MBUNGE MGIMWA AMETUMIA JUMLA YA SHILINGI 119,200,000 KATIKA UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI, ZAHANATI NA NYUMBA ZA WAFANYAKAZI KATIKA KIJIJI KIBENGU

January 08, 2018
 Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza na wananchi katika moja ya shule ambayo inahitajika kujengewa vyumba viwili ya madarasa na kukarabati vyumba vingine vitatu kwa gharama za wananchi na mbunge mwenyewe akichangia kwa asilimia kubwa kuboresha maendeleo ya sekta ya elimu kwa wananchi na wanafunzi wa jimbo hilo
 Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza mmoja ya walimu pamoja viongozi kutoka kwenye ofisi yake ya mbunge ambao alikuwa ameongoza nao katika kukagua na kutatua changamoto za wananchi kwenye kata ya Kibengu
 Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akitoa mfano wa kufanya kazi kwenye ujenzi wa vyumba vitatu vya shule ya msingi Kibengu ambako nako wananchi wamechangia nguvu zao
 Katibu wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM wilaya ya Mufindi akiwa na katibu wa mbunge idara ya uhamasishaji na michezo Lwimbo nao wakijumika na wananchi katika ujenzi wa shule ya msingi Kibengu
 Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza na viongozi katika eneo ambalo vyumba vitatu vya madarasa vinajengwa
 Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akizungumza kwenye eneo ambalo ofisi ya kijiji inajengwa ajili ya kurahisisha kutoa huduma kwa wananchi
Mbunge wa jimbo la Mufindi KaskaziniMahamuod Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Kibengu Zakayo Kilyenyi sambamba na katibu wa mbunge idara ya uhamasishaji na michezo Lwimbo

 Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kushirikiana na wananchi  wa kijiji cha Kibengu wametumia jumla ya shilingi milioni mia moja kumi na tisa na laki mbili (119,200,000) katika ujenzi wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa shule zilizopo katika kijiji hicho lengo likiwa katika kuboresha sekta ya elimu na afya kwa wananchi.

Akizungumza na wananchi katika kijiji hicho mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa alisema kuwa ameamua kuwekeza katika elimu na afya kwasababu wananchi wakifanikiwa kupata vitu hivyo viwili kwa wakati watafanya maendeleo kwa kasi kubwa kulingana na wakati uliopo na kuendana na mazingira wanayoishi.

“Hivi ndio vipaumbele vyangu kwa kijiji hiki kwa wakati huu maana nimegundua kuwa changamoto kubwa ni kuwa shule nyingi za msingi zilijengwa miaka mingi iliyopita sasa zimechakaa na sio rafiki kwa wanafunzi kuwasaidia kupata elimu bora hivyo nimeanza na hilo pamoja na kuchangia maendeleo kwa kuboresha sekta ya afya ili wananchi wakiugua waweze kutibia hapa hapa kijiji kwa kuwa nina uhakika huduma itakuwa inatolewa kwa ustadi mkubwa na yenye ubora unaotakiwa” alisema Mgimwa

Mgimwa alieleza kuwa pesa hiyo itatumika katika maeneo yafuatayo ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Kibengu utatumia gharama ya shilingi milioni thelathini (30,000,000) hadi kukamilika kwake,kuingiza umeme zahanati na kwenye nyumba za waganga imegarimu kiasi cha shilingi 1,200,000/=,ujimbaji wa kisima shilingi 2,00,000/=,ujenzi wa nyumba za walimu mbili kwa moja itagharimu kiasi cha shilingi 25,000,000/= na shule ya msingi Kibengu kutafanyika ujenzi wa madarasa matatu ambayo yatagharimu kiasi cha shilingi 21,000,000/=.

