MKWASA ATAJA KIKOSI CHA NYOTA 27

MKWASA ATAJA KIKOSI CHA NYOTA 27

May 18, 2016

Kocha Mkuu wa timu ya Soka ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa ameita kikosi cha wachezaji 27 watakaounda Taifa Stars ambacho kinajiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017).
Mkwasa maarufu kama Master, alitangaza kikosi cha timu hiyo leo Mei 18, 2016 mbele ya Kocha Msaidizi, Hemed Morocco na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kuiva Misri, kikosi hicho kitafunga safari hadi Kenya kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambao wenyeji wameuombea Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwamba utambulike na kuingia kwenye rekodi za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuingia kwenye mchakato wa kupima viwango vya soka.
Katika kikosi hicho, Mkwasa amemuita beki Mlinzi mahiri wa Young Africans, Nadir Haroub maarufu kama Cannavaro huku akimwacha beki mwingine wa Young Africans, Kelvin Yondani kwa sababu ya sentahafu huyo anatumikia kadi mbili za njano alizoonywa katika michezo iliyopita.
“Yondani ana kadi mbili za njano,” amesema Mkwasa ambako katika kikosi chake amewateua makipa, Deogratius Munishi (Young Africans), Aishi Manula (Azam FC) na Benny Kakolanya (Tanzania Prisons) wakati mabeki ni Horoub, Mwinti Haji na Juma Abdul (Young Africans), Aggrey Moris, David Mwantika na Erasto Nyoni (Azam FC), Mohammed Hussein (Simba) na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohammed Ibrahim na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Ismail Issa (JKT Ruvu), Juma Mahadhi (Coastal Union) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), Mbwana Samatta (KDC Genk), Elias Maguli (Stand United), Ibrahim Ajib (Simba), John Bocco (Azam), Deus Kaseke (Young Africans) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).
KATIBU MKUU UJENZI ATAKA TAARIFA NDANI YA SIKU MBILI UHARIBIFU WA FLOW METER NA CAMERA BANDARINI

