*RAIS KIKWETE AMFARIJI JAJI WARIOBA KWA KUFIWA NA MKWE WAKE

May 17, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha kumbukumbu alipokwenda kuhani msiba wa mama mkwe wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba,Marehemu Hedwig Laurent Ojjik, Oysterbay jijini Dar es salaam leo. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mama mkwe wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba,Marehemu Hedwig Laurent Ojjik,Oysterbay jijini Dar es salaam leo. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji wanafamilia bada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mama mkwe wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Marehemu Hedwig Laurent Ojjik,  Oysterbay jijini Dar es salaam leo. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Jaji Joseph Warioba na mkewe Mama Evelyne Warioba walipokwenda kuhani na kutoa heshima za mwisho katika msiba wa mama mkwe wa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Marehemu Hedwig Laurent Ojjik,   Oysterbay jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mama Evelyne Warioba  alipokwenda kuhani msiba wa mama yake mzazi Marehemu Hedwig Laurent Ojjik  Oysterbay jijini Dar es salaam leo.  PICHA NA IKULU

*MTOTO WA MSEMAJI WA IKULU, BRIAN SALVA RWEYEMAMU AZIKWA LEO JIJINI DAR

May 17, 2014

  Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Bw. Salva Rweyemamu na mkewe Isabella wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wao Private Brian Salva Rweyemamu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo. 
Salva na mkewe wakiweka shada la maua...
 Dada wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu wakiweka shada la maua wakati wa mazishi katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salva Kikwete wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Private Brian Salva Rweyemamu wakati wa mazishi  katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2014.
Rais Kikwete aongoza Harambee Kanisa la KKKT Bumbuli

Rais Kikwete aongoza Harambee Kanisa la KKKT Bumbuli

May 17, 2014


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Naibu waziri Mawasiliano Sayansi na Technolojia na mbunge wa Bumbuli January Makamba wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Bumbuli Shughuli hiyo imefanyika katika Hotel ya Golden Tulip leo(Ijumaa) Tarehe.16.05.2014 makamba 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wimbo wa wanabumbuli mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip kwa ajili ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Kilutheri la Bumbuli, Kushoto ni askofu mkuu wa KKKT Dr.Gerhas  Malasusa, Watatu Kulia ni Dkt.Steven Munga wa Lushoto na kulia ni mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na teknolojia Mh.January Makamba Katika harambee hiyo jZaidi ya Shilingi milioni mia tatu zilipatikana(picha na Freddy Maro).
MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI MJINI DODOMA

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI MJINI DODOMA

May 17, 2014

PG4A9487
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi  Mteule wa Tanzania nchini Sweden, Dora Msechu kabla ya mazungumzo yao,ofisini kiwa Waziri Mkuu  mjini Dodoma,  May 16, 2014. Balozi huyo mteule alkwenda kuaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A9494
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda  akizungumza na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Sweden, Dora Msechu, ofisini kwake mjini Dodoma May 16, 2014. Balozi huyo Mteule alikwenda kuaga. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)
PG4A9513
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William  Lukuvi, bungeni mjini Dodoma May16, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A9520  
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Naibu wake, Pereira Sirima  (kulia) wakipongezwa na Wabunge baada ya bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo, bungeni mjini Dodoma May 16, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A9525 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Makambako, Deo Sanga (kushoto) na Mbunge wa Viti Maaliam, Lediana Mng’ong’o bungeni mjini Dodoma May 16, 2014. (Picha na O

MKURUGENZI MWAMBAO FM,DC MKINGA MBONI MGAZA WAWAONGOZA WAKAZI WA MKOA WA TANGA KUMSINDIKIZA MFAUME KIKWATO

May 17, 2014
MKUU WA WILAYA YA MKINGA,MBONI MGAZA KATIKA AKIBADILISHANA MAWAZO NA ALIYEKUWA MHARIRI MKUU WA RADIO MWAMBAO FM  YA TANGA,BENEDICT KAGUO LEO  KWENYE MAZISHI YA MTANGAZAJI WA RADIO HIYO MFAUME KIKWATO ALIYEFARIKI JUZI NA KUZIKWA LEO KWENYE MAKABURI YA MWANGOMBE JIJINI TANGA.

MKURUGENZI MTENDAJI WA MWAMBAO FM ,AHMED SIMBA AKIBADILISHANA MAWAZO NA MWENYEKITI WA TANGA PRESS CLUB HASSAN HASHIM LEO KWENYE MAZISHI HAYO





WAANDISHI WA HABARI MKOANI TANGA WAKIWA MSIBANI WA PILI KUTOKA KUSHOTO NI SOPHIA WAKATI WA GAZETI LA UHURU,EVELINE BALOZI WA RADIO HURUMA


ULIMWENGU, SAMATA WAJIUNGA STARS

May 17, 2014
Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wametua Dar
es Salaam leo (Mei 17 mwaka huu) mchana, na kujiunga moja kwa moja kwenye kambi ya Taifa Stars kwa ajili ya michuano ya Afrika dhidi ya Zimbabwe (Mighty Warriors).

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo itafanyika kesho (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Washambuliaji hao wa Taifa Stars wamewasili saa 7.25 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines wakitokea Khartoum, Sudan ambapo jana (Mei 16 mwaka huu) timu yao ya TP Mazembe ilicheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya huko.

Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mechi hiyo, kwani kimepata mechi za kirafiki na mazoezi ya kutosha kwenye kambi iliyoanzia Tukuyu mkoani Mbeya ambapo kulikuwa na utulivu mkubwa.

Naye Kocha Msaidizi wa Zimbabwe, Kalisto Pasuwa amesema hawaifahamu vizuri Taifa Stars lakini wamekuja kwenye mechi hiyo itakayoanza saa 10 jioni kwa ajili ya kushinda, na kuwataka washabiki wajitokeze kwa wingi kuona kiwango cha timu yake.

Milango kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Ghana wakiongozwa na Joseph Odartei Lamptey itakuwa wazi kuanzia saa 6 kamili mchana, na tiketi zitapatikana katika magari maalumu uwanjani hapo.

Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu, sh. 10,000 kwa VIP C na B, na sh. 20,000 kwa VIP A.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)