January 30, 2014
NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI AKIONGEA NA WATUMISHI
IMG_0785Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel akiongea  na Watumishi wa Wizara naTaasisi zake katika Kikao cha cha kujadili Fursa mbalimbali kwa Maendeleo ya Wizara  kilichofanyika  Jijini Dar es Salaam leo
IMG_0828Mtendaji Mkuu wa TSN Bwana Nderumaki akiwasilisha mada katika Kikao cha kujadili Fursa mbalimbali kwa maendeleo ya Wizara na Taasisi zake kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Benjamin Sawe wa Wizara ya Habari)

January 30, 2014

SERIKALI YA TANZANIA NA FINLAND ZATILIANA SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO WA KUFANYA KAZI KWENYE SEKTA YA MADINI

1Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisalimiana na Waziri Mkuu wa Finland,  Jyrki Katainen wakati alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, wakati Serikali za nchi hizo mbili ziliposaini Mkataba wa Makubaliano ya Kufanya Miradi ya Pamoja ya Sekta ya Madini.
2Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen kabla ya kutiliana na saini Mkataba wa Makubaliano ya Kufanya Miradi ya Pamoja ya Sekta ya Madini kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam .
3Waziri Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen akizungumza na wadau wa sekya  ya Madini wa Serikali ya Tanzania na Finland, wawakilishi wa taasisi za jiolojia na wadau wa sekta hiyo kutoka nchi hizo mbili, kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
January 30, 2014

NAIBU WAZIRI WA MAJI AZURU DAWASA NA DAWASCO

IMG_0417Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi za DAWASA. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Said El Maamry na Kulia ni Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa. IMG_0464Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Said El Maamry. IMG_0480Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akizungumza katika mkutano alipotembelea DAWASA. IMG_0560Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala akimwonyesha ripoti ya DAWASCO, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO.
January 30, 2014

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA KILIMANJARO YATEMBELEA KIJIJI CHA RUVU JIUNGENI KILICHOKUMBWA NA MGOGORO WA ARDHI

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ruvu Jiungeni, iliyoko katika Kata ya Ruvu, wilayani Same, alipotembelea kijiji hicho akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, kijiji hicho kimekuwa katika mgogoro wa wakulima na wafugaji kwa zaidi ya miaka 20 sasa tangu mwaka 1987.
Wanakiji katika kijiji cha Ruvu Jiungeni, iliyoko katika Kata ya Ruvu, wilayani Same, wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa mkoa huo, Leonidas Gama wakati alipotembelea kijiji hicho kutatua mgogogro wa siku nyingi kati ya wakulima na wafugaji

Wanakiji katika kijiji cha Ruvu Jiungeni, iliyoko katika Kata ya Ruvu, wilayani Same, wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa mkoa huo, Leonidas Gama wakati alipotembelea kijiji hicho kutatua mgogogro wa siku nyingi kati ya wakulima na wafugaji
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruvu Jiungeni Lepuruka Laize, akifafanua kiini cha mgogoro wa siku nyingi baina ya wakulima na wafugaji katika kijiji, mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
January 30, 2014


MWILI WA SHEKH WA MKOA WA MARA WAWASILI UWANJA WA NDEGE MUSOMA
 NDEGE ILIYOBEBA MWILI WA MAREHEMU SHEKH ATHUMANI MAGEE

 MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA AKIELEKEA KWENYE NDEGE KUONGOZA WAOMBOLEZAJI
January 30, 2014

Lowassa ameanza safari, ni ndefu kiasi gani?

 
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akiwasalimia wananchi waliohudhuria sherehe za mwaka mpya nyumbani kwake wakiwamo wabunge, viongozi wa dini, wafanyabiashara wakubwa na wakazi wa Mkoa wa Arusha na viongozi wa CCM. Kushoto ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Godluck ole Medeye na kushoto mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Onesmo ole Nangole. Picha ya Maktaba 
*******
“Nimefarijika sana leo kuwaona hapa marafiki zangu wengi. Ninapowatazama hadi machozi yananitoka na kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani nyote mnajua nia na ndoto yangu…WanaCCM msiwe na shaka, tutavuka kwa nguvu zetu... Wingi wenu huu unanipa faraja katika safari yetu na kwa kumtegemea Mungu tutashinda.”  ni kauli ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Lowassa alitangaza hivi karibuni kuanza rasmi kwa safari hiyo aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo anasema itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, majisafi na maendeleo ya uhakika.
Alitoa kauli hiyo katika ibada ya shukrani na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika ya Monduli Mjini mkoani Arusha.
Bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, Lowassa anawataka waliohudhuria ibada hiyo waungane na kaulimbiu yake, ‘Tulifurahi pamoja, tulihuzunika pamoja na tutashinda pamoja’.
Hafla hiyo ya kimkakati, ilihudhuriwa  na baadhi ya wabunge, wengi wakiwa wa CCM, wenyeviti wa mikoa kadhaa wa chama hicho, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM, viongozi wa jumuiya za chama na wengineo.
Licha ya kutoweka bayana aina ya safari anayoanza, Lowassa ni miongoni mwa wanaCCM wanaotajwa kuwa wanaowania urais, kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Dalili hizi za Lowassa kuutaka urais na kutafuta kabla ya kipenga kupulizwa, zimeishtua CCM na kumtahadharisha kuwa atapoteza sifa ya kupitishwa ifikapo 2015.
Safari tangu 1995
January 30, 2014

