Wanadiaspora watakiwa kuekeza nyumbani

Wanadiaspora watakiwa kuekeza nyumbani

May 01, 2016
Nembo ya ZADIA
Na Mwandishi wetu Washington 
Wazanzibari waishio nchi za nje wametakiwa kuwekeza nyumbani kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya taifa.
Wito huo ulitolewa jana na maofisa kutoka Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zaznzibar (ZSSF) wakati wakizungumza na Wazanzibari waishio nchini Marekani.
Akizungumza kwenye mkutano huo uliondaliwa na Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA), Meneja wa Mipango na Uwekezaji kutoka ZSSF Bwana Khalifa Muumin Hilal alisema kuwa Taasisi yake ina miradi kadhaa ya uwekezaji inayoendeshwa kwa ushirikiano na Benki ya Watu wa Zanzibar, na kwamba inawahamasisha Wazanzibari waishio Ughaibuni kuwekeza katika miradi hiyo.
Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa nyumba za kisasa katika eneo la Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar ambao ujenzi wake tayari umeanza na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu.
Bwana Hilal alifafanua kuwa eneo hilo litakuwa na majengo ya nyumba za kuishi yenye urefu wa ghorofa saba, ambapo kila ghorofa itakuwa na nyumba mbili.
"Kutakuwa na nyumba za vyumba viwili, vitatu na vinne" alifafanua Meneja Hilal, na kuongeza kuwa nyumba hizo zitapatikana kwa bei nafuu.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ATUNUKU VYETI KWA WASHIRIKI WA KAMPENI YA SIKU 10 YA USAFI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO (KINAPA)

May 01, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akitoa vyeti kwa wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zilizosaidia katika kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Zoezi la utoaji Vyeti limefanyika katika lango la Marangu wakati wa hafla fupi ya kuwapokea washiriki wa zoezi hilo la usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza na washiriki wa kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) muda mfupi mara baada ya kurejea. 
Baadhi ya Washiriki wa Kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadicky alipokuwa mgeni rasmi katika Hafla ya kutunuku vyeti kwa washiriki pamoja na wamiliki wa kampuni.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza katika Hafla hiyo.
Baadhi ya Washiriki wa zoezi hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Siha ,Dkt Charles Mlingwa akizungumza katika hafla hiyo baada ya kukaribishwa huku akiwasilisha ombi la zoezi kama hilo la usafi lielekezwe katika lango la kupandia mlima la Londros lilopo wilayani Siha.
Baadhi ya Washiriki wa zoezi hilo ambao wanajulikana kama Wagumu.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Mtango Mtahiko akizungumza juu ya mafanikio ya kampeni ya siku 10 ya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Mhandisi Aisha Amour akifuatilia shughuli hiyo ya kutunuku vyeti ilivyokuwa ikiendelea .
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Betrita Loibook akizungumza katika hafla hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)Betrita Loibook akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akiliongoza kundi la watu waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kufanya usafi muda mfupi baada ya kurejea kutoka katika kilele cha mlima huo.
Baadhi ya washiriki wa zoezi hilo.
Washiriki wa zoezi la usafi katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick huku wakionesha vyeti walivyotunukiwa baada ya kufanikisha zoezi hilo.
Washiriki wakifurahia vyeti.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza jambo na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
DK. SHEIN AONGOZA SIKU YA KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI ZANZIBAR

DK. SHEIN AONGOZA SIKU YA KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI ZANZIBAR

May 01, 2016

ds1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi,  wakipita mbele yake wakati wa sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
ds2 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi,(pichani) Vijana waliobeba bango kutoka Ofisi ya Makamo wa Pili ya Rais akipita mbele yake wakati wa sherehe za sikuya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
ds3 
Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika  Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,[Picha na Ikulu.]
ds4 
Baadhi ya Vingozi na Wafanyakazi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika  Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,[Picha na Ikulu.]
ds5 
Baadhi ya Vingozi na Wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika  Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo mgeni rasmin akiwa Baadhi ya Vingozi na Wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika  Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,[Picha na Ikulu.]
ds6 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wakinyanyua mikono juu kuashiria Mshikamano wakati wa sherehe za kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani,ambazo sherehe zimewajumuisha  mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi katika  Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
ds7 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi zawadi Musssa Yussuf wa ZSSF Laki Sitafedha taslim  akiwa mfanyakazi Bora Chama cha ZAFICOWV katika sherehe za Siku ya wafanyakazi Duniani Zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
ds8 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi zawadi Bi.Asya Rajab Said fedha taslim laki tano,kutoka Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  akiwa mfanyakazi Bora Chama cha ZUPHE katika sherehe za Siku ya wafanyakazi Duniani Zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
ds9 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi pamoja na Wananchi wakati wa Kilele cha siku ya Wafayakazi Duniani sherehe zilizofanyika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF) WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI KWA MARA YA KWANZA

