KIKAO CHA BARAZA KUU UWT TAIFA CHAFANYIKA KWA KISHINDO MJINI DODOMA

October 17, 2017
 Katibu Mkuu wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Idara ya Oganaizesheni Pereila Silima wakiwasili ukumbini tayari kwa ajili ya kusimamia Kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyo ngazi ya Taifa, kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017. 
 Wajumbe na waalikwa wakishangilia baada ya viongozi wa meza kuu kuwasili ukumbini kuanza Kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyo ngazi ya Taifa, kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017. 
 Wajumbe na waalikwa wakishangilia baada ya viongozi wa meza kuu kuwasili ukumbini kuanza Kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyo ngazi ya Taifa, kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017.
 Wajumbe na waalikwa wakishangilia baada ya viongozi wa meza kuu kuwasili ukumbini kuanza Kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyo ngazi ya Taifa, kilichofanyika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Oktoba17, 2017.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) na Katibu wa NEC Oganaizesheni Pereila Silima wakifurahi baada ya kuwasili ukumbini
 Katibu Mkuu wa UWT Amina Makilagi akitoa maelezo ya awali kuanza kikao hicho
 "kikao hiki tutakiendesha kwa mujibu wa Katiba yetu hii ya UWT..." anafafanua Amina Makilagi
 Makilagi akitangazia wajumbea kumchagua Mwenyekiti wa muda wa kuendesha kikao hicho. Mwenyekiti wa muda ilibidi achaguliwe kutokana na aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Taifa Sophia Simba, kuvuliwa uongozi kutokana na kupatikana na hatia ya kuisaliti CCM wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita.
 Wajumbea wakipiga kura za kunyoosha mikono kuchagua Mwenyekiti wa muda wa kikao hicho
 Wajumbea wakipiga kura za kunyoosha mikono kuchagua Mwenyekiti wa muda wa kikao hicho ambapo walimchagua Diana Chilolo kutoka Singida
 Diana Chilolo akienda meza kuu
 Katibu Mkuu wa UWT Amina Makilagi akiwa amesimama kumlaki meza kuu Diana Chilolo
 Diana Chilolo akikaribishwa meza kuu
 Katibu wa NEC Oganaizesheni Pereila Silima (kushoto) akiwa amesimama baada ya kutambulishwa kwa wajumbe na Katibu Mkuu wa UWT Amina Makilagi (kulia), Utambulisho huo ulifanyika baada ya Mweneyekiti wa muda wa kikao hcho Dina Chilolo (katikati) kuketi.
SERIKALI YALIPA MADENI YA NDANI BILIONI 190 KATIKA KIPINDI KIFUPI

SERIKALI YALIPA MADENI YA NDANI BILIONI 190 KATIKA KIPINDI KIFUPI

October 17, 2017
IMG_1275
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akisalimiana na badhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera alipowasili katika Ofisi hiyo ili kuzungumza na  watumishi wa Mamlaka hiyo.
IMG_1280
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera kuhusu masuala ya kiutendaji alipofanya ziara ya kikazi katika  Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani humo.
IMG_1290
Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Kagera, Bw. Adam Ntoga, akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani Kagera.
IMG_1338
Baadhi ya Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia kuhusu uadilifu katika kazi na utoaji wa elimu kwa mlipakodi baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara ya kikazi katika Ofisi hiyo.
IMG_1345
Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera, alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa huo ambapo amewaasa kuwa waadilifu katika kazi zao.