KATIBU MKUU UJENZI ATAKA TAARIFA NDANI YA SIKU MBILI UHARIBIFU WA FLOW METER NA CAMERA BANDARINI

May 18, 2016

FL1 
Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Hebel Mhanga( wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho( wa pili kulia) kuhusu ufanyaji kazi wa mifumo ya kuendesha mita ya kupimia mafuta (flow meter) uliojengwa eneo la Kwa Mwingira Mji Mwema Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na katibu Mkuu huyo leo Mei 18,2016.
FL2 
Meneja Mradi /msimamizi wa Ujenzi wa mradi wa Mita za kupimia mafuta Mhandisi Mary Mhayaya (kulia) akitoa maelezo kwa  Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho (kushoto) kuhusu mfumo wa kompyuta wa mita ya kupimia mafuta unavyofanya kazi kwa kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa wa utendaji kazi wa mita hiyo leo Mei 18,2016.
FL3 
Habour Master Kapteni Abdul Mwengamuno kutoka Mamalaka ya Bandari ya Dar es Salaam(kulia) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho (kushoto) hatua za kuzingatia wakati wa upakuaji wa mafuta kutoka kwenye meli mpaka kwenye mita za kupima mafuta ambapo mafuta hayo huchujwa kuondoa uchafu kwa kupitia mitambo maalum iliyofungwa kwenye mita hiyo.
FLO4 
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho akipanda ngazi kuelekea kwenye pambu na valvu zilizofungwa kwenye mita ya kupimia mafuta(Flow Meter) wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua utendaji kazi wa mita hiyo leo Mei 18,2016.
FLO5 
Meneja Mradi /msimamizi wa Ujenzi wa mradi wa Mita za kupimia mafuta Mhandisi Mary Mhayaya(kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho (wa pili kushoto) kuhusu hitilafu iliyojitokeza katika moja ya valvu zilizoko kwenye  mita hiyo, upande unaoendeshwa  kwa kutumia  mfumo wa digitali  hali iliyosababishwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.Mita hiyo sasa inatumia mfumo wa analojia na  hatua ya urejeshaji wa valvu hiyo katika hali yake ya awali inafanyiwa kazi na mkandarasi aliyepewa zabuni ya kujenga mita hiyo leo.
FLO6 
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho ( wa pili kulia) akitoa maagizo kwa Mamlaka ya Bandari kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ikiwemo hitilafu ya kamera za ulinzi na baadhi ya valvu kwenye mita ya kupimia mafuta na kuwasilisha taarifa ofisi kwake Jumatatu Mei 23 namna ya watakavyoshughulikia mapungufu yaliyojitokeza.
FLO7 
Meneja Mradi /msimamizi wa Ujenzi wa mradi wa Mita za kupimia mafuta Mhandisi Mary Mhayaya akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamliho (mwenye Kaunda suti) kuhusu ufanyaji kazi wa mtambo unaochuja mafuta kwa lengo la kudhibiti na kuzuia mafuta machafu kuingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam leo Mei 18,2016.
FLO8 
Mita ya Kupimia Mafuta (Flow Meter) iliyojengwa eneo la kwa mwingira, mji Mwema Kigamboni  Jijini Dar es salaam . Utaratibu wa kujenga uzio na paa kufunika mtambo huo unaendelea kupitia mkandarasi aliyepewa jukumu la kujenga mradi huo ili kuhimarisha ulinzi na usalama wa mita hiyo.( Picha na Raymond Mushumbusi na Aron Msigwa -MAELEZO)
………………………………………………………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence- Maelezo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Uchukuzi) Mhandisi Dkt. Leornad Chamuriho ameutaka uongozi wa Bandari unaosimamia Mitambo ya Kupimia Mafuta Nchini (Flow Meter) iliyoko Kigamboni kutoa taarifa ya kuharibika kwa mitambo hiyo ndani ya siku mbili.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika mitambo hiyo  na kubaini upungufu katika vitendea kazi ikiwemo kamera ya kufuatilia mwenendo bandarini hapo, “valvu, sloptank” na kuchelewashwa kwa ujenzi wa kufunikwa kwa mitambo.
“Ifikapo Jumatatu nipatiwe taarifa kuhusu matengenezo ya vifaa hivi, hatua zilizochukuliwa na mnieleze lini ukarabati wake utakamilika” alisema Dkt. Chamuriho.
Aidha, aliongeza kuwa dhumuni la Serikali ni kuhakikisha vifaa hivyo vinafanya kazi ili kulinda mapato yatokanayo na mafuta yanayoingia nchini ili Serikali ipate kodi halali na hivyo kuongeza mapato ya nchi na kuondoa malalamiko kwa wateja.
Naye Meneja Mradi wa Mitambo ya Kupimia Mafuta kutoka Mamlaka ya  Bandari nchini Mhandisi Mary Mhayaya ameeleza kuwa uharibifu wa vifaa hivyo umesababishwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na tayari vifaa hivyo vimeanza kufanyiwa kukabarati.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Hebel Mhanga amesema ofisi yake inajukumu la kuhakikisha inatoa huduma sahihi kwa wateja wanaotumia mitambo hiyo iliyopo bandarini  hapo na Serikali inapata mapato kulingana na huduma iliyotolewa.
Mradi wa Mitambo ya Kupimia Mafuta nchini  ipo katika majaribio kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo tayari meli tatu zimefanyiwa majaribio ya upakuaji wa mafuta huku moja ikiwa imefanyiwa vipimo.

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAJ. GEN. GAUDENCE MILANZI AONGOZA MKUTANO WA 23 CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA HIYO

May 18, 2016

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati),  Naibu Katibu Mkuu Angelina Madete (kulia) na Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii Wilfred Msemo (kushoto) wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa “Solidarity Forever” wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jana tarehe 17 Mei, 2016 katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, tawi la Bustani, Jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza wakati akifungua Mkutano wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Jijini Dar es Salaam. 
 
Katika salamu zake amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao katika kutekeleza lengo kuu la Wizara ambalo ni kuendeleza uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Kukuza Utalii nchini. 
 
Amewataka watumishi wote wa Wizara kuwa waadilifu, wabunifu, kufanya kazi kwa ushirikiano, kuepuka vitendo vya rushwa na makundi yasiyokuwa na tija kwa Wizara na Serikali kwa ujumla. 
 
