KENYA YATINGA NUSU FAINALI KWA KUIFUNGA RWANDA 1-0, SASA KUCHEZA NA KILI STARS

December 07, 2013

Na Mahmoud Zubeiry, Mombasa
TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars itamenyana na wenyeji, Kenya, Harambee Stars katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Desemba 10, mwaka huu Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Mshambuliaji wa Kenya, Haambee Stars, Jacob Keli akiwatoka mabeki wa Rwanda, AmavubiBayisenge Emery kulia na Tubane James kushoto Uwanja wa Manispaa, Mombasa leo.

Hiyo inafuatia Kenya kuifunga Rwanda 1-0 katika Robo Fainali ya pili CECAFA Challenge jioni hii Uwanja wa Manispaa, Mombasa Kenya, bao pekee la beki wa Azam FC ya Dar es Salaam, Joackins Atudo kwa penalti dakika ya 56.
Mapema katika Robo Fainali ya kwanza, Stars iliwatoa mabingwa watetezi, Uganda kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Robo Fainali nyingine zitachezwa kesho, Ethiopia na Sudan na Zambia na Burundi, Uwanja wa Manispaa pia.

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO KIKUU BAGAMOYO

December 07, 2013
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata keki ya mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013, kulia Mkuu wa Chuo hicho Petired Bishop Elinasa Sendoro, kushoto Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Costa Ricky Mahalu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.

UVCCM TANGA KUANZA ZIARA KESHO MKOANI TANGA.

December 07, 2013

IMEWEKWA JUMAMOSI:DESEMBA 7 SAA 6:45 JIONI.

 JUMUIYA wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga(UVCCM) inatarajia kuanza ziara yake kesho kwa mkoa mzima wa Tanga kukutana na viongozi wa umoja huo ngazi za wilaya pamoja na kufanya mikutano ya hadhara.


Akizungumza leo na Blog hii,Mwenyekiti wa Umoja huo,Abdi Makange amesema ziara hiyo itakuwa na lengo la kukutana na mabaraza ya umoja wa vijana kila wilaya ili  kuwekeana mikakati mbalimbali ya kuufanya umoja huo uzidi kuwa imara pamoja na kuwashukuru wajumbe wa umoja huo.



Amesema  suala lengine watakalolifanya katika ziara hiyo ni kuangalia uhai wa jumuiya hiyo kwenye wilaya hizo utakaoendena sambamba na ufunguzi wa matawi ya umoja huo lengo likiwa ni kuuimarisha



Makange amesema ziara hiyo kwa kila wilaya zitakuwa zikihitimishwa na ufanyikaji wa mikutano ya hadhara ambapo wananchi wa wilaya husika watapata nafasi ya kupata sera makini za umoja huo ambazo zitakuwa zikitolewa na viongozi wake.