MWENYEKITI WA CCM, KIKWETE AOMBA WAZEE KUUNGA MKONO UONGOZI WA RAIS MAGUFULI

February 05, 2016
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akilakiwa na  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida leo, kaba ya kukutana na kuzungumza na wazee wa Singida Mjini. Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Mary Maziku.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisubiri kuvalishwa skafu baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida leo. Kushoto ni Mama Salma Kikwete. na Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Singida Mary Maziku na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
 Chipukizi wakimvalisha Skafu Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akienda katika Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, akiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete, Nape na Mary Maziku
 Kikwete akijadiliana jambo na Nape
 JK akiwasalimia wananchi
 JK akizungumza baada ya kupatiwa taarifa ya CCM Mkoa wa Singida. Kushoto ni Mary Maziku Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida
 Kina mama wakitumbuiza kwa ngoma kumlaki Kikwete Ofisi ya CCM mkoa wa Singida
 JK akisalimiana na mmoja wa wanachama wa CCM 
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akionyesha jengo lililokuwa Ofisi ya TANU mkoa wa Singida miaka ya 75 akiwa katibu msaidizi wa TANU wa wilaya


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipiga picha na mke wake Mama Salma Kikwete, leo, mbele ya nyumba ambamoishi  mjii Singida mwaka 1975, wakati huo akiwa katibu Msaidizi wa  TANU  wilaya ya Singida mjini. Kikwete yupo mkoani Singida kwa ajili ya kuongoza Maadhimisho ya Miaka 39 ya CCM, abayo kilele chake kitaifa ni kesho

 JK akisalimiana na wazee alipowasili kuzungumza nao mjini Singida leo

Na Richard Mwaikenda,Singida
MWENYEKITI  CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amewaomba wazee kote nchini, kumuunga mkono Rais John Magufuli katika uongozi wake ili kumpa
moyo wa  kuwatumikia Watanzania.

Alisema, kipindi ambacho Dk Magufuli ameingia madarakani hadi sasa ni mda mfupi, hivyo si vema kuanza kudodosa na kulaumu panapopwaya, badala yake Wazee na watanzania kwa jumla wazidi kumuunga mkono ili kumtia moyo wa kutekeleza  yote aliyokusudia kuyafanya kwa manufaa ya taifa.

Kikwete alitoa ombi hilo alipokuwa akizungumza katika mkutano na wazee wa Mkoa wa Singida, ambapo alisema kuwa kuongoza bila ushauri wa wazee nchi inaweza kuyumba.

"Kuongoza nchi bila wazee mambo hayaendi vizuri na  ukikosa mzee kwenye jahazi wapiga makasia vijana wanaweza kuanza kuzozana na chombo kwenda mrama, lakini wakiwepo wazee watawaongoza vizuri  na chombo/ nchi kwenda  salama". Alisema Kikwete huku akishangilia na wazee.

Si Kila mzee ni mwasisi wa chama, kila mwenye mvi na mwasisi, wengine wameingia kwenye chama wazee. 

Alisisitiza kwamba ukitaka nchi itulie kamata wazee, lakini ukiongoza nchi kwa kutumia vijana  pekee nchi inaweza kuyumba, na itafika mahali mtakosa mahali pa kushika. Alisema kuwa hata yeye kwa mara ya kwanza .alipokwenda kuomba ubunge jimboni kwake Bagamoyo, Pwani aliunda kamati ya wazee ambayo ilimsaidia sana.

Wazee ni sehemu ya matumaini ya chama na Serikali, panapokuwepo  wazee hapaharibiki jambo. "Nawashukuru sana wazee endeleeni kukijenga chama na kuiunga mkono Serikali inayoongozwa sasa na Dk John Magufuli." Alisisitiza Kikwete na kuongeza kuwa,

"Hata kwenye chama chetu tumeunda Baraza la Washauri la Wazee wasitaafu, ambapo wengi walipinga, hata hao wazee tuliowataka waunde baadhi yao walipinga, lakini mwisho walikubali kwa masharti kwamba wawe wanaitwa panapotokea jambo kubwa litakalohitaji ushauri wao."

