VIONGOZI TFF WANAUSHABIKI NA YANGA-SIMBA SC.

October 16, 2015


Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba SC imelalamika kwamba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) haliwatendei haki kwa sababu uongozi wake umesheheni watu wa Yanga SC.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba, imefikia TFF wamekata kabisa mawasiliano na klabu yao.
Poppe amesema kwamba TFF sasa hawajibu hata barua za Simba SC wanapoandika kuhoji au kuomba ufafanuzi wa jambo lolote.
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amesema kwamba imefikia wakati wanashindwa hata kujua namna gani wanaweza kupata haki zao nyingine za msingi, kutokana na ‘kuchuniwa’ na TFF.
Hans Poppe amesema TFF haiwatendeo haki kwa sababu viongozi wengi ni Yanga SC 

“Inafahamika kwamba Rais wa TFF (Jamal Malinzi), Katibu wake (Mwesigwa Selestine) wote ni Makatibu wa zamani wa mahasimu wetu, Yanga SC. Na bado wapo wengine wengi pale TFF ambao wametoka Yanga akina Baraka Kizuguto.
“Lakini kwa sababu wanaongoza chombo cha kitaifa, wanapaswa kutenda haki, yaani inaonekana kabisa TFF wanaikandamiza Simba na wanaibebea Yanga,”amelalamika Poppe.
Akifafanua, mfanyabiashara huyo maarufu nchini, amesema TFF hawajajibu barua yoyote ya Simba SC kwa mwaka huu na hawaelewei sababu ni nini.
“Watuonyeshe wao, ni barya ipi ya Simba SC wamejibu mwaka huu, malalamiko yetu ya mchezo dhidi Yanga hawakujibu, Suala la Messi (Ramadhani Singano) hawakujibu. Hata tunapojibu barua zao za adhabu wanazotuandika ili kuomba ufafanuzi, pia hawatujibu. 
“Labda watuambie basi kwamba barua zetu tunatakiwa kuzipitishia Yanga SC ndiyo watujibu, tutafanya hivyo, tutaandika na kuwapelekea Yanga waweke muhuri wao ipelekwe TFF, tujibiwe, hiyo ndiyo shida yetu,”amesema.
Hans Poppe amesema kwamba mchezaji wao Ramadhani Singano ‘Messi’ amehamishiwa Azam FC kinyume cha utaratibu na kila wapodai haki yao hawasikilizwi. “Mchezaji wa Yanga (Donald Ngoma) alimpiga kichwa mchezaji wetu (Hassan Kessy) na tukapeleka ushahidi wa picha za video, hakuchukuliwa hatua na wala hatukujibiwa,”. 
“Lakini Juma Nyosso (wa Mbeya City) alimdhalilisha John Bocco (wa Azam FC) akachukuliwa hatua baada ya saa 24 kwa ushahidi wa picha,”amesema.
Aidha, amesema kwamba Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeiamuru klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia iilipe Simba SC dola 300,000 za Kimarekani za manunuzi ya mshmbauliaji Emmanuel Okwi, lakini wanashindwa kufuatulia kwa sababu TFF haiwasikilizi tena.
“Kwa kweli tupo wakati mgumu mno, tunashindwa hata kuelewa tunacheza hii ligi kwa sababu gani, inaonekana tunawasindikiza watu ambao tayairi wameandaliwa kwa namna yoyote wawe mabingwa,”amesema. 

Rais Kikwete aongoza maelfu ya waombolezaji kwenye mazishi ya Dkt AbdallahKigoda mjini Handeni, Tanga

October 16, 2015
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi Oktoba 15, 2015 kuongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Waziri huyo aliyekuwa pia Mbunge wa Handeni kwa zaidi ya miongo miwili

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi kwenye kitabu cha maombolezo  nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi Oktoba 15, 2015 kuongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Waziri huyo aliyekuwa pia Mbunge wa Handeni kwa zaidi ya miongo miwili
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji dada wa marehemu Dkt. Asha Kigoda  nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi Oktoba 15, 2015 kuongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Waziri huyo aliyekuwa pia Mbunge wa Handeni kwa zaidi ya miongo miwili
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiifarifi familia  nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi Oktoba 15, 2015 kuongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Waziri huyo aliyekuwa pia Mbunge wa Handeni kwa zaidi ya miongo miwili
 Sehemu ya waombolezaji kwenye msiba huo
 Spika Anne Makinda msibani hapo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wa serikali na wa kidini   nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Marehemu Dkt Abdallah Kigoda mjini Handeni Alhamisi Oktoba 15, 2015 akiongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Waziri huyo aliyekuwa pia Mbunge wa Handeni kwa zaidi ya miongo miwili
 Bw. Saidi Yakub akiendeshe shughuli hiyo
 Sehemu ya waombolezaji
 Sehemu ya waombolezaji
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Uledi Mussa akisoma wasifu wa marehemu

