SIASA ZA CHUKI NA CHAFU HAZIWEZI KULETA MAENDELEO KATIKA TAIFA LETU

January 12, 2017
 Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Mhandisi Shaban Kaswaka (kushoto), akimtambulisha kwa wananchi Mgombea Udiwani kupitia chama hicho Kata ya Kijichi, Abdallah Shamas katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Mwanamtoti Temeke jijini Dar es Salaam jana.
 Mgombea Udiwani kupitia chama cha CUF wa Kata ya Kijichi, Abdallah Khalid Shamas akihutubia katika mkutano huo.
 Wasanii wa kundi la Sanaa la Mwamuko wakitoa burudani kwenye mkutano huo.
 Wafuasi wa CUF wakimkaribisha mgombea udiwani wa Kata ya Kijichi wakati alipokuwa amewasili kwenye mkutano wake wa kampeni.
 Meza kuu katika mkutano huo.
 wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Sera za CUF zikitolewa.
 Mkutano ukiendelea.
Wafuasi wa chama cha CUF wakiinua mikono kukubali kumpigia kura mgombea wa chama hicho.

Na Dotto Mwaibale

MGOMBEA  Udiwani  Kata ya Kijichi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Abdallah Khalid Shamas amewataka wananchi na wagombea wenzake kuacha siasa za chuki na chafu ili kuiletea maendeleo kata hiyo na taifa kwa ujumla.

Shamas alitoa ombi hilo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika eneo la Mwanamtoti Kijichi Dar es Salaam jana wakati akijinadi kwa wapiga kura.

"Siasa  chafu za chuki na  zinazowatenganisha wananchi kutokana na itikadi za vyama vyao hazifai na haziwezi kuleta maendeleo katika kata hiyo na taifa kwa ujumla" alisema Shamas.

Alisema siasa chafu zilizokuwepo katika eneo hilo la Mwanamtoti zilifikia hatua ya kugawana makaburi jambo ambalo lilikuwa ni hatari katika kushirikiana.

Akizungumzia baadhi ya vipaumbele vyake iwapo atachaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo alisema cha kwanza ni kuhakikisha eneo la Mwanamtoti wanapata shule ya msingi ambayo itawasaidia watoto wa eneo hilo kutotembea umbali mrefu wa kwenda shuleni.

Alitaja kipaumbele chake cha pili ni kuhakikisha eneo hilo linapata zahanati pamoja na kukaa na wataalamu wa taasisi za fedha kuona namna ya kuanzisha Saccos au chombo cha fedha ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi wa kata hiyo kukopa na kufanikisha maendeleo yao.

Mgombea huyo amewaomba wananchi wa eneo hilo Januari 22, mwaka huu wamchague ili awatumikie baada ya kata hiyo kukosa maendeleo kwa zaidi ya miaka 20.

Uchaguzi huo mdogo wa ngazi ya udiwani unafanyika katika kata hiyo kufuatia aliyekuwa diwani kufariki dunia mapema mwaka jana na nafasi hiyo kuwa wazi.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA SHINYANGA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 53 MAPINDUZI YA ZANZIBAR

January 12, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwasalimia wananchi wa Shinyanga waliofika katika uwanja wa mpira wa Kambarage katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kwaya ya KKKT Shinyanga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. PICHA NA IKULU

SBL inalaani kusambazwa kwa video isiyo na maadili kwenye mitandao ya kijamii

January 12, 2017



Taarifa kwa vyombo vya habari

Dar es Salaam Januari 12, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti inapenda kuarifu wateja wake na  umma na kwa ujumla kuwa  video isiyo na maadili   iliyosambaa mtandaoni  ikiwa inaonesha msanii akiigiza  na kuimba wimbo wenye  mahadhi ya taarabu  mbele ya bango la  lenye nembo  Serengeti Premiur Lager haihusiani na wala haikusambazwa na  Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)..

Tunapenda kuweka bayana kuwa onesho la msanii huyo halikuidhinishwa na SBL Pia  msanii huyo sio sehemu na hajawahi kuwa mmoja wa mawakala wetu wanaotoa huduma za kutangaza bidhaa zetu.

Video hiyo ambayo haikukaa na wala kuzingatia maadili ya sanaa pamoja na maonesho ya wazi inatoa picha mbaya na hata maudhui ya sanaa husika jambo ambalo  haliwezi kufanya na taasisi inayohesimika ndani ya jamii kama SBL.

SBL imekuwa mstari wa mbele  katika kulinda na  kusimamia maadili katika shughuli zake  za kijamii  ikiwa ni pamoja na kuhamasisha  unywaji wa kistaarabu.

Tunauhakikishia umma na wateja wetu kuwa  SBL inafanya shughuli zake za kijamii kwa kuangalia mambo yenye tija kwa jamii na sio vinginevyo.