WAZIRI WA MALIASILI DKT.KIGWANGALLA ATEMBELEA MELI YA MFALME WA OMAN

October 17, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema  Tanzania na Nchi ya Oman wamefanya mazungumzo ya pamoja ya namna ya kukuza sekta ya Utalii baina ya nchi hizo mbili ambapo watashirikiana katika muingiliano wa Watalii watakaokuwa wakitokea moja kwa moja Oman na kuja Tanzania.
“Tumeweza kuzungumzia ushirikiano wa sekta ya Utalii. Hii ni pamoja na kuanzisha soko la pamoja  kati ya Oman na Tanzania. Watalii wanaokwenda Oman wanaotaka kuja nchi za Afrika basi waunganishwe moja kwa moja kutoka Oman na kuja Tanzania kwani wenzetu wana watalii wengi kuliko sisi. Hivyo ujio wao hapa nchini ni faida kubwa kabisa na tumejifunza mengi katika sekta hii.
Pia tumeweza kujifunza namna wenzetu wanavyoitangaza nchi yao  na sisi tutatumia uzoefu huo kuboresha sekta hii ya Utalii kama dhamana tuliyopewa” alieleza Dk. Kigwangalla.
Awali Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ iliyofika mapema jana Jijini Dar e Salaam ikiwa katika msafara wa kitaifa kati ya Serikali ya Oman na Tanzania.
Aidha, katika tukio hilo Mh. Waziri DK. Kigwangalla aliweza kuungana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu Hassan katika chakula cha mchana ndani ya Meli hiyo ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said  ijulinakanyo kama ‘Fulk Al Salamah’.
Meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ ipo nchini hadi Oktoba 21.2017. ambapo ipo nchini kusambaza ujumbe wa ‘Amani na upendo’ duniani ambapo  ikitoka Tanzania  inatarajia kuelekea Mombasa Kenya kwa madhumuni hayo hayo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Bi.Maitha bint Saif Al Mahrouqi wakati Dk. Kigwangalla alipotembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman iliyopo nchini.

Moja ya alama za kuvutia za Taifa la Oman

Moja ya usafiri unatumika katika nyanja za Utalii nchini Oman

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dkt.Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Bi.Maitha bint Saif Al Mahrouqi wakati Dk. Kigwangalla alipotembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman iliyopo nchini.

Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Bi.Maitha bint Saif Al Mahrouqi akitoa maelezo kwa Waziri wa Maliasili Dk. Kigwangalla alipotembelea meli hiyo ya kifahari ya Mfalme wa Oman iliyopo nchini.

Wadau wakutana Jijini Mwanza kujadili changamoto za uchumi

October 17, 2017
Makamu wa Rais wa TCCIA, Joseph Kahungwa akizungumza kwenye majadiliano hayo.
 Binagi Media Group
Mafunzo ya majadiliano yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA mkoa wa Mwanza, yametamatika hii leo Jijini Mwanza.

Majadiliano hayo yalianza jana Oktoba 16,2017 kwa kuwahusisha wadau wa sekta za umma na binafsi ili kujadili changamoto za kiuchumi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.

Tunaye Makamu wa Rais wa TCCIA nchoni ambapo anazungumzia majadiliano hayo kwa kina.
Mwenyekiti wa TCCIA, Elibariki Mmari akizungumza wakati wa majadiliano hayo
Mwenyekiti wa TCCIA, Elibariki Mmari (kushoto) akizungumza wakati wa majadiliano hayo. 

MAHAKAMA YATOA AMRI NG’OMBE WALIOTAIFISHWA KUPIGWA MNADA

October 17, 2017


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina katikati, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Aaron Mbogho, kushoto kwake  katibu tawala wa wilaya ya Mwanga Bw. Yusuph  Kasuka wakiangalia ng'ombe waliotaifishwa  wakati wakinywa maji katika kijiji cha Mgagau wilayani Mwanga.


Waziri Mpina , Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Maria Mashingo na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Aaron Mbogho wakijadili jambo baada ya kuongea na wanahabari kuhusu amri ya mahakama ya kupiga mnada ngombe walitaifishwa na Serikali.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina katikati, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Aaron Mbogho, kushoto kwake  katibu tawala wa wilaya ya Mwanga Bw. Yusuph  Kasuka wakiangalia ng'ombe waliotaifishwa  wakati wakinywa maji katika kijiji cha Mgagau wilayani Mwanga.


