TRA KUCHAMBUA RIPOTI YA KITUO CHA UTAFITI CHA KODI CHA KIMATAIFA (ICTD)

December 09, 2014


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade, kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo, Prof Mick Moore, wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha
 Wataalamu wa kimataifa  wa masuala ya kodi  wakiendesha mjadala katika mkutano wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya kodi,mkutano uliofanyika jana  jijini Arusha ,Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), Milly Nalukwago (kushoto), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade (katikati) na  Mtaalam wa Kodi wa Uingereza, Rhiannon Mc Cluskey.
Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA RISHED BADE kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo Prof MICK MOORE wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha


Mwakilishi  wa Channel Ten Arusha, Jamila Omar (katikati) , Mwakilishi wa kituo cha Star TV Arusha, Ramadhani Mvungi ,Iddy Uwesu wa Azam tv Arusha wakifanya mahojiano maalumu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)  Rished Bade jijini Arusha wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo.

 ***********

Mamlaka ya mapato nchini TRA imeanza kuchambua ripoti ya utafiti uliofanywa na kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya kodi na maendeleo inayobainisha changamoto mbalimbali za ulipaji kodi katika
maendeo mbalimbali nchini.

Zoezi la uchambuzi wa ripoti hizo linatajwa kuwa na shabaha ya kuangalia mapungufu yaliyopo na kuboresha mifumo ya sheria na ulipaji kodi kwa hiari.

Sehemu ya Taarifa ya utafiti uliofanwa katika kipindi cha mwaka uliopita na kituo cha kimataifa cha kodi na  maendeleo katika mikoa mbalimbali nchini, inabainisha mazingira tofauti ya ulipaji wa kodi ambapo baaadhi ya maeneo yameonekana kuwa katika changamoto kubwa za ukwepaji kodi.

Kamishana wa TRA Rished Bade kizungumza Jijini Arusha wakati wa Mkutano wa kimataifa baina yao na kundi la wataalamu, wanaofanya utafiti kuhusu masuala ya kodi duniani amesema pamoja na mapitio ya ripoti za utafiti wa taasisi hiyo,fursa hiyo inatoa mwanya kwa wataalamu wa ndani kujifunza mbinu za kushughulikia changamoto za walipa kodi wanaofanya biashara za kimataifa.


Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo Profesa Mick Moore ameeleza kusudio la tafiti zao katika nchi mbalimbali za Afrika kuwa unalenga kuimarisha mifumo ya kodi hususani katika sekta za maliasili zikiwemo Madini,Gas na Mafuta.

Katika hatua nyingine Mamlaka ya mapato nchini TRA imeibuka kinara kwa kuwa na hesabu bora miongoni mwa taasisi za serikali kwa mwaka 2013-2014 zinazotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA ambapo kamishna wa mamlaka hiyo akizungumza Jijini hapa katika hafla ya kukabidhiwa ushindi huo amesema hatua hiyo inazidi kuwajengea imani walipa kodi juu ya utendaji wa chombo hicho.

Raha tele tabu ya nini?: zinaonyesha ongezeko la idadi ya walipa kodi chini,idadi iliyopo sasa inatajwa kuwa ndogo kulinganisha na mataifa mengine kutokana na mfumo wa kibiashara usio rasmi unaopelekea kupunguza idadi ya walipa kodi wanaofikia milioni moja nukta nane hivi sasa.
SHEREHE ZA UHURU MIAKA 53 UWANJA WA UHURU LEO

SHEREHE ZA UHURU MIAKA 53 UWANJA WA UHURU LEO

December 09, 2014
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika  katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo. [Picha na Ikulu.]unnamed1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika  katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo. [Picha na Ikulu.]unnamed2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika  katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo. [Picha na Ikulu.]unnamed4Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikitoa salamu ya heshma wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo katika sherehe  za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara, [Picha na Ikulu.]unnamed5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Kitaifa wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, [Picha na Ikulu.]unnamed7Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, [Picha na Ikulu.]unnamed8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, [Picha na Ikulu.]unnamed9Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa  Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.]unnamed10Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Makamo wa Pili wa  Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.]unnamed11Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.]
unnamed12Baadhi ya wananchi kutoka mitaa mbali mbali ya Jiji la Dar es Salaam na Mikoa jirani wakiwa katika   Uwanja wa Uhuru  Jijini Dare Salaam katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambazo hufanyika kila mwaka,[Picha na Ikulu.]unnamed13Mabalozi  wa Nchi mbali mbali wanaoziwakilisha Nchi zao hapa nchini pamoja na Wananchi wakiwa katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru  ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, [Picha na Ikulu.]unnamed14Mabalozi  wa Nchi mbali mbali wanaoziwakilisha Nchi zao hapa nchini wakiwa katika Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, [Picha na Ikulu.]