 Waombolezaji
 Sehemu ya waombolezaji
 Brigedia Jenerali Mstaafu  Ngwilizi akiongea machache kuhusu marehemu
 Rais Kikwete akipeana mikono na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema ZanzibarSalumu Mwalimu, ambaye aliwakilisha UKAWA kwenye mazishi hayo
 Ndg. Muhammad Seif Khatibu akisoma rambirambi za CCM 
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Mathias Chikawe akitoa rambirambi za serikali

 Waombolezaji knamama msibani hapo
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally (mwenye kipaza sauti mkononi) akiongoza swala ya maiti
 Rais Kikwete akiwa anaongozana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman akitoa pole kwa waombolezaji
 Watumishi wa Bunge wakibeba jeneza lililo na mwili wa marehemu kuelekea kaburini
 Mazishi
 Mtoto wa marehemu akiweka udongo kaburini
 Rais Kikwete akiweka udongo kaburini 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman akiwa na Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. John Kijazi kwenye mazishi hayo.
PICHA ZOTE NA IKULU
RAIS TFF ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI

RAIS TFF ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI

October 16, 2015
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa kiongozi wa klabu hiyo Emmaneul Makaidi aliyefariki Dunia jana mkoani Lindi.
Katika salam zake, Malinzi amewapa pole wafiwa, ndugu, jamaa, marafiki, wapenzi wa klabu ya Simba pamoja na wadau wa mpira wa miguu nchini, kufuatia kifo hicho cha kiongozi huyo.
Marehemu Emmanuel Makaidi alipata kuwa kiongozi wa klabu ya Simba 1960-1970 katika nafasi mbalimbali zikiwemo nafasi za Katibu mwenezi, Katibu Mkuu na kukaimu Uenyekiti wa klabu ya Simba kabla ya kujiunga na masuala ya kisiasa.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini na watanzania, TFF inawapa pole wafiwa na kuwatakia faraja katika kipindi hichi cha maombelezo.

MAGUFULI AHUTUBIA KISIWANI PEMBA LEO,AAHIDI KUULINDA MUUNGANO KWA NGUVU ZOTE.

October 16, 2015
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Pemba jioni ya leo kwenye kutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani ya Kale mjini Pemba.

Katika mkutano huo wa Kampeni,Dkt Magufuli ameahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano,atadumisha na kuulinda Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ulioanzishwa na Waasisi wetu akiwemo Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere pamoja na Abeid Amani Karume.Dkt Magufuli kesho atahutubia kwenye mkutano mkubwa wa kampeni mjini Unguja.
Wananchi wa Kisiwani Pemba wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale ,wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kura kwa wananchi hao. 
Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akiwahutubia wakazi wa Pemba jioni ya leo kwenye kutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani ya Kale mjini Pemba.Dkt Shein amewataka wakazi wa Kisiwani Pemba kuilinda amani iliyopo ndani ya kisiwa hicho na kuwa Wananchi wakajitokeze kwa wingi kupiga kura siku ya Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu Mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana Mama Shadia Karume mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Gombani ya Kale kwa ajili ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein kabla ya mkutano wa kampeni kuanza jioni ya leo kisiwani Pemba.
Umati wa wakazi wa kisiwani Pemba kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wa kiswani Pemba wakifuatilia mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo,kwenye uwanja wa Gombani ya kale kisiwani humo.
Wananchi wa kiswani Pemba wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein walitumia jukwaa na mkutano huo kuwaomba kura za kutosha ili wakaiongoze Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano.

PICHA NA MICHUZI JR-PEMBA


-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.

UNICEF YAKABIDHI MAGARI KUMI( 10) YA KUBEBEA WAGONJWA MKOANI MBEYA

October 16, 2015
Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Unicef Dkt Jama Gulaid akitoa hotuba katika sherehe ya makabidhiano ya magari ya kubebea  wagonjwa Mkoa wa Mbeya15 Octobar  2015

Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Ndugu Prisca Butuyuyu akitoa taarifa ya huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika Mkoa wa Mbeya kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa 15 Octobar 2015.