Alisema mmoja wa viongozi aliyekuwa msitari wa mbele kuunda baraza hilo, alikuwa Rais msitaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye alitoa ushauri wa kuitwa kutoa ushauri panapotokea jambo kubwa na kwamba hata wakitoa ushauri, viongozi waliopo madarakani wawe hiari kuukubali au kuukataa'.

Aliwataka wazee kuendelea kuiunga mkono serikali ya sasa ambayo kwa hivi sasa imetimiza muda mfupi wa miezi mitatu ambaye ni sawa na mtoto mdogo anayekua.


Alisema kuwa Jambo kubwa ni kuwaunga mkono, kuliko kuwalaumu ama sivyo watavunjika moyo, ndani ya miaka mitano itakuwa hasara. watieni moyo ili wajiamini wahudumie vizuri zaidi ili nchi isonge mbele kimaendeleo.

Kikwete alisisitiza kuwa hata yeye akitakiwa kwenda kutoa ushauri atakwenda, na akiwa na jambo la kushauri atakwenda pia, lakini aliwaasa kuwa  si kila jambo wazee watake kwenda kutoa ushauri, itachelewesha mambo mengi.


JK akisalimiana na wazee alipowasili kwenye mkutano ambapo alizungumza na wazee wa mkoa wa Singida

 JK akiwasili katika mkutano na wazee wa Mkoa wa Sindida leo
 Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungmza kabla ya kumkaribisha Mke wa Mwenyekiti wa CCM, Salma Kikwete kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Singida
 Mama Salama Kikwete akizungumza katika mkutano huo
 Katibu wa Baraza la Wazee Mkoa wa Singida,Athuman Sima akisoma risala mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Singida, Juma Mudida akiapa mbele ya Jakaya Kikwete kuwa yupo tayari kupambana na mtu yeyote alatayepingana na utumbuaji wa majipu unaofanywa na Rais Magufuli
 Jakaya Kikwete akizungumza katika mkutano na wazee amabapo amewaomba kuunga mkono uongozi wa  Rais John Magufuli ili nchi isonge mbele kimaendeleo.
 JK akiagana na mmoja wa wazee baada kumaliza kuzungumza nao
 JK akiagana na wazee baada ya kumaliza mkutano


Baadhi ya wazee wakiondoka baada ya kuzungumza na JK mjini Singida leo

MWENYEKITI WA CCM, RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AZUNGUMZA NA WAZEE SINGIDA, AWATAKA WANZEE NCHINI KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

February 05, 2016

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akikaribishwa baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida leo, kaba ya kukutana na kuzungumza na wazee wa Singida Mjini. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisuniri kuvalishwa skafu baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida leo. Kushoto ni Mama Salma Kikwete. na Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Singida Mary Maziku na Katibu wa NEC Itukadi na Uenezi, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Kikwete akipokea salama za Chipukizi wa CCM
 Chipukizi wakieda kumvalisha skafu Mweyekiti wa CCM Kikwete
 Chipukizi wakimvalisha Skafu Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. Kulia ni Nape
 Kijana wa Chipukuizi akionyesha ukakamavu wake baada ya kumkaribisha Singida, Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akienda katika Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, akiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete, Nape na Mary Maziku
 Kikwete akiwasalimia wananchi waliokuwepo nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Singida
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipanda ngazi kuingia Ofisi ya Mwenyekiti wa CCM mkoawa Singida
 Jk akiigia ukumbini
 Jk akisaaini vitabu vya  wageni
 Mama Salma Kikwete akisaini vitabu vya wageni
SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU UDHALILISHWAJI ALIYOFANYIWA MTANZANIA  NCHINI INDIA