“Hizi ni gharama katika kijijicha Kibengu ambazo nimechangia na wananchi wangu hivyo napenda kuwapa habari vijiji na vitongoji vingine kwenye jimbo langu kuiga mfano wa kijiji cha Kibengu na kitongoji cha Mitanzi kwa kujituma kuleta maendeleo” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa alisema kuwa wananchi wa kitongoji cha Mitanzi katika kijiji cha Kibengu nao wamekuwa wakitoa ushirikiano na kufanikisha kufanya maendeleo katika maeneo yafuatayo ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa ya shule ya msingi Mitanzi utagarimu kiasi cha shilingi milioni kumi na saba (17,000,000) uchimbaji wa kisima  shilingi 1,000,000/=, ukarabati wa madarasa mawili shilingi 17,000,000 kutona na yalivyo haribika, kuingiza umeme kwenye nyumba za walimu na madarasa shilingi 5,000,000/=

“Ukaingalia tumetumia nguvu kubwa na wananchi kufanikisha haya japo kuna maeneo bado hatujamalizia na ninauhakika tutamalizia lakini bado kunawatu wanasema eti sifanyi kazi sasa sijui wataka niwe ninawapa pesa mikononi mwao ili wajue maendeleo yapo” alisema Mgimwa

Mgimwa alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuendelea kumuunga mkono katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo kwa kuwa wanajinea kazi anayoifanyia hivyo wasikubali kulishwa maneno na watu wasiopenda maendeleo.

Kwa upande wake mtendaji wa kijiji cha Kibengu Dominicus Nyaulingo alimshukuru mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa jitihada zake za kuleta maendeleo kwa kushirikiana na wananchi na kahidi kuwa watandelea kuzitangaza kazi anazozifanya ili wananchi wote wajue anafanya kazi gani na kupunguza maneo ambayo yamekuwa yakisemwa bila kuwa na ushaidi juu ya utendaji wa mbunge huyo.

“Kweli kabisa mbunge wetu amekuwa akifanya kazi kubwa sana ila sisi tumekuwa hatuzisemi kazi za mbunge kwa wananchi hivyo kuchochea chuku baina ya wananchi na mbunge hivyo kuanzia leo nitakuwa ninazisemea kazi za mbunge kila kwenye mkutano wa kijiji” alisema Nyaulingo

RC TELACK AFANYA ZIARA KUKAGUA KILIMO CHA PAMBA NA MTAMA WILAYANI KISHAPU

January 08, 2018
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack amefanya ziara ya kukagua kilimo cha zao la Pamba na Mtama wilayani Kishapu kwa ajili ya kuendelea kuhamasisha wakulima kulima mazao hayo kwa wingi kwa njia za kitaalamu ambayo yatawafanya wakue kiuchumi na mkoa kwa ujumla.
RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA GAVANA WA BENKI YA TANZANIA ( BOT) ANAYEMALIZA MUDA WAKE PROFESA NDULU IKULU ZANZIBAR

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA GAVANA WA BENKI YA TANZANIA ( BOT) ANAYEMALIZA MUDA WAKE PROFESA NDULU IKULU ZANZIBAR

January 08, 2018

DSC_7430
RAIS wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Gavana wa Benki ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu, alipofika Ikulu Zanzibar kumuaga rasmin kwa kumaliza muda wake wa Kazi BOT, hafla hiyo imefanyika leo IkuluZanzibar 8-1-2018 .
DSC_7514
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na mgeni wake Gavana wa Benki ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu, wakitoka katika ukumbi baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Zanzibar kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Kazi BOT
DSC_7531
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Benki ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu na maofisa wa BOT aliofuatana nao .
Picha na Ikulu
WAZIRI JAFO AKEMEA UTATU USIO MTAKATIFU KATIKA MANUNUZI YA KAZI ZA TARURA