MKUU WA WILAYA YA KOROGWE ATOA WITO KWA KAMPUNI ZA MAWASILIANO KUSAMBAZA ZAIDI HUDUMA ZAO WILAYANI HUMO

December 09, 2014


Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo wa kwanza (kulia) akikata utepe kuzinduzua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu Korogwe mjini, katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.Hafla hiyo imefanyika hivi karibuni.
Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kulia)akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo(kushoto)kuhusiana na kifaa cha Router chenye uwezo wa kuunganisha zaidi ya watu nane kutumia huduma ya intaneti wakati wa uzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu wilaya ya Korogwe mjini.Katikati ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu na anaeshuhudia kulia ni Abubakary Lubuva.
Mfanyakazi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu Korogwe mjini,Maudy Mbaga(kulia)akitoa huduma kwa wateja wa kwanza waliofika katika duka hilo baada ya kuzinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya hiyo Mrisho Gambo(hayupo pichani)
Baadhi ya wateja wakipatiwa huduma mbalimbali na mfanyakazi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu Korogwe mjini, Abubakary Lubuva(kushoto)duka hilo lilizinduliwa rasmi na Mkuu wa wilaya hiyo Mrisho Gambo(hayupo pichani)

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo,ametoa ushauri kwa Makampuni ya Mawasiliano kufungua zaidi vituo vya kutoa huduma kwa wateja mkoani Tanga na maeneo mengine ya miji midogo inayokua kwa kasi ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.Alitoa ushauri huo wakati akifungua duka la Vodacom Tanzania lililopo Korogwe mjini ambapo pia alitoa pongezi kwa hatua hiyo.

Katika kuhakikisha wakazi wa Korogwe na maeneo jirani wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita imefungua duka jipya katika eneo la Korogwe mjini.

Korogwe ni moja ya kituo maarufu katika mkoa Tanga ambacho wanapitia wasafiri wengi wanaotumia barabara ya kuelekea mikoa ya Kaskazini ya Moshi,Tanga na Arusha.Vilevile mji huu unakuwa kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa wafanyabiashara wanaowekeza eneo hili.

Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma kwa mawakala wa M Pesa na uuzaji wa bidhaa za Vodacom na litawawezesha wateja wa eneo hilo na vitongoji vyake wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa ya Kaskazini na nchi jirani kupata huduma bora.Mtandao wa Vodacom unaongoza kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika mkoa wa Tanga.

Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard , alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.

“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu.”Anasema Richard

Vodacom ina mtandao wa maduka 86 na wakala mbalimbali wa kuuza bidhaa zake nchini na duka lililofunguliwa leo ni la pili kufunguliwa katika mkoa wa Tanga.
Nyalandu: Hatuna mpango kufukuza Wamasai Loliondo

Nyalandu: Hatuna mpango kufukuza Wamasai Loliondo

December 09, 2014

unnamed8
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akijaribu kurusha mkuki alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
unnamed
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiagana na mzee wa kimasai mara baada ya kumaliza mkutano uliokuwa na lengo la kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
unnamed1
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Raphael Rong’oi akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu (aliyekaa kwenye pikipiki).
unnamed2
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wa jamii ya kimasai mara baada ya kumaliza mkutano nao.
unnamed4
Wamasai wakichukua kumbukumbu muhimu katika mkutano wao na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.
unnamed5
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Wamasai waliokusanyika kwa ajili ya kusikia tamko la serikali juu ya uvumi wa kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
unnamed6
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akionja maji kutoka katika kisima kilichojengwa kwa ajili ya kutatua tatizo la maji katika katika eneo la Loliondo.
………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, amesema habari zinazodai kuwa Serikali inataka kuwaondoa wakazi wa zaidi ya 40,000 katika eneo la Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha hazina ukweli wowote. Novemba mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza, liliandika habari kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai wanaoishi eneo hilo. Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu. Akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai wilayani Ngorongoro mwishoni mwa wiki, Nyalandu alisema habari hizo hazina ukweli wowote isipokuwa zina lengo la kuchafua taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa. Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao. “Nami niwahakikishie wanajamii wa Loliondo, Ngorongoro na wanajamii wote wa kimasai ambao wametishiwa nyau, kuwa serikali ya Tanzania haina mpango wowote wa kumfuata na kumfukuza mtu yoyote,” alisema.

WANANCHI WAUWA MAJAMBAZI WAWILI.

December 09, 2014


MAJAMBAZI wawili wamefariki dunia na wengine kukimbia kusikojulikana kwa kupata kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya jaribio la  kupora mishahara ya wafanyakazi katika kiwanda cha Chokaa cha Meelkh Limietd kilichopo Amboni Jijini Tanga kushindikana.

Tukio hilo lilitokea Novemba 7 mwaka huu majira ya saa saba na nusu mchana ambapo majambazi hao walifika kiwandani hapo kwa lengo la kuporwa fedha hizo ambazo walishindwa kuzipata katika jaribio.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Juma Ndaki(Pichani Juu aliyesimama) alisema kuwa tukio hilo litokea Mtaa wa Amboni Kata ya Amboni Tarafa ya Mzizima ambapo majambazi hao walikwenda wakitumia usafiri wa pikipiki yenye namba za usajili MC36ABE aina ya Honda.

Aliwataja majambazi waliouwawa kuwa ni Timoth Charles(36) mkazi wa Mkwajuni jijini Dar es Salaam pamoja na Mwinyimkuu Hamisi(46) mkazi wa Chanika Jijini Dar es Salaam ambapo walifariki dunia wakiwa njiani wakipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kwa matibabu.

Alisema kuwa katika tukio majambazi wenzao walifanikiwa kukimbia na kutokomea kusikujulikana wakati msako mkali ukiendelea ili kuweza kuwabaini waliokimbia kuweza kuchukuliwa hatua.


Hata hivyo Kaimu Kamanda huyo alitoa wito kwa kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi kwa kuwauwa wanzao ambao wanadhaniwa kuwa ni wahalifu wa makosa mbalimbali ikiwemo ujambazi badala yake wawakamate na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria.

   “Huo sio utaratibu mzuri wa kujichukulia sheria mikononi kwa kuwaadhibu waahalifu ni vema mnapowakamata mkawapeleka kwenye vyombo ya sheria ili waweze kuchukua hatua kuliko kufanya hivyo “Alisema Kaimu Kamanda Ndaki.

Katika hatua nyengine aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu kwenye maeneo yao ili kuweza kudumisha hali ya amani na usalama iliyopo hapa nchin.

WAZIRI MKUU AKAGUA MABEHEWA MABEHEWA MAPYA YA TRL JANA

December 09, 2014



Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe wakikagua moja ya mabehewa mapya ya TRL yaliyonunuliwa kwa fedha ya serikali wakati alipokwenda kwenye Bandari ya Jijini Dar es salaam leo Desemba 8, 2014 kupokea mabehewa hayo.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia kwake) na Naibu Waziri wake, Dkt. Charles Tizeba (kulia) kukagua baadhi ya mabehewa mapya ya Shirika la Reli nchini (TRL) yaliyonunuliwa na kwa fedha za serikali wakati alipokwenda kwenye bandari ya jijini Dar es salaam leo Desemba 8,2014.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akiangalia jiko ambalo liko ndani ya behewa la daraja la pili kwenye moja ya mabehewa 22 yaliwasili nchini mwisho wa wiki, katika bandari ya jijini Dar es Salaam, leo Desemba 8,2014.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akishuka kwenye moja ya mabehewa 22 yakiyowasili nchini mwisho wa wiki, leo mchana katika bandari ya Dar es Salaam.Mh. Pinda alifika Bandarini hapo  kukagua mabehewa hayo. Waziri Mkuu amempongeza Waziri wa Uchukuzi pamoja na watendaji wake kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Kuimarisha usafiri wa Reli nchini. Utekelezaji wa mradi huu ni mojawapo wa Miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa(BRN).
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akimsikiliza Naibu Waziri wake, Dkt. Charles Tizeba leo mchana katika bandari ya Dar es Salaam.