BOT YASHIRIKI KWENYE MAONESHO NANENANE JIJINI MBEYA

August 01, 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akisalimiana na Naibu Gavana, Bw. Julian BanzI Raphael, alipotembelea banda la BoT kwenye Maonesho ya Wakulima (Nane Nane) yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Afisa Benki kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bw. Andrea Chimbotela, akizungumza na mwananchi alietembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.


Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Malipo kutoka Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Bw. Nestory Maro, akifafanua jambo kwa mwananchi alietembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Ujumuishi wa Huduma za Fedha, Bw. Ramadhani Myonga, akielezea jambo kwa mwananchi alietembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Kushoto ni Mchumi kutoka Kurugenzi ya Ustawi na Ujumuishi wa Huduma za Fedha BoT, Bw. Lucas Magazi.      
Afisa kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki BoT, Bi. Neema Hashim, akitoa elimu kuhusu historia ya noti na sarafu za Tanzania kwa wananchi waliotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Naibu Gavana, Bw. Julian BanzI Raphael, akizungumza na Meneja Mawasiliano BoT, Bi. Victoria Msina, alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Kulia ni Meneja Idara ya Fedha na Utawala Tawi la BoT Mbeya, Bw. Agathon Kipandula.

MAKAMU WA RAIS DKT PHILIP MPANGO AIPONGEZA NIC INSURANCE KWA KUTOA BIMA ZA KILIMO

August 01, 2023

 Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya

MAKAMU wa Rais Dkt.Philip Mpango ameipongeza NIC Insurance kwa kuwaponya wakulima kwa changamoto zinapowakuta wa kilimo.

Dkt.Mpango ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la NIC kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Dkt.Mpango amesema kuwa NIC Insurance iendelee kutoa elimu zaidi kuhusiana bima za kilimo kwa kuongeza wigo wakulima kufikiwa na bima.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema NIC Insurance ni kampuni ya kwanza kutoa bima ya kilimo ambayo imesaidia wakulima.

Bashe amesema kuwa mwaka juzi NIC Insurance ililipa bima kwa baadhi ya mazao mbalimbali waliokumbwa na majanga.

Hata hivyo amesema kuwa amesema kuwa kazi iliopo ni kuongeza uwigo mazao mbalimbali katika kuhakikisha wakulima wanakuwa na uhakika pale wanapopata majanga.
Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango akisoma kipeperushi cha taarifa cha NIC Insurance wakati alipotembelea banda la NIC Insurance kwenye Ufunguzi wa Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango akipata Maelezo kuhusiana na NIC kuwa kampuni ya kwanza kutoa bima za kilimo kutoka kwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati alipotembelea banda la NIC Insurance kwenye Ufunguzi wa aonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango akipokelewa na Meneja wa NIC Insurance Justine Iseni wakati alipotembelea banda la NIC Insurance kwenye Ufunguzi wa Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
WIKI YA AZAKI 2023 YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR

WIKI YA AZAKI 2023 YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR

August 01, 2023

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga, (wa pili kushoto), akiwa na Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustini Ndugulile pamoja na wadau wengine wakipiga makofi mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi rasmi wa Wiki ya Azaki iliyozinduliwa leo Agosti 1,2023 Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Azaki iliyofanyika leo Agosti 1, 2023, Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Wiki ya AZAKi 2023, Justice Rutenge akizungumza katika hafla hiyo kuelezea namna kaulimbiu ya mwaka huu ilivyobeba dhima nzima ya Wiki ya Azaki.

Benki ya CRDB yatwaa tuzo nne za kimataifa nchini Nigeria

August 01, 2023

 

 

Lagos, Nigeria. Tarehe 1 Agosti 2023: Taasisi kubwa zaidi ya fedha nchini, Benki ya CRDB imenyakua tuzo nne za kimataifa za umahiri katika ugavi zijulikanazo kama Africa Procurement and Supply Chain Awards (APSCA) 2023 jijini Lagos nchini Nigeria.

Benki yenyewe imeshinda tuzo mbili huku viongozi wake nao wakinyakua tuzo mbili kwa kutambua mchango wao katika kusimamia na kuongoza taratibu na viwango vya ununuzi na ugavi.

Katika hafla hiyo iliyo iliyofanyika katika Hoteli ya Oriental, Benki ya CRDB imenyakua tuzo ya umahiri katika ubunifu kwenye ununuzi na ugavi (sekta ya benki) na tuzo ya taasisi yenye idara bora ya ununuzi na ugavi. Pia, Mkurugenzi Mtendaji wake, Abdulmajid Nsekela akitambuliwa kama Afisa Mtendaji Mkuu Anayewezesha vyema Idara ya Ununuzi na Ugavi huku Mkuruguzi wa Ununuzi wa Benki ya CRDB, Pendason Philemon,  akitunukiwa tuzo ya mchango mkubwa kwenye taaluma ya ununuzi na ugavi katika sekta ya benki akiwa miongoni mwa viongozi 50 wa eneo hilo waliotambuliwa katika awamu hii ya tano ya APSCA.