WAZIRI JAFO AKEMEA UTATU USIO MTAKATIFU KATIKA MANUNUZI YA KAZI ZA TARURA

January 08, 2018

1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Amos Makala wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wataalaamu wa Wakala wa Barabara mijini na Vijijini(TARURA) yaliyofanyika Jijini Mbeya.
2
Mkurugenzi wa barabara Vijijini Mhandisi Abdul R.Digaga akitoa taaarifa ya awali kwa mgeni rasmi kuhusiana na mafunzo ya masuala ya Ununuzi wa Umma na Usimamizi wa Mikataba ya Ujenzi na matengenezo ya barabara na Maadili katika kazi za TARURA yaliyofunguliwa leo Jijini Mbeya.
3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wahandishi, wajumbe wa bodi ya zabuni na wataalamu wengine wa TARURA wa mikoa saba ya Nyanda za juu kusini wakati wa mafunzo ya Ununuzi na maadili yanayofanyika Jijini Mbeya.
4
Baadhi ya wataalamu wa TARURA wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi,OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo wakati akifungua mafunzo ya Manunuzi na Maadili Jijini Mbeya.
5
Katika Picha ya pamoja ni ni Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Aliyekaa katikati) pamoja na viongozi wa Mkoa pamoja na TARURA na washiriki wa mafunzo kutoka Mkoa wa Njomba.
6
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa barabara Vijijini Mhandisi Abdul R.Digaga baada ya ufungzuzi wa mafunzo ya TARURA jijini Mbeya.
………………
Nteghenjwa Hosseah, Mbeya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka watumishi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijiji(Tarura) kuvunja utatu usio mtakatifu katika kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara zinazoendelea kutangazwa katika maeneo mbalimbali Nchini.
Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa kufungua mafunzo ya Siku Sita ya watalaam wa Tarura kutoka katika Mikoa saba ya Nyanda za Juu kusini kuhusiana na masuala ya Ununuzi wa Umma na Usimamizi wa Mikataba ya Ujenzi na matengenezo ya barabara na Maadili katika kazi za TARURA yenye   takribani miezi sita sasa tangu kuanzishwa kwake.
Waziri Jafo amesema “Ninaposema Utatu mtakatifu namaanisha Afisa Manunuzi, Mhasibu na Mhandishi wa Tarura katika eneo husika hawa ndio huwa wanaamua nani apewe kandarasi kwa mujibu wa mahusiano na makubaliano wanayoyajua wao.
” Huu Utatu usio mtakatifu katika kazi za Umma ufe kuanzia leo na Mkandarasi apewe kazi kwa kuzingatia uwezo wake wa kitaalam na kifedha katika kukamilisha kazi hiyo na sio mahusiano na makubaliano nje ya vigezo vilivyowekwa”.
Katika Utatu huu ninauouzungumzia kuna mahusiano ya karibu sana na Rushwa na inafahamika wazi kuwa Rushwa hupofusha wataaalam kuona na kutathmini uwezo wa Mzabuni, huzorotesha kazi iliyopangwa kufanyika na kuwanyima wananchi haki yao ya Msingi ya huduma bora za barabara na tutakaowabaini wakiendeleza kasumba hii tutawachukulia hatua za kisheria na kinidhamu alisema Jafo.
Akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala amesema wamejiandaa kikamilifu kusimamia kazi za Tarura na baada ya uzinduzi wa kitaifa walizindua tena Kimkoa ili kuwafahamisha wananchi wa Mkoa huu umuhimu wa Taasisi hii, ili waweze kumiliki Kazi zinazofanywa na Tarura na kuwaeleweshe lengo la kutoka kazi za barabara kutoka Halmashauri na kusimamiwa na Tarura.
“Tarura imekuja kuboresha kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na Baraza la Madiwani, Kamati za kudumu pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi sasa TARURA  wamekuja kutekeleza kitaalam zaidi, namna ya usimamizi, manunuzi, mikataba ili tuweze kupata matokea bora na ya haraka.
Naye Mkurugenzi wa Tarura Eng. Abdul R. Digaga  amesema Mafunzo haya ni mpango wa Kimakakati wa  Tarura katika kupambana na Rushwa katika utekelezaji wa miradi ya Ujenzi na matengenezo ya barabara, mgongano wa maslahi, matumizi mabaya  ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara na ukosefu wa Uadilifu miongoni mwa watendaji. 
Mafunzo hayo ambayo yalianza kufanyika katika kanda mbalimbali Nchini na kanda hii ya Nyanda za juu kusini ni ya mwisho kufanyika kwa wataalam wa Tarura wa kada mbalimbali na imejumuisha Mikoa ya Mbeya, Songwe, Ruvuma,Rukwa,Katavi na Iringa na Njombe.

