DTB YAUAGA MWAKA KWA STYLE YA KIPEKEE

January 25, 2016



Wafanyakazi wa Tawi la Benki ya DTB Makao Makuu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya tawi lao kupata tuzo ya Tawi Bora Tanzania 2015 kati ya matawi 24 ya benki hiyo ambapo 10 yapo Dar es Salaam na 14 mikoani. Meneja wa Tawi hilo, Shahista Karim (katikati) akiwa ameshikilia tuzo hiyo aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu (hayupo pichani) katika sherehe za kufunga mwaka zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Ledger Plaza ulioko Bahari Beach.




PITON CHINI: Wanawake wa benki ya DTB wakicheza muziki wa asili katika sherehe za kuaga mwaka katika usiku uliokuwa na kauli mbiu ya ‘Usiku wa Afrika’. Sherehe hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Ledger Plaza ulioko katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Kati ya mambo ambayo sherehe hiyo ilisherehekea ni pamoja na kutambua mafanikio benki hiyo ilipata katika mwaka 2015. Kati ya matawi yote 24 nchini, Tawi la Masaki na lile la Makao makuu yaliibuka washindi na kujizotea tuzo. DTB ina matawi 10 Jijini Dar es Salaam na 14 mikoani.




Buddha ya washiriki wakipakua chakula katika ghafla hiyo







Dance ilisakatwa chapati maelezo, JUU na CHINI baadhi ya wafanyakazi wa DTB kutoka katika matawi mbalimbali ya Benki hiyo wakiwajibika ipasavyo




KWA HISANI YA IMMA MATUKIO

“WATANZANIA WAASWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII”

January 25, 2016



.
WATANZANIA wameshauriwa kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii iliyopo hapa nchini iili kuweza kupunguza ukali wa maisha kwani itawasaidia kuepukana na gharama za matibabu ambazo zitakuwa zikilipwa na mifuko husika wakati wanapokumbana na majanga mbalimbali.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Afisa Mwandamizi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Usimamizi na Uzibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA),Amina Ally wakati wa semina ya kuhamasisha maafisa wa mageraza mkoani Tanga kuhusu umuhimu wa kujiunga na mifuko ya Hifadhi ya Jamii.


Alisema kuwa mifuko hiyo ina manufaa makubwa pamoja na kupunguza ukali wa maisha kwa watumishi wa kada mbalimbali na kulinda maslahi yao yakiwemo mahitaji ya kijamii ili kuweza kuondokana na gharama za matibabu wanapokuwa wakiugua na majanga mengine.

Aidha licha ya hivyo mifuko hiyo imekuwa na faida kubwa kwenye nchi katika uwekezaji inawafanya wanachama wa mifuko husika kupata unafuu katika upatikanaji wa masuala yote ya msingi wakati panapokuwa pamejitokeza mambo ya dharura na kwamba hukabiliana nayo bila kujali hali ya kipato au michango ya muhusika.

   “Ukiangali mifuko hii ya hifadhi ya Jamii imekuwa mkombozi mkubwa sana kwa jamii lakini pia inasaidia kuweza kukabiliana na ugumu wa maisha uliopo sambamba na kupunguza umaskini kwa watanzania waliojiunga nayo kwenye kunufaika na mambo mbalimbali ikiwemo huduma za matibabu “Alisema Amina.

Hata hivyo alitaja mifuko ambayo alidaia kuwa ndio kimbilio kubwa la watanzania walio wengi hapa nchini kuwa ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF),Mfuko wa Pensheni wa (PPF),Mfuko wa Pensheni wa Wafanyakazi wa Serikali (GEPF),Mfuko wa Pensheni wa (LAPF) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF).

Alisema kuwa licha ya kupatikana mafanikio kwenye mifuko lakini zipo changamoto ambazo zinawakabili ikiwemo wafanyakazi wa sekta zisizokuwa rasmi kushindwa kujiunga kwenye Mifuko ya Hifadhi za Jamii hivyo aliwashauri washiriki wa semina hiyo kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri kuielimisha jamii namna wanavyoweza kujiunga nayo ili waweze kunufaika.

WAZAZI MKOANI MWANZA WASIKITIKA ELIMU BURE KUWABAGUA WANAFUNZI WA ELIMU YA WATU WAZIMA

January 25, 2016
Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wanaosoma kitengo cha elimu ya Watu Wazima katika Shule ya Sekondari Pasiansi iliyopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameiomba Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi hao ili nao waweze kunufaika na mpango wa elimu bure nchini.

Wazazi hao wametoa ombi hilo hii leo baada ya kumalizika kwa kikao baina yao na uongozi wa Shule hiyo pamoja na Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza, sanjari na viongozi wengine akiwemo diwani wa Kata ya Pasiansi pamoja na Afisa elimu Sekondani katika Manispaa ya Ilemela.

Malalamiko yao yanafafanua kwamba, hawakuambiwa tangu awali kuwa watoto wao wanasoma elimu ya Watu Wazima, malalamiko ambayo hata hiyo yamekanushwa na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Joseph Bangirana.

