Mgeni
rasmi, Mkuu wa Wilaya Kilombero, Hassan Masala, akifungua mafunzo ya
matumizi ya simu kwa habari katika ukumbi wa Mazingira Kibaoni, Ifakara
03 Februari 2014 yanayolenga kukuza taaluma ya upashaji habari kwa
kutumia simu. Kushoto ni Afisa Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bi. Christa
Njovu na Kulia ni Mkufunzi kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu.
Na. Mwandishi wetu
Demokrasia
vijijini itapatikana iwapo vyombo vya habari jamii vitatumika
kikamilifu na kutekeleza wajibu wake wa kupasha habari kwa kutumia
teknolojia mpya.
Akifungua
mafunzo ya wiki moja katika Ukumbi wa Mazingira, Kibaoni Ifakara
yanayowashirikisha wanahabari jamii kutoka Pemba, Unguja, Pangani,
Ifakara na Kyela, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Hassan Masala amesema
mbinu za kisasa zinahitajika kuelimisha jamii na mambo gani yafanyike
ili kupata uongozi bora vijijini na taifa kwa ujumla.