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE. DOTTO MASHAKA BITEKO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

January 08, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimmkabidhi nyenzo za kazi Mhe. Dotto Mashaka Biteko baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakimsikiliza Mhe. Dotto Mashaka Biteko akila kiapo cha Uadilifu cha Viongozi wa Umma baada ya kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakimsikiliza Mhe. Dotto Mashaka Biteko akiongea machache baada ya kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakimsikiliza Spika Job Ndugai akizungumza machache baada ya Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mhe. Dotto Mashaka Biteko baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mhe. Dotto Mashaka Biteko baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini waliohudhuria kwenye hafla ya kuapishwa Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 8, 2018. PICHA NA IKULU.

CHUO CHA IFM MABINGWA LIGI YA VYUO

January 08, 2018
Chuo cha IFM wametwaa ubingwa wa Ligi ya Vyuo vya Elimu ya Juu mkoa wa Dar Es Salaam baada ya kuishinda Chuo cha Ardhi kwa magoli 6-4 kwenye mchezo wa fainali iliyochezwa kwenye Ufukwe wa Coco Jumapili Januari 7, 2018.
Kufika fainali IFM ilicheza na Chuo cha TIA kwenye mchezo wa nusu fainali ambao walishinda kwa penati 3-2 baada ya kutoka sare ya mabao 7-7.
Ardhi kwenye nusu fainali waliishinda DIT kwa magoli 9-6 ushindi uliowapa nafasi ya kucheza fainali na IFM na kupoteza.
Mchezo huo wa fainali ulilazimika kwenda kwenye muda wa nyongeza baada ya muda wa kawaida timu hizo kumaliza zikifungana magoli 4-4 na katika muda wa nyongeza IFM wakajipatia magoli yao yaliyowapa ubingwa.
Kwenye Ligi hiyo mchezaji Jarufu Juma wa Chuo cha DIT ameibuka kuwa kinara wa mabao akifunga magoli 17

RAIS KARIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA ATHUMAN CHAMA

January 08, 2018
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Athuman Juma “Chama” maarufu kama Jogoo aliyefariki usiku wa kuamkia leo Januari 8, 2018 kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili.
 
Katika salamu hizo za rambirambi Rais Karia amesema ni mshtuko mkubwa kumpoteza mchezaji huyo wa zamani na ametoa pole kwa familia yake,ndugu jamaa na marafiki.
 
Rais Karia amesema TFF inatoa rambirambi kwa familia ya marehemu kutokana na msiba huo. 
 
“Ni masikitiko makubwa kumpoteza Chama ambaye alilitumikia taifa naungana kumuombea marehemu na ninatoa pole kwa familia yake,wana familia ya mpira wa miguu ,ndugu na jamaa zake wa karibu pamoja na marafiki,Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya Marehemu Athuman Juma Chama .Amina. Inna Lillah wa Innalillah Rajaun.”
 
Enzi za Uhai wake Marehemu Chama pamoja na kuichezea timu ya Taifa katika ngazi ya klabu alicheza kwenye vilabu vya Pamba na Yanga.

DALILI KWAMBA BADO UNA UCHOVU WA LIKIZO NA NAMNA YA KUKABILIANA NAZO

January 08, 2018
Na Jumia Travel Tanzania


Ni hali ya kawaida kujisikia hali ya uchovu mahala pako pa kazi hususani baada ya kurudi kutoka likizo au mapumziko. Na inawezekana bado miongoni mwa wafanyakazi wenzako hawajarudi kutoka mapumzikoni. Achilia mbali bado kusikia salamu za, “likizo yako ilikuaje?” Au “Natumaini ulikuwa na mapumziko mema,” zikitawala kila unapokutana na watu.

Endapo unajisikia mwili na akili ni vizito kuanza na majukumu ya mwaka huu mpya basi kuna uwezekano mkubwa  hizo ni dalili za uchovu wa likizo. Na ukweli ni kwamba haupo peke yako, ni hali ya kawaida ambayo watu wengi hupitia kipindi kama hiki sehemu tofauti duniani.


Changamoto ni kwamba watu wengi huwa hawajijui kama bado wana uchovu wa likizo au mpaka waje kugundua inakuwa ni muda mrefu umepita. Jumia Travel ingependa kukushirikisha mambo yafuatayo ambayo ni dhahiri kwamba bado una uchovu wa likizo na namna yakukabiliana nao.