Mwakilishi UNICEF Dkt Jama Gulaid kulia akimkabidhi Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Kastro Msigala taarifa muhimu za magari hayo yenye thamani ya shilingi mil 700 .

Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya pamoja na wageni waalikwa wakishiriki kikamilifu tukio la makabidhiano ya magari ya wagonjwa  Mkoa wa Mbeya 15 Octobar 2015 kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF.

Timu ya Uendeshaji wa huduma za za Afya Mkoa wa Mbeya

Kastro Msigala Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za makabidhiano ya magari kumi ya kubebea wagonjwa ambayo yametolewa na shirika la kimataifa la UNICEF Octobar 15 mwaka huu.

Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mbeya Kastro Msigala akikata utepe kuashiria kupokea rasmi msaada wa magari hayo kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF msaada ambao umegharimu kiasi cha shilingi Mil 700.


Meza kuu katika  picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Mbeya na wawakilishi wa Shirika la UNICEF.

Meza kuu katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa Halmashauri za Mkoa wa mbeya .

Meza Kuu katika picha ya Pamoja na timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa wa Mbeya .

Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi shirika la UNICEF.


 
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa  linalo shughulikia watoto Duniani (UNICEF) limekabidhi msaada wa magari kumi  ya Kubebea wagonjwa yenye tahamni ya shilingi mil 700.7  kwa serikali ya Mkoa wa Mbeya .


Aidha shirika hilo lina mpango wa kuboresha vituo 184 vya kutolea huduma za afya katika mkoa huo wa mbeya ambavyo ni vituo afya na hospital 30 pamoja na zahanati 154  sanjali na kuvipatia vifaa muhimu vya kutolea mafunzo kwa watumishi wake.


Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Octobar 15 mwaka huu  Mwakilishi wa shirika la  UNICEF   nchini Tanzania Dkt Jama Gulaid  amesema shirika hilo limetenga kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya mradi huo.


Amesema mchango wa UNICEF katika sekta afya na lishe hapa mkoani mbeya imepanua wigo kutoka halmashauri mbili za mkoa huo hadi kufikia halmashauri zote katika kipindi cha miaka miwili .


Aidha Dtk, Jama amesema katika kukabiliana na magonjwa na vifo vya watoto na wanawake wajawazito ,UNICEF imechangia vifaa tiba muhimu ikiwa ni pamoja vile vya uchunguzi wa ujauzito ,upasuaji  sanjali na vifaa kuwasaidia watoto wachanga kupumua mara wanapo zaliwa na vifaa vingine vya utoaji wa huduma katika idara ya uangalizi maalumu  ICU.


Aidha  amewataka viongozi hao wa mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanaweka juhudi kubwa zaidi katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa kuhakikisha kwamaba kina mama wajawazito wote wanapata huduma za afya bure kwa wakati.


Awali akisoma  taarifa ya huduma za afya ya uzazi na mtoto katika mkoa mbeya mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto Ndugu Prisca  Butuyuyu amesema toka shirika hilo la UNICEF  lianze kufanya mwaka 2012 huduma za afya zimeimalika kwa kiasi kikubwa hususani kwa kuweza kuzuia vifo vya uzazi na vya watoto wachanga.


Amesema kwa ujumla hali ya vifo hususani vilivyokuwa  vinatokea katika vituo vya huduma vimepungua kutoka 140  kwa mwaka 2012 na kufikia vifo 94 kwa kwa mwaka 2014 pamoja na kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 602 kwa mwaka 2012 hadi kufikia 568  mwaka 2014 ambapo punguzo hilo ni sawa na asilimia 33.9 na 5.7 kwa watoto wachanga.


Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kaimu katibu Tawala Ndugu Kastro Msigala amelishukuru shirika hilo kwa msaada wa magari hayo sanjali na kutoa wito kwa viongozi  wa halmashauri ambao ni wakurugenzi na waganga wakuu kuhakikisha wanayatunza magari hayo ili yaweze kutoa huduma stahiki kwa wananchi.


Msaada huo wa magari imegawanywa katika halmashauri zote mkoa huo wa mbeya ambazo ni Ileje,Mbozi,Mbeya vijijini,Rungwe,Busokelo,Mbarali pamoja na Kyela na Momba .

Mwisho

(Imeandaliwa na Jamiimojablog Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya  0759406070 )