RC SHIGELLA:WANAWAKE WANA MCHANGO MKUBWA KWA JAMII

March 10, 2018
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto akilakiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa wakati alipokwenda kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake dunia ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Kange jijini Tanga
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa wakati alipokwenda kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake dunia ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Kange jijini Tanga
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akisalimia na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim wakati alipokwenda kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake dunia ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Kange jijini Tanga
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto akilakiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Tanga mara baada ya kuwasilia kwenye viwanja hivyo wakati alipokwenda kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake dunia ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Kange jijini Tanga kulia ni mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa anayefuata ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (Ras) Mhandisi Zena Saidi
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akisalimiana na watumishi mbalimbali wakati alipokwenda kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake dunia ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Kange jijini Tanga
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akisalimiana na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemens wakati alipokwenda kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake dunia ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Kange jijini Tanga
 Sehemu ya wanawake wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Kange Jijini Tanga
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katika akipokea maandamano ya wanawake wakati wa maadhimisho ya siku yao kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa benki ya Amana wakati alipotembelea banda lao kwenye maadhimisho hayo wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (Ras) Mhandisi Zena Saidi
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa benki ya Amana wakati alipotembelea banda lao kwenye maadhimisho hayo wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (Ras) Mhandisi Zena Saidi
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi wakiangalia bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wanawake
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kulia akifuatilia matukio mbalimbali kwenye maadhimisho hayo kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi na anayefuatia ni Diwani wa Kata ya Maweni(CCM) Calvas Joseph
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza wakati wa maadhimisho hayo
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza katika maadhimisho hayo
 Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga,Faidha Salim katika akishiriki kuimba wimbo na wakina mama wa ngomba ya msanja wakati wa maadhimisho hayo
 Diwani wa Viti Maalumu (CCM) Kata ya Chumbageni Saida Gadafi akimtunza msaanii aliyekuwa akitumbuiza kwenye maadhimisho hayo
Sehemu ya wanawake kutoka Taasisi ya BRAC wakifuatilia maadhimisho hayo 
 
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella amesema wanawake wana mchango  mkubwa kwa jamii hivyo wanapaswa kuheshimiwa na kupewa kipaumbele ili waweza kupata mafanikio.

Aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo alisema lazima jamii iwaheshimu wanawake na kuwapa nafasi ili waweze kutimiza ndoto zao kwani wao ndio kila kitu.

Alisema wanawake ndio nguzo kubwa ya kuweza kusaidia chachu ya maendeleo kwa jamii hivyo lazima wapewe nafasi ya kuchangamkia fursa zilizopo.

"Tuna uhakika na mama zetu waliotuzaa,kutulea na kutunyonyesha lakaini hatuna uhakika na Baba zetu maana wao  hivyo lazima tuwaheshimu na kuwapa kipeumbele kwa kila jambo "Alisema.

Alisema mwanamke ni kila kitu katika maisha hivyo wanastahili kupewa pongeza kutokana na namna wanavyosaidia kuilea jamii na hatimaye kuweza kutimiza malengo yao.

"Sisi duniani kote tuna uhakika na mama zetu maana wao ndio waliotuzaa na kutulea na kunyonyesha lakini hatuna uhakika na baba zetu hivyo lazimatuwaheshima na kuwajali maana ndio wametufikishaa hapa mwanamke ndio kila kitu ni mama, dada, shangazi,bibi na my sweet darling Alisema RC Shigella.

Hata hivyo alisema ni vema wanawake waheshimiwe na ndio maana serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli anawapenda na kuwathaminina ndio maana akamteuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu katika nafasi ya juu kumsaidia.

"Hivyo hii inaonyesha namna anavyowathamini na kutambua mchango wenu kwenye kuchochea kasi ya ukuaji waa maendeleo"Alisema

Alisema tuna wajibu wa kuhakikisha tunaenzi jitihada za Rais wetu kwa kuthamini wanawake na kuwapa nafasi ili waweze kutimiza malengo yao waliojiwekea kufikia.

Mkuu huyo wa mkoa alisema jamii inawajibu wa kuwawezesha wanawake kupitia Taasisi mbalimbali kwa kuwapa nafasi za uongozi kwenye viwanda vilivyopo mkoani Tanga kwa kuzingatia jinsia na usawa.

RAIS MAGUFULI AZINDUA BARABARA YA ISAKA-USHIROMBO, AZUIA WANANCHI KUHAMISHWA KUPISHA UJENZI WA CHUO

March 10, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati wa dhifa ya uzinduzi wa barabara ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132, Leo 10 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Sehemu ya mamia ya wananchi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli  wakati wa sherehe za uzinduzi wa barabara ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132, Leo 10 Machi 2018.

