SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZA KODI ZINAZOIKABILI SEKTA BINAFS

SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZA KODI ZINAZOIKABILI SEKTA BINAFS

December 07, 2017
IMG_6962
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) , akitolea ufafanuzi masuala kadhaa yanayohusu changamoto za kodi katika Sekta Binafsi wakati wa mkutano kati ya Serikali na Sekta hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma
IMG_6725
Kaimu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda nchini CTI, Dkt. Samuel Nyantahe akizungumza jambo wakati wa mkutano kati ya Serikali na Sekta Binafsi uliofanyika mjini Dodoma.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango
…………..
Benny Mwaipaja, Dodoma
WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewaahidi wafanyabiashara na wawekezaji nchini kwamba serikali italifanyiakazi suala la kodi katika Bajeti ijayo ya mwaka 2018/2019 ili kuboresha zaidi  mazingira ya uwekezaji na biashara kupitia sekta binafsi.
Dokta Mpango ameyasema hayo mjini Dodoma katika mkutano wa tatu kati ya Serikali na Sekta binafsi ambapo masuala mbalimbali yanayohusu kodi yamejadiliwa ikiwa ni mwendelezo wa Serikali kutaka kuiimarisha Sekta hiyo ili iweze kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Alisema kuwa Serikali imedhamiria kupunguza ama kuondoa kabisa kero zinazoikabili sekta binafsi ikiwemo malalamiko ya muda mrefu ya utitiri wa kodi ili sekta hiyo iweze kuwa na nguvu na kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa viwanda utakaokuza pato la taifa na ajira nchini.
Alisema Serikali inatambua kwamba sekta binafsi ndiyo nguzo ya ukuaji wa uchumi wa Taifa ndio maana inajitahidi kupata maoni ya wadau kuhusu namna ya kuboresha mazingira yao ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini ili kuharakisha maendeleo ya nchi.
“Ni lazima dukuduku za sekta binafsi tuzisikilize, tuzitafakari na kuzifanyia kazi ili uchumi uweze kwenda kwa kasi zaidi tuwaondoe wananchi wetu kwenye umasikini na vijana wetu wapate kazi’ Alisema Dkt. Mpango.
Alisema wakati wa kuandaa bajeti yam waka 2018/2019, serikali itaweka mfumo wa kodi utaoiwezesha Sekta Binafsi kukua na kuimarika zaidi ili iweze kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya watanzania kwa ujumla.
“Katika mjadala huu  nimefurahia kusikia maoni ya sekta binafsi ambapo pamoja na kupendekeza maeneo ya kupunguza kodi, lakini pia wamezungumzia namna ya kuongeza wigo wa kuongeza mapato ya Serikali” Aliongeza Dkt. Mpango.
Hata hivyo, Dkt. Mpango, alitahadharisha jumuiya ya wawekezaji na wafanyabiashara nchini kwamba wanapojadili juu ya masuala ya kodi, wakumbuke kwamba Serikali ina mzigo mkubwa wa kuhudumia jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, maji, afya, barabara, miundombinu ya usafiri na usafirishaji ikiwemo reli na mingine mingi.
Alitolea mfano uzalishaji wa maji katika miji mikuu ya Wilaya na miji midogo ni lita milioni 99.5 kwa siku wakati mahitaji ni lita milioni 273 kwa siku, sawa na 36.4%.

“Miradi ya maji ya Kitaifa uzalishaji ni lita milioni 59.5 ikilinganishwa na mahitaji ya lita 119 kwa siku, sawa na 50% ya mahitaji” Alisisitiza Dkt. Mpango

Alibainisha kuwa vifo vitokanavyo na uzazi ni 556 katika kila vizazi hai 100,000 wakati lengo ni kuvipunguza visizidi vifo 265 katika kila vizazi hai 100,000 itakapofika mwaka 2020.

