AFRICAN SPORTS WAANZA VEMA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA, YAICHAPA KILUVYA UNITED KAMOJA TU.

May 10, 2014


NA SAID KARSANDAS, MOROGORO.

MABINGWA wa soka Tanzania bara 1988 African Sports “Wanakimanumanu” leo wameanza vema michuano ya Ligi ya Mabingwa wa mikoa mara baada ya kuibamiza Kiluvya United  bao 1-0 mchezo uliochezwa kwenye dimba la soka Jamhuri mkoani hapa.

Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani wa hali ya juu ambao mpaka timu zote zinakwenda mapumziko hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi.

Wakionekana kujipanga baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake,African Sports waliweza kucheza vema wakiwa na wachezaji wake mahiri waliowasajili msimu huu.

Ilikuwa ni dakika ya 76 mashabiki wa timu ya African Sports walipoinuka kwa shangwe na nderemo kutokana na shuti kali lililopigwa na James Mendy na kuzama wavuni.

Akizungumzia mchezo huo,Kocha Mkuu wa timu hiyo,Ally Manyani alisema ushindi huo umewapa matumaini makubwa ya kuendelea kujipanga ili kuweza kupata matokeo mazuri lengo likiwa kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Mwisho.

AURORA ATAKA MSHIKAMANO COASTAL UNION.

May 10, 2014
NA SALMAH MUHIDINI,TANGA.
MWENYEKITI wa Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora amewataka wapenzi na wanachama wa timu hiyo kuendeleza mshikamano lengo likiwa kupiga hatua mbele za kimaendeleo kwenye mikakati waliojiwekea.

Aurora aliyasema hayo hivi karibuni baada ya kufungua matawi mawili ya klabu hiyo moja likiitwa Saigon lililopo Mabanda ya Papa na Coastal Nyumba lililopo katikati ya Jiji la Tanga ambapo jumla ya wanachama wapya 120 walipokelewa.

Alisema ni vema hasa kwenye kipindi hiki cha kuelekea usajili wanachama na wapenzi wapaswa kuonyesha mshikamano na utulivu ili viongozi waliopewa mamlaka waweze kufanya kazi hiyo kubwa iliyopo mbele yao lengo likiwa ni kujiandaa vema na ligi kuu.

   “Ndugu zangu wanachama na wapenzi tusibaguane tuungane pamoja kwani tunajenga nyumba moja kwanini tugombee fito, badala yake tuwe kitu kimoja kuhakikisha timu yetu inapata maendeleo makubwa “Alisema Aurora.

Katika hatua nyengine,Mwenyekiti huyo alisema usajili wa timu hiyo msimu huu utakuwa ni wa kihistoria kutokana na mikakati mizuri waliojiwekea uongozi huo kuhakikisha wanasajili wachezaji wazuri watakaofanya vizuri kwenye kikosi hicho cha wagosi wa kaya.

MVUA YAHARIBU CHEMBA ZA CHOO KATIKA SHULE YA MSINGI ZINGIBARI

May 10, 2014