PINDA KUFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI TANGA ALHAMISI

September 24, 2013
NA AMINA OMARI,TANGA.
WAZIRI Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la uwekezaji la kanda ya Kaskazini linalotarajiwa kufanyika Septemba 26 hadi 27 mwaka huu Mkoani Tanga.
Akiongea na waandishi wa habari hapo leo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa alisema kuwa waziri Mkuu anatarajiwa kuwasili Mkoani humo kesho majira ya saa kumi na Moja kwa ajili ya kushiriki kwenye kongamano hilo.
Alisema kuwa kongamano hilo lenye lengo la kutangaza fursa za uwekezaji na kimaendeleo zilizoko kwenye mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Manyara na Arusha zinatarajiwa kuhudhuriwa na wageni 450 kutoka nje ya Tanzania.
“Tayari tumepata wageni wenye nia ya kushiriki ili kujionea fursa zilizopo takribani 450 wamethibitisha ushiriki wao kutoka nje ya Tanzania achiambali  wale wadau kutoka kwenye Halimashauri zetu mbalimbali zilizoko kwenye ukanda wa kaskazini”alisema RC Gallawa.
Aidha alieleza kuwa kongamano hilo litakuwa na midahalo ,maonyesho ya raslimali zilizopo ,maeneo ya uwekezaji pamoja na fursa zinazopatikananaili kumvutia mwekezaji  kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kuichumi kwenye mikoa hiyo.
Pia aliwataka wakazi wa jiji la Tanga kuhakikisha wanaituma fema fursa ya uwekezaji hasa kwa wafanyabiashara wa mnumba za kulala wageni na waendesha biashara za chakula kutoa huduma bora kwa wageni watakao fika kwa wingi kwenye kongamano hil

TWIGA STARS YAPANGIWA ZAMBIA AWC

September 24, 2013
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) imepangiwa kucheza na Zambia katika mechi za kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika mwakani nchini Namibia.

Twiga Stars itaanzia ugenini jijini Lusaka ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Februari 13 na 15 mwakani wakati ile ya marudiano itafanyika kati ya Februari 28 na Machi 2 mwakani jijini Dar es Salaam.

Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Zambia, raundi ya pili ambayo ndiyo ya mwisho itacheza na mshindi kati ya Botswana na Zimbabwe. Mechi ya kwanza itakuwa Dar es Salaam kati ya Mei 23 na 25 mwakani wakati ile ya marudiano itakuwa kati ya Juni 6 na 8 mwakani.

Nchi 25 zimeingia katika mashindano huku mabingwa watetezi Equatorial Guinea, makamu bingwa Afrika Kusini na Cameroon iliyoshika nafasi ya tatu katika fainali zilizopita zikiingia moja kwa moja katika raundi ya pili.

MABINGWA ARS KUPONGEZWA DAR

September 24, 2013
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya Airtel Raising Stars (ARS) ya Tanzania imeandaliwa hafla ya kuipongeza kwa kunyakua ubingwa katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika nchini Nigeria.

Hafla hiyo ya kuipongeza pamoja na kupata chakula cha mchana itafanyika leo (Septemba 24 mwaka huu) saa 6 mchana kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski na kuongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.

Timu hiyo iliyorejea nchini jana (Septemba 23 mwaka huu) usiku katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo iliifunga Kenya. Kwa upande wa wavulana, timu hiyo ilitolewa na Zambia katika hatua ya nusu fainali.

Michuano hiyo ilishirikisha timu kutoka nchi za Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Gabon, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Tanzania, Uganda na Zambia.

Kombaini ya timu hizo zilizokuwa chini ya makocha Rogasian Kaijage na Abel Mtweve iliundwa baada ya mashindano ya Airtel Raising Stars yaliyohusisha wasichana na wavulana wenye umri wa chini ya miaka 17 na kufanyika jijini Dar es Salaam wiki ya kwanza ya Septemba mwaka huu.