TAARIFA MAALUM YA POLISI MKOA WA DODOMA KUKAMATWA KWA MANAMKE LEO LIVE!!


Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi DAVID MISIME (SACP) anawashukuru wananchi wa kondoa kwa jinsi walivyotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kufanikisha kumkamata mwanamke aliyeiba mtoto mchanga wa siku moja tarehe 20.01.2014 huko katika maeneo ya Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.

Mtoto huyo wa jinsia ya kiume alizaliwa tarehe 19.01.2014 huko katika zahanati ya Thawi. Mama yake mzazi SALMA S/O ZUBERI, mpare, mkazi wa kijiji cha Mwembeni, Kata ya Changaa - Kondoa, alipatwa na matatizo ambayo yalimlazimu kuhamishiwa katika hospitali ya Wilaya ya Kondoa. Wakati mama huyo akiwa anapatiwa matibabu na daktari alibidi mkwe wake aitwaye HADIJA D/O SAID awe anambeba mtoto huyo mchanga. Alitoka naye nje na ndipo akakutana na AMINA D/O JUMANNE MWASI, 22 Yrs, mkazi wa Mningani, Kondoa mjini, alianza akuongea na nyanya wa kichanga hicho cha siku moja baada ya kuzoeana na mwanamke ambaye alijieleza kuwa amelazwa hapo hospitali kutokana na ujauzito aliomba kumshika au kumpakata mtoto huyo.

Mama mkwe huyo alitoka kwenda kutafuta chakula ili mgonjwa atakapomaliza matibabu aweze kula. Baada ya muda alirudi akashangaa kutokumwona mama ambaye naye alikuwa amejifanya ni mjamzito haonekani, alijaribu kumtafuta maeneo mbalimbali na kuuliza watu mbalimbali bila mafanikio ndipo akaamua kutoa taarifa Polisi.

Kwa vile taarifa zilikuwa zimetolewa maenoe mbalimbali wananchi wema walimtilia mashaka mwanamke aliyeiba mtoto na andipo kwa ushiriano mkubwa baada ya kumfuatilia kwa karibu sana Polisi wakafanikiwa kumtia mbaroni tarehe 29.01.2014 wakati alipompeleka motto huyo hospitali ya Wilaya kwani mtoto alianza kuugua.

Baada ya mahaojiano alikubali kuwa alimuiba mtoto huyo na hata uchunguzi wa kitaalamu umebaini mwanamke huyo hajajifungua siku za karibuni.

Ninatoa wito kwa wananchi kutokuamini watu wasiwafahamu kwa asilimia mia, hata kama wanalugha nzuri kiasi gani pia nawatahadharisha wanawake waliokosa watoto kwa muda mrefu utatuzi wake sio kuiba watoto wa watu wengine.

DAVID MISIME – SACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA
chanzo blog ya wananchi.
January 30, 2014

NAIBU WAZIRI WA FEDHA MH;MWIGULU NCHEMBA ATEMBELEA OFISI NDOGO ZA HAZINA MKOA WA JOMBE

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara,Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Njombe wakati alipotembelea Ofisi Mpya ya Hazina Ndogo Mkoa wa Njombe mapema leo Asubuhi ya Tar.30/01/2014Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara Mh;Mwigulu Lameck Nchemba akibadilisha mawazo na Mkuu wa Wilaya wa Wanging'ombe Wakati wakitoka Kutembelea Ofisi Ndogo Mkoa wa Njombe. .
Mh;Mwigulu Nchemba akioneshwa moja ya Chumba cha Mapokezi ya Wageni kwenye Ofisi za Hazina Ndogo.
Picha zote na Habari Kwanza Blog
January 30, 2014

NAIBU WAZIRI ATEMA CHECHE TRA,AWAPA AGIZO LA KUHAKIKISHA HUDUMA ZOTE ZA TRA ZINAPATIKA MKOA WA NJOMBE

Naibu Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba hii leo akiwa kwenye Ziara yake ya Kikazi Mkoani Njombe ameagiza Bodi na Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Kuhakikisha Wanajenga Ofisi ndani ya Mkoa wa Njombe(M) haraka sana ilikuondoa Usumbufu Kwa Wafanyabiashara na Wananchi wanapohitaji huduma muhimu kama Leseni,Tin Number n.k.
 
