WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AJITAMBULISHA KWA RAIS DR.MWINYI.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AJITAMBULISHA KWA RAIS DR.MWINYI.

September 11, 2023

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Januari Makamba (wa pili kulia) alipofika kujitambulisha na Ujumbe wake wa Uongozi mpya wa Wizara hiyo Ikulu Jijini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu] 11/09/2023 .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akizungumza na Uongozi mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliongozwa na Mhe.Januari Makamba (wa pili kulia) alipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo kujitambulisha na Ujumbe wake..[Picha na Ikulu] 11/09/2023 .

TANGA UWASA YATUMIA MILIONI 20 KUKARABATI MTANDAO WA MAJI TAKA USAGARA

September 11, 2023

 

Meneja wa Mazingira wa Tanga Uwasa Nasibu Ramadhani akikagua mtandao wa maji taka katika eneo la Usagara Jijini Tanga ambao wameufanyia ukarabati mkubwa
Meneja wa Mazingira Tanga Uwasa Nasibu Ramadhani akikagua mtandao wa maji taka katika eneo la Usagara Jijini Tanga ambao wameufanyia ukarabati mkubwa
Muonekano wa chemba zilizokarabatiwa
Muonekano wa chemba zilizokarabatiwa


Na Oscar Assenga, TANGA

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) imetumia milioni 20 kwa ajili ya kuukarabati mtandao wa maji taka wa zamani katika eneo la Usagara maarufu kama Bandari Chafu.

Akizungumza Meneja wa Mazingira wa Tanga Uwasa Nasibu Ramadhani alisema uamuzi wa kuukarabati mtandao huo wa maji taka waliufanya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa wa eneo hilo tokea 2018.



Alisema malalamiko hayo yalikuwa yanahusiana na miuondombiu ya maji taka eneo hilo kuwa chakavu na hivyo kuhatarisha afya zao na hivyo kuomba mtandao huo uliojengwa na TPA miaka ya nyuma na hivyo baada ya kubinafishwa nyumba hizo.



Alisema hivyo wanawaomba Tanga Uwasa iwarebishie mfumo huo ambapo awali ulikuwa baada ya kuona changamoto hizo waliamua watenge fedha Milioni 20 kwa ajili ya kuukarabati mtandao huo.



Alisema katika ukarabati wa mtandao huo ulihusisha ukarabati wa chemba kubwa ambazo zinapokea maji taka kutoka kwenye maeneo hayo na ukarabati wa chemba ndogo ndogo ambazo zinaunganisha bomba na bomba na maeneo yenye bomba chakavu .



“Hayo ndio maeneo tuliyoyakarabati na tunatarajia kukarabati na mwaka huu tutakamilisha mpango huo wa ukarabati kukamilisha mfumo hiyo ili kuuwezesha kuishi muda mrefu hiyo itasaidia kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza”Alisema



Hata hivyo alitoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kuhakikisha miundombinu ya maji taka kuhakikisha hawaweki taka ngumu na wanaitunza ili iweze kukaa muda mrefu
TAASISI 13 ZA KIMATAIFA KUANGAZIA HAKIMILIKI ZA ARDHI JIJINI ARUSHA

TAASISI 13 ZA KIMATAIFA KUANGAZIA HAKIMILIKI ZA ARDHI JIJINI ARUSHA

September 11, 2023

 

Ni mkutano wa Siku tatu unaozikutanisha Taasisi za Kimataifa kutoka mataifa 13 barani Afrika kujadili utekeleza wa hakimilki za ardhi kwa wenyeji wa bara la Afrrika baada ya tafiti kuonesha ongezeko la uelewa wa hakimilki za ardhi hususani kwa wenyeji wa Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.

Mkutano huu   ni hatua muhimu ya kimkakati kuendeleza uwajibikaji na hatua zitakazopelekea utekelezaji wa Mkutano wa Kimataifa wa Mazingira wa mwaka 2023 kwa lengo la kuimarisha utashi wa kisiasa, kukusanya rasilimali na kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa hakiardhi barani Afrika.

Mgeni rasmi wa Mkutano huu ni Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati  Dkt. Doto Biteko, Taasisi zitakazoshiriki katika Mkutano ni pamoja na Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Mawaziri wa kisekta kutoka Nchi 13 za Afrika na utafanyika katika hoteli ya Mount Meru ya Jijini Dodoma tarehe 12 Septemba mwaka huu.

