kibaha, Goodson Hare akizungumza jambo wakati wa kutizama biashara zinazofanywa na wajasiriamali walionufaika na mpango wa PSSN wa TASAF kutoka kijiji cha Vikuge, Kibaha.
DSC_0553
Ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini akiwemo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) wakiwasili kwenye kijiji cha Mwanabwito.
DSC_0518
Ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini na viongozi wa TASAF katika picha ya pamoja walipotembelea shamba la miti katika kijiji cha Mwanabwito mkoani Pwani.
Usia Nkhoma Ledama
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama (katikati) akifafanua jambo kwa baadhi ya wajumbe wa msafara wa washirika wa maendeleo nchini wakati wa ziara hiyo.

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA ATAKA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPATIWA ELIMU .

April 23, 2016

Habari na picha na  John Nditi, Morogoro
WAZAZI na walezi wenye watoto wenye ulemavu wilayani Mvomero , mkoa wa  Morogoro wametakiwa kuwapeleka shule ili waweze kupata elimu itakayokuwa ni mkombozi wao kwa maisha yao ya baadaye katika kujiletea maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi,  imeelezwa.

Rai hiyo ilitolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, George Jackson Mbijima ,Aprili 20, 2016  wakati wa uzinduzi wa Darasa la watoto wenye ulemavu , katika kijiji cha Changarawe, Kata ya Mzumbe , wilayani humo. 
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru , Mbijima , alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi na jamii kwa ujumla, kuwapeleka watoto wenye ulemavu katika shule hiyo kwa kuwa elimu pekee ndiyo itakayowakomboa.
“ Serikali ya Tanzania imeweka mazingira mazuri ya kusoma kwa watoto wa makundi yote wakiwemo wenye ulemavu wa aina mbalimbali , kwani elimu pekee ndiyo mkombozi wao katika suala la kujitegemea siku za usoni...hivyo jamii itambua hilo na kuwajali watoto wenye ulemavu na si kuwaficha majumbani” alisema Mbijima.
Naye Mwalimu wa  darasa la  watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi ya Changarawe ,  Doreen Msuya, aliiomba serikali ya Wilaya, mkoa na Serikali kuu, kuona uwezekano wa kujenga hosteli ya watoto wenye ulemavu katika eneo la shule hiyo.

Msuya alisema , hatua hiyo itawezesha watoto wengi wanaoshindwa kufika kutokana na ulemavu wao waweze kuishi karibu na shule na kunufaika na elimu ambayo itawasaidia katika maisha yao baadae.
Hivyo alisema , mradi huo wa darasa la wanafunzi wenye mahitaji maalumu ulianzishwa mwaka 2013 baada ya kufanyika sense ya watoto wenye mahitaji maalumu na kubaini watoto 26 ambao kwa kipindi hicho walikauwa majumbani ingawa umri wa kuanza shule ulikuwa umefika.
 Msuya alisema , mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana kati ya halmashauri ya wilaya ya Mvomero na wanajamii wa kijiji cha Changarawe ambao hadi sasa wanafunzi 42 wapo darasani , kati ya hao wavulana 27 na wasichana 15.
“ Kupitia mradi wa darasa hili umeweza  kuibua watoto sita waliokuwa wamefichwa  nyumbani  ambao ni wenye ulemavu wa aina mbalimbali” alisema Msuya.

“ Kuazishwa kwa darasa la watoto wenye ulemavu katika shule hii ya Changarawe  kumesaidia  kuibuliwa ndani ya jamii watoto wa aina hiyo waliokuwa  mitaani na nyumbani bila ya matumaini yeyote ya baadaye “ alisisitiza Mwalimu Msuya.

Akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake , mwanafunzi wenye ulemavu , Steven Petro (14) wa darasa la tano shuleni hapo, kuanzishwa kwa darasa hilo kumewawezewa wao kupata elimu na hivyo kuwa na matarajio mazuri ya siku za usoni.
Naye mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa, alihimiza wazazi kuhakikisha watoto wanapata fursa ya kuandikishwa shule ya awali na msingi ikiwa na kuwandeleza hadi elimu ya juu kwa vile elimu ndiyo ufunguo wa maisha.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika wilaya ya Mvomero  ulipitia, kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kuonwa  miradi  mitano ya maendeleo yenye thamani zaidi ya Sh  milioni 688.6 ukiwemo  wa  darasa la watoto wenye mahitaji maalumu.
Tayari Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake katika Manispaa ya Morogoro, halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Mvomero , Ulanga na Kilombero tangu ulipozinduliwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan , Aprili 18, mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro.

 Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga , mkoa wa Morogoro wakifuatilia jambo wakati wa ugeni wa Mwenge wa Uhuru .
 Kikundi cha Wanawake cha Mvomero kikionesha bidhaa zao.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa , George Jackson Mbijima akifuatana na Mkuu wa wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, Betty Mkwasa  kuangalia bidhaa za kikundi cha wanawawake.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, George Jackson Mbijima akimkabidhi hati kwa klabu ya wapinga rushwa ya Twikale wose  Lugono, Mwenyekiti wa klabu , Kondo Mahawa.
 Mgangazaji wa TBC Swedi Mwinyi , ( kati kati ) akiwa pamoja na mshereheshaji mwenzake ( kushoto) wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge  wa Uhuru 2016, uwanja wa Jamhuri wa Morogoro.  
 Mjasilimali wa Kimasai  akiwa na  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa pamoja  na mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa.
 Mkuu wa Takukuru wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, Eufrasia Kayombo ( kushoto) akisaini hati ya uzinduzi wa klabu ya wapinga rushwa Twikale wose , Lugono kilichopo wilaya ya Mvomero.
 Mkuu wa wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, Betty Mkwasa akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru , baaada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Muhingo Rweyemamu ( hayupo pichani).
 Mkuu wa wilaya ya Ulanga, mkoa wa Morogoro, Christina Mndeme, ( kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe ( kushoto),kuanza mbio zake Aprili 22, 2016
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa , wakitoka  kuweka  jiwe la msingi jengo la kuhifadhia dawa na vifaa tiba katika hospitali ya wilaya ya Ulanga.
 Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru, baada ya kuvuka katika kivuko cha Mv Kilombero 11 kutokea wilaya ya Ulanga. (1)
Mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo, Steven Petro  wa darasa la tano shule ya Msingi Changarawe, wilaya ya Mvomero akisoma risala.

WIZARA YA UJENZI ,UCHUKUZI NA MAWASILIANO YAENDELEA NA MCHAKATO WA UKUSANYAJI MAONI JUU YA UBORESHAJI SERA YA TAIFA YA (TEHAMA)MKOANI MBEYA .

April 23, 2016
Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Simu katika Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera akizungumza na wanahabari katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu jijini Mbeya( TIA ) juu ya zoezi la uchukuaji maoni na ushauri kwa wadau katika kuboresha sera ya Taifa ya Habari ,Teknologia na Mawasiliano (TEHAMA).

Mhandisi  Enock Mpenzwa Idara  Mawasiliano  toka Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Forest jijini Mbeya waliofika kwa ajili ya zoezi la utoaji maoni na ushauri juu ya uboreshaji wa sera mpya ya Taifa ya TEHAMA katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu TIA jijini Mbeya April 22 ,2015.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Forest jijini Mbeya wakiwa katika foleni ya kujiandikisha ili kutoa maoni yao na ushauri juu ya uboreshaji wa sera ya Taifa ya TEHAMA,zoezi ambalo limefanyika katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Mbeya (TIA) April 22 ,2015.

Mwanafunzi shule ya sekondari Forest jijini Mbeya Mariam Jordan akijiandikisha kwa ajili ya kutoa maoni yake katika zoezi la uboreshaji wa sera ya Taifa ya TEHAMA zoezi ambalo limeratibiwa na Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ,katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Jijini Mbeya( TIA)

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Jijini (TIA)wakijibu baadhi ya Maswali kama sehemu ya ukusanyaji maoni ili kuboresha sera ya TEHAMA .



Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Jijini (TIA) na wadau mbalimbali kutoka Mkoani Mbeya wakijibu baadhi ya Maswali kama sehemu ya ukusanyaji maoni ili kuboresha sera ya TEHAMA .



Na Emanuel Madafa,Mbeya(Jamiimojablog)

Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano  imetoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kutoa maoni na mapendekezo ili yatumike kuboresha Sera mpya ya Taifa ya Habari  Teknologia ya Mawasiliano(TEHAMA) ya (2016) ili kuisaidia serikali kutatua changamoto za upatikanaji wa habari na mawasiliano katika jamii

Wito huo umetolewa jijini Mbeya  na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia maswala ya simu katika Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera wakati wa zoezi la uchukuaji maoni lililofanyika katika viwanja vya chuo cha Uhasibu (TIA) jijini Mbeya .

 Amesema Teknolojia ya habari na mawasiliano hapa nchini imekuwa ikikua kwa kasi kubwa katika kipindi cha miaka kumi tangu serikali ilipotunga sera kwa mara ya kwanza mwaka 2003.

  Amesema hali hiyo imechangia kuwepo kwa miundombinu ya huduma za mawasiliano   kila mahala  na kufanya matumizi kuwa makubwa ambapo zaidi ya watu milioni 39 wanatumia mawasiliano ya simu hivyo kufanya kuibuka kwa changamoto mbalimbali katika sekta hiyo.