Tunashukuru sana kwa kuendelea kushirikiana nasi

Imetolewa na

Mkurungezi wa Mkurungezi wa Mahusiano

Serengeti Breweries Limited.

FURAHIA OFA HIZI ZA 'TRAVEL WEDNESDAY' KUTOKA JUMIA TRAVEL

January 12, 2017

Na Jumia Travel Tanzania


Kila siku ya Jumatano ya kila wiki, Jumia Travel (www.travel.jumia.com) huwa inawaletea wateja ofa za punguzo la bei kutoka hoteli mbalimbali nchini Tanzania ambazo hudumu mpaka siku ya Ijumaa.


Ofa hizi humuwezesha mteja kuchagua na kulipia sehemu anayoitaka kwa njia ya mtandaoni au pindi atakapowasili hotelini. Lengo kubwa ni kumuwezesha kila mtu kufurahia utajiri wa sehemu lukuki za kuvutia zinazopatikana kila kona ya nchi kwa gharama nafuu.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA MWIGUMBI-MASWA (50.3) MKOANI SIMIYU

January 12, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka watatu kutoka kulia Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa wakwanza kulia pamoja na viongozi wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengiene  akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa mradi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS  Mhandisi Cristianus Ako kabla ya kuweka jiwe la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS  Mhandisi Cristianus Ako kabla ya kuweka jiwe la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye Ubao kwa kutumia Chaki zinazotengenezwa na Kiwanda cha Chaki cha Maswa Mkoani Simiyu. Rais Dkt. Magufuli aliwapongeza wenye kiwanda hicho na kuwashauri kukipanua zaidi ili kiweze kuwafikia Watanzania wengi wenye mahitaji ya Chaki.
LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA KESHO IJUMAA

LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA KESHO IJUMAA

January 12, 2017
Wakati timu pinzani ‘derby’ za JKT Ruvu na Ruvu Shooting zikitarajiwa kuchuana kesho Ijumaa Januari 13, 2017 kwenye Uwanja wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Bodi ya Ligi Kuu, imetangaza tarehe rasmi za michezo mitatu ambayo awali haikupangiwa tarehe katika ratiba.
Mbali ya ‘derby’ ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting, Jumamosi Januari 14, 2017 kutakuwa na mchezo mwingine wa upinzani kati ya Stand United na Mwadui FC – zote za Shinyanga na zitapambana kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.
Kadhalika siku hiyo ya Jumamosi Januari 14, 2017 Kagera Sugar itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika mchezo mwingine wa VPL.
Jumapili Januari 15, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu ya Vodacom ambako Mbao itakuwa mwenyeji wa African Lyon ya Mwanza katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kadhalika Jumatatu Januari 16, 2017 kutakuwa na mchezo mmoja tu ambako Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Michezo mitatu ambayo haikupangiwa tarehe hapo awali kwa alama ya TBA ikiwa na maana ya kutajwa baadaye (To Be Announced), tayari Bodi ya Ligi – chombo cha Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), kinachosimamia na kuendesha ligi, imepanga tarahe.
Tarehe hizo ni Januari 17, 2017 – siku ya Jumanne kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Majimaji itakayowaalika mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Young Africans ya Dar es Salaam katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Kadhalika mechi nyingine ziliopangiwa tarehe na muda ni kati ya Mtibwa Sugar itakayocheza na Simba, Jumatano Januari 18, 2017 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mchezo huu wa Azam na Mbeya City utaanza saa 1.00 usiku wakati michezo yote tajwa hapo juu itaanza saa 10.00 jioni lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa mashabiki kushuhudia mechi nyingi kupitia Kituo cha Televisheni cha Azam - Wadhamini wenza wa ligi hiyo.
Ligi hiyo ambayo pia inabarikiwa na Benki ya Diamond Trust (DTB), Mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom iliyokuza ubora wa huduma zake hapa nchini katika mawasiliano ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na intaneti yenye kasi.
..…………………………………………………………………………..............
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MAJALIWA AFUNGUA UKUMBI WA SACCOS YA MELI NNE ZANZIBAR NA KUZUNGUMZA