Akipokea tuzo kwa niaba ya Nsekela, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dkt Benson Bana amesema ni furaha kubwa kwake kuungana na Watanzania wenzake, hasa wafanyakazi wa Benki ya CRDB ambayo imeliheshimisha taifa kwa kushinda tuzo nne za umahiri katika ununuzi.

“Naipongeza sana Benki ya CRDB, viongozi na wafanyakazi wake hasa Bwana Abdulmajid Mussa Nsekela ambaye amepewa tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu anayewezesha vyema Idara ya Ununzi na ndugu yangu Philemon ambaye amezawadiwa tuzo ya juu katika masuala ya ununuzi. Ni heshima kwa Watanzania, Benki ya CRDB imetuweka mbele na kutuheshimisha na imeendelea kuunga juhudi za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan za kuifungua nchi kwani Tanzania sasa inasikika Nigeria na imesikika Afrika na sio kusikika tu bali kuzoa tuzo katika eneo la ununuzi kimataifa,” amesema Balozi Bana.

Tuzo za APSCA huwatambua wataalamu, idara na taasisi zenyeumahiri,  mchango au umakini mkubwa katika kuzingatia viwango vya hali ya juu katika ununuzi na ugavi kimataifa. Hili linafanywa kwa imani kwamba ununuzi unaozingatia viwango vya kimataifa ni muhimu kwani unaweza kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza ufanisi wa taasisi na jamii kwa ujumla.

Akielezea ushindi uliopatikana, Philemon amesema kila mwaka APSCA hutoa tuzo hizo, lakini Benki ya CRDB imeshiriki kwa mara ya kwanza mwaka huu ambao umeshuhudia washiriki 83 wakichuana na Benki kuibuka kidedea tena kwa kishindo.

“Ilikuwa furaha na fahari ya aina yake kwa benki yetu kuitwa jukwaani mara nne kwenda kupokea tuzo za umahiri mbele ya mamia ya wataalamu wa fani ya ununuzi na ugavi. Ulikuwa usiku mzuri kwa Benki ya CRDB na kampuni ya mawasiliano ya MTN ya nchini Nigeria tuliong’ara Zaidi kwa kupata tuzo nyingi, nne kila taasisi. Tuzo hizi zinadhihirisha uwezo mkubwa wa Watanzania kwamba tunaweza kushindana kimataifa na kutoka kimasomaso hivyo tujielekeze kupambana na wenzetu kutoka popte duniani,” amesema Philemon.

Kwa upande wake, Nsekela amesema usimamizi wa ununuzi na ugavi ni suala nyeti ambalo ni zaidi ya kuhamisha bidhaa kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mteja.

“Kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa sawia, kunahitaji jicho makini la menejimenti. Bila idara imara ya ununuzi na ugavi, benki haiwezi kutoa huduma bora kwa wateja wake. Mchango wa idara hii unajenga msingi wa mafanikio ya benki katika maeneo mbalimbali. Nimefuahi kuona idara yetu ununuzi na ugavi pamoja na menejimenti yake ikitambuliwa  kutokana na umahiri wake kwa kuzingatia kanuni zinazotakiwa na kukubalika duniani kote. Naahidi nitaendelea kuipa ushirikiano kadri itakavyohitajika,” amesema Nsekela.

Mkurugenzi huyo ameeleza kwamba Bara la Afrika kwa sasa linatekeleza mkataba wa eneo huru la biashara unaoruhusu  biashara, bidhaa na huduma  kufanyika bila mipaka na pia raia wa kiafrika kuvuka mipaka bila vikwazo hivyo kufungua soko la zaidi ya watu bilioni 1.3. Ili kulihudumia kiushindani soko hili, kampuni na taasisi zinapaswa kufanya biashara na kutoa huduma kwa kuzingatia vigezo na viwango vya kimataifa.

“Benki ya CRDB inakusudia kutoa huduma zake kwa watu wengi katika soko hili kubwa. Hilo litafanikiwa kwa kuwa Benki inajikita katika umahiri wa kutoa huduma viwango vya kimataifa. Tuzo hizi tulizoshinda ni uthibitisho kwamba huduma zetu ni za kiwango kikubwa zinazolenga kukidhi malengo na matarajio ya wateja wetu,” amesisitiza Nsekela.

Kwa miaka minne mfululizo, tuzo za APSCA zilikuwa zinafanyika nchini Ghana. Zikifanyika nchini nigeria mwaka huu, tuzo hizo zimeandaliwa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Ununuzi na Usimamizi wa Ugavi (CISCM)), Taasisi ya Ununuzi na Ugavi Ghana (GIPS) na Chama cha Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi Nigeria (APPON).

--