Na Mathias Canal, Kahama-Geita 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Leo 10 Machi 2018 amezindua barabara ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132 iliyojengwa na kukamilika kwa kiwango cha lami.

Katika sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo katika Eneo la Nyasubi, Kahama Mjini Mhe Rais Magufuli amesema kuwa Barabara hiyo ni chachu ya ukuaji wa uchumi na kiungo cha Mikoa ya Shinyanga, Geita na Kagera pia ni sehemu ya kurahisisha na kuimarisha mahusiano chanya ya kibiashara baina ya nchi za Uganda, Rwanda na Burundi.

Rais Magufuli amewataka wafanyabiashara nchini kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa kwani serikali inatumia zaidi ya shilingi Bilioni 269 kununua dawa nje ya nchi hivyo endapo watajenga viwanda hivyo vya dawa serikali itawanufaisha wafanyabiashara wa ndani ya nchi kwa kununua bidhaa hizo.

Kama alivyojipambanua katika kuwatetea wanyonge Mhe Rais Magufuli ameagiza kutohamishwa wananchi waliovamia eneo la ardhi ya Wizara ya Elimu, wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (MWAMVA), na kusema kuwa wananchi hao ndio waliompigia kura na hatimaye kuwa Rais wa nchi hivyo hawapaswi kunyanyaswa.

Aidha, aliwataka wananchi wengine kutoendelea na ujenzi wa nyumba za makazi katika Mtaa wa Igomelo, Kata ya Malunga ili eneo lililosalia la hekari 40 ndilo litumike kujenga chuo hicho.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewashukuru wabunge wa Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wabunge wengine wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitisha sheria ya madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 ambayo inataka kuwa na uchumi fungamanishi kwa wananchi kupitia rasilimali zao.

Aidha, serikali imekuwa ikikusanya mapato mengi kupitia sekta ya madini ambapo mwaka 2014/2015 ilikusanya jumla ya shilingi Bilioni 168.09, mwaka 2015/2016 ilikusanya zaidi ya Bilioni 205, mwaka 2016/2017 ikikusanya jumla ya Shilingi Bilioni 213.365

Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Bugalama (CHADEMA), Katibu mwenezi Kanda ya ziwa  (CHADEMA) na wanachama wengine 50 wamejivua uanachama wa Chadema mbele ya Rais Magufuli na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi huku wakisema kuwa wameridhishwa na utendaji wake katika kuwatumikia watanzania.

Mradi wa ukarabati wa barabara hiyo ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132 iliyojengwa na kukamilika kwa kiwango cha lami ni sehemu ya barabara kutoka Isaka hadi Lusumo yenye kilomita 1334 iliyokuwa imejengwa mwaka 1980 na mwanzoni mwaka 1990 hivyo imetumika kwa kipindi cha miaka 20 bila kufanyiwa marekebisho.

Dhifa ya uzinduzi wa barabara hiyo umehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainab Telack, Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Mhe Elius John Kuandikwa (Mb), Naibu waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale, na Wabunge wa Mkoa wa Shinyanga.


MNEC SALIM ASAS BADO ANAUMIZWA NA USHINDI WA MBUNGE MSIGWA WA MWAKA 2015

March 10, 2018
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas  akiwahutubia wajumbe wa baraza kuu la umoja wa wanawake manispaa ya Iringa na kusema kuwa bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho hakukitegemea.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo akimtoa hofu MNEC Salim Asas juu ya kukomba jimbo baada ya kulipoteza kwa kusalitia mwaka 2015
 Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa kwenye baraza hilo kwa ajili ya kujifunza na kutoa mapendekezo pale wanapopata nafasi
 Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa walipokuwa wakimsikiliza kwa umakini mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas alipokuwa anatoa ya moyo kuhusu kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2015

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho hakukitegemea.

Akizungumza wakati wa baraza la UWT manispaa  ya Iringa Asas alisema kuwa usaliti ulifanywa katika uchaguzi wa mwaka 2015 umekuwa ukimuumiza hadi sasa na kitendo anafikiri kitadumu moyoni mwake hata kwa miaka kumi kwakuwa bado anakumbuka mara kwa mara.

“Naombeni niongee ukweli kitendo kilichofanywa na wanaccm wa manispaa ya Iringa katika uchaguzi wa mwaka 2015 kilikuwa kitendo ambacho ni usaliti mkubwa ambao unaumiza sana kichwa changu” alisema Asas

Asas alisema kuwa uchaguzi huo kulikuwa na wanaccm wengi ambao mchana walikuwa ccm na usikuwa walikuwa kwa wapinzani hivyo lazima tuondoe usaliti kwenye chama bila hivyo tutaendelea kushindwa kila siku.

