MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA

MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA

February 01, 2016

1
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwasili Bungeni katika kuanza kikoa cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
3
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza sala ya kuliombea Bunge kabala ya kuanza kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
4
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji akiwasilisha hoja ya Serikali kuhusu Mpango wa Maendeleo mwa mwaka mmoja katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Yussuf Massauni akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
6
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
7
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
8
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbalawa wakati kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
9
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelline Mabula akijibu hoja toka kwa wabunge katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
10
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.nape Moses Nnauye akijadiliana jambo na Waziri wa NChi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe January Makamba wakati kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
11 12
Baadhi ya wabunge wakifatila kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

UMOJA WA WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE YA HEGONGO,MUHEZA WAANGUSHA PARTY LA NGUVU DAR

February 01, 2016
 Wanafunzi waliowahi kusoma miaka ya 80 katika Shule ya Sekondari ya Hegongo, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, wakicheza muziki wakati wa hafla yao ya kukumbukana iliyofanyika kwenye Mgahawa wa City Sports Lounge, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Martine Jengo (kulia) na Mzee Hassan wakiserebuka
 Mmiliki wa TSN Group, Farouq Baghoza (kulia), ambaye pia alisoma katika shule hiyo, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kumbukumbu.


 Mmiliki TSN Group,  Farouq Baghoza (kulia) akiwa na wanafunzi aliosoma nao katika shule ya Hegongo,  Mkurugenzi wa Mgahawa wa City Sports Lounge, Benny Kisaka (kushoto) pamoja na Gerald Yambi ambaye ni mwanachama maarufu Kundi la  Friends of Simba. Baghoza aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa Saidia Taifa Stars Ishinde.
 Sasa ni wakati wa mlo




 Mwanafunzi Edwin Pemba (kushoto) akiwa na Mwalimu John Sebo (katikati) aliyewahi fundisha katika Shule ye Sekondari ya Hegongo.
 Aliyewahi kuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Hegongo, John Sebo akishukuru kualikwa na waliokuwa wanafunzi wake katika hafla hiyo muhimu.Kulia ni Mwanafunzi Benny Kisaka ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa Mgahawa wa City Sports Lounge.

 Hawa walimaliza Kidato cha Nne katika shule hiyo 1985.
 Hawa walisoma katika shule hiyo na kumaliza Kidato cha Nne miaka ya tisini

MKURUGENZI MKUU WA TUME YA USHINDANI AKABIDHI VIFAA VYA MUZIKI KWA JESHI LA MAGEREZA

MKURUGENZI MKUU WA TUME YA USHINDANI AKABIDHI VIFAA VYA MUZIKI KWA JESHI LA MAGEREZA

February 01, 2016

1
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akitoa maelezo mafupi kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya muziki kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza. Hafla hiyo ilifanyikia Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Jijini Dar es salaam, Januari 29, 2016.
2
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja gitaa la muziki ikiwa ni moja wapo ya vifaa vya muziki vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza.
3
Kamishna Jenerali wa Magereza akijaribisha kupiga gitaa la muziki baada ya kukabidhiwa vifaa vya muziki katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo(wa kwanza kulia).
4
Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya muziki ambavyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi la Magereza.
5
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Dkt. Fredrick Ringo(hayupo pichani).
6
Baadhi ya vifaa vya muziki venye vilivyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza kama vinavyoonekana katika picha. Vifaa hivyo vitatumika kukuza vipaji vya Wanamuziki wa Jeshi hilo(Picha na Kitengo cha Habari, Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).
BALOZI SIMBA AWAPONGEZA WAOKOAJI AJALI YA MV KILOMBERO

BALOZI SIMBA AWAPONGEZA WAOKOAJI AJALI YA MV KILOMBERO

February 01, 2016

1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati) pamoja na ujumbe wake, wakiingia katika lango kuu la kuingilia abiria wakati alipotembelea eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero II na kushuhudia shughuli za uokoaji wa magari, utafutaji miili ya watu na uokoaji wa kivuko hicho ukiendelea. Balozi Simba alifanya ziara ya kikazi mkoani Morogoro kwa kutembelea miradi ya maendeleo ya Jeshi la Magereza mkoani humo.
2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akisalimiana na Askari wa Kikosi cha Wanamaji wa Uokoaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao wanashiriki katika shughuli za uokoaji miili ya watu waliozama baada ya kivuko cha MV Kilombero II kuzama Januari 27.
3
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akiongozana na ujumbe wake kuelekea eneo la tukio ambapo kivuko cha MV Kilombero II kilizama wiki iliyopita. Kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa. Katikati ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, SACP Dkt. Kato Lugainunura.
4
Katibu Tawala Wilaya ya Kilombero, Yahya Naniya (kulia), akitoa maelezo juu ya shughuli za uokoaji zinavyoendelea kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wa tatu kushoto) na ujumbe aliofuatana nao mara baada ya kufika eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero II wiki iliyopita. Naibu Katibu Mkuu alikuwa mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki kwa ziara ya kikazi.
5
Wasamaria wema waliojitolea kushiriki zoezi la uokoaji katika ajali ya kivuko cha MV Kilombero II kilichotokea wiki iliyopita mkoani Morogoro, wakimuelekeza dereva wa gari la kunyanyua vitu vizito (halipo pichani), wakati wa uokoaji wa moja ya magari yaliyozama wakati wa ajali hiyo.
6
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) na ujumbe aliofuatana nao wakiangalia shughuli za uokoaji zinavyoendelea mara baada ya kivuko cha MV Kilombero kuzama huku baadhi ya vitu vikiokolewa.
7
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akiondoka eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero mara baada ya kushuhudia shughuli za uokoaji zikiendelea vizuri.
(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
TFF YAIPONGEZA RUVU SHOOTING