Serikali na Taasisi za Kimataifa barani Afrika wanaangazia usalama wa watu na jamii za jadi kama nyenzo muhimu ya amani ya Jamii na maendeleo endelevu ya kiuchumi barani Africa aidha pamoja na juhudi hizi sheria na sera za zilizotungwa miaka 15 iliyopita bado hazijatekelezwa na kuna fursa chache miongoni mwa Taasisi na Taasisi na baadhi ya Mataifa barani Afrika.

CHONGOLO AZUNGUMZA NA WADAU MBALIMBALI WA DEMOKRASIA NCHINI

September 11, 2023

 



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Godfrey Chongolo akizungumza na wadau mbalimbali wa demokrasia nchini, wakiwemo Viongozi wa Vyama vya Siasa, Waandishi wa Habari, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Asasi za Kiraia na makundi mengine, waliohudhuria uzinduzi rasmi wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia Kutathmini Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi na Hali ya Siasa nchini, uliofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 11, 2023, jijini Dar Es Salaam.

Mkutano huo unaofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) unawashirikisha Wadau wa Demokrasia, wakiwemo Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia, Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kimila.

WAZIRI PROFESA NDALICHAKO AFUNGUA SEMINA KWA WASTAAFU WATARAJIWA WA PSSSF

September 11, 2023

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, mara baada ya kuzunguzma na wastaafu watarajiwa 

 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DAR ES SALAAM.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amefungua semina elekezi kwa Wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2023.

Akizungumza na wastaafu hao kutoka mkoa wa Dar es Salaam, Profesa Ndalichako aliipongeza PSSSF kwa kuandaa semina hiyo iliyobeba kauli mbiu isemayo “Wekeza Mafao yako Sehemu Salama kwa Uhakika wa Ukwasi”.

Alisema lengo la semina hiyo ni kuwajengea wastaafu wake watarajiwa uelewa na ufahamu juu ya umuhimu wa kufanya maamuzi sahihi ya kukuza vipato vyao baada ya kustaafu ili kuleta tija na uendelevu wa kipato.

“Usia wangu kwenu ni kuyatumia vyema madini ya elimu mtakayoyapata hapa kwa kushikilia mambo makuu matatu nayo ni kuwa na mtazamo chanya, kuweka mipango makini na kutimiza ndoto binafsi baada ya kustaafu.” Alisema Profesa Ndalichako.

Alisema kustaafu ni wajibu kwa kila mtumishi hivyo hakuna budi kuendeleza maisha mazuri hata baada ya kustaafu.

Alisema ni vema mtumishi akatambua kuwa safari ya kustaafu inaanza pale anapoanza ajira, hivyo ni muhimu kujiandaa kimipango na kifedha ili kufurahia maisha ya uhuru lakini umakini katika usimamizi wa fedha.

“Matumizi ya busara ya fedha baada kustaafu ni muhimu zaidi kwani kwa kiasi kipato kinapungua na nguvu za kufanya kazi zinaenda zikipungua siku hadi siku,” aliasa.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema PSSSF inatarajia kuwa na wastaafu 11,000 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024.

Alisema Wastaafu watapatiwa mafunzo ya elimu ya uwekezaji katika masoko ya fedha, taarifa za nyaraka na utaratibu wa kufuata wakati wa kustaafu, kujiandaa kisakolojia baada ya kutoka kwenye utumishi, umuhimu wa kutunza mazingira tunayoishi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, na uhalifu wa kimtandao ambao unawaathiri wastaafu wengi.

“Mfuko katika kutambua na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, una mpango wa kutoa mche mmoja wa mti kwa kila mstaafu wa PSSSF.

“Mpaka sasa tuna wanachama 739,000 na lengo hapa ni kila mmoja aweze kupanda na kuutunza mche tutakaompatia pindi atakapofikia wakati w akustaafu.”Alifafanua CPA. Kashimba.