“Unakuta rasilimali zilizokuwa zinatolewa na  chama cha mapinduzi zote zinatumika kwa wapinzani kuhakikisha wanaiangusha ccm,sasa hicho kitu ndio ambacho kinaniumiza sana kichwa hadi hii leo” alisema Asas

Asas aliutaka umoja wa wanawake (UWT) manispaa ya Iringa kufanya kazi kwa umoja unatakiwa na kuhakikisha kuwa ccm inakuwa ila na isiyo na makundi ili kufika mwaka wa uchaguzi wanashinda kwa kishindo kwa kutumia umoja wao.

“Nawaombe muutunze umoja huu ambao sasa mnao hadi kipindi cha uchaguzi wowote ule ambao upo mbele yetu na kuhakikisha kuwa tunashinda kila chaguzi kwa kishindo kwa kuwa nyie akina mama ndio huwa mnakula ambazo haziamishiki” alisema Asas

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo alimuhakikishia MNEC Salim Asas kuwa kosa lilofanyika mwaka 2015 halitajirudia tena katika chaguzi yoyote ambayo itakuwa inafanyika katika manispaa ya Iringa.

“Ndugu MNEC kwa kweli tumejifunza na tunajutia kitu kilichofanyika mwaka 2015 hivyo tunakuhadi kuwa kwenye umoja wetu wa wanawake Manispaa ya Iringa hakitaa tokea kama kilivyotokea,na tutashinda chaguzi zetu kwa kuwa kila mtu anaumia na kilichotokea mwaka 2015” alisema Jongoo

Jongoo alimshukuru MNEC kwa kurudisha umoja kwa wanaccm mkoa wa Iringa kwa kuwa anafanya kazi kubwa kuhakikisha kila kitu kinakuwa kama kinavyokusudiwa na kuhakikisha umoja ambao umetengenezwa na viongozi wapya unadumu hadi watakapomaliza uchaguzi.

“Mheshimiwa MNEC umoja ambao tunao hivi sasa tunatakiwa kuulinda na kuudumisha hadi kipindi cha chaguzi zote na kuhakikisha kuwa ccm inashinda kwa kushinda na kuendelea kuwa ngoja ya chama hicho kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Jongoo

RAIS MAGUFULI AZINDUA BARABARA YA UYOVU-BWANGA (KM 45)

March 10, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa uzinduzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa kilomita 45, Leo Jumamosi 10 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akikata utepe ishara ya uzindua wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa kilomita 45, Leo Jumamosi 10 Machi 2018. 
Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akimshuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule na vituo vya afya Wilayani bukombe wakati wa dhifa ya uzinduzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa kilomita 45, Leo Jumamosi 10 Machi 2018.
Mamia ya wananchi Wilayani Bukombe Mkoa wa Geita wakimlaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuzindua barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa kilomita 45, Leo Jumamosi 10 Machi 2018. 

Na Mathias Canal, Ushirombo-Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Leo Jumamosi 10 Machi 2018 amezindua rasmi barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa kilomita 45 ambayo imekamilika kwa kujengwa kwa kiwango cha lami.

Katika dhifa hiyo iliyofanyika katika Kijiji cha Runzewe Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita, Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ni nchi ya tano kwa ukuaji wa uchumi barani Afrika hivyo wananchi wanapaswa kuwapuuza wanasiasa wanaohubiri kuporomoka kwa uchumi kwa matakwa ya kujiimarisha kisiasa.

Alisema katika kipindi cha miaka miwili serikali imefanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha sekta mbalimbali kwa usimamizi nzuri katika rasiliamali Madini, kuboresha sekta ya elimu ambapo wanafunzi wanasoma bure kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari.

Alisema kuwa, bajeti ya mwaka 2015 katika sekta ya afya ilikuwa ni Bilioni 31 lakini serikali kwa kutambua umuhimu wa kuimarisha afya za watanzania ambapo sasa bajeti imefikia shilingi Bilioni 239 na hayo ni matokeo ya umoja na amani iliyopo nchini.

Rais Magufuli amesema amani iliyopo nchini Tanzania imejengwa chini ya uasisi wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ikasimamiwa vyema na marais wastaafu Mhe Ally Hassan Mwinyi, Mhe Benjamin Mkapa pamoja na Mhe Jakaya Mrisho Kikwete.

"Mambo yanayofanywa na serikali hayawezi kuyafurahisha mataifa mengine hivyo mataifa hayo yanawatumia watanzania wenyewe kutengeneza chuki dhidi ya serikali yao" Alikaririwa Rais Magufuli

Aliongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo imekuwa sehemu ya Kuchochea shughuli za maendeleo ya kijamii katika usafirishaji wa mazao, kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa, sambamba na kuongeza pato la Mkoa wa Geita na Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Rais Magufulu amewasihi wananchi Kutovamia hifadhi za Taifa badala yake kuwa wavumilivu na kuiacha serikali ifanye, kwani watatumwa wataalamu wa Wizara ya ardhi na maliasili ili kuratibu na kuona namna ya kuyagawa maeneo kwa ajili ya wafugaji na wakulima.