May 01, 2016

 Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki matembezi ya kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani  (May day), hapa matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1, 2016.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MFUKO wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) kwa mara ya kwanza umeshiriki kwenye matembezi ya kusherehekea siku ya Wafanyakazi, maarufu kama MAY DAY jijini Dar es Salaam leo Mei 1, 2016.
Matembezi hayo yaliyoshirikisha wafanyakazi kutoka sekta ya Umma na Binafsi, ambazo ndio wadau wakubwa wa Mfuko huo, yalianzia kwenye ofisi za Shirikisho la Vyamavya Wafanyakazi, TUCTA, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kupita barabara ya Nkurumah, Nyerere na kisha kupinda barabara ya Chang’ombe hadi uwanja wa Uhuru ambako yalipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda.
WCF ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Bunge ya Fidia kwa wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008 ukiwa na wajibu wa kutoa Mafao ya Fidia kwa mfanyakazi apatwapo na madhara mahala pa kazi.
Tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo, juhudi za kutangaza hudumazake kwa wadau zimekuwa zikiendelea mfululizokwa kutoa elimu kupitia semina, maonyeshona makongamano lakini pia kupitia vyombo vyahabari na kwa siku ya Mei Day imekuwa ni fursa kubwa ya WCF kuungana na wadau wake wakubwa.
 Wafanyakazi wa WCF wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuruwakati wa matembezi ya kilele chasiku ya wafanyakazi Duniani
 Matembezi yakiwa yameingia Uwanja wa Uhuru

Vyama Vya Siasa Vimekutana Kujadili Mapendekezo ya Mfumo Wa Utatuzi wa Migogoro Ndani na Baina ya Vyama

May 01, 2016

Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini ambalo linaundwa na  wawakilishi wawili kutoka kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu wamekutana mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa GEPF uliopo Victoria Jijini Dar es salam kujadili mapendekezo ya mfumo wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama vya siasa .

Mapendekezo hayo yalitolewa na Mtaalamu wa utatuzi wa Migogoro Bw. Ghalib Galant ambaye awali alifanya utafiti wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama  vya siasa  nchini chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa  na kwa udhamini  wa UNDP  kupitia mradi wake wa “Democratic Project” ukiwa na lengo la kuiboresha sura namba 258 ya Sheria ya Vyama vya Siasa  ya mwaka 1992 ili kuendana na mahitaji ya ukuaji wa demokrasia nchini. Utafiti huo ulishirikisha wadau mbalimbali wa demokrasia ya vyama vingi nchini vikiwemo vyama vya siasa.

Akiwasilisha mapendekezo, Msajili Msaidizi Bi. Piencia C. Kiure ,alisema kuwa  ilipendekezwa kuwa Sheria ya Vyama vya Siasa nchini iweke masharti yanayohusu utaratibu  wa kutatua migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa “ migogoro  ndani ya chama ni lazima ishughulikiwe kwanza ndani ya chama cha siasa  na kufikia tamati kwa mfumo wa utatuzi wa migogoro uliowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama, kabla ya kuwasilishwa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa  kwa ajili ya upatanishi” ilikaririwa  sehemu ya mapendekezo

“Upatanishi ukishindikana mgogoro husika uwasilishwe kwenye Baraza  la Uamuzi la Migogoro ya Vyama vya Siasa kwa uamuzi. Ikiwa muhusika wa mgogoro asiporidhika na uamuzi wa Baraza  la Uamuzi wa migogoro ya vyama vya siasa atawasilisha mgogoro husika Mahakama Kuu mbele ya Majaji watatu kwa mapitio ya uamuzi wa Baraza. Muhusika asiporidhika  na uamuzi wa Mahakama Kuu, atakata  rufaa Mahakama ya Rufaa” ilifafanua sehemu ya Mapendekezo.

