MWALIMU GODFREY GODWIN KIHENGU NA MISS MARIAM BARAKA BINAGI WAUAGA RASMI UKAPERA.

December 30, 2015
Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akiwafungisha ndoa Bi.Mariam Baraka Binagi (wa pili kulia) wa Rebu Tarime, Mara pamoja na Mwalimu Godfrey Godwin Kihengu (wa pili kushoto) wa Nyansurura Tarime, Mara ikiwa ni katika ibada iliyofanyika jana Desemba 30,2015 katika Kanisa Anglikana Buhemba Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Picha na BMG (Binagi Media Group)
Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akimkabidhi bwana harusi cheti cha ndoa
Mchungaji Kiongozi wa Jimbo la Tarime Samweli Nyageswa akimkabidhi bibi harusi cheti cha ndoa
Maharusi wakionyesha vyeti vyao vya ndoa
Bi.Mariam Baraka Binagi (Kushoto) akiwa pamoja na bwana harusi Godfrey Godwin Kihengu.
Bibi harusi akimlisha keki bwana harusi
Maharusi wakinyweshana Shampeni
Maharusi Wakiwa katika picha ya pamoja na Wachungaji
Maharusi Wakiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake akiwemo mama yake mzazi pembeni ya bibi harusi
RAIS MAGUFULI ATANGAZA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU KATIBU WAKUU WAPYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS MAGUFULI ATANGAZA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU KATIBU WAKUU WAPYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

December 30, 2015


GUL1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitangaza Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakisikiliza kwa makini.
GUL2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwaonesha orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakishuhudia.
GUL3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwaonesha orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakishuhudia
GUL4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Mara baada ya kumkabidhi orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliwateua leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha zote na IKULU
………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.
Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
  1. Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi – Ombeni Sefue
  1. Katibu Mkuu Ikulu
Peter Ilomo
  1. Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
Dkt. Laurian Ndumbaro
  1. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)
Dkt. Deo  Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu – Afya)
Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu – Elimu)

Waraghbishi wilayani kahama wapania Kumkomboa Mwanamke

December 30, 2015
Na Krantz Mwantepele .Kahama

Wanawake ni nguzo muhimu sana katika uchumi wa watanzania wengi. Mwanamke ana ushawishi mkubwa na hasa pale anapoamua kuwa chachu ya maendeleo. Na hasa anapowezeshwa kufanya hivyo.

Katika kufanikisha hili waraghbishi wameamua kutoa mafunzo ya uraghbishi kwa makundi mengine ya jamii. Mojawapo ya kundi hilo ni la wanawake. Waraghbishi wapya toka katika kijiji cha Nyandekwa, kati ya hao wapo 9 ambao ni wanawake.
Mmoja wao ni Anna Alphonce, Mwenyekiti wa kitongoji cha Busolo, katika kijiji cha Nyandekwa. Akielezea jinsi alivyoanza uraghbishi alisema:
“Mi niliona kuna kikundi wanakaaga humu karibu kila jioni. Na kila nilipokuwa napita jirani na hapa naona watu wamejaa, basi nikapenda namimi nijiunge nao na hasa baada ya kujua nini wanafanya. Na hapo ndipo nilipoanza uraghbishi,”





Anna Alphonce (katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Busolo akifafanua jambo wakati akielezea uraghbishi anaofanya .




