RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AZINDUA UJENZI WA HOTELI YA JAZ ARORA MICHAMVI ZANZIBAR

January 11, 2024




Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kulia akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi Uzinduzi wa Ujenzi wa Hoteli ya JAZ ARORA Michamvi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza jambo wakati akitembelea moja kati ya Vyumba vya Hoteli ya Jaz Arora katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Uzinduzi wa Ujenzi wa Hoteli hio Michamvi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.


- Advertisement -


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Jaz Arora Diego Torrado wakati akitembelea moja kati ya Vyumba vya Hoteli katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Uzinduzi wa Ujenzi wa Hoteli hio Michamvi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Viongozi mbalimbali akitembelea baadhi ya Sehemu za Hoteli ya Jaz Arora katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Uzinduzi wa Ujenzi wa Hoteli hio Michamvi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Viongozi mbalimbali akitembelea baadhi ya Sehemu za Hoteli ya Jaz Arora katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Uzinduzi wa Ujenzi wa Hoteli hio Michamvi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Uzinduzi wa Ujenzi wa Hoteli hio Michamvi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Muwekezaji wa Hoteli ya Jaz Arora Tawfiq El Kady akitoa maelezo ya Mradi katika hafla ya Uzinduzi wa Ujenzi wa Hoteli hio Michamvi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Mkurugenzi wa Mtendaji wa ZIPA Sharif Ali Sharif akitoa maelezo ya kitaalamu katika hafla ya Uzinduzi wa Ujenzi wa Hoteli hio Michamvi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Ujenzi wa Hoteli ya Jaz Arora Michamvi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Ujenzi wa Hoteli ya Jaz Arora Michamvi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR


WAZIRI MKUU MAJALIWA AIPONGEZA DCEA KWA UKAMATAJI MKUBWA WA DAWA ZA KULEVYA

January 11, 2024

 Dar es Salaam, Tanzania


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 10, 2024 amefanya ziara makao makuu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuipongeza Mamlaka hiyo kufuatia ukamataji wa dawa za kulevya zaidi ya Tani 3, zilizokamatwa Disemba, 2023.

Akizungumza na Maafisa wa DCEA, Waziri Majaliwa, amesema kuwa, Serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na mamlaka hiyo katika kupambana na dawa za kulevya, huku akidai kuwa, kukamatwa kwa dawa hizo ni ushindi mkubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya.

‘‘Nimekuja kuona mwenyewe zile dawa mlizokamata... lakini pia kuwapongeza kwa kazi nzuri mliyoifanya, mafanikio haya yanaanza kuleta sura ya kwamba Tanzania si mahali sahihi kwa kuzalisha, kusafirisha, kuuza na sio mahali pazuri kwa Matumizi ya Dawa za kulevya’’,amesema Majaliwa.

Pia amesema ameitaka kuendelea kufanya kazi kwa bidii, ili kuhakikisha kuwa dawa za kulevya zinatokomezwa nchini, huku akiahidi kuwa, Serikali itaendelea kuiwezesha mamlaka hiyo, ili iweze kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

"Nawaomba Mamlaka muendelee kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa dawa za kulevya zinatokomezwa nchini na sisi kama Serikali tutaendelea kuiwezesha mamlaka hii ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi,"ameongeza Majaliwa.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, amemshukuru Waziri Majaliwa na serikali kwa ujumla, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Mamlaka kufanikisha kazi zake.

‘‘Naomba kukushuru wewe Mhe. Waziri Mkuu kwa kuendelea kuisimamia mamlaka katika kutekeleza kazi zake vizuri chini ya maelekezo na maagizo yako, ambayo unayatoa mara kwa mara kupitia kwa wasaidizi wako na sisi kama watumishi tunahakikisha tunatekeleza maagizo yako kwa weledi na ufanisi mkubwa, ili kuhakikisha malengo ya Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana na kuwa salama", amesema Lyimo.

Disemba mwaka jana, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ilikamata dawa za kulevya zaidi ya tani 3 katika eneo la Kibada, Dar es Salaam, dawa hizo ni aina ya Heroin na Methamphetamine, ambapo kiwango cha dawa hizo za kulevya ni kikubwa ambacho hakiwaji kukamatwa nchini tangu shughuli za udhibiti zianze kufanyika.

KAMATI YA BUNGE YAIPA MBINU MIKOA KUDHIBITI MICHANGO SHULENI

January 11, 2024

 OR-TAMISEMI


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Denis Londo ametoa rai kwa mikoa yote nchini kuwa na mfano wa fomu maalumu ya wanafunzi kujiunga na masomo ya sekondari itakayodhibiti michango isiyo ya lazima.

