Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi ya Tigo imeingia mtaani kwa kishindo na kutoa simu za Samsung S8 zenye ofa ya mwaka mzima

July 04, 2017
Meneja Chapa wa Tigo Tanzania, William Mpinga, akizungumza na wakazi wa Tegeta Nyuki, Dar es Salaam, wakati wa kampeni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi iliyofanyika katika viwanja vya stendi ya eneo hilo ambapo wateja wa tigo walizawadiwa zawadi mbalimbali, ikiwamo simu aina ya Samsung S8 yenye thamani ya Sh milioni 1,900,000


Balozi wa Tigo Jaza Ujazwe, Lukas Mwavile ‘Joti’, akiwaburudisha wakazi wa Tegeta Nyuki, wakati wa kampeni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi iliyofanyika katika viwanja vya stendi ya eneo hilo ambapo wateja wa tigo walizawadiwa zawadi mbalimbali, ikiwamo simu aina ya Samsung S8 yenye thamani ya Sh milioni 1,900,000.
Balozi wa Tigo Jaza Ujazwe, Lukas Mwavile ‘Joti’, akiwaburudisha wakazi wa Tegeta Nyuki, wakati wa kampeni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi iliyofanyika katika viwanja vya stendi ya eneo hilo ambapo wateja wa tigo walizawadiwa zawadi mbalimbali, ikiwamo simu aina ya Samsung S8 yenye thamani ya Sh milioni 1,900,000.

Balozi wa Tigo Jaza Ujazwe, Lukas Mwavile ‘Joti’, akionyesha umahiri wake wa kupiga debe katika moja ya daladala zinazofanya safari zake Tegeta Nyuki Wazo, wakati wa kampeni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi iliyofanyika katika viwanja vya stendi ya eneo la hilo ambapo wateja wa tigo walizawadiwa zawadi mbalimbali, ikiwamo simu aina ya Samsung S8 yenye thamani ya Sh milioni 1,900,000

ZIMEBAKI SIKU 10 KUFANYIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHUKRANI NI JULAI 15 UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

July 04, 2017
Dr. Mengi ataka wasambazaji kushawishi uwekezaji

Dr. Mengi ataka wasambazaji kushawishi uwekezaji

July 04, 2017
Makampuni ya Tanzania ya uwakala wa usambazaji wa bidhaa za kutoka nje ya nchi, wameshauriwa kuyashawishi makampuni ya nje kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa hapa hapa nchini. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam wakati akitembelea mabanda ya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kutaka kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akielekea kukagua baadhi ya matrekta katika banda la Kampuni ya Agricom akiambatana na Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda (kulia kwa Dr.Mengi) alipotembelea kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.[/caption] Akifuatana na Mkurugenzi wa TPSF Bw. Louis Accaro, Afisa Biashara wa Tan-Trade Bw. Mohamed Mkadara, na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wajasiriamali Bi. Jacquiline Maleko, Dr Mengi ametembelea mabanda mbalimbali, yakiwemo yaliyopo chini ya mwamvuli wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda, na Kilimo – TCCIA, Mfuko wa Fursa sawa kwa wote-EOTF, na Banda la Kampuni ya Agricom, ambayo Mkurugenzi wake Mtendaji Bi. Angelina Ngalula alielezea jinsi ilivyojipanga kusambaza zana za kisasa za kilimo ili kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji. Katika majumuisho yake Dr Mengi alishauri Tan-Trade na TPSF washirikiane katika kuangalia namna ya kuboresha zaidi maonyesho hayo, hususan katika kuboresha mabanda ya maonyesho ili yalingane na hadhi halisi ya kimataifa. Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda (kushoto) akitoa maelezo kuhusu ubora wa matrekta hayo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kushoto) alipotembelea kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom, Bi. Angelina Ngalula (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi alipotembelea banda la kampuni hiyo kujionea huduma zao kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mratibu wa miradi na mshauri wa Maisha Finance Ltd, ambao ni wakopeshaji wa zana zote za kilimo yakiwemo Matrekta ya kampuni ya Agricom, Erasmus Erneus akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wateja, Apollos Rweikiza aliyetembelea banda la Agricom katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko (wa pili kushoto) alipowasili kwenye banda la TWCC yanakoendelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Fedha, Masoko na Usafirishaji wa C.E Holdings Ltd, wauzaji wa vito vya Afrika, Maria Pagama akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi alipotembelea banda la TWCC kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akifurahia jambo na wanawake wafanyabiashara kwenye banda la TWCC katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha ya juu kulia ni Noreed Mawalla wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC). Mkurugenzi wa Tanfood and Spice Co. Investment watengenezaji wa bidhaa za kutunza ngozi zinazotokana na mimea, Bi. Rona akitoa maelezo ya bidhaa halisi za kutunza ngozi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi alipotembelea banda la TWCC kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitoa maelekezo kwa Noreed Mawalla wa TWCC (katikati) wakati akitembelea banda la Chama cha wafanyabiashara wanawake kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitazama bidhaa mbalimbali katika banda la Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) lililopo katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimuongoza Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi mara baada ya kuwasili katika banda la EOTF kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Joane Art Craft, Culture & Desigin, Bi. Joane Baigana (kulia) alipotembelea banda la EOTF kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitazama kazi mbalimbali za wakinamama wajasiriamali kwenye banda la EOTF katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akisalimiana na wanawake wajasiriamali wanaofadhiliwa na EOTF akiendelea kutembelea wajasiriamali katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Anayemuongoza ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akisaini kitabu cha wageni katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu lililopo ndani ya banda la EOTF yanakoendelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitazama moja ya vitabu katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu lililopo ndani ya banda la EOTF. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akipata maelezo ya huduma mbalimbali za mikopo riba nafuu kwa wanawake kutoka kwa Afisa Huduma kwa Wateja wa Tanzania Women's Bank, Renita Michael (kulia) ndani banda la EOTF wakati alipotembelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa na Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko. 
WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA NA MATUKIO BUNGENI MJINI DODOMA