Akiwa kama mwenyekiti mwanamke wa kitongoji aliweza kutumia nafasi yake kufanya uraghbishi kwa anaowaongoza. Kwa kuwa kilikuwa ni kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu, aliitisha mikutano kwenye kitongoji chake kwa lengo la kutoa hamasa ya wananchi kujitokeza kwa wingi. Kwa nafasi yake aliweza kuyafikia makundi ya wazee, vijana na wanawake. Ingawa kati ya hawa wanawake ndio walikuwa washiriki wazuri.
“Msisitizo kwenye mikutano yangu ilikuwa ni kupiga kura kwa amani. Niliwasihi Vijana wetu wasiwe chanzo cha vurugu na badala yake wawe walinzi na kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira ya utulivu,”
Haya ni maelezo ya mwenyekiti huyo akielezea jinsi alivyotumia nafasi yake kwenye kufanya hamasa ya amani. Akaongeza,
“Kwangu mimi haya ni mafanikio kwa sababu kweli uchaguzi umefanyika kwa amani katika kitongoji change.”
Mraghabishi mwingine ni Matrida Peter toka katika kijiji cha Nyandekwa, yeye uraghbishi wake alifundishwa na Elizabeth Ngaljalina toka kijiji hicho hicho. Baada ya kufundishwa yeye alichoamua kufanya uraghbishi kwa vijana wa kijiji cha Nyandekwa pamoja na wale waliokuwa mashuleni pia.
Akielezea jinsi ambavyo anafanya uraghbishi kwa vijana, Matrida anasema,
“Nafundisha makuzi ya ujana ili kuweza kutimiza ndoto zao. Kwanza nawaelewesha kuhusu mabadiliko ya miili yao hasa wanapoingia hatua ya kubalehe na kuvunja ungo. Hii inawasaidia jinsi ya kujikinga na maambuzi ya virusi vya ukimwi.”
Uraghbishi wake hauishii kwa vijana walio nje ya shule, hivyo alikwenda kumtembelea ili aweze kupata fursa ya kutoa elimu hiyo hasa kwa wanafunzi ya shule ya msingi. Walengwa wakubwa wakiwa ni wanafunzi wa kuanzia darasa la nne mpaka la saba. Akielezea rika la watoto hao, Matrida anasema:
“Watoto wa siku hizi wana maumbo makubwa, hivyo hao wa darasa la nne mpaka la saba sio wadogo kiumbo na wengi ndio wapo kwenye huo umri. Wanahitaji mwongozo manake makuzi siku hizi yameachwa kwa wazazi na wao mda mwingine wanaona aibu kuongea nao,”
Matokeo ya uraghbishi huu wa mwanamama Matrida ni kuongeza kwa watoto wenye uelewa wa mipango ya uzazi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Kwani maambukizi katika wilaya ya Kahama yapo juu kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini.
Uraghbishi una maana tofauti tofauti kwa wanawake hawa wa kijiji cha Nyandekwa, kama anavyoelezea Mariam Stephano aliyeanza uraghbishi mwezi Septemba 2015:
“Uraghbishi kwangu mimi ni kutetea haki za vijana na mabinti, na sio tu kutetea bali kujua na falsafa yake ya jinsi ya kutenda ili kufanikisha lengo hilo ninaloliangalia kama  ndio jukumu langu,”
Wakati Suzan Stephano yeye analinganisha uraghbishi na haki za kikatiba. Huku akisisitiza umuhimu wa kuthaminiwa kwa mwanamke katika kijiji chao na taifa kwa ujumla. Na yeye pia anakiri kwa uraghbishi ni falsafa ya jinsi ya kutenda.

Waraghbishi wanawake toka katika kijiji cha Nyandekwa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kitongoji cha Busola akielezea uraghbishi wake katika ngazi ya kitongoji


Mraghbishi mwingine ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Bujika, Adam Joseph yeye alijiunga na uraghbishi mwezi Septemba 2015, kwa kutumia nafasi yake uwenyekiti alitambulisha uraghbishi kwenye kitongoji chake.

“Cha kwanza nilichofanya ni kuongea na mtendaji wa kijiji na kukubaliana tunahitaji kufanya hamasa kwa vijana ili wawe wanafika katika mikutano ya vijiji. Hivyo nikaanza kupita kwenye vijiwe na kuwahamasisha vijana waweze kufika mikutanoni. Na tuliwalenga vijana wote wa kike na wa kiume,” anaelezea Adam.