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU UDHALILISHWAJI ALIYOFANYIWA MTANZANIA NCHINI INDIA

February 05, 2016

Serikali imetoa tamko la kulaani kitendo kilichotokea nchini India kwa mwanafunzi wa kike wa kitanzania kuvuliwa nguo na kutembezwa barabarani ambapo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na kimataifa imetoa tamko la kulaani suala hilo kwa kuitaka Serikali ya india kuchukua hatua.
Akitoa tamko hilo Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema ni kweli kwamba kuna mwanafunzi wa kike wa kitanzania alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji nchini India kwa kuvuliwa nguo na kutembezwa barabarani suala ambalo lilizua mijadala mikubwa nchini kuhusu udhalilishaji huo.
“Wizara yetu imezungumza na Balozi wa India nchini na kumweleza ni kwa jinsi gani watanzania wamefadhaika na kusononeshwa na kitendo alichofanyiwa mtanzania mwenzao huko India na Balozi alituhakikishia kwamba amewasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi yake na kusema Serikali ya India kwa kushirikiana na Jeshi la polisi nchini humo wamefanikisha kuwakamata wote waliohusika na kitendo hicho na kuwafikisha mahakamani kujibu mashataka hayo”
“Pia Serikali ya India imeahidi kutoa ulinzi kwa wanafunzi wa kitanzania na wenye asilia ya Afrika  wanaosoma huko ili kuwalinda na kuwaepusha na vitendo hivyo vinavyofanya na raia ambao hawana nia njema kwa mahusiano mazuri ya kimataifa yaliyopo kati ya India na Tanzania”Alisema Mhe. Mahiga.
Serikali ya Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na Serikali ya India kwa miaka mingi sasa na kutokana na kitendo hiki kilichotokea nchini India,Waziri wa Mambo ya Nje ya India amefatana na Balozi wa Tanzania nchini humo kwenda Mji wa Bangalo ili kuongea na wanafunzi wakitanzania na wale wenye asili ya Afrika wanaosoma huko ili kujenga mahusiano mazuri na wazawa ikiwa ni jitihada za kupunguza vitendo hivyo kutokea mara kwa mara.
Imendaliwa na Raymond Mushumbusi – MAELEZO
SERIKALI YATENGA BILIONI 60 KUFUFUA GENERAL TYRE ARUSHA.

SERIKALI YATENGA BILIONI 60 KUFUFUA GENERAL TYRE ARUSHA.

February 05, 2016




Shillingi Billioni 60 zinategemea kutumika kufufua kiwanda ya matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha ambacho kimesharudi mikononi mwa Serikali, na fedha hizo zitatumila kurekebisha mitambo ya umeme ya kiwanda hicho na kupata mitambo mipya itakayoendana na teknolojia ya utengenezaji wa matairi duniani.

Akijibu swali la Mhe. Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) lililouliza ni lini serikali itafufua kiwanda cha matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha kwani ni tegemeo kwa ajira kwa wananchi wa Jijini la Arusha,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles John Mwijage amesema kiwanda hicho kimesharudi mikononi mwa Serikali na wako mbioni kukifufua ili kianze kufanya kazi ya kuzalisha matairi nchini.

“Tumeanzisha viwanda nchi ili kuzalisha bidhaa na kutoa ajira kwa watanzania na sio kuwatesa wananchi kwa kukosa ajira au kuagiza bidhaa ambazo tunaweza kuzalisha hapa hapa nchini, hivyo basi Serikali kupitia Wizara yangu tutatenga fedha kwa ajili ya kufufua kiwanda hiki ili kianze kufanya kazi mara moja”

“Sio tu tutafufua kiwanda cha General Tyres pekee bali tunafatilia viwanda vyote ambavyo vimekiuka sheria na kanuni kwa kutoviendeleza viwanda hivyo ili kuvirudisha mikononi mwa Serikali au kuwatafuta wawekezaji wengine watakaoweza kuviendesha viwanda hivyo” Alisema Mhe. Mwijage.

Aidha Mhe. Charles  John Mwijage amesema ni kweli makampuni mengi yaliyobinafsishwa hayakufanya vizuri katika uendeshaji wake ukiacha mifano ya makampuni machache yanayofanya vizuri yakiwemo Tanzania Breweries Limited (TBL),Morogoro Polyester 21st Century na Tanzania Cigarette Company Limited (TCC), hivyo Wizara yangu ikishirikiana na Msajili wa Hazina juu ya Viwanda ilifanya tathmini iliyoonesha kuwa mashirika mengi yaliyobinafsishwa hawakutekeleza mikataba ya mauziano kikamilifu.

Ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha makampuni yote haya yanazalisha kwa tija ili tupate bidhaa,kodi ya Serikali na ajira kwa wananchi wa Tanzania ili kutimiza adhma ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ya kuwa na Tanzania yenye viwanda kwa maendeleo ya taifa.

Serikali kupitia Wizara yetu inaboresha mazingira ya uwekezaji hali itakayowajengea imani kwa wawekezaji na kupelekea kupanua zaidi shughuli zao za kibiashara na pia kuendeleza mpango wa Viwanda vidogo na vya kati unaoshirikisha SIDO na Halmashauri za Wilaya na Mikoa ili kuanzisha Viwanda vya Mkoa vya kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo,Uvuvi na ufugaji kupitia njia hii ajira nyingi zitaongezeka na kupunguza tatizo la ajira nchini.

Imeandaliwa na Raymond Mushumbusi – MAELEZO

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWATEMBELEA WAHADZABE NA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA JAMII HIYO

February 05, 2016


Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukikatisha misitu na mabonde wakati ukielekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa ambako jamii hiyo inaishi. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia Sola zinazosukuma maji kwenye kisima cha mradi wa maji yanayotumika kwenye kijiji pamoja na shule ya msingi ya Munguli iliyopo wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya mradi wa maji wa kijiji cha Munguli kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ndani ya hosteli ya shule ya msingi Munguli ambayo wanasoma watoto wa Kihadzabe.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakulima wakati akiwa njiani kuelekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakulima wakati akiwa njiani kuelekea kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribishwa kijiji cha Kibampa na wakazi wa hapo amabao ni Wahadzabe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akifurahia jambo na kijana wa kabila la Kihadzabe 
   Wahadzabe wakiwa kwenye kikao maalum kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakishiriki kupanda mihogo kwenye shamba ya la Wahadzabe kwenye kijiji cha Kibampa wilaya ya Mkalama.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai akimuelekeza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana namna Wahadzabe wanavyosaga mtama kwa kutumia jiwe. 

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo ameweka historia ya kuwa kiongozi wa nne mkubwa wa Kitaifa kufika kwenye kijiji cha Munguli na Kibampa ambavyo wanaishi jamii ya Wahadzabe .Kijiji cha Munguli kilitembelewa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere, akifuatiwa na aliyekuwa Makamu wake Abdu Jumbe na Mama Sofia Kawawa.

Jamii ya Wahadzabe inaishi kwa kutegemea uwindaji,kula matunda ya porini,mizizi ,wadudu na miti hata hivyo juhudi kubwa zimefanyika kuanza kuwafundisha kilimo, kuwapeleka watoto shule ,zaidi ya Wahadzabe  305 wanasoma kwenye shule ya msingi Munguli, pamoja na vijana zaidi ya 50 kupelekwa kujiunga na JKT.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone kwa jitihada zake za kuwasaidia jamii ya Wahadzabe ikiwa pamoja na kuhakikisha wanapata elimu, wanajifunza kilimo lakini pia uamuzi wa kupima maeneo ya Wahadzabe ili wamiliki ardhi yao wenyewe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiwa kwenye nyumba maalum ya chifu wa wahadzabe pamoja na Mwenyekiti wa Wahadzabe Edward Mashimba na Mama Sarah Philipo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakitoka kwenye nyumba ya Chifu wa Wahadzabe iliyopo kijiji cha Kibampa kata ya Mwangeza wilaya ya Mkalama mkoani Singida
 wakazi wa kijiji cha Kibampa ambaco wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba (kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kibampa ambako wakazi wake ni jamii ndogo yenye kaya 300 ya Wahadzabe,kushoto ni Mwenyekiti wa Wahadzabe Ndugu Edward Mashimba (kushoto) ambaye alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kihadzabe