Alionya kuwa, Mtumishi yeyote atakeenda kinyume cha sheria na taratibu hatosita kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kuachishwa kazi ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano ya “HAPA KAZI TU”
 
Maj. Gen. Milanzi alimuwakilisha Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ambaye yupo Mkoani Dodoma kwa ajili ya majukumu mengine ya Kiserikali (Bunge la bajeti).
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii wakiimba wimbo wa kuashiria umoja wa wafanyakazi (Solidarity Forever).
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo wakiimba wimbo wa umoja wa wafanyakazi “Solidarity Forever”
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)
MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA

MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA

May 18, 2016

index 
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi(kushoto) akibadilishana mawazo leo mjini Dodma na Naibu Katibu wa Bunge (uendeshaji) Bw.John Joel (kulia) .(Picha na Tiganya Vincent,Dodoma)
SU1 
Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge(kushoto) akibadilishana mawazo leo mjini Dodoma na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe.Joseph Mbilinyi(kulia) wakati wa mapumziko ya mchana.
SU2 
Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao pia wamewahi kuwa walimu wakiwa katika picha ya pamoja leo mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana.
SU4 
Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao pia wamewahi kuwa walimu wakiwa katika picha ya pamoja leo mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mchana.
SU5 
Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe.James Mbatia (kushoto) akibadilishana mawazo leo mjini Dodma na Mbunge wa Chalinze Mhe.Ridhiwan Kikwete (kulia) wakati wa mapumziko ya mchana.
SU7 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo  Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akibadilishana mawazo leo mjini Dodoma na  Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Ibrahim Raza(kulia)
Picha na Tiganya Vincent-Dodoma.
JESHI LA MAGEREZA NCHINI LASAINI MKATABA WA UFUNDISHAJI ELIMU YA UJASILIAMALI KWA WAFUNGWA LEO DAR ES SALAAM

JESHI LA MAGEREZA NCHINI LASAINI MKATABA WA UFUNDISHAJI ELIMU YA UJASILIAMALI KWA WAFUNGWA LEO DAR ES SALAAM

May 18, 2016

MIN1
MIN4 
Jeshi la Magereza limesaini Mkataba (MoU) na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Technoserve – Tanzania kushirikiana katika ufundishaji wa wafungwa mafunzo ya Ujasiriamali wakiwa wanakaribia kumaliza vifungo vyao magerezani ili stadi hizo ziwasaidie kumudu maisha mapya baada ya kutumikia adhabu zao.
Programu hii itaendeshwa katika Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Mfuko wa “Master Card”  kwa vijana wa kike na kiume wenye umri kati ya miaka 18 hadi 30 hivyo wafungwa walioko katika Magereza yaliyomo Mkoani humo na wengine wenye sifa toka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ili kupata mafunzo kupitia progamu ya uimarishaji wa maendeleo ya vijana vijijini kupitia biashara “STRYDE” inayoendeshwa na Taasisi hiyo.
Takwimu za sasa zinaonesha kwamba kati ya asilimia 30 na 35 ya wafungwa wanaomaliza vifungo vyao hurejea magerezani.Hivyo, mafunzo haya yatalenga kuwafanya  wanapomaliza vifungo vyao waweze kupata maarifa ya kuanzisha shughuli zao wenyewe za kujipatia kipato halali na kuacha vitendo vya uhalifu katika jamii wanamoishi vinavyowafanya kurejea magerezani.
Aidha,  mafunzo haya ya Ujasiriamali yatajikita katika kuwafundisha kilimo biashara, matumizi mazuri ya fedha binafsi, uwezo wa kutumia ujuzi, ubunifu na tafakari ya kina katika kufanya maamuzi, mpango biashara, mawazo ya biashara na uwezo wa kuandaa mpango biashara n.k.
Ushirikiano huu ni mkakati endelevu wa Jeshi la Magereza katika kuboresha Programu za Urekebishaji wa wafungwa magerezani ili wawe raia wema na wenye tija katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Program za Ujasiriamali kwa wafungwa zinaendeshwa pia katika baadhi ya Magereza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Dorcas International na New Life in Christ katika Gereza la Karanga – ushonaji viatu, ufumaji na uokaji mikate, Gereza Arusha – uokaji mikate, ufundi seremala na ufumaji.
Jeshi la Magereza linawakaribisha wadau wa ndani na nje kushirikiana katika urekebishaji wa tabia za wafungwa ili wawe na michango chanya katika jamii na Taifa kwa ujumla.