Akili yako. Endapo kumbukumbu za matukio uliyoyafanya kipindi cha mapumziko bado zinajirudia mara kwa mara basi ujue ni dalili upo kwenye uchovu wa likizo.


Nguvu yako. Endapo mwili bado unajisikia uchovu, kwa maneno mengine tunaweza kusema kwamba kila unachotaka kukifanya unakuwa ni mzito kufanya hivyo, basi ujue una uchovu wa likizo.

Hali yako. Kuna wakati unakuwa na ari ya kufanya kazi iliyopo mbele yako lakini kila ukijitahidi kuanza inakuwa ni vigumu akili yako kuwa makini. Hii ni dalili nyingine kwamba bado una uchovu wa likizo.


Usingizi wako. Kipindi cha mapumziko ilikuwa ni vigumu kulala kwa wakati kwani haukuwa na hofu ya kuwa na majukumu siku inayofuatia. Hivyo ulikuwa unalala muda wowote unaotaka na kwa kiwango chochote ulichokitaka. Lakini sasa itabidi kulala kwa wakati na kuamka muda ambao utakufanya uwahi kwenye shughuli zako ipasavyo. Kama unajisikia usingizi unaupata kwa tabu au haupati usingizi ndani ya muda muafaka basi hiyo ni dalili nyingine ya uchovu wa likizo.

Hamu yako ya kula. Kipindi cha likizo watu wengi huwa hawazingatii ratiba ya kula au aina ya vyakula wanavyokula. Kwa sababu huwa ni kipindi ambacho tunaupumzisha mwili na akili kutokana na pilikapilika za mwaka mzima, suala la kuzingatia vyakula vya kula huwa halipo. Endapo bado haujisikii kula chochote au aina fulani ya vyakula basi ujue hali ya kujisikia bado upo mapumzikoni haijatoka mwilini na akilini mwako.   


Dalili zote hizo hapo juu ni kwamba bado unakabiliana na uchovu wa likizo ambao ni vigumu kuondoka mwilini na akilini mwako kwa haraka kama unavyotarajia. Umefikia wakati sasa wa kuondokana na hali hiyo ili uendelee na majukumu yako kama kawaida kwani kipindi cha mapumziko kimekwishapita.

Namna ya kurudia hali yako ya kawaida.


Fuatilia kwa karibu mienendo yako ya sasa. Inawezekana kwamba ulikuwa na wakati mzuri kipindi cha likizo, moyo na akili yako bado unakukumbusha namna ilivyokuwa. Suluhu ni kubadili ratiba ya shughuli ulizozifanya ili kuendana na shughuli ulizonazo kwa sasa.  

Fanya mazoezi. Mbinu nyingine itakayokusaidia zaidi ni kwa kufanya mazoezi mepesi aidha ya viungo au hata kutembea jioni mara baada ya kazi. Mazoezi huufanya mwili na akili kuondokana na uchovu na kuupatia ari na nguvu mpya ya kufanya mambo mengi kwa ufanisi zaidi.

Hakikisha unazingatia mlo wenye afya na usingizi wa kutosha. Ni wakati sasa wa kurudi kwenye ratiba ya mlo wenye afya kama ilivyokuwa awali. Kwani inaaminika kwamba namna pekee ya kuufanya mwili na akili yako kujisikia vizuri ni kupitia mlo wenye afya na usingizi wa kutosha. Kujinyima usingizi wa kutosha ni ni sawa na kujipatia mateso bila ya kujijua. Kwa hiyo, acha kujitesa!  

Mshirikishe rafiki au mtu wako wa karibu namna unavyojisikia. Hii hali haikutokei wewe peke yako bali ni watu wengi. Hivyo basi, kwa kumshirikisha mtu wako wa karibu inaweza kuwa ni tiba mbadala. Huwezi kufahamu atakuwa na ushauri wa aina gani ili kukusaidia kuishinda hiyo hali. Jumia Travel inaamini kwamba lazima utakuwa na mtu wako wa karibu ambaye unaelewana naye, anakufahamu vya kutosha na kamwe hatosita kukusaidia pale unapohitaji msaada katika kujinasua na hali kama hii. Kushindwa kufanya hivyo kunaweza kukuhatarishia shughuli zako kutoenda sawa na kukupoteza fursa mbele yako bila ya kujijua.   