Aidha Dkt. Mpango alisema kuwa huduma za msingi zinazotolewa na Serikali hususan, ulinzi wa nchi, usalama wa raia, na mali zao, utawala, usimamizi wa rasimali za nchi, na ujenzi wa miundombinu ya msingi isiyo na mvuto kwa sekta binafsi,  lazima ziendelee kugharamiwa na Serikali.

Dkt. Mpango alielezea pia namna misaada na mikopo kutoka kwa wadau wa maendeleo inavyopungua mwaka hadi mwaka ambapo alisema mikopo yenye masharti nafuu ilishuka kutoka shilingi trilioni 1.3 mwaka 2013/14 hadi shilingi bilioni 495 mwaka 2015/2016

Alifafanua kuwa misaada kutoka kwa washirika hao wa maendeleo imeshuka kutoka shilingi trilioni 1.5 kwa mwaka 2013/2014 hadi sh. Trilioni 1.23 mwaka 2015/2016.

Vilevile alieleza kuwa kiwango cha ulipaji kodi kwa hiari miongoni mwa wafanyabiashara na wawekezaji bado hakiridhishi na ukwepaji kodi/uvujaji wa mapato ya Serikali bado ni matatizo sugu hivyo kuitaka Sekta Binafsi iyatupie macho mambo hayo wakati wakijadili na kushauri namna Serikali inavyoweza kuboresha kodi ili mambo hayo ya msingi ya kuihudumia jamii yasikwame

Wakizungumza kwa niaba ya Sekta Binafsi, Mwenyekiti wa Shirikisho la wenye viwanda hapa nchini Dokta Samuel Nyantahe na mmoja wa wafanyabiashara Bw. Boaz Ogola, wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa nia yake ya dhati ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara hapa nchini na kwamba wako tayari kushirikiana nayo ili kutimiza azma yake ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa kuwa wameiona nia njema ya Serikali ya kufikia hatua hiyo
Mkutano huo wa siku moja umewakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi huku agenda kuu ya mkutano huo ilikuwa kujadili kwa undani masuala mbalimbali ya kodi ambapo Sekta binafsi imependekeza mambo kadhaa ambayo Serikali imeahidi kuyafanyiakazi.

ZAIDI YA BAJAJ 150 ZAMAKATWA WILAYANI KOROGWE KUTOKANA NA MAKOSA MBALIMBALI

December 07, 2017
ZAIDI ya Bajaji 150 zimekamatwa wilayani Korogwe mkoani Tanga kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo madereva kuendesha bila kuwa na leseni huku wakipakia abiria.
Ukamataji huo umefanyika wakati wa operesheni maalumu inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani hapa inayoendeshwa na Mamlaka ya Usimamizi wa vyombo vya majini na nchi kavu Sumatra mkoani Tanga.

Akizungumza jana,Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Tanga,Dkt Walukani Luhamba alisema bajiji hizo zilikamatwa wakati wa ukaguzi ambao waliufanya kuangalia iwapo madereva wanaendesha vyombo hivyo wana leseni.

Alisema lengo la operesheni hiyo ni kuhakikisha wanazibiti ajali
zisizokuwa za lazima kwa watumiaji wa vyombo hivyo ikiwemo kufuatwa kwa sheria za usalama barabarani.

“Katika operesheni hii tumekamata bajaji zaidi ya 150 ambao wameliki na madereva wamepewa onyo kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani na kutokurudia tena makosa yao “Alisema.

Aidha alisema pia licha ya kukamata bajaji hizo lakini pia walikamata pikipiki zaidi ya 170 ambapo kwenye Halmashauri ya Bumbuli walikamata pikipiki 60, Handeni Vijijini walikamata pikipiki 40 huku Korogwe wakikamatwa 70.

Hata hivyo alisema operesheni hiyo bado inaendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Tanga lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha watumiaji wanafuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima.