Semina kama hii ilifanyika mwaka 2021 kwa wastaafu watarijiwa 3700 bara na visiwani na mwaka huu pia elimu itawafikia wastaafu kwenye mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani, alisema CPA. Kashimba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (wapili kushoto) akimpatia mche wa mti, moja wa wastaafu wakati w aufunguzi wa semina kwa wastaafu watarajiwa wa PSSSF jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2023. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kushoto) na Meneja wa PSSSF Kanda ya Ilala, Bi. Uphoo Swai.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na wastaafu watarjiwa jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na wastaafu watarjiwa jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2023. Kulia ni CPA. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu, PSSSF.
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo, wakiwemo wastaafu na wawezshaji (watoa mada).
Semina ikiendelea
CPA. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu, PSSSF, akizungumza na wastaafu watarajiwa
CPA. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu, PSSSF, akizungumza na wastaafu watarajiwa
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mhgeni rasmi.
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mhgeni rasmi.
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mhgeni rasmi.
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.
Baadhi ya watendaji wa Mfuko.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Bw. James Mlowe, akiongoza semina hiyo.

Baadhi ya watendaji wa Mfuko.

Baadhi ya watendaji wa Mfuko.
Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa, akizungumza mwanzoni mwa semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mhgeni rasmi
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mhgeni rasmi
Mmoja wa wastaafu akizunhguzma

MAAFISA UVUVI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO YA SHERIA YA UTUNZAJI WA WANYAMA BAHARI YA MAREKANI

September 11, 2023

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


WATAALAMU wa Uvuvi kutoka Tanzania Bara na Visiwani wameanza Mafunzo ya kujengewa uwezo kwenye masuala ya Sheria ya Utunzaji wa Wanyama bahari ya Marekeni ambayo yanatolewa na Wataalamu wabobezi kutoka nchini Marekani.

Akizungumza na Waandishi wa habari wakati akifungua Mafunzo hayo leo Septemba 11,2023 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe amesema Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinauza mazao ya bahari pamoja na mazao hai kutoka baharini na wanauza mazao hayo hadi Marekeni.

"Wao Marekani ili ufanye nao biashara lazima ufahamu sheria zao, kupitia Shirika la Kimataifa la USAID waliona ni vizuri walete wataalamu ili wawafundishe maafisa Uvuvi wa Tanzania". Amesema

Aidha Prof. Shemdoe amesema mafunzo hayo namna mojawapo ya kulitangaza soko la mazao ya uvuvi katika nchi yetu ya Tanzania ambapo itafungua mwanya wa kupata wawekezaji wakubwa katika sekta ya mazao ya wanyama bahari.

Pamoja na hayo amewasisitizia maafisa hao wazingatie mafunzo hayo wanayopewa kwasababu sio wote uhudhuria mafunzo hayo ya mazao bahari hivyo wawe mabalozi na wakufunzi kwa wengine ambao hawakufika katika mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yanatolewa kwa siku tano ambapo yameanza leo Septemba 11,2023 na kufikia tamati Septemba 15,2023.



Waziri Gwajima: Wajasiriamali wanawake na vijana changamkieni fursa za IMBEJU

September 11, 2023

 

Dar es Salaam. Tarehe 11 Septemba 2023: Akizindua Maonesho ya Imbeju ya Wajasiriamali Ilala 2023, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima amewahimiza wafanyabiashara wadogo nchini hasa wanawake na vijana kuchangamkia fursa ya mafunzo, ushauri, na mitaji wezeshi inayotolewa na CRDB Bank Foundation kupitia program ya IMBEJU.

Waziri Gwajima amesema wanawake na vijana ndio injini ya uchumi wa taifa kwani ni kundi lenye uwezo mkubwa wa kuchangia mafanikio ya kijamii na kiuchumi. Hata ripoti ya Sensa na Makazi ya mwaka 2022, amesema inadhihirisha hilo ikibainisha kuwa asilimia 51 ya watu wote nchini ni wanawake na asilimia 75 ni vijana hivyo makundi haya mawili kuwa sehemu muhimu ya nguvukazi ya taifa.
“Hata hivyo, wanawake na vijana wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwamo mila na desturi kandamizi, elimu duni, ukosefu wa mitaji na stadi za ujasiriamali. Serikali imechukua hatua mbalimbali zinazolenga kujenga uchumi jumuishi na shirikishi ili kuwakomboa kiuchumi, ni wakati sasa wa kila mjasiriamali mdogo kuzitumia fursa zinazotolewa na CRDB Bank Foundation na Benki ya CRDB kwani mkizitumia vizuri, itakuwa rahisi kukabiliana na changamoto hizi na kukuza biashara zenu,” amesema Waziri Gwajima. 