Aidha kumekuwa na msisitizo wa kufuata mtiririko wa hatua katika utatuzi wa migogoro kama ilivyobainishwa hapo juu ili kuepusha migogoro ndani ya vyama  kwenda moja kwa moja  Mahakamani ambako huchukua muda mrefu  na kuathiri ukuaji wa demockaria ndani na nje ya vyama vya siasa hapa nchini.

Wakichangia katika mjadala huo, baadhi ya wajumbe walikubaliana na hoja kuwa  vyama vya siasa vitatue kwanza migogoro yake ndani ya vyama na kwamba pale tu itakaposhindikana ndipo ipelekwe kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Wajumbe walishindwa kukubaliana katika  hoja ya uwepo wa Baraza la Uamuzi  wa Migogoro ya vyama vya siasa, wapo walioona haja ya uwepo wake  na wapo walipendekeza kuwa majukumu ya Baraza hilo yafanywe na Baraza la Vyama vya siasa lililopo sasa jambo lililosababisha kutokukubaliana katika hoja hiyo.

Pamoja na michango iliyotolewa , Wajumbe wameishauri Serikali kuona umuhimu wa kuwekeza katika Baraza la Vyama vya Siasa  ili kusaidia utatuzi wa migogoro nchini kwa kuwa imebainika kuwa machafuko katika nchi nyingi duniani yamesababishwa na machafuko katika masuala ya siasa.

Akihitaji ufafanuzi wa  hatua gani imefikiwa katika uboreshaji wa Sheria ya Vyama vya siasa, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa, Mhe. Peter Kugar Mziray aliiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa  kutoa ufafanuzi. 

Naye Msajili Msaidizi, Bw. Sisty Nyahoza akitoa ufafanuzi alisema tayari vyama vyote vya siasa vimeshapelekewa barua vikiombwa kuwasilisha mapendekezo kwa ajili ya kuboresha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na kwamba Ofisi inafanya jitihada za kupokea mapendekezo kutoka kwa wadau wa siasa na ikishakamilisha upokeaji huo, mapendekezo hayo yatawasilishwa kwenye kamati ya Katiba na Sheria.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Peter Kuga Mziray akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam . Kulia ni Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa na Mhe. Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti wa Baraza.
Msajili Msaidizi (Elimu kwa umma na Gharama za uchaguzi) Bi. Piencia C. Kiure akiwasilisha mada ya Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa katika baraza la Vyama vya Siasa lilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.

Bw. John Cheyo mmoja wa wajumbe wa Baraza la vyama vya siasa akichangia hoja wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Baraza la vyama vya Siasa baada ya kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
WAFANYAKAZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI MKOA WA DAR ES SALAAM.

WAFANYAKAZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI MKOA WA DAR ES SALAAM.

May 01, 2016

index 
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakiwa katika maandamano wakipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (hayupo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Mafoto Blog
index1
Bunge lapitisha Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora 2016/2017

Bunge lapitisha Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora 2016/2017

May 01, 2016

J1 
Naibu Waziri wa nchini, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiingia ukumbi wa Bunge siku ya kupitishwa bajeti ya Wizara hiyo mwishoni wa wiki mjini Dodoma.
J2 
Waziri wa nchini, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akitoa hoja ili Bunge liidhinishe na kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Wizara hiyo mjini Dodoma.
J3 
Naibu Waziri wa nchini, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akijibu hoja zilizoelekezwa na Wabunge kwenye Wizara hiyo kabla Bunge kuidhinisha na kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 mwishoni wa wiki mjini Dodoma.
J4 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angellah Kairuki akitoa hoja ili Bunge liidhinishe na kupitisha bajeti ya Wizara hiyo ya mwaka 2016/2017 mwishoni wa wiki mjini Dodoma.
J5 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu fedha za Serikali wakati wa kupitisha bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora ya mwaka 2016/2017 mwishoni wa wiki mjini Dodoma.
J6 
Wabunge wakiendelea na kikao cha Bunge cha bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora ya mwaka 2016/2017 mwishoni wa wiki mjini Dodoma.
Waziri Mhagama atoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014

Waziri Mhagama atoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014

May 01, 2016

G1 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (kushoto) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 na jinsi dawa hizo zinavyoathiri afya na nguvu kazi ya taifa. Kulia ni Mfamasia Sehemu Elimu, Habari na Takwimu Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya nchini Amani Masami.
G2 
Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)