Ofisa Sumatra huyo pia alitoa onyo kali kwa wamiliki wa mabasi ya mikoa na wilayani kuacha kupandisha nauli katika kipindi hiki cha mwishoni mwa mwaka na watakaobainika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.
WAZIRI MPINA AITAKA KAMPUNI YA GAME TRACKING SAFARIS (TGTS) KUONDOKA KWENYE RANCHI YA UVINZA KABLA YA JANUARI 2018

WAZIRI MPINA AITAKA KAMPUNI YA GAME TRACKING SAFARIS (TGTS) KUONDOKA KWENYE RANCHI YA UVINZA KABLA YA JANUARI 2018

December 07, 2017
d
Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mh.Luhaga Mpina  (katikati) kitoa maamuzi ya kuitaka Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS)  kuondoka katika eneo la hekta 20000 kwenye vitalu  tisa vilivyomo kwenye Ranchi  ya Uvinza ifikapo tarehe 1/1/2018.
a
Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mh.Luhaga Mpina  akizungumuza na Meneja wa Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) Audax Kalulama katika simu alipotembelea Ranchi ya Uvinza leo na kuamuru mwekezaji huyo kuondoka kabla ya Januari Mosi mwakani kutokana na Mwekezaji huyo kukaa katika eneo hilo kinyume cha Sheria.
b
Sehemu ya Ranchi  ya Uvinza.
.c
Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mh.Luhaga Mpina  (katikati) akiwasikiliza walinzi wa   Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS) hawapo pichani wakitoa maelezo alipotembelea Ranchi ya Uvinza .
…………………………………………………………………….
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina  ameutaka uongozi wa  Kampuni ya Game Tracking Safaris(TGTS)  kuangalia na kupitia nyaraka walizonazo  ili kuona uhalali wa umiliki wa eneo la hekta 20000 kwenye vitalu  tisa vilivyomo kwenye Ranchi ya Uvinza inayomilikiwa na  Kampuni ya Ranchi za za Mifugo za Taifa (NARCO)kabla ya Selikali kuwatoa kwa nguvu ifikapo tarehe 1/1/2018.
 Waziri Mpina ametoa maelekezo  hayo leo alipotembelea Ranchi ya Uvinza kuangalia shughuli mbalimbali  katika Ranchi hiyo ambapo ametoa muda wa hadi Januari mosi mwakani  kwa mwekezaji huyo kuondoka katika eneo hilo  endapo atabaini kuwa amekuwa akikaa kimakosa kuanzia katika  vitalu namba 41 hadi 49.
Aidha Waziri Mpina amesema  endapo Mwekezaji huyo ataendelea kubaki  baada ya tarehe Mosi Januari, Serikali itamuondoa kwa nguvu  na atatakiwa kulipa gharama  zote za fidia na usumbufu.
 “Ninakuagiza  angalia  taarifa  mbalimbali ulizonazo kuhusu  umiliki wa eneo hili kama utaona  umeendelea  kukaa  hapa  bila kufuata taratibu tafadhali  uondoke mara mmoja ili kupisha Serikali kuendelea na shughuli zake” alisisitiza Mpina
Waziri Mpina  amemuagiza Meneja Mkuu wa NARCO, Profesa  Philemoni Wambura  kuwaandikia  barua  ya kuwaondoa wawekezaji wote katika Ranchi hiyo ambao hawajaendeleza kwa zaidi ya asilimia 40  na kwamba wawekezaji ambao wamewekeza kwa zaidi ya asilimia arobaini wanatakiwa kukamilisha malipo yote kabla ya Januari mosi mwakani.
Alionya wawekezaji kuacha tabia ya kuidanganya serikali kwamba wanauwezo wa kuwekeza katika vitalu  ili wapewe lakini wanabadili matumizi baada ya kupewa. Aliongeza kwamba  Serikali imegundua  baadhi ya wawekezaji wanaopewa vitalu wanawakodisha wafugaji kutoka nchi jirani  na kujipatia faida wakati  Serikali haipati chochote.
Awali, Meneja wa (TGTS)   Audax Kalulama  akizungumza kwa simu  na Waziri Mpina kutoka Arusha amesema kwamba  eneo hilo wanamiliki  kihalali na kuomba muda ili wawasiliane na Wizara  ya Mifugo kuonyesha  taarifa  za umiliki wa eneo hilo.
Waziri Prof. Mbarawa Awapa Hadi Feb 1, 2018 Wadaiwa JNIA