NSSF YATOA ELIMU KUHUSU HIFADHI YA JAMII KWA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA.

May 18, 2016

SHIRIKA la  Taifa la  Hifadhi ya Jamii (NSSF) yazidi kutoa elimu juu ya hifahdi ya jamii kwa wananchi mbalimbali ikiwa ni  mpango maalamu wa kuwafikia wanachama  wengi zaidi.

Katika mkoa wa Arusha NSSF imetoa elimu kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika soko la Kilombero. Zoezi hilo litaendelea kesho tarehe 19/05 katika eneo la soko la Kilombero.
Afisa Masoko na Uhusiano  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amani Marcel (kushoto), akimkabidhi mwanachama mpya fulana wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero Jijini Arusha. 
Wananchi wakiwa katika foleni ya kujiandikisha uanchama wa NSSF wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero jijini Arusha.
Afisa wa NSSF Bi. Irene Mshanga akimwandikisha mwanachama Mpya wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi inayoendelea katika soko la Kilombero jijini Arusha.
 Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Amina Mbaga Akitoa ufafanuzi kwa Mwanchama mpya wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi inayoendelea katika Soko la Kilombero Jijini Arusha leo.
Afisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Anna Nguzo Akitoa ufafanuzi kwa Mwanchama mpya wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi inayoendelea katika Soko la Kilombero Jijini Arusha leo.

TRA YAFUNGUA MAFUNZO YA AWAMU YA PILI KWA WAFANYAKAZI WAKE.

May 18, 2016

 Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo  akizungumza  wakati wa hafla kufungua mafunzo ya awamu yapili ya wafanyakazi wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Amesema kuwa wameamua kuanzisha mpango huo kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato  ili kufundisha wafanyakazi wa TRA maadili na nyenzo za utendaji kazini  pamoja na kuendesha mafunzo ya dini ili kuwafanya wafanyakazi wawe wacha Mungu katika kazi zao.
 Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA, Victor Kimaro akizungumza na wafanyakazi wa malaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakati  wa kufungua mafunzo ya awamu ya pili kwa wafanyakazi wake 200. Pia amewataka wafanyakazi wote wanatakiwa wafanye kazi kwa maadili hususani upande wa ukusanyaji kodi na Chuo hicho kimewafundisha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa ushindani katika maeneo ya kazi ili kuliletea taifa maendeleo yaliyokusudiwa.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar es Salaam leo. wakati wa kufungua mafunzo ya maadili kwa wafanyakazi wa TRA ambao wamefanya usaili na kufanikiwa kufunzu kusoma mafunzo hayo kwa wafanyakazi kwaajili ya kujifunza mambo mtambuka ya tasinia ya TRA. Lengo la kuwapa mafunzo hayo ni kutaka kuijenga Mamlaka ya Mapato (TRA) mpya.Kulia ni Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Isaya Jairo na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasiliamali watu na utawala katika chuo cha Kodi(TRA), Victor Kimaro wakiwa katika mkutano wa kufungua mafunzo ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata  akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata na  Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo wakikata utepe kuzindua ripoti ya mafunzo kwa wanafunzi wa malaka ya Mapato Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata (Katikati walioshika vitabu ),Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo(Kulia) na Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA, Victor Kimaro (kushoto) wakionyesha vitabu vya mafunzo kwa wafanyakazi wa TRA jijini Dar es Salaam leo.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata  akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TRA jijini Dar es Salaam leo. Wafanyakazi hao ndio wanaohudhulia mafunzo hayo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata  amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo  walilojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika  mwaka wa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10. Ameyasema hayo wakati wa  hafla ya uzinduzi  wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa ya ajira za taasisi hiyo.
Mkuu wa chuo cha Kodi (TRA), Profesa Isaya Jairo.
Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA, Victor Kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo.

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA KAMISHINA MKUU WA SEKRETARIETI YA MAADILI JAJI KAGANDA.

May 18, 2016

  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na  Kamishna Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili, Jaji Salome Kaganda wakati alipofanya mazungumzo  naye ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Kamishna Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili, Jaji Salome Kaganda ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza  Kamishna Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili, Jaji Salome Kaganda wakati alipozungumza naye ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila ofisini kwake Mjini Dodoma.