Ng’ombe walioamriwa na mahakama kupigwa mnada, mnada utapigwa siku ya ijumaa.






                NA MWANDISHI MAALUM - MWANGA

NG’OMBE waliotaifishwa na serikali katika wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, wamatarjiwa kupigwa mnada kufuatia uamuzi wa mahakama.
 Hayo yameelezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, wakati alipokwenda kukagua lindo la ng’ombe hao, jana eneo la Mgagao, wilayani Mwanga, walikohifadhiwa.

“Kufuatia uamuzi wa mahakama, ng’ombe hawa watauzwa kwa njia ya mnada siku ya Ijumaa, Oktoba 20, mwaka huu, kutokana na hali za ng’ombe hawa kutokuwa nzuri”, alisema.

Aliongeza, “Tayari mahakama imeridhia ombi la serikali la kutoka kuuzwa kwa ng’mbe hawa na ishamteua dalali wa kufanya mnada huo ambaye ni Marepelanto ya mjini Moshi na kazi hii itafanywa haraka kutokana na ng’ombe wengine kuanza kufa, kama mlivyosikia tayari sita wameshakufa”.

Aidha alisema serikali itaanza operesheni maalum ya kuwakamata ng’ombe walioingizwa nchini kinyume cha sehria kuanzia Jumatatu ijayo.

“Baada ya operesheni ya hapa Kilimanjaro, nilitoa siku saba kwa Mikoa mingine kuiondoa mifugo iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria kupitia Mikoa hiyo, muda huo umekwisha, Jumatatu tunaanza ingine itakayochukua siku 15 ili kuhakikisha mifugo hiyo inaondolewa yote”, alisema.

Akijibu maswali kutoka kwa baadhi ya viongozi wa eneo hilo, Bw. Mpina alisema kuwa iwapo kuna mifugo ya wenyeji ilikamatwa wakati wa operesheni hiyo wapeleke orodha ya wenye ng’ombe hao kwa kupitia ngazi husika ili waweze kurudishiwa.

“Wenyeji wenye ng’ombe waliokamatwa watumie taratibu kuzifuatilia kwa kuanzia kwa viongozi wa maeneo wanayotoka hadi ngazi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ikidhibitishwa bila mashaka mifugo hiyo ni ya kwao zitatumika taratibu zinazohitajika kisheria kwa kuwa ng’ombe hizi sasa ni mali ya serikali”, alisema.

Aidha alitoa onyo kwa viongozi hao kuhakikisha wanafanya zoezi hilo kwa weledi na kwamba iwapo watafanya udanganyifu hatua kali za kisheria zitachuliwa dhidi yao bila kujali nyadhifa zao.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo, aliyeiongoza operesheni hiyo, alisema kuwa mwendelezo wa operesheni hiyo umepelekea serikali kukamata ng’ome wengine takribani 2,000.

“Tunawashukuru Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kutupatia ndege ambayo ilitusaidia sana katika zoezi hili tulilofanya kupitia vyombo vya ardhini na angani”, alisema.

Alisema kuwa amebaini ya kuwa wizara ya Mifugo na Uvuvi ina changamoto ya uhitaji wa vifaa kama ndege kwani operesheni hiyo imebainisha wazi uhitaji huo.

Awali akitoa rai yake kwa niaba ya wafugaji wenyeji ambao ng’ombe zao zimekamatwa kufuatia operesheni hiyo, Diwani wa Kata ya Kirya, Bw. Nyange Laizer aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa ng’ombe hizo kurudishiwa wenyewe.

“Unajua sisi malisho yetu tunafanya hapa hapa na ndiyo maana operesheni hii ikawakumba na watu wetu na hii ni kutokana na ukweli kuwa huwezi kutofautisha ng’ombe za hapa kwetu na zile zinazoingizwa kinyume cha sheria”, alisema.

Uamuzi huu wa mahakama unakuja baada ya ng’ombe hao kutaifishwa na serikali hivi karibuni baada ya kuingizwa hapa nchini kinyume cha sheria.