Waziri Prof. Mbarawa Awapa Hadi Feb 1, 2018 Wadaiwa JNIA

December 07, 2017
DSC_3220
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati mbele) akiwa katika chumba cha mikutano cha Kampuni ya ujenzi ya Kimataifa ya Uholanzi (BAM) linalojenga Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) alipofanya ziara. (Wa kwanza kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela na (wa kulia) ni Balozi wa Uholanzi nchini, Jeroen Verheul.
DSC_3246
Mkandarasi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Wolfgang Marschick (katikati kushoto) akitoa maelezo ya ujenzi huo leo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanza nia (TAA), Bw. Richard Mayongela.
DSC_3258
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela wakati walipokuwa wakitembelea ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII). Nyuma ni Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Johannes Munanka.
DSC_3261
Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Bw. Wolfgang Marschick (Kulia) akimuonesha waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) leo alipotembelea jengo hilo. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati).
DSC_3308
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye miwani mbele) akimsikiliza Mkandarasi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Bw. Wolfgang Marschick (aliyenyoosha mkono) na wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela.
DSC_3322
Balozi wa Uholanzi nchini, Bw. Jeroen Verheul akiongea na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof.Makame Mbarawa (wa tatu kulia) alipofanya ziara ya kutembelea jengo hilo leo. Wengine katika picha ni Bw. Wolfgang Marschick (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (pili kulia).
DSC_3392
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (aliyesimama mbele), leo akiongea na wadau wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), kwenye ukumbi wa Watu Mashuhuri (VIP). Mbele kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela.
………..
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka wadau wanaofanya shughuli mbalimbali zinazohusisha na kodi ya pango kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Julius Nyerere (JNIA), kuhakikisha ifikapo Februari 1, 2018 wawe wameshalipa madeni yao.
Prof. Mbarawa alisema leo wakati alipoongea na wadau hao kwenye ukumbi wa watu Mashuhuri wa JNIA-TBII, wakati walipozungumza nao kujadili masuala mbalimbali.
Alisema baadhi ya wadau wameshalipa madeni yao kati ya bil 10 zilizokuwa zinadaiwa na sasa zimesalia bil. 3.7 ambapo amewataka baada ya kumalizika kwa sherehe za Krismas na Mwaka Mpya wahakikishe wanakamilisja madeni yao.
“Hatutasita kumuondoa mtu yeyote atakayekuwa akiendelea kudaiwa kwani atakuwa hana sifa za kupangisha katika majengo haya ya viwanja vya ndege kwa kuanzia TBI na hapa TBII,” alisema Prof. Mbarawa.
Hatahivyo, aliyapongeza mashirika na ofisi ambazo zimekuwa zikilipa kwa wakati fedha za pango, ambapo uaminifu huo utawasaidia kupata nafasi katika jengo jipya la la tatu la abiria, ambalo litakuwa linauwezo wa kuhudumia abiria milioni sita (6) kwa mwaka.
Pia amewataka wale wasiowaaminifu wachague kulipa madeni ya pango au wanaodaiwa na serikali au kuondoka, ili kutoa nafasi kwa Watanzania wengine ambao wanania ya dhati ya kufanya biashara na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wasimamizi wakuu wa viwanja vya serikali.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela alisema tayari zabuni mbalimbali zimeshatangazwa na kuwataka wadau waliowaaminifu kujitokeza kuwania na kupata nafasi ya kufanya shughuli zao kwenye eneo la JNIA.
“Tumeshatangaza zabuni hizo na kama mhe. Waziri alivyosema zitakuwa za uwazi zikishirikisha wataalamu na tunauhakika watapatikana watu wenye mapenzi mema ya kufanya biashara na serikali” alisema Bw. Mayongela.
Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa alitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) na kuridhishwa na kasi ya ujenzi, ambapo amewapongeza TAA, Tanroads na Kampuni ya ujenzi ya Kimataifa ya Uholanzi (BAM).
Naye Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Bw. Mayongela, alisema kukamilika kwa jengo hilo kutatoa fursa nyingi za biashara zikiwemo uwekezaji katika hoteli, kumbi za mikutano, ofisi, migahawa, maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali, huduma za kifedha (benki) na karakana za ndege.
Balozi Maiga katika Maadhimisho Siku ya Mshikamano na Wapalestina Dar