Vijana walimwambia mwenyekiti wao kwamba wao hawasikilizwagi wakija kwenye mikutano na hivyo hawaoni umuhimu wa kuja kwenye mikutano ya vijiji. Majibu haya yalimpelekea mwenyekiti kuitisha mkutano uliowausisha vijana na wazee kwa pamoja.

“Nimeshaitisha mikutano miwili, muamko bado si mkubwa sana kwani bado vijana hawaoni umuhimu wa kushiriki mikutano hii. Lakini hili halinikatishi tamaa najua hapa ni mwanzo tu,” anaelezea Adam.


Kwa hakika hizi ni harakati za kweli katika kumwezesha mwanamke na jamii kwa ujumla. Waraghbishi kwa pamoja wanakili kwamba uraghbishi ni falsafa ya kutenda. Swali la msingi kwetu sote, je na sisi tunatenda na kama ndio tunatumia falsafa gani.


                                   CHANZO; MWANAHARAKATI MZALENDO
photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"

Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde afanya ziara makao makuu ya Tigo leo

December 30, 2015



Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde  akizungumza na wafanyakazi wa tigo baada ya kufanya ziara mapema leo  katika makao  makuu ya Tigo kijtonyama  jijini Dar es laam 

Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na waandishi wa habari na wafanyakazi wa tigo   baada ya kufanya ziara mapema leo  katika makao  makuu ya Tigo kijitonyama Dar es laam 

Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez , akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika mkutano alioshiriki pia Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde  baada ya kufanya ziara katika makao  makuu ya Tigo Kijtonyama  jijini Dar es laam
Dar es Salaam, 30th December 2015- Tigo Tanzania leo imepokea kwa furaha ugeni wa ghafla wa Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Kijitonyana jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mavunde ambaye alikuwa ameongozana na waandishi wa habari na maofisa kutoka ofisi za uhamiaji alitinga ofisini hapo mnamo saa nne asubuhi ya Jumatano ya tarehe 30 Desemba na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bwana Diego Gutierrez pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni ya Tigo.
Bwana Gutierrez alimtembeza Naibu Waziri kwenye idara mbalimbali za kampuni hiyo huku akitambulisha huduma zinazotolewa na kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na Mhe. Waziri.
Kampuni ya Tigo imekuwa mstari wa mbele kwenye sekta ya mawasiliano kwa kutoa huduma na bidhaa zenye ubunifu na manufaa makubwa kwa jamii, hivyo kuchangia kwa kiasi kukubwa sana kuendeleza sekta hii muhimu kupitia njia mbali mbali kama kutoa ajira, kuchangia pato la taifa, kuchangia maendeleo ya jamii na kuwezesha watanzania wajiendeleze kiuchumi na kijamii kupitia mawasiliano ya bei nafuu.

Bwana Gutierrez alisema kampuni ya Tigo imefurahishwa mno na ugeni huo huku akiongeza kuwa ugeni huo unadhihirisha kwamba serikali imeonesha kwamba inajali huduma zinazotolewa na mashirika ya sekta binafsi.

Bwana Gutierrez alisema “Tutaendelea kushirikianana na serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa sekta ya mawasiliano inakua zaidi na inaleta mabadiliko lukuki kwenye maisha ya watanzania na nchi nzima kwa ujumla. Tigo imejikita kwenye kupanua wigo wa mawasiliano kuhakikisha kila mtanzania popote alipo anaweza kuwasiliana kwa bei nafuu, kupitia mtandao bora na wenye huduma zenye uhakika".