TFF YAIPONGEZA RUVU SHOOTING

February 01, 2016

malinziArst 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake, Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Ruvu Shooting kwa kufanikiwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.
Malinzi ametuma salamu hizo kwa Mwenyekiti wa klabu ya Ruvu Shooting, Col. Charles Mbuge, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji na kuwataka kujipanga kwa maandalizi ya nguvu msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Ruvu Shooting imekua timu ya kwanza kupanda ligi kuu msimu huu baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa na kufikisha alama 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutoka katika hilo la B.
Washindi wawili kutoka maundi ya A, na B wataungana na Ruvu Shooting kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao huku timu zote zikiwa zimebakiza michezo miwili miwili kabla ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza msimu huu.
SERIKALI YAPANGA KUFANYA MATUMIZI YENYE TIJA

SERIKALI YAPANGA KUFANYA MATUMIZI YENYE TIJA

February 01, 2016

index 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango akiwasilisha mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.katika kikao cha Tano cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 imejipanga kufanya matumizi yeneye tija kwa kuelekeza bajeti kubwa kwenye mambo muhimu hasa sekta zenye za kutoa huduma na zile zenye kuleta maendeleo ya nchi moja kwa moja.
Akiwasilisha mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Phillip Mpango amesema mwongozo wa mpango na bajeti umezingatia mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/2017 pamoja na kuzingatia sera za uchumi na hadi sasa sera za bajeti kwa mwaka 2016/2017 zinaonesha jumla ya shilling trillion 22.9 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika kipindi hiki.
“ Kati ya mapato hayo,serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla ya shillingi trillion 14.1 sawa na ongezeko la asilimia 14.1 ikilinganishwa na makadirio ya mwaka 20015/2016, na kwa mapato yasisiyo ya kodi na mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri ni shilling trillion 1.1.
“ katika mwaka wa fedha 2016/2017,Serikali tunatarajia kukusanya jumla ya shilling trilllioni 14.1 kutoka kwenye vyanzo vya kodi ,sawa na asilimia 13.2 ya pato la taifa hii ni sawa na ongezeko la asilimia 14 ukilinganisha na matarajio ya kukusanya jumla ya shilling trillion 12.3 kwa mwaka wa fedha 2015/2016” Alisema Mhe. Mpango.
Mhe Philip Mpango amesema mapato yote yatakusanywa na Wizara ya Fedha na Mipango, hivyo basi maafisa,Masuuli,wa Wizara,idara za serikali,Wakala,Taasisi,Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa watatakiwa kuwasilisha mapato yote yatakayokusanywa na kuwasilisha kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali na yatagawiwa kulingana na bajeti iliyoidhinishwa. \ Aidha amesema Serikali itahakikisha Mashirika ya Umma yaliyoundwa kwa lengo la kujiendesha kibiashara yanajiendesha kwa faida bila ya kutegemea ruzuku ya Serikali, na ameyataja baadhi ya mashirika hayo kuwa ni Shirika la Umeme(TANESCO),Shirika la Reli ya Tanzania Zambia (TAZARA), Shirika la Reli ya Kati (TRL), Shirika la Ndege (ATCL),Wakala wa Vipimo (WMA), Bodi ya Mazao, na mashirika mengine.
Serikali itahakikisha kuwa inahimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuelekeza matumizi kwenye maeneo yenye tija kwa manufaa ya watanzania wote.
BALOZI WA SWEDEN AMTEMBELEA SPIKA OFISINI KWAKE

BALOZI WA SWEDEN AMTEMBELEA SPIKA OFISINI KWAKE

February 01, 2016

1 
Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt akisaini kitabu cha Wageni alipomtembelea leo ofisini kwake tarehe 01 Febuari, 2016 Mjini Dodoma. Kulia kwake ni Afisa wa Ubalozi wa Sweden Bw. Ludvig Bontell.
3 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnittaliyemtembelea leo Ofisni kwake Mjini Dodoma
4 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifanunua jambo wakati akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt. Wengine katika picha ni maafisa wa Ubalozi wa Sweden na Wabunge.
5 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pmoja na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt na Maafisa wengine wa Ubalozi wa Sweden na wa Bunge
6 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiaagana na Balozi wa Sweden Nchini Bi. Katarina Rangnitt mara baada ya kuzungumza anye ofisini kwake. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Sweden Bw. Ludvig Bontell.
9 
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Bw Neville Meena akifafanua jambo kwa Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah wakati alipomtembele Ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo. Kuli kwa Spika ni Naibu Katibu wa Bunge-Shughuli za Bunge Bw. John Joel.Wengine katika picha ni Viongozi wa Jukwaa la Wahiri na Maafisa wa Bunge.
(Picha na Ofisi ya Bunge)
 MALINZI AMPONGEZA MAKUNGA

MALINZI AMPONGEZA MAKUNGA

February 01, 2016
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Theophil Makunga kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) mwishoni mwa wiki.
Katika salamu hizo, Malinzi amempongeza Makunga kwa nafasi hiyo aliochaguliwa na kusema imani waliyonayo wahariri wenzake juu ya utendaji wake wa kazi ndio kumepelekea wao kumchagua kuongoza jukwa hilo.
Aidha Malinzi amewapongeza Deodatus Balile aliyechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na Neville Meena aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa jukwaa hilo na kuahidi kuwa TFF itaendelea kushirikiana nao.