Amesema ili kufahamu changamoto wanazo kutananazo wananchi pamoja na mtizamo wao  katika utumiaji wa mawasiliano,  wizara hiyo imeamua kuweka utaratibu wa kuweka vituo vya kukuza ubunifu katika jamii katika kila mkoa ambapo kila mwananchi anakuwa huru katika kutoa maoni yao na ushauri ili kuisaidia serikali katika kupanga mikakati ya kuweza kuzitatua changomoto hizo.

Huwezi kukaa ofisini ukatunga sera ambazo haziwahusu mwananchi wa kawaida hivyo lazima twende  kwa wananchi na kujua wanahitaji nini ili kutunga sera na kuweza kuzitatuaAlisema Mwela .

Aidha amesema kuwa kila maoni yanayotolewa na wananchi serikali inayathamini katika kuweza kutoa muelekeo wa sekta ya mawasiliano kwani sekta hiyo bado inamchango mkubwa sana katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Hata hivyo amesema bado wizara inakabiliwa na changamoto mbalimbali  ikiwa ni elimu ndogo kwa waanchi juu ya utunzaji wa miundombinu ya sekta ya mawasiliano hususani mkongo wa taifa sanjali na wizi wa mafuta kwenye minara ya simu hivyo amewataka wananchi kuwa walinzi wa miundombinu hiyo ili kuendelea kukuza sekta hiyo sanjali na kulahisisha upatikanaji wa huduma kwa jamii.

Amesema zoezi hilo la uchukuaji maoni kwa wananchi juu ya uboreshaji wa sera ya TEHAMA itaendelea inchi nzima katika mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani.


MBAO FC YAPANDA LIGI KUU

MBAO FC YAPANDA LIGI KUU

April 23, 2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitangaza klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao kutoka katika kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza chini (StarTimes League).
TFF imeitangaza Mbao FC kfuatia maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF yaliyotolewa April, 2016 ya kuzishusha daraja timu nne kutoka kundi C baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo.
Mbao FC imeshika nafasi ya kwanza kundi C kwa kuwa na pointi 12 baada ya kufutwa kwa matokeo ya timu za Geita Gold, Polisi Tabora, JKT Oljoro na JKT Kanembwa zilizokumbwa na mkasa huo wa upangaji matokeo.
Timu ya Mbao FC inapanda ligi kuu (VPL) msimu ujao, sambamba na timu za African Lyon ya jijini Dar es salaam pamoja na Ruvu Shooting ya mkoa wa Pwani.
Wakati huo huo kikao cha Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF kinatarajiwa kukaa Jumamosi ijayo April, 30 jijini Dar es salaam kujadili rufaa mbalimbali ambazo zimekatwa na kutokana na maamuzi ya kamati ya Nidhamu ya TFF.
Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF itasikiliza rufaa za wafuatao waliokata rufaa
(i) Saleh Mang’ola,
(ii) Yusuph Kitumbo,
(iii) Amos Mwita,
(iv) Fateh Remtullah,
(v) Timu ya JKT Oljoro,
(vi) Timu ya Polisi Tabora.
Aidha Kamati ya Nidhamu ya TFF itakutana Jumapili Mei Mosi kupitia taarifa mbalimbali zilizowasiliswa katika kamati hiy

WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI YA MEATU WAPANDA MITI YA MATUNDA WALIOHAIDIWA NA SERIKALI

April 23, 2016
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakishusha miti ya Matunda kutoka kwenye gari iliyoibeba mapema leo, miti hiyo walihaidiwa na Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Bw. Paschal Lugali, mfanyakazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu akipanga miche ya miti ya matunda mapema leo, ikiwa ni ahadi ya serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira.

 Afisa Misitu Mwandamizi kutoka Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Raisi bw. George Kafumu akiangalia miche ya miti ya matunda baada ya kuiwasilisha katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu mapema Leo.
 Afisa Misitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Bw. Sunday Anut akipanga miche ya miti ya matunda kitaalamu leo, baada ya kuipokea Wilayani humo mapema leo.
Miche ya miti ya matunda, ikiwa imepangwa baada ya kupokelewa mapema Leo katika halmashauribya wilaya ya Meatu,baada ya serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira kutekeleza ahadi yake ya kugawa miti elfu ishirini na saba (27,000) Katika mkoa wa Simiyu. (Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Makamu wa Raisi)
Baadhi ya wakazi wa jimbo la kisesa mkoani Simiyu katika picha pamoja na miche ya miti ya matunda waliyo ipokea kutoka serikalini kupitia Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira.