WATOTO 13,266 MKOANI TANGA WANUFAIKA NA HUDUMA ZA AFYA ZITOLEWAZO NA UHIC

July 07, 2016
Lee Kwiwoon akuzungumza na washiriki wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo vijana(Keepers) katika vijana waliofundishwa kuhudumia watoto katika masuala ya Afya na Lishe
   
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika mafunzo hayo

JUMLA ya watoto 13,266 wenye umri chini ya miaka 10 wamenufaika mkoani hapa na huduma za afya  zitolewazo na taasisi ya Kikorea ijulikanayo kama UHIC (United Help for International Children) .
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo kanda ya Tanzania,  Lee Kwiwoon alitoa taarifa hiyo hapa mwishoni mwa juma lililopita katika mkutano uliojumuisha madaktari, manesi na wahudumu wa afya kutoka wilaya tatu za mkoa huu, ambazo zimelengwa katika mradi wa taasisi hiyo.

Mkurugenzi huyo alisema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutoa huduma kwa watoto wenye matatizo mbalimbali ya kiafya yanayowapata wenye umri chini ya miaka 10.

Aliwaeleza wanasemina hao kwamba watoto wengi walio katika umri chini ya miaka 10 hukumbwa na magonjwa mengi, hasa malaria, upungufu wa damu na utapiamlo. Magonjwa mengine ni pamoja na kifua, kuzaliwa njiti na kuharisha. 

Lee aliwaambia maofisa na manesi pamoja na wahudumu wa afya kwamba jukumu kubwa la taasisi yake ni kuzuia magonjwa yanayowanyemelea zaidi watoto wadogo pamoja na kuhakikisha watoto hao wanakua katika afya bora.

Alifahamisha kwamba taasisi hiyo ya UHIC imeanzisha mradi ujulikanao Keepers' ambao unawafundisha na kuwapatia mafunzo vijana wanaotoa huduma ya kuokoa maisha ya watoto kutoka janga la njaa, maradhi na kuwasaidia waishi katika mazingira mazuri ya kiafya.

"Afya na uzuiaji wa magonjwa yawapatayo watoto wengi mkoani Tanga ni suala linalozungumzika na hivyo kuwafanya wadau kuamua kujitolea kuanzisha taasisi zitakazosaidia kuondoa adha hiyo kwa watoto wetu", alisema Lee.

Mkurugenzi huyo alibanisha kuwa taasisi ya UHIC ni ya kimataifa iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa huduma endelevu za afya kwa watoto waishio maeneo ya vijijini (pembezoni) mkoani hapa.

Alisema wamechagua wilaya tatu ambazo ni Pangani, Muheza na Tanga kuwa za mfano katika kuanza na mradi huo ambapo jumla ya vijiji 27 vitahusika. Alisema taasisi yake ina jukumu la kugawa dawa na kwamba wahudumu 24 tayari wamekwishapatiwa mafunzo ya kuhudumia watoto hao katika vijiji husika.

Akizungumza katika mkutano huo, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Maggid alisema mkoa umepoteza maisha ya watoto wapatao 653 kutokana na magonjwa mbalimbali, yakiwemo malaria, kikohozi, upungufu wa damu na kuharisha.

Pamoja na kupongeza msaada huo wa Korea akisema kuwa umefika wakati ukihitajika sana, lakini akataka wataalamu wanaopelekwa kwenye vijiji hivyo wapewe ushirikiano unaofaa.

Mapema, akifungua semina hiyo, Kaimu Mkuu wa Mkoa waTanga, Mayassa Hashim alisikitishwa na vifo hivyo ambapo alisema vingeweza kuzuilika kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wazazi . 

Hata hivyo, Mayassa ambaye pia ni OfisaElimu wa Mkoa, alieleza matumaini kwamba ujio wa taasisi hiyo pamoja na madawa na wataalamu wao itasaidia kuondoa vifo visivyotarajiwa vya watoto wadogo.

AKINAMAMA DAKAWA WAFUGA NYUKI KUPAMBANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

July 07, 2016


Ofisa Nyuki wa Wilaya ya Mvomero, Oscar Kunambi (aliyechuchumaa kushoto) akisaidiana na mwanakikundi cha Dakawa Green Voices, Neema Obeid, kuweka vizuri mzinga.
DK.KIGWANGALLA AFUNGA RASMI JUBILEE YA MIAKA 50 YA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO JIJINI MWANZA

DK.KIGWANGALLA AFUNGA RASMI JUBILEE YA MIAKA 50 YA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO JIJINI MWANZA

July 07, 2016

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za watu binafsi zikiwemo zile za kidini na kijamii katika kufanikisha maendeleo ambapo amelipongeza Kanisa la Waadventista wa Sabato la Ilemela Jijini Mwanza kwa hatua yake kujenga Hospitali ya Kisasa ambayo itakuwa msaada katika Wilaya hiyo.

Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la ufungaji wa sherehe za miaka 50 ya Jubilee ya kuanzishwa Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika jiji la Mwanza tukio lililofanyika siku ya Julai 3.2016 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Akitoa hotuba za kufunga sherehe hizo, Dk. Kigwangalla amelipongeza kanisa la Kirumba kuwa na jubilee ya miaka 50 Lakini pia amelipongeza kwa huduma ya malezi ya vijana wa kanisa hilo wakingali wadogo na kwamba kwa kufanya hivo ni kuliandaa kanisa na Taifa kwa ujumla kuwa na viongozi waadilifu.

Dk. Kigwangalla ameyataka madhehebu ya dini yawe mstari wa mbele katika kukemea maovu ili Taifa lidumu kuwa na Amani.

“Uwepo wenu tunaupongeza kwani naamini mumekuwa mstari wa mbele katika kuliombea Amani Taifa hili na pia kuwaombea ulinzi watu mbalimbali pamoja na kutoa misaada, huduma za Afya na mambo mengine mbalimbali. Hii ni faraja sana na Serikali tutaendelea kuwaunga mkono.

Aidha, katika hutuba hiyo, Dk. Kigwangalla aliwahakikishia uongozi wa kanisa hilo kuwa Hospitali yao mpya inayojengwa Serikali itakuwa nao bega kwa bega na kuaahidi kutoa ushirikiano katika suala hilo la ujenzi pamoja na uendeshaji wa Hospitali hiyo kwa lengo la kuboresha afya za Wananchi wote.

Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla alikemea vitendo vilivyoanza kushamili ikiwemo baadhi ya watu kushabikia masuala ya mapenzi ya jinsia moja ambapo ikiwemo suala la ushoga.

“Serikali haipo tayari kuona vitendo vya ushoga vinafanyika kwa wananchi wake lakini pia kuzitangaza kwa jamii. Wizara yangu itakutana na NGOs, zote za Kijamii na taasisi zilizosajiliwa ambazo pia zingine zipo chini ya Wizara yetu kukaa nazo na kujua ni zipi zinajihusisha na masuala haya iwe kwa kutetea ushoga ama kubariki vitendo hivi, tutawachukulia hatua kali za kisheria na hata kuzifuta kabisa” alimalizia Dk. Kigwangalla.

Aidha, katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla alipata kutembelea ujenzi wa Hospitali hiyo mpya na ya kisasa inayotarajiwa kukamilika kwake hapo baadae na kisha kuwasili kwenye viwanja vya CCM Kirumba ambapo pia alipata kukagua gwaride la vijana wadogo, wa kati na wa kanisa hilo ambao ni pamoja na vijana waliopatiwa mafunzo ya Kiroho, Kimwili na Kikakamavu wakiwemo Wavumbuzi (adventure) Watafuta njia (path finder-Pf), Mabalozi na Kiongozi Mkuu (Master Guide)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati mwenye suti ya bluu) akiwa katika jengo la kisasa linalojengwa kwa ajili ya Hospitali ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo namna ya miundo ya Hospitali na viwango vyake..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kanisa hilo
Kituo cha Afya kilichopo kwa sasa kikiendelea na huduma
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakitoka walipotembelea jengo hilo la Hospitali linalojengwa..
Picha ya jengo hilo la Hospitali pindi litakapokamilikaMuonekano wa mbali katika jengo hilo la kanisa
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akivikwa skafu maalum wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kilumba katika sherehe za kufunga Jubilee ya miaka 50 ya kanisa hilo Jijini Mwanza.
Heshima zikitolewa kwa mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakishuhudia matembezi ya sherehe hizo
Matembezi ya sherehe hiyo yakiendelea
Sehemu ya umati wa watu katika tukio hilo la Jubilee ya Miaka 50
Vikundi vya matembezi yakiendelea
Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo
Vijana wadogo wa Path Finde-(PF) wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zao. 
Vijana wadogo wa Path Finde-(PF) wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zao
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akielekea kukagua gwaride la vijana hao
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua gwaride hilo
Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo
Vijana PF wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi (Hayupo pichani)
Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo

Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula akitoa salamu katika tukio hilo
Vijana wakiwa katika hali ya ukakamavu katika tukio hilo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubia katika tukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokea vitabu kama kutoka kwa uongozi wa kanisa hilo vyenye mafunzo mbalimbali 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishuka katika jukwaa kuu mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mzee Mark Boman.  Mzee Boman ni miongoni mwa Wazee waanzilishi wa kanisa hilo ambalo kwa sasa limetimiza Jubilee ya Miaka 50.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla ateta jambo na Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mzee Mark Boman ambaye ni Mzee wa kanisa hilo. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Mwanza).

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI DK. PALLANGYO AJIONEA ZOEZI LA UOKOAJI VIWANJA VYA SABASA

July 07, 2016
 Ofisa wa Matukio ya Dharura wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico), Jeremia Ibambasi (kulia), akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo ya uokoaji kwa mtu aliyemeza hewa chafu katika kiwanda cha uchanjuaji dhahabu katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016 alipotembelea Banda la Wizara hiyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo (kulia), akiangalia waokoaji wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico) jinsi wanavyomsaidia  mtu aliyevuta hewa chafu kwenye kiwanda cha uchanjuaji dhahabu nje ya banda la Wizara ya Nishati na Madini katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam 2016 katika viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo mchana.
 Hapa mfanyakazi wa Stamico, Paul Thobias (katikati), akionesha jinsi anavyosaidiwa na wataalamu baada ya kuvuta hewa chafu kiwandani.
 Zoezi la kumtoa nguo majeruhi likiendelea. Nguo hizo zinahisiwa huwenda zikawa na hewa hiyo ya sumu.
 Majeruhi akiendelea kutolewa nguo.
 Wananchi wakifuatilia zoezi hilo kwa karibu huku wengine wakiwa wameshika tama.
 Waokoaji wakiondoka na majeruhi wakimpeleka lilipo gari la kubebea wagonjwa tayari kumpeleka mgonjwa Hospitali.
 Hapa  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo akiagana na maofisa mbalimbali wa wizara yake baada ya kwisha kwa zoezi hilo la uokoaji.
 Hapa  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo akiagana na maofisa mbalimbali wa wizara yake baada ya kwisha kwa zoezi hilo la uokoaji.
 Hapa  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk Juliana Pallangyo akiagana na Ofisa wa Matukio ya Dharura wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico), Jeremia Ibambasi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)