Akizungumza na Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe hii leo (30/01/2014) kwenye Ukumbi wa TURBO,Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa Ofisi yake imedhamiria kuhakikisha Njombe inapatiwa huduma zote zinazohusu TRA ilikuondoa usumbufu wanaoupata Wananchi hivi sasa kusafiri nje ya Mkoa kupata huduma.

Kwa muda mrefu Njombe kumekuwa na Ofisi ya TRA ambayo inatoa baadhi ya huduma kama Malipo ya Kodi,Kwenye Ulipaji wa Leseni,Tin No, n.k Wananchi wamekuwa wakilazimika kwenda Mikoa ya karibu kama Mbeya na Iringa kwaajili ya Kushughulikia huduma hizo.
chanzo;Habari kwanza Blog
January 30, 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU DAR

 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri na Manaibu Waziri waliokuwa wakiapisha Ikulu Dar es Salaam, leo wakati alipokuwa akiwasili katika hafla hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Ummy Mwalimu, kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.

 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Kaika Saning’o Telele, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakia katika picha ya pamoja na Waziri na Manaibu Waziri walioapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wapya katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka (kulia) ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.
January 30, 2014

*TAMKO LA JOHN MALECELA KUHUSU WANAOJINADI KUWANIA URAIS 2015


Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.

Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhi ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUTOANDIKA HABARI ZA UCHOCHEZI

January 30, 2014
Na Elizabeth Kilindi,Bumbuli
WAANDISHI   wa habari nchini wametakiwa kutoandika habari zinazochochea mifarakano katika jamii kwa misingi ya chuki,dini rangi au itikadi za kisiasa na badala yake watumie kalamu zao kuandika habari zitakazoleta  manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Diwani  wa  Kata  ya  Millingano,Hozza  Mandia wakati  akizungumza na TANGA RAHA BLOG  na kueleza kuwa waandishi wanatakiwa kuzingatia haki za pande zote mbili na kusisitiza uadilifu katika kutoa habari hizo.
WAZEE WAIOMBA SERIKALI KUWAJENGEA UZIO.

WAZEE WAIOMBA SERIKALI KUWAJENGEA UZIO.

January 30, 2014
Na Elizabeth Kilindi,Muheza.

WAZEE  wanaoishi kwenye kambi ya Ukoma Iliyopo Ngomeni wilayani Muheza wameiomba serikali kuwajenga uzio kwenye kambi hiyo ili kuwanusuru na vibaka wanaowavamia mara kwa mara na kupora mali zao ikiwemo mifugo pamoja na  ujenzi wa vyoo bora.

Ombi hilo wakati  wakipokea Msaada wa nguo na chakula kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Tanga  wakati taasisi hiyo ilipo kwenda kutembelea kambi hiyo ili kubaini changamoto zinazowakabili.

HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA YAKUSUDIA KUTUMIA BILIONI 61.

January 30, 2014
                            Na Elizabeth Kilindi,Tanga.
                     
HALMASHAURI  ya  Jiji la Tanga imekusudia kutumia  zaidi ya tsh billion 61.1 kwa ajili  ya uendeshaji  wa  miradi mbalimbali ya  Jiji hilo  na utoaji wa huduma kwa wananchi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015.
 
Hayo yalielezwa na meya wa Jiji la Tanga, Omari Gulled wakati akitoa taarifa kwa wananchi  kuhusiana na mchakato wa bajeti ya halmashauri hiyo na mipango  iliyopo  ya  uendeshaji wa shughuli za maendeleo kwa wananchi wake.

SERIKALI YATAKIWA KUONDOA KWENYE VIFAA VYA UJENZI WA NYUMBA.

January 30, 2014
Na Elizabeth Kilindi,Mkinga.
MWENYEKITI  wa kamati ya   kudumu ya Bunge ya  Ardhi, Maliasiri na Mazingira James Lambeli, ameitaka serikali kuondoa kodi  kwenye vifaa vya  mradi wa ujenzi wa nyumba za  gharama  nafuu unaoendeshwa na Shirika la Nyumba Tanzania (NHC)  ili kumuwezesha mwananchi wa hali ya chini kuondokana na makazi duni.

Lembeli aliyasema hayo  baada ya  taarifa ya mradi huo iliyosomwa hapo juzi, mbele ya kamati hiyo na Kaimu Mkurugenzi wa uendeshaji wa shirika hilo, Benedict  Kilimba na kueleza kuwa kodi za serikali zimesababisha  bei ya nyumba hizo kuwa kubwa.