Vilevile, Waziri amesema Serikali inafanya kazi usiku na mchana kuwawezesha wanawake kiuchumi hivyo inaendelea kutekeleza mkakati wa kutimiza malengo ya Jukwaa la Kimataifa ya Kukuza usawa wa Kijinsia hususan katika Haki na Usawa wa Kiuchumi.

Uwezeshaji wa wanawake na vijana, amesema ni suala linalotiliwa mkazo katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya 2050, na Sera ya Maendeleo na Jinsia ya Mwaka 2000. 
Maonesho hayo ya wajasiriamali yanayofanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia Septemba 11 mpaka 13 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yameandaliwa na Taasisi ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Wilaya ya Ilala yakiwakusanya zaidi ya wajasiriamali 3,000 wa halmashauri hiyo, Jiji la Dar es Salaam na Tanzania nzima kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema benki inathamini shughuli za kijasiriamali kwa kutambua kuwa zimekuwa msaada mkubwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya taifa. 
“Tunaamini ili sekta hii itoe mchango wake kikamilifu katika kukuza uchumi wa Taifa, kunahitajika huduma na mifumo shirikishi itakayowawezesha wajasiriamali kutimiza malengo yao. Imani hii ndio iliyoishawishi Benki yetu ya CRDB kuanzisha kitengo maalum kwa ajili ya kuhudumia wateja wa kundi hili tangu mwaka 2005,” amesema Nsekela.

Kutokana na jitihada hizo, amesema Benki ya CRDB imekuwa kinara katika uwezeshaji wajasiriamali kwani hadi robo ya pili mwaka huu imetoa mikopo ya zaidi ya Shilingi trilioni 3.4 kwa wajasiriamali 200,000 huku wajasiriamali wengine 50,000 wakinufaika na mafunzo yaliyotolewa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema juhudi za kuwajengea ujasiri wajasiriamali wanaoshiriki maonesho hayo pia yanazihusisha mamlaka nyingine za Serikalina sekta binafsi ikiwamo TRA, BRELA, SIDO, VETA, NHIF, NIDA, Wakala wa Ununuzi Serikalini (PPRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA), kampuni ya GS1, NSSF, Shirika la Bima la Taifa (NIC) huku Benki ya CRDB ikiwapa elimu ya fedha na fursa za mikopo ilizonazo.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amesema maonesho hayo ni mwanzo wa safari endelevu ya kuwapa wajasiriamali nchini fursa ya kuonyesha biadhaa zao hivyo kunufaika na soko kubwa la ndani na watakapokuwa tayari watoke nje ya mipaka ya Tanzania.
“Maonesho haya ni sehemu ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa wajasiriamali wetu kwa kuwatengenezea masoko ya huduma na bidhaa zao kupitia programu yetu ya IMBEJU. Katika maonesho wajaisiriamali wanawake na vijana wamepata fursa ya kuonesha huduma na bidhaa zao bure bila kuingia gharama zozote za maonesho. Niwakaribishe watanzania kuwaunga mkono wajasiriamali wetu ili waweze kuku, jambo ambalo litachochea ukuaji wa uchumia wa Taifa letu,” amesema Tully.

Tully amesema hadi sasa, IMBEJU imewafikia zaidi ya biashara changa za vijana 700 kupitia program shindani, na zaidi ya wanawake wajasiriamali 100,000. Kwa upande wa mitaji wezeshi CRDB Bank Foundation imeshatoa Shilingi milioni 250 kwa wajasiriamali kwa zaidi ya 100, na leo hii imekabidhi mitaji wezeshi ya pikipiki 9 na bajaji 4 kwa wajasiriamali wanawake. Aliongezea kuwa zoezi la kutoa mitaji wezeshi linaendelea nchi nzima na kuwa Shilingi bilioni 5 zimetengwa. 
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Bank Foundation, Martin Warioba alimhakikishia Waziri Gwajima kuwa taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wanawake na vijana ili kujenga uchumi jumuishi ambao watu wote wanafursa ya kushiriki na kufaniki. “Nikuahidi Mheshimiwa Waziri huu ni mwanzo tu, malengo yetu ni kuyafanya maonesho haya kuwa endelevu hapa Wilaya ya Ilala, lakini matarajio yetu ni kwanda nchi nzima,” amesema.