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA NA MATUKIO BUNGENI MJINI DODOMA

July 04, 2017
kia1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungungumza na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni, 4, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kia2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 4, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kia3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
kia4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mufindi Kusini, Medard Kigola kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu
kia5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Faida Bakari kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kia6
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Msalala, Ezekiel  Maige (kulia) na Mbunge wa Bukene,  Selemani Zedi kwenye Jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Julai 4, 2017. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kia7
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge, Abdallah Ulega wa Mkuranga  (kushoto) na Stephen Masele kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kia8
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS SUDAN KUSINI

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS SUDAN KUSINI

July 04, 2017
unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudani Kusini Mhe. Jenerali Taban Deng Gai ambapo mazungumzo yao yalihusu kuendelea kudumisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili.
1
Mazungumzo hayo yamefanyika wakati mkutano wa 29 wa wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Afrika, jijini Addis Ababa ukihitimishwa.
2 3
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

UAMUZI WA KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI TFF

July 04, 2017
Kamati ya Utendaji (EXCOMM) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imekutana tena leo Jumanne Julai 4, 2017 katika kikao cha dharura ambako ilijadili mgawanyiko katika Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Kamati hiyo ya utendaji inakutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) ya Katiba ya TFF inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6). Kikao cha Kamati hiyo kilianza saa 8.58 alasiri hadi saa 10.51 jioni.

Katika kikao chake kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za shirikisho, Karume jijini Dar es Salaam Kamati iliamua kufanya mabadiliko madogo katika Kamati zake za Kisheria na Kamati za uchaguzi kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 44 (7) na Ibara ya 52 inayotoa mamlaka ya kufanya mabaduiliko hayo.

Katika Kamati ya Uchaguzi, EXCOMM imeteua Mawakili kuongoza kamati hiyo wakiongozwa na Msomi Wakili Revocatus Kuuli; Mheshimiwa Wakili Mohammed Mchengelwa; Msomi Wakili Malangwe Mchungahela; Msomi Wakili Kiomoni Kibamba na Msomi Wakili Thadeus Karua.

Katika Kamati ya Rufaa Uchaguzi, EXCOMM imeteua Msomi Wakili, Abdi Kagomba kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Kenneth Mwenda na wajumbe ni Msomi Wakili  Rashid Sadalla, Mhe. Jabir Shekimweri na Mohammed Gombati.

Kadhalika katika kamati za kisheria za TFF, ikianzia Kamati ya Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Hamidu Mbwezeleni kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Msomi Wakili Steven Zangira na wajumbe ni Mhe. Glorius Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.

Kamati ya Rufaa na Maadili, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Ebenezer Mshana kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Naibu Kamisha katika Jeshi la Polisi (DCP), Mohammed Mpinga na Wajumbe ni Msomi Wakili Benjamin Karume; Dk. Lisobine Kisongo na Mrakibu Msaidizi wa Polisi - ASP Benedict Nyagabona.

Kamati ya Nidhamu ya TFF, EXCOMM imeteua Tarimba Abbas kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Peter Hella huku Wajumbe wakiwa ni Boniface Lyamwike, Dk. Billy Haonga na Kassim Dau.