Kuhusu kuitembelea Tigo, Mh. Mavunde alisema: "leo tumetembelea kampuni ya Tigo, kwa ajili ya kujitosheleza vipi kampuni hii inajali waajiri wake, na katika ziara hii tumebaini mambo kadha ambayo tungependa kampuni ya Tigo, ivifanyie kazi kwa mfano kwenye maswala ya afya na usalama, na pia tungependa kuona mikataba baina ya Tigo na watoa huduma wake, pia serikali ya awamu ya tano, ipo makini kuhakikisha sheria inafuatwa ili tuwe na jamii inayozingatia sheria"

photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"

JK,WAZIRI LWENGE WAKAGUA MITAMBO YA MAJI WAMI,CHALINZE

December 30, 2015

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (katikati), akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.
Rais Jakaya Kikwete na Lwenge wakiangalia mitambo ya kusafisha maji

Wakiwa katika picha ya pamoja
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete , akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge (kushoto kwake) wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani leo.Wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akionesha kitu walipotembelea mitambo ya maji Wami

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge katika mitambo hiyo.

NAIBU WAZIRI WA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO, ANNASTAZIA WAMBURA ATEMBELEA TCRA LEO JIJINI DAR.

December 30, 2015

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura akipewa maelekezo na Naibu Mkurugenzi wa maswala ya utangazaji wa Televisheni wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Frederick Ntobi mara baada ya kutembelea chumba cha maswala ya mawasiliano hasa ya Televisheni  leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Mkurugenzi wa maswala ya Posta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Haruni Lemanya akizungumza na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) leo jijini Dar es Salaa mara baada ya Naibu waziri kutembelea katika ofisi ya Maswala ya Posta katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) WA kitengo cha TTMS, Mhandisi Gabriel Mruma akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura kutembelea katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.  
Baadhi ya Kazi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kwa upande wa mitandao ya Simu za mkononi na maswala ya Miamala ya Pesa katika mitandao ya simu kilichopo katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura akizungumza na wafanyakazi pamoja na wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari na wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura jijini Dar es Salaam leo.

MHE. KAIRUKI AENDELEA NA ZIARA KATIKA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YAKE KUHIMIZA UWAJIBIKAJI

December 30, 2015

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (wa pili kulia) akizungumza na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akimsikiliza Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akiwahimiza watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma kuwajibika alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akitazama nyaraka inayoandaliwa kutunzwa katika nakala laini (soft copy) alipoitembelea Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa mapema leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akitazama moja ya kifaa cha kutunzia kumbukumbu alipoitembelea Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa mapema leo.

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR YASAINI MIKATABA MIWILI YA UJENZI NA MAKANDARASI M/S.HUMPHREY CONTRUCTION LIMITED YA ARUSHA NA MINDSET TECHIES (T) YA DAR ES SALAAM.

December 30, 2015

 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khadija Bakari Juma akitoa ufafanuzi kwa Wadau waliohudhuria hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba miwili ya Ujenzi baina ya Wizara yake na Makandarasi kutoka M/S. Hamphrey Construction Limited ya Arusha na Mindset Teches (T) ya Dar es Salaam Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Zanzibar.
 Wadau mbalimbali waliohudhuria katika sherehe za kutiliana saini mikataba hiyo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khadija Bakar Juma na Mkandarasi wa Kampuni ya M/s.Humphrey Construction Limited ya Arusha wakitiliana saini Mkataba wa kupanua Taasisi ya Maendeleo ya Utalii iliopo Maruhubi.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khadija Bakar Juma na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi M/s. Humphrey Construction Limited ya Arusha wakibadilishana Mikataba baada ya kutiliana saini.
 Mkandarasi wa Kampuni ya M/s. Mindset Techies (T) Limited ya Dar es Salaam Thabit Kombi akitia saini Mkataba wa Ujenzi wa Kupanua Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khadija Bakar Juma na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi M/s. Mindset Techies (T) Limited ya Dar es Salaam Thabit Kombi wakibadilishana Mikataba baada ya kutiliana saini.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya habari Utamaduni Na Michezo Zanzibar Issa Mlingot Ali akizungumza na Wadau waliohudhuria katika Mkutano huo.