Mhe. Londo ametoa rai hiyo kwenye ziara ya Kamati hiyo mkoani Iringa na kuonesha kufurahishwa na kile kinachofanyika katika mkoa huo kwa kuwa na fomu hiyo inayoonyesha kiwango cha mwisho cha michango kwa shule zote mkoani humo.

"Kipindi hiki cha kufungua shule na uandikishaji ukiwa unaendelea kuna baadhi ya maeneo kumekuwa na michango mingi na kila shule inajipangia na baadhi walimu wanashiriki kukiuka Sera na Miongozo ya Elimu hii si sawa ni vyema kila mkoa ukategeneza fomu maalumu kwa ajili ya kudhibiti michango,"amesema Mhe. Londo

Aidha, Kamati hiyo imetoa maelekezo mwanafunzi yeyote apokelewe na aingie darasani kama alivyo na asizuiliwe kusoma kutokana na kukosa michango wala sare ya shule na asome hadi hapo atakapoipata.

Naye,Mjumbe wa Kamati Mhe. Saashisha Mafue amesema hatua hiyo inasaidia wazazi wasibambikiwe michango mingi na kwamba jambo hilo ni la kuigwa.

Kamati hiyo imekamilisha ziara yake mkoani Iringa na kuelekea mbeya.





AGIZO LA RAIS SAMIA LATEKELEZWA,TANI 150,000 ZA KOROSHO ZASAFIRISHWA KUPITIA BANDARI YA MTWARA.

January 11, 2024

 Tani 150,000 za Korosho ghafi zimesafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutumika kikamilifu kwa Bandari hiyo kusafirisha korosho zote ghafi zinazolimwa Katika Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania( TPA) Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Ferdinand Nyathi amesema tangu kuanza kwa msimu wa korosho Bandari hiyo imehudumia Meli zaidi ya 18 za makasha, Meli tatu zikiwa zimeleta makasha matupu na Meli 15 zimesafirisha Korosho ghafi.

“ Mpaka sasa tumeshasafirisha tani laki moja na nusu na mpaka mwishoni mwa Januari tutakuwa tumeshasafirisha tani laki mbili. Tunakushukuru sana Serikali kwa maelekezo yake ambayo yameongeza ufanisi wa Bandari.” Amesema Nyathi.

Aidha amewashukuru Wadau wa Bandari na kampuni ambazo ziliamua kuwekeza katika Bandari hiyo ikiwamo Kampuni ya kuhudumia Makasha ya CMA na kampuni ya Meli ya Mediteranian Shipping kwa kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha usafirishaji wa korosho ghafi.







TANESCO YASHIRIKI MAONESHO YA 10 YA KIMATAIFA YA BIASHARA ZANZIBAR

January 11, 2024


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeshiriki kwenye maonesho ya 10 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar.

Maonesho hayo yamezinduliwa Januari 10, 2024 na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi, ambapo alizipongeza Taasisi zote ziizoshiriki katika maonesho hayo.

Ushiriki wa TANESCO katika maonesho hayo ni kupata nafasi ya kukutana na wadau , ikiwemo wawekezaji pamoja na fursa za kibiashara ambapo sambamba na kutoa huduma bora za Umeme , TANESCO pia imejipanga kujiendesha kibiashara.

Maonesho hayo yana washiriki zaidi ya 500 na yamebeba kauli mbiu isemayo "Biashara mtandao kwa maendeleo ya Biashara na Uwekezaji"

TANESCO inawakaribisha wakazi wote wa Zanzibar, Pemba na maeneo jirani katika banda lao la maonesho lililopo katika viwanja vya Fumba, Zanzibar kuanzia tarehe 7-19, Januari 2024 ili kujifunza miradi ya kimkakati inayoendelea, fursa za uwekezaji kwenye miradi ya umeme na huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)

PSSSF YAUNGANA NA WADAU WA MICHEZO KUCHANGIA TIMU ZA TAIFA

January 11, 2024


MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeungana na wadau wa michezo nchini, kuchangia timu za taifa za Tanzania zinazoshiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Taifa Stars, ambayo inashiriki michuano ya AFCON 2023, inayotarajiwa kuanza Januari 13, 2024 nchini Ivory Coast.

Katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya timu hizo, iliyoongozwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, kwenye hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Januari 11, 2024, PSSSF imenunua kupitia mnada, jezi ya marehemu Joel Bendera kwa shilingi milioni 11.

Marehemu Bendera alikuwa kocha mzalendo wa kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki AFCON kwa mara ya kwanza mwaka 1980.

Pichani, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto), akikabidhi jezi hiyo, kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian Luhemeja (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (watatu kushoto) na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama PSSSF, James Mlowe.