Naye, Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe Elius John Kuandikwa na Mtendaji Mkuu wa Tanroads nchini Mhandisi Patrick Mfugale walisema kuwa usanifu wa barabara hiyo ulifanywa mwaka 2006 na kampuni mbili za kitanzania kwa jumla ya Shilingi Milioni 207.6 ambapo barabara hiyo imesanifiwa kubeba na kutumika kwa miaka 20 kwa upana wa mita 9.5

Walisema Ujenzi wa barabara hiyo uliokamilika Octoba mwaka jana umegharimu jumla ya shilingi Bilioni 45.454, ambapo msimamizi amelipwa shilingi Bilioni 2.3 huku akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa mkandarasi hadi mwezi Octoba mwaka huu. 

Dhifa ya uzinduzi wa barabara hiyo umehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Mhe Elius John Kuandikwa, Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale.

SORING WOMEN INTERNATIONAL WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2018

March 10, 2018
Meneja wa Udhibiti na Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta-Yambi akizungumza wakati wa mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women International iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Soring Women International, Luphurise Lema akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2018 aliyoandaa jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa Clouds FM/TV na mchoraji katuni mahiri, Ali Masoud 'Masoud Kipanya'  (katikati) akiwa katika moja waendesha mjadala wa nafasi ya mwanamke katika maadhimisho ya siku wanawake Duniani  leo jijini Dar es Salaam. Kutoka ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura, na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soring Women International, Luphurise Lema (kushoto).
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura (katikati) akichangia mada ya nafasi ya mwanamke katika jamii katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mchoraji wa Katuni na Mtangazaji wa Clouds Radio/TV, Ali Masoud 'Masoud Kipanya' (kushoto)  na Mratibu wa UN Global Compact Network  Tanzania, Emmanuel Nnko (kulia) na Dk. Florence Temu kutoka AMREF (wa kwanza kulia).
 Mchangiaji wa Shirika la AMREF, Dk. Florence Temu akichangia mada katika siku wanawake duniani.
 Mratibu wa UN Global Compact Network  Tanzania, Emmanuel Nnko akichangia mada katika siku wanawake duniani.
Waendesha mjadala wa nafasi ya mwanamke wakiwa katika picha ya pamoja.
Meneja wa Udhibiti wa Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta - Yambi akitoa shukrani zake kwa  wageni waalikwa katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya Soring Women International, Luphurise Lema akitoa shukrani za pekee kwa wadau waliojitokeza kumuunga mkono katika shughuli yake ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Dunia aliyoiandaa jijini Dar es Salaam.
 Mwasisi wa Vikoba nchini Tanzania, Devota Likokola akichangia mada.
 Akinamama waliohudhuria katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. Wanawake wanaweza kuleta mabadiliko ya maendeleo katika jamii ikiwa watasimama imara kwa pamoja na kuwezesha wenzao ambao hawana elimu ya kutosha. Hayo yamesemwa na mapema leo Machi 10, 2018 na Meneja wa Udhibiti na Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta-Yambi wakati akizungumza katika mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women International iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa wanawake wanaweza kufanya mabadiliko kwa kila mmoja kuwa imara na kuamsha wanawake wengine ambao hawajafikiwa na fursa zikiwemo cha uchumi au za ubunifu za kuweza Marsha amasema kuwa kuadhimisha siku ya wanawake lazima kulete mabadiliko sio kuadhimisha tu halafu hakuna matokeo chanya yanayoonekana kwa wanawake tutakuwa hatujatenda haki katika kujipambanua ili kuweza kufikia malengo kwa wale wale walioasisi. Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Soring Women International, Luphurise Lema amesema kuwa wakati alipokuwa anafanya kazi aliona kuwa watu waliosoma nje ya ndio wana akili lakini alitambua kuwa sio hivyo tofauti yake ni kujiamini tu na kuamini kila kinachofanyika hata mwanamke anaweza. Luphurise amesema kuwa kila mwanamke asimame imara na kuamini kila anachofanya anaweza kuleta mabadiliko hata ya dunia. Nae mtangazaji wa Clouds FM/TV na mchoraji katuni mahiri Ali Masoud ‘Masoud Kipanya’ ambaye ni mchora katuni na mtangazaji wa Cloud Radio/Tv ja ya Watengeneza mjadala, Ali Masoud ‘Masoud Kipanya’ amesema kuwa wanawake ni watu muhimu na majukumu anayofanya mwanamke akipewa mwanaume hawezi kuyafanya isipokuwa alioanzisha kauli kuwa hawawezi ndio imewafikisha wanawake lakini wakaze buti wanaweza kuleta mabadiliko.