January 16, 2014

WANAWAKE WAWILI WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA MKOANI ARUSHA

GEDSC DIGITAL CAMERA
Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya Mkoa wa Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Aben Mgode akiwaonyesha waandishi wa habari misokoto 5000 pamoja na baadhi ya magunia 16 ya madawa ya kulevya aina ya bangi yaliyokamatwa kutokana na misako mbalimbali iliyofanyika mkoani hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

WAZIRI MKUU AKAGUA ENEO LA MAAFA YA MAUAJI YA WAKULIMA KITETO

January 16, 2014
Eneo la Mtanzania  wilayani Kiteto  ambalo ni moja kati ya maeneo ya  makazi  yaliyovamiwa na watu wanaodaiwa kuwa wafugaji  ambapo watu watatu waliuawa na nyumba kuchomwa moto. Mlheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda alitembelea eneo hilo Januari  16, 2014.
January 16, 2014

CCM TAIFA KUFANYA SHEREHE ZAKE ZA MIAKA 37 MKOANI MBEYA!!


 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godphrey Zambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki alisema sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika Februari 2, Mwaka huu.

PICHA ZA MATUKIO YA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KATA YA KIOMONI ZA CCM LEO

January 16, 2014
MWENYEKITI WA JUMUIYA YA UMOJA WA VIJANA WILAYA YA TANGA,SALIM PEREMBO AKIWA ENEO LA UZINDUZI WA KAMPENI LEO KUSHOTO NI MJUMBE WA BARAZA KUU TAIFA UVCCM SAA MAMY MOHAMED

CCM WILAYA YA TANGA YAANZA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KWA KISHINDO,YAPOKEA WANACHAMA WAPYA 115,15 KUTOKA CUF

January 16, 2014

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA TANGA,KASIM MBUGHUNI KULIA AKIMDANI MGOMBEA WA UDIWANI KATA YA KIOMONI KUPITIA CHAMA HICHO  KAULI MAKAME KAULI LEO MARA BAADA YA KUZINDUA RASMI KAMPENI HIZO

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA TANGA (CCM)KASSIM MBUGHUNI KULIA AKIMFUNDA MGOMBEA WA UDIWANI KATA YA KIOMONI LEO KUPITIA TIKETI YA CHAMA HICHO.

KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA TANGA,LUCIA MWIRU KULIA AKIPOEA BENDERA YA KUASHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA YA KIOMONI JIJINI TANGA LEO
January 16, 2014

*WAENDESHA BODABODA WA JIJINI ARUSHA WAANDAMANA KUPINGA KUZUILIWA KUEGESHA PIKIPIKI ZAO KATIKATI YA JIJI

Waendesha Bodaboda wa Jijini Arusha wakiwa wamekusanyika huku wakiimba kuwashinikiza askari kufungua vizuizi vilivyowekwa barabarani kuanzia leo asubuhi kwa ajili ya kuwazuia kupita kuingia maeneo ya katikati ya jiji, ambapo wamezuiliwa kuegesha pikipiki katika maeneo ya katikati ya Jiji na kuamua kuandamana ili kupinga utaratibu huo.
Waendesha pikipiki wakiandamana na baadhi wakiwa na mabango.

TUZO YA MAKOCHA TANZANIA KUTOLEWA MACHI 8 MKOANI MOROGORO.

January 16, 2014
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Benard Mwalala, kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola na wa Azam FC, Kally Ongala ni baadhi ya wachezaji wanaotarajiwa kuunda timu ya Makocha itakayocheza mchezo wa kirafiki na TASWA FC katika kusindikiza tuzo ya makocha wa mpira wa miguu Tanzania inayotarajiwa kutolewa Machi 8, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mtandao huu, afisa mtendaji wa tuzo hiyo, Fredrick Luunga alisema mchezo huo pia utatumika kumuenzi aliyekuwa mweka hazina na mchezaji wa Taswa FC, Sultan Sikilo na aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba SC, James Kisaka, waliofariki dunia hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
MORO SISTERS KUANZA KUJIFUA JANUARI 20.

MORO SISTERS KUANZA KUJIFUA JANUARI 20.

January 16, 2014
Na Daudi Julian,Morogoro.
TIMU mpya ya soka ya wanawake ya Moro Sisters inatarajia kuanza mazoezi Januari 20, mwaka huu, katika uwanja wa Shujaa uliopo mjini Morogoro.

Akizungumza na Mtandao huu, kocha wa timu hiyo, Charles Sendwa ‘kocha mtaalamu’ alisema maandalizi kwa ajili ya kuanza mazoezi hayo yanakwenda vizuri na kwamba yatakuwa yakianza saa 9.00 alasiri ili saa 10 jioni kuipisha timu ya Burkina Faso inayotumia pia uwanja huo kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza.

CCM YAVUNA WANACHAMA WAPYA 111 KATA YA MWAZANGE.

January 16, 2014
MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YA TANGA KASSIM MBUGHUNI KULIA AKITO KADI KWA MMOJA YA WANACHAMA WAPYA WALIOJIUNGA NA CHAMA HICHO JUZI.