Awali wazazi hao walisema kuwa hawako tayari kulipa ada kwa ajili ya watoto wao wanaosoma katika shule hiyo, jambo lililomlazimu Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza kueleza bayana kwamba, wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima hawanufaiki na mpango wa elimu bure nchini kwa kuwa Serikali haitoi ruzuku kwa ajili yao.

Ufafanuzi huo ukaungwa mkono na Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela.

Wakati ufafanuzi huo ukitolewa, mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ya Pasiansi akasisitiza suala la wao kuondolewa ada ili nao wanufaike na mpango wa elimu bure.

Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima katika shule ya Sekondari Pasiansi, kilianzishwa Mwaka 2014 na kuanza kupokea wanafunzi waliomaliza darasa la Saba waliokuwa na ufaulu wa chini ya Wastani wa pinti 100 kwa lengo la kuwapa fursa ya kupata elimu ya Sekondari ambapo mbali na michango mingine, wanafunzi hao wanalipa ada ya Shilingi Laki Moja na Elimu Hamsini kwa mwaka.
Kikao Kikiendelea
Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwa Wazazi juu ya suala la Elimu Bure nchini.
Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza
Andrea Swai kutoka Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Mwalimu Joseph Bangirana ambae ni Mkuu wa Shule Pasiansi Sekondari akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Diwani wa Kata ya Pasiansi Mhe.Japhesi Joel Rwehumbiza akitoa ufafanuzi wake. Amewapongeza wazazi kwa kufuatilia masuala ya elimu yanayowahusu
Mdau wa Elimu Mkoani Mwanza, Peter Matonyi akitoa mchango wake juu ya suala la elimu bure kwa wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mwenyekiti wa Mtaa wa Pasiansi Mkoani Mwanza, Emmanuel Masuka akifafanua jambo
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Wanalalamikia suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Kutoka Pasiansi Sekondari Jijini Mwanza, Mimi ni Mzee wa Karanga fotoooooooo, GB Pazzo wa Binagi Media Group

RAIS DK. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA VITAMBULISHO VYA TAIFA, DICKSON MAIMU

January 25, 2016

Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu (pichani) kuanzia leo.

Aidha, baada ya utenguzi  huo, Maimu amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao. Mkurugenzi wa Tehama, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.

 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

RAIS DK. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA VITAMBULISHO VYA TAIFA, DICKSON MAIMU

January 25, 2016

Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu (pichani) kuanzia leo.

Aidha, baada ya utenguzi  huo, Maimu amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao. Mkurugenzi wa Tehama, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.

 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

DC KAWAWA ATEMBELEA MRADI WA MAJI

January 25, 2016
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa akisukuma pampu ya maji katika moja ya visima vinavyojengwa na mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya wakazi wa kata ya Mwendakulima, wengine ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo (aliyeinama)  akijiandaa kukinga maji hayo kwa mikono. Aliyesimama kulia kwa DC Kawawa ni Meneja wa Uendelezaji wa mgodi wa Buzwagi, George Mkanza.


Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa akinywa maji katika moja ya visima vilivyochimbwa na Mgodi wa Buzwagi katika kata ya Mwendakulima ambapo mgodi huo unampango wa kutekeleza miradi kumi na tano ya ujenzi wa visima virefu vya bomba, wanaoshuhudia ni Meneja Uendelezaji wa Mgodi George Mkanza (wa kwanza kushoto) na Diwani wa kata ya Mwendakulima

TBS YATEKETEZA BIDHAA ZA MAREKANI,CHINA

January 25, 2016
 Katapila likizikanyagakanyaga kwa lengo la kuziharibu bidhaa mbalimbali zikiwemo pampasi na dawa za meno zilizopitwa na wakati na zingine zisizo na ubora katika Dampo la Pugu Kinyamwezi, Dar es Salaam.  Bidhaa hizo zenye thamani ya sh. mil. 20, kutoka Marekani na China zilikamatwa  na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. (PICHA ZOTE  NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)




Na Charity James

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeteketeza bidhaa hafifu na zilizokwisha muda wake zenye thamani ya sh. milioni 20 kutoka nchini Marekani na China.

Akizungumza wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo,Dar es Salaam jana, Ofisa habari wa TBS, Roida Andusamile alizitaja bidhaa hizo kuwa ni dawa za meno, pampas, sabuni za kuogea na wipes.

Alisema miongoni mwa bidhaa hizo zilikuwa ni kwaajili ya kutoa msaada katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara huku nyingine zikiingizwa kwaajili ya biashara.

"Kazi ya kuteketeza bidhaa zenye ubora hafifu ni endelevu lengo letu ni kuhakikisha tunaepusha madhara kwa watumiaji ambao wanashindwa kutambua bidhaa hafifu," alisema.