MBUNGE WA LUSHOTO KUWALIPA KADI ZA MATIBABU ZA (CHF) WAZEE WASIOJIWEZA KATA YA MLOLA

January 08, 2018
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi “Bosnia” akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani Lushoto mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara na kusikiliza kero zinazowakabili wakati wa ziara yake
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi “Bosnia” kulia akisikiliza kwa umakini maswali ya wananchi wa Kijiji cha Lwandai
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi “Bosnia” akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho wakati wa ziara yake kusikiliza changamoto zinazowakabili
Mmoja wa wakazi wa Kijiji hicho akiuliza swali katika mkutano huo wa hadhara
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi “Bosnia” kushoto akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa CCM kata ya Mlola baada ya kumaliza mkutano wake na wananchi
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi “Bosnia” katikati akimsikiliza mkazi wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani Lushoto mara baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara.
MBUNGE wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia amesema atawalipia kadi za Afya ya Jamii (CHF) wazee wote wasiojiweza wenye umri wa miaka sitini na kuendelea waliopo kwenye kata ya Mlola wilayani Lushoto ili waweze kupata huduma za matibabu bure wakati wanapokuwa wakiugua.

Hatua ya mbunge huyo ina lengo la kusaidia matibabu kwa wazee hao kwani baadhi yao wanayakosa kutokana na kukosa fedha hiyo kupitia mpango huo wanaweza kutibiwa wakati wowote na kuondokana na changamoto zinazowakabili.

Aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani humo ambapo alisema wazee wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo hivyo wanapokosa huduma za matibabu kutokana na ukata wa fedha sio jambo nzuri kwani wanapaswa kusaidiwa.

“Kwa kweli kama mnavyojua ndugu zangu wazee wetu wana mchango mkubwa sana katika maendeleo lakini changamoto kubwa ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo kila wakati ni kuhusu gharama za matibabu wanapokuwa wakiugua hivyo mimi Mbunge wenu nimeona niwalipie “Alisema.

“Lakini pia nikuagize Afisa Mtendaji wa Kata ya Mlola, Saidi Kimweri uniorodheshehe majina ya wazee wote waliopo kwenye eneo lako ambao hawajiwezi kuanzia miaka sitini kwa lengo la kuweza kuwakatia kadi za CHF waweze kupata matibabu bure pia hakikisha unapita nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuwabaini wahusika “Alisema Mbunge huyo

Ahadi hiyo inatokana na swali lililoulizwa mkazi wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola Ayoub Fundi  kwa mbunge huyo katika mkutano wa hadhara kuhusu wazee wasiojiweza watasaidiwa vipi kuweza kupata huduma za matibabu katika vituo vya afya, zahanati na hospitali kutokana na uwezo mdogo walionao.

“Mh mbunge sisi wazee tusijiweza utatusaidiaje tuweze kupata matibabu tunapokuwa tukiugua maana tunakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa ni hasa namna ya kupata fedha zitakazo tusaidia kutibiwa wakati wa maradhi “Alisema.

Alisema kwani baadhi yao wamekuwa ni wazee sana na hivyo hawana namna ya kuweza kutafuta fedha za kuweza kusaidia kutibiwa wakati wanapokuwa wakiugua hivyo wanamuomba awasaidie kwenye jambo hilo ambalo ni muhimu kwa ustawi wa
maisha yao.

Kwa upande wake,Afisa Mtendaji huyo wa kata ya Mlola Saidi Kimweri alihaidi kutekeleza agizo hilo kwa vitendo na baadae kuweza kumfikishia ili aweze kusaidia jambo hilo ambalo litakuwa mkombozi mkubwa kwa wazee hao.