Balozi Maiga katika Maadhimisho Siku ya Mshikamano na Wapalestina Dar

December 07, 2017

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mheshimiwa Balozi Maiga akizungumza kwenye sherehe ya Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestine, kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Towers,5 Desemba 2017.  
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kulia) akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyofanyika tarehe 5 Desemba 2017 jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wajumbe wa Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina. Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na
Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour wakiwa katika hafla hiyo. 
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kushoto) akitembelea picha za maonesho kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyofanyika tarehe 5 Desemba 2017 jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na ubalozi wa Parestina nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC). 
Hafla ya kuadhimisha Siku ya Mshikamano na Watu wa Palestina, iliyoandaliwa na ubalozi wa Parestina nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) ikiendelea. 
Wajumbe wa Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina wakipata picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo.

Ecobank Tanzania yasaidia kupatikana kwa maji safi kwa Shule ya Hananasif

December 07, 2017


Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Mwanahiba Mzee – kulia, akimkabidhi vitabu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Hananasifu Idda Uisso iliyopo wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Mwanahiba Mzee akijaribu moja ya mifereji ya maji salama katika wa Shule ya Msingi Hananasifu iliyopo wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Mwanahiba Mzee akikata utepe kuashiria upatikanaji wa maji Shule ya Msingi Hananasifu iliyopo wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso..
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Hananasifu Idda Uisso akimwonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank baadhi ya mifereji ambayo kwa sasa inatoa maji salama baadhi ya kufanyiwa ukarabati na benki hiyo.
Mmoja wa mfanyakazi wa Ecobank akinawa kuashiria kuanza kupatikana kwa maji salama baada benki hiyo kutengeneza miundombinu na kusafisha mifereji iliyokuwa imeziba katika shule ya Msingi ya Hananasifu iliyopo wilaya ya Kinondoni.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule ya Msingi Hananasifu, Kinondoni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso.
Diwani wa Kata ya Hananasifu akitoa neon la shukrani kwa uongozi wa Ecobank Tanzania. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule ya Msingi Hananasifu, Kinondoni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso. 
Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo na maeneo yenye uhitaji wa maji kwa wanafunzi na waalimu wote wa shule ya Msingi ya Hananasif iliyopo katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo hufanyika kila mwaka katika nchi 33 barani Afrika ambapo Ecobank inafanya biashara.

Msaada huo wa Ecobank Tanzania kusaidia shule hiyo kupata maji safi umetolewa leo ikiwa njia moja wapo ya kuadhimisha kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya Ecobank inayosema ‘Maji Salama, Ishi na Afya njema’ Safe Water, Healthy Living’

Mbali na Ecobaank kutoa msaada huo, wafanyakazi wa Ecobank Tanzania pia wamejumuika kwenye kufanya usafi wa mazingira shuleni hapo kwa kuzibua mitaro ya maji taka yote pamoja na kuweka dawa kwenye kisima cha maji shuleni hapo ili kuhakikisha wanafunzi wanapata maji safi na salama.

Kwa upande wa elimu, Ecobank pia imetoa vitabu kwa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na kutoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwenye mitihani yao kuanzia darasa la kwanza hadi la sita.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bi Mwanahiba Mzee alisema benki hiyo imekuwa ikiadhimisha siku ya Ecobank kwa kutoa sehemu ya faida wanayopata kwa Jamii inayowazunguka.