Alisema bidhaa zote zinazoingia nchini ziwe za biashara au misaada ni lazima zipimwe kwa lengo la kuondoa changamoto ya kuwauzia au kugawa zikiwa ni hafifu au kuisha muda wake.

Kwa upande wake, Ofisa Mdhibiti Ubora wa TBS, Salome Emmanuel alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuakikisha wanaingiza bidhaa zenye ubora na kuongeza wafanyabiashara ndio walinzi tosha wa kuhakikisha bidhaa hafifu haziingizwi nchini hivyo ni vizuri wakafuata sheria kukwepa tatizo hilo.





KUMEKUCHA DODOMA HAPA KAZI TU HALF MARATHON.

January 25, 2016
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akiwa na Mwe3nye3kiti wa Chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro,( KAA) Liston Methacha wakati wa uzinduzi rasmi wa mbio za Dodoma Hapa Kazi tu Half Marathoni 2016 zinzotarajia kufanyika January 30 mwaka huu mjini Dodoma.
Baadhi ya wadau wa Riadha wakifuatiia mkutano wa uzinduzi wa Mbio za Dodoma Hapa kazi tu Half Marathon 2016 uliofanyika katika Hotel ya Nyumbani mjini Moshi.
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza na wanahabari (hawako pichani ) wakati wa uzinduzi rasmi wa Mbio hizo.
Kocha wa timu ya taifa ya Riadha ,Francis John akiwa na wanariadha ,Alphonce Felix na Said Makula waliofuzu viwango vya kushiriki mashindano ya Olyipiki ,walipotamburishwa mbele ya wanahabari .
Raisi wa RT ,Mtaka kifanya mahojiano na Mwandishi wa habari ,Enos Masanja wa Azam TV.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania(RT) limeandaa mbio fupi kwa ajili ya kuhitimisha siku 100 za rais Dk.John Pombe Magufuli kuwa Ikulu zitakazotimua vumbi jumamosi hii januari 30 mwaka  huu mjini Dodoma.

Mbio hizo zimepewa jina maalumu la Dodoma ‘hapa kazi tu’ Half Marathon ambazo zitashirikisha washiriki mbali  mbali wakiwamo waheshimiwa wabunge,mawaziri,wanafunzi,walemavu na wanariadha wakongwe nchini.

Akizindua mbio hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki zinazodhaminiwa na Kampuni ya JSM,Rais wa shirikisho hilo,Anthony Mtaka alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa mbio hizo ambazo zimeandaliwa na kuendeshwa na shirikisho hilo ni kufufua michezo hapa nchini.

Pia alisema mbio hizo zitatumika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kutimiza siku 100 tangu aingie maradakani ambazo zitakuwa februari 14 mwaka huu.

Kwa mujibu wa rais huyo wa RT,mbio hizo zimegawanywa katika makundi matatu ambako mbio za kwanza ni za kilomita 2.5 ambazo zitashirikisha wabunge,mawaziri,walemavu,wanafunzi ,wazee na watu mbalimbali.

Mbio za kilomita 5 ambazo ni za kujifurahisha zitashirikisha wakimbiaji wote na mbio za nusu marathon ambazo zitakuwa ni mbio za ushindani washindi watapata zawadi .

Akitangaza zawadi  kwa washindi,Mtaka alisema mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaumme na 
wanawake atapata zawadi  ya piki piki yenye thamani ya sh,Milioni 2.8,mshindi wa pili akipata bati 100,wa tatu bati 40,mshindi wa nne akipata sh,200,000 huku mshindi wa tano akiondoka nash,100,000.
Mshindi wa sita hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha sh,50,000 kila mmoja huku waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa  ndiye atayakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mbio hizo na atashiriki  mbio za kilomita 2.5.

Wanafunzi waatakaopenda kushiriki mbio hizo watasajiliwa kwa sh,500,huku vwasio wanafunzi wakisajiliwa kwa sh,1,000 na wingine ambao hawakutajwa ni kundi gani wakisajiliwa kwa sh,5,000 na fedha hizo kwa mujibu wa Mtaka zitasaidia kambi ya wanariadha watakaoshiriki michuano ya Olimpiki.

Uzinduzi huo pia ulitumika kuwatambulisha wanariadha wawili ambao wamekidhi vigezo vya kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mapema mwezi Agosti mwaka huu  ambako nchi zaidi ya 216  kutoka kila kona ya dunia zitashiriki.

Wanariadha hao ni Alphonce Felix ambaye ana wastani wa muda wa kukimbia wa saa 2:12.01 na Said Makula ambaye muda wake wa kukimbia ni saa 2:13.27 na watatumia mbio hizo mjini Dodoma kama majaribio yao ya kitaifa kati ya majaribio sita ya kitaifa kabla ya kwenda Brazil.

Julai 6 mwaka jana,Felix alishiriki mbio za Gold Coast Marathon nchini Australia na kumaliza nafasi ya sita huku Makula akishiriki mbio za Casablanca Marathon oktoba 25 mwaka jana  na kumaliza katika nafasi ya nne.