January 12, 2017

*Awataka viongozi kuwa wawazi
*Awashauri kuanzisha viwanda 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Melinne saccos kuhakikisha wanakuwa wawazi na kutoa taarifa za hesabu za umoja huo kila wakati ili wanachama waweze kuwa na takwimu sahihi. 
Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 11, 2017) wakati akizindua saccos hiyo yenye mtaji wa zaidi ya sh. bilioni moja kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinguzi Matukufu ya Zanzibar. 
Waziri Mkuu alisema viongozi hao wanatakiwa kuwa wawazi kwa wanachama wenzao jambo ambalo litawajengea uaminifu hivyo kuwezesha umoja huo kudumu na kufikia malengo yaliyokusudiwa. 
Alisema vyama vingi vya ushirika nchini vimekufa kutokana na viongozi wake kutokuwa waaminifu hivyo Serikali hatokubali kuona suala hilo linatokea katika umoja huo kwani litakwamisha maendeleo. 
Aidha, Waziri Mkuu aliwapongeza wananchi hao kwa kuanzisha saccos hiyo kwani wameweza kutimiza ndoto ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ya kuondokana na umasikini, dhuluma na unyonge. 
Waziri Mkuu alisema saccos hiyo itawawezesha baadhi ya wanachama kuanzisha miradi ya ujasiriamali na wengine kuongeza mitaji hivyo kukuza biashara zao na kuondokana na umasikini. 
Awali, Waziri Mkuu alizindua ukumbi wa kisasa wa mikutano unaomilikiwa na saccos hiyo na kuwapongeza wananchi hao kwa kubuni miradi ya maendeleo itayowaongezea kipato na kuweza kujikwamua kiuchumi. 
Hata hivyo aliwataka wanachama hao kuendeleza mshikamano wao na kuendelea kushirikiana na Serikali ambayo imejipanga kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo ya ujasiriamali hasa kwa walio katika vikundi vya uzalishaji. 
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwashauri wanachama wa umoja huo kufikiria uwezekano wa kuanzisha viwanda ili kukuza mitaji yao. Pia vitawezesha umoja kuongeza za fursa za ajira nchini. 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  Mama Asha Seif Idd kabla ya kufungua ukumbi wa SACCOS ya Melinne  mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  Mama Asha Seif Idd kabla ya kufungua ukumbi wa SACCOS ya Melinne  mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar 
 Waziri  Kassim Majaliwa , viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakimsikiliza  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd wakati  alipozungumza  baada ya Waziri Mkuu kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar
 Baadhi ya wananchama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua ukumbi wa SACCOS hiyo 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shamrashamra  za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar januari 11, 2017.   Kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd

MLIPUKO WA INJILI KUTOKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA

January 12, 2017
Ni mlipuko wa injili na habari njema takatifu kwa watu wote.
Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba, Ilemela Jijini Mwanza, chini ya Mchungaji na Mwinjilisti wa Kitaifa na Kimataifa, Dkt.Daniel Moses Kulola, linawakaribisha watu wote kwenye ibada zake.

Kila Jumapili ibada ya kwanza inaanza saa 12:00 asubuhi, ibada ya pili saa 1:00 kamili na ibada ya tatu ni saa 4:30 asubuhi huku ibada za katikati ya wiki zikifanyika jumatano na ijumaa kuanzia saa 10:00 alasiri.

Njoo ukutane na nguvu ya Mungu kutoka kwa wapakwa mafuta wa Bwana, wakiongozwa na Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola ambaye huduma zake zimefanyika Baraka katika mikoa mbalimbali nchini na hata nchi za nje ikiwemo Kenya, Rwanda, Burundi, DRC Congo, Zambia, Malawi, Dernimark, Sweden, Marekani na nyinginezo nyingi.

Njooni nyote wenye kujawa na misukosuko maishani ikiwemo kuteswa na majini, uchawi, kutozaa, maombezi ya kazi na biashara huku mkibarikiwa na kwaya mbalimbali ikiwemo Havila Gospel Singers, Revival Kwaya, New salvation na Hot spear choir bila kuwasahau waimbaji kama Sarah Emmanuel,  Aggness Akrama, Happy Shamawele,  Mitagato, Ndangeji, paschal, Allen, God's Reign, Samuel Daniel Kulola mzee wa Vocal bila kusahau huduma ya Kusifu na Kuabudu inayopigwa mubashara yaani #Live.

Kama hiyo haitoshi, Mahubiri, Mafundisho na Maombezi ya Mchungaji Daniel Moses Kulola yatakujia Mubashara kwa njia ya mtandao kupitia Facebook kila siku ya alhamisi kuanzia saa tisa kamili mchana kwenye ukurasa wake uitwao Daniel Moses Kulola.
Kwa msaada na ushauri wa kiroho, piga simu nambari 0767 74 90 40 na Mungu atakubariki.

COSATO CHUMI ATATUA TATIZO LA MASHUKA KATIKA ZAHANATI,VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI

January 12, 2017
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi mashuka kwenye moja ya Zahanati ilikuwa na upungufu wa mashuka katika kata ya Isalavanu wakati wa ziara yake ya kukagua na kugundua changamoto za zahanati za jimbo la mafinga mjini
 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi kushoto akiwa na katibu wake pamoja na mfanyakazi wa zahanati matanana wakati wa ziara yake
 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwasalimia wananchi wa kata ya Isalavanu wakati wa ziara yake