Kamati ya Rufaa ya Nidhamu, EXCOMM imeteua Msomi Wakili Rahim Shaban kuwa Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Siza Chenja huku Wajumbe wakiwa ni Abbas Mtemvu; Amani Mulika, Amin Bakhressa na Stella Mwakingwe.

TEHAMA yaongeza ufanisi a kazi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC)

July 04, 2017
Je unajua jinsi TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Usikose kuangalia kipindi hiki

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MRADI MKUBWA WA MAJI SENGEREMA MKOANI MWANZA

July 04, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine  akifungua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wa Sengereza kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 33 ya awali.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi huo mkubwa wa maji kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Antony Sanga wakati alipoanza ukaguzi wa mradi huo kabla ya kuufungua.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Maji   Eng. Gerson Lwenge wakati akielekea kukagua mradi wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wa Sengereza kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 33 ya awali.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kufungua mradi huo wa maji Wilayani Sengerema.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimongeza Mwanachama mpya wa CCM ambaye alikuwa Kada maarufu wa CHADEMA kanda ya Ziwa Hamis Tabasamu mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo, Sengerema mkoani Mwanza.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na waandishi wa habari  mbalimbali wa mkoani Mwanza ambao walishiriki katika kazi ya ufunguzi wa mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo, Sengerema mkoani Mwanza.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya amani ya Mkoa wa Mwanza Sheikh Hassan Kabeke mara baada ya kufungua mradi huo wa maji.

Mkurugenzi Taasisi ya Doris Mollel Azinduwa Duka la Kadi

July 04, 2017

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la Kampuni ya Plus Events Cards, Mwenge Sokoni wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses na Mkurugenzi Mkuu, Raimond Njuu (kushoto) wakishuhudia.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Plus Events Cards, Raimond Njuu (kushoto) mara baada ya kuzindua tawi jipya la Kampuni ya Plus Events Cards, Mwenge Sokoni wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses akishuhudia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses (kushoto) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (kulia) sehemu ya bidhaa zinazouzwa na duka hilo mara baada ya kuzinduliwa. Kampuni ya Plus Events Cards, wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja imezinduwa tawi jipya Mwenge Sokoni jijini Dar es Salaam.

Hapa ikikatwa keki ya pongezi na viongozi wa Kampuni ya Plus Events Cards.

Picha ya pamoja ya wageni waalikwa baada ya uzinduzi

Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Bi. Doris Mollel amezinduwa tawi jipya la duka la kadi la Kampuni ya 'Plus Events Cards' Mwenge, Sokoni Jijini Dar es Salaam huku akiwataka wajasiliamali wadogo na wakubwa wauzaji wa bidhaa hizo kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo ili wajipatie kipato. Bi. Mollel ametoa kauli hiyo alipokuwa akizinduwa tawi hilo, linalofunguliwa kusogeza huduma za uuzaji kadi za kisasa jumla na rejareja kwa wananchi eneo hilo.
Pamoja na hayo, Bi. Doris Mollel aliwashauri wananchi kupenda kununua bidhaa halisi na kuachana na bidhaa feki kwani zimekuwa na madhara huku zikilikoseshea taifa mapato. Alisema bidhaa nyingi feki haziingii kwa utaratibu rasmi nchini hivyo licha ya madhara kwa watumiaji zimekuwa zikilikosesha taifa mapato.
"...Nashauri Watanzania wenzangu tupende kununua bidhaa halisi zinazoendana na thamani ya fedha tunazotoa. Uzuri sasa hivi wauzaji wengine wamekuwa wawazi wanakwambia hii ni bei rahisi kwa kuwa ni feki na hii ndio bidhaa halisi...tujenge utamaduni wa kutumia bidhaa bora na halisi kwa manufaa yetu na taifa," alisisitiza Bi. Doris Mollel.
Aidha aliipongeza kampuni ya Plus Events Cards wauzaji wa kadi na maua ya maharusi kwa kusogeza huduma zake eneo la Mwenge na kutoa fursa kwa wajasiriamali kuwatembelea kwa ajili ya kusambaza bidhaa hizo Dar es Salaam na hata mikoani. Aliongeza kuwa hatua hiyo si tu imesogeza huduma kwa wahitaji bali imetoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata bidhaa za kadi kirahisi na kuzisambaza kwa wahitaji.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Plus Events Cards mara baada ya uzinduzi. Wa kwanza kushoto na kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa duka hilo tawi la Mwenge Sokoni.