PICHA NA ABDALLA OMAR ( HABARI- MAELEZO ZANZIBAR)
WAZIRI WA AFYA, MHE. UMMY MWALIMU ATEMBELEA MSD, AAHIDI KUWA BALOZI WAO NA KUWATATULIA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI IKIWEPO DENI WANALOIDAI SERIKALI

WAZIRI WA AFYA, MHE. UMMY MWALIMU ATEMBELEA MSD, AAHIDI KUWA BALOZI WAO NA KUWATATULIA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI IKIWEPO DENI WANALOIDAI SERIKALI

December 30, 2015
ummy-msd 175
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea moja ya ghala la kuhifadhia dawa iliyopo makao makuu ya MSD,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laureane Bwanakunu na watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD Prof.Idris Mtulia.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuahidi kuwa balozi wa kuhakikisha deni la serikali linalipwa ili kuiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Waziri huyo ameeleza hayo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu kueleza kuwa ukosefu wa fedha na deni la serikali ni changamoto kubwa inayoathiri utekelezaji mzuri wa majukumu ya MSD.
Mbali na hilo, Waziri wa Afya amesema mbali na deni hilo, hata kiasi cha fedha kinachotengwa na serikali kwaajili ya hospitali, vituo vya afya na zahanati na kununua dawa hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala hilo lifanyiwe kazi mapema, huku akisisitiza hata kiasi hicho kidogo kinachopatikana kitumike vizuri.
Katika hatua nyingine ameishauri Bohari ya Dawa kuanza utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kuhakikisha dawa muhimu zinapatikana wakati wote na kuiagiza MSD itangaze kwenye vyombo vya habari dawa zote ambazo zinapelekwa vituoni, zahanati na kwenye hospitali, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa tayari MSD imeshaanza kubandika kwenye mbao za matangazo za hospitali orodha ya dawa inazofikisha.
Waziri huyo ambaye alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Donald Mbando na watendaji wengine pia alitembelea maghala ya kuhifadhia dawa ya MSD, jengo la ofisi linalojengwa pamoja na kuwa na mkutano na menejimenti ya MSD, ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza MSD kwa hatua iliyofikia ya kuweka nembo ya GOT kwenye vidonge vyake ili kudhibiti upotevu wa dawa za serikali pamoja na kuanzisha maduka ya dawa Muhimbili, na mengine yanayotarajia kufunguliwa hivi karibuni mkoani Mbeya, Arusha na Mwanza.
Waziri Ummy Mwalimu alihitimisha kwa kusema kuwa ajenda yake kuu ni upatikanaji wa dawa kwa wakati, kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alivyoaainisha, hivyo MSD itekeleze majukumu yake ipasavyo kwani mafanikio ya MSD ni mafanikio kwake pia.
ummy-msd 178
Waziri Ummy akiuliza jambo kwa wafanyakazi wa bohari hiyo.
ummy-msd 185
Waziri huyo akiendelea na ukaguzi wa maghala hayo, kulia ni Mkurugenzi wa Ugavi Misanga Muja na kushoto ni mwenyekiti wa Bodi ya Bohari hiyo.
ummy-msd 190
Baadhi ya watumishi wakiendelea na kazi ya kuhakiki dawa kwenye moja ya ghala mojawapo.
ummy-msd 191
Waziri Ummy akielekea kwenye ujenzi wa jengo jipya linaloendelea kujengwa, ambapo linatarajiwa kumalizika kujengwa mwezi Juni, 2016 ,Kushoto ni Katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Donnan Mmbando.
ummy-msd 198
Mkurugenzi wa MSD Bwanakunu akieleza dira,malengo na majukumu ya Bohari hiyo.
ummy-msd 202
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiangalia dawa zilizowekwa nembo ya serikali (GoT) ambayo itasaidia udhibiti wa upotevu wa dawa nchini.
ummy-msd 205
Waziri huyo akionesha kopo la dawa la Bohari ya dawa.
ummy-msd 220
Waziri Ummy akimuonesha ukurasa wa ugawaji fedha za bohari Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya dawa Prof.Idris Mtuliya.(Picha zote kwa Niaba ya Wizara ya Afya).