“Tuliguswa sana baada ya kupewa taarifa kuwa shule ya Hananasif ina jumla ya wanafunzi 728 lakini miundombinu ya maji imeziba na kubakia na sehemu moja tu ambayo inatumiwa na shule nzima. Vyoo havina maji na hivyo imekuwa ni changamoto ya kiafya kwa wanafunzi, walimu na watu wengine kwenye shule hii, tukaona ni vyema kuja kusaidia ” alieleza Mwanahiba Mzee 

Bi Mzee, alisema kutokana na Benki yake kutoa msaada huo, pamoja na vitabu vya kiada, motisha yaa zawadi kwa wanafunzi itasaidia kutoa hamasa kwa wanafunzi kuendelea kuongeza bidii kwenye masomo yao zaidi

“Ecobank Tanzania inatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora pamoja na kuboresha elimu ikiwa ni dhamira yetu katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua kiwango cha elimu hapa nchini, aliongeza Bi Mwanahiba Mzee .

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Hananasif Mwalimu Idda Uisso Alitoa shukrani kwa juhudi za Ecobank Tanzania kwa kuhakikisha shule hiyo inapata maji salama. “Nachukua hii fursa kuwapongeza uongozi wa Ecobank Tanzania kuchagua kuja shule ya Hananasif kwani hapa kuna shule zingine nyingi.

Alisema changamoto kubwa ilikuwa ni maji kwani kwa Idadi kubwa ya wanafunzi walionao maji safi na salama ni muhimu. “Kwa msaada wa mamboresho ya miundombinu yote mliyofanya, kwa sasa tuna uhakika wa maji safi na salama kwa waalimu pamoja na wanafunzi” alisema.

Vile vile alitoa shukrani za dhati kwa msaada wa vitabu pamoja na zawadi kwa wanafunzi bora kwani kutaongeza hamasa kwa wanafunzi. “Sisi kama shule tumekuwa tukifanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa lakini kwa msaada wa vitabu na kuhamasisha wanafunzi, nina uhakika na ninawaahidi Ecobank tutaendelea kufanya vizuri zaidi”.

Ecobank sasa inafakisha miaka 8 hapa nchini Tanzania huku ikiwa na matawi ya kutoa huduma bora za kibenki katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha

-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

Fundisho la wiki' Dada Jasmini! alivyo vuka majaribu ya kusalitiwa na Mume!

December 07, 2017
Inatia huruma kwa Dada Jasmini Shabani aliye kutikana maeneo ya Buguruni Rozana, ambaye kapitia majaribu na misukosuko katika maisha ya ndoa yake, ikiwa ni pamoja na kusalitiwa na Mume wake wa kwanza pindi alipokuwa na ujauzito wa miezi mitano.

Katika maisha ya ndoa kuna changamoto nyingi zinazo sikitisha lakini kwa upande mwingine zinazo chekesha. Amini  ukisema Ndoa ni sawa na neno SIRI maana yaliyomo ndani Mungu ndio anajua unaweza ukakutana na wanandoa yaani Mke na Mume wameongozana wakiwa na nyuso za furaha kumbe mioyo yao haipatani kama Chui na Mbuzi.


Ukifikiria sana ndoa unaweza sema labda ndoa nyingi huwa zinatokea kama ajali, yaani utafikiri wanalazimishwaga. Kiukweli usipo lizika na uliye mchagua sasa huwezi kulizika maisha yako yote. Mpende mwenzio kama ujipendavyo hata vitabu vya mungu viliandika.

AGPAHI YAMWAGIWA SIFA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BORESHA MKOANI SIMIYU

December 07, 2017

Meneja wa Shirika la AGPAHI kanda ya ziwa, Dk. Nkingwa Mabelele akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za shirika hilo katika kikao cha ushauri cha mkoa wa Simiyu (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT Mjini Bariadi Desemba 5,2017. Picha zote na Derick Milton - Simiyu News blog