NHIF YAWAPIGA MSASA WAKOREA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

November 11, 2015

 Mkurugenzi wa Mfuko wa bima ya Afya ya Jamii (CHF) Eugen Mikongoti, akizungumza na Wadau wa Maendeleo ya Mfuko wa  Kimataifa wa Afya wa Korea kuhusiana na utekelezaji wa  mifumo ya habari na mawasiliano ya uzalishaji na ufuatiliaji wa madai ya watoa huduma za afya kwa wanachama katika mkutano  uliofanyika leo ndani ya Hoteli ya Blue Pearl  Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Mifumo ya Habari wa (NHIF)   Ali Othman akitoa mada katika Mfuko wa  Kimataifa wa Afya wa Korea kuhusu utekelezaji wa  mifumo ya habari na mawasiliano ya uzalishaji na ufatiliaji wa madai ya watoa huduma za afya kwa wanachama katika mkutano  uliofanyika leo katika Hoteli ya Blue Pearl  Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya ushirikiano na Maendeleo kutoka Korea, Chun Chang Bae,  akitoa mada katika mkutano wa Maendeleo Mfuko wa  Kimataifa wa Afya wa Korea jijini Dar es Salaam.
 Maofisa wa wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF) wakiteta jambo kabla ya mkutano  kuanza katika hoteli ya Blue Peal jijini Dar es Salaam.
 Mkurugezi wa Mfuko wa bima ya Afya ya Jamii (CHF) Eugen Mikongoti, akifafanua jambo mbele ya wandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Glub ya jamii

NHIF YAMKABIDHI MKUU WA MKOA WA TANGA MWANTUMU MAHIZA MASHUKA 150

November 11, 2015
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza
akipokea mashuka 150 kutoka kwa Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga,Ally Mwakababu kwa ajili ya vituo vitatu vya Afya,Maramba,Mkinga na Lanzoni vilivyopo wilayani Mkinga mkoani
hapa







 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza akiwa kwenye
picha ya pamoja na viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) mkoani Tanga ofisini kwake mara baada ya kupokea mashuka 150 kwa ajili ya vituo vitatu vya Afya,Maramba,Mkinga na Lanzoni vilivyopo wilayani