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI IMEUNDA TIMU YA WATAALAMU 15 KUFUATILIA UTEKELEZAJI ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA KATIKA MIKOA 26 TANZANIA BARA

January 08, 2018
 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu 15 ya Wizara hiyo walioko katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatilia na kusimamia kikamilifu zoezi la upigaji chapa ambapo Dk Mashingo alisema mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa hadi kufikia Januari 31 mwaka huu haijulikani Serikali nini kuhusu mifugo hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria Mashingo akiwaonesha wafugaji sehemu sahihi ambayo ng’ombe anatakiwa kupigwa chapa ili kuepuka kuharibu ngozi baada ya kushiriki zoezi la upigaji chapa katika Kijiji cha Igalula wilayani Tanganyika mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu 15 iliyoundwa na Wizara hiyo kufuatiliaji na kusimamia upigaji chapa kabla ya Januari 30 mwaka huu
NA  MWANAHAMISI MSANGI, WMVU
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imeunda timu ya wataalamu 15 iliyopo katika mikoa 26 ya Tanzania bara ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Mifugo) Dk. Maria Mashingo kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa mifugo yote nchini kabla ya kufika tarehe ya mwisho ya muda wa nyongeza wa Januari 31 mwaka huu.
Timu hiyo ya wataalamu imeanza kutekeleza majukumu yake Januari 4 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Maria Mashingo wilaya 30 ambazo bado hazijaanza zoezi la chapa na zimetiliwa mkazo katika ufuatiliaji ikiwemo Monduli,  Kilwa, Liwale, Ruangwa, Mafia.
Aidha, Wilaya nyingine ni Sikonge, Tabora, Urambo, Mwanza, Ilemela Manispaa, Magu, Ukerewe, Buchosa, Tarime, Kyerwa, Ngara, Newala, Newala Mjini, Tandahimba, Nanyamba, Mtwara, Mikindani Manispaa, Masasi, Masasi Mjini, Nanyumbu, Moshi DC, Hai, Same, Rombo, na Kigamboni.
Dk.  Mashingo amesema suala la upigaji chapa mifugo lipo kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa mifugo Namba  12 ya Mwaka 2010 ili kudhibiti magonjwa ya mifugo pamoja  na wizi wa mifugo, kuimarisha usalama wa afya na mazao ya mifugo pamoja na kudhibiti usafirishaji na uhamaji holela wa mifugo.
Amesema jumla ya ng’ombe millioni 19, 219,487 sawa na theluthi mbili ya ng’ombe  wote milioni 28, 829,231 walioko nchini ambapo mpaka sasa jumla ya ng’ombe milioni 7, 701,661 sawa na asilimia 38.5 ndio wamepigwa chapa ambapo wamechangia kiasi cha shs. Bilioni 3, 700,830,500 kwa malipo ya Tsh 500 kwa kila ng’ombe.
Hivyo, Tathmini iliyofanyika kutokana na taarifa zilizokusanywa kutoka halmashauri zinaonesha kwamba, kati ya malengo waliojiwekea, Halmashauri 62 wamepiga chapa zaidi ya asilimia 50; Halmashauri 43 zimepiga kati ya asilimia 10 hadi 50; Halmashauri 23 zimepiga chini ya asilimia 10 na Halmashauri 30 hazijaanza lakini ziko kwenye maandalizi.
Ametaja baadhi ya changamoto zilizochangia kuathiri utekelezaji wa zoezi la chapa ni wafugaji kukataliwa kupiga chapa mifugo yao kwa kisingizio kuwa ni wavamizi na wahamiaji haramu katika Wilaya za Kibiti, Rufiji, Sumbawanga, Tanganyika, Kibondo.
Pia kutofautiana kwa gharama za uchangiaji ambapo baadhi ya wafugaji waliogomea kiwango cha sh 1000/= ambacho ni kinyume na kiwango elekezi cha sh 500/= kwa kila ng’ombe mfano katika Wilaya za Chunya na Tanganyika.
Vilevile fedha zilizochangwa kugharamia zoezi la chapa kutotolewa kwa wakati katika baadhi ya Halmshauri ikiwemo Mbarali na Misungwi hivyo kukwamisha utekelezaji wa kazi hiyo.
Timu hiyo ya watalaamu imegawanyika katika makundi saba kwenye mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Singida, Dodoma, Morogoro, Pwani, Dar es Salaam.
Mikoa mingine ni Tabora, Katavi,Rukwa, Kigoma, Shinyanga, Simiyu, Mara,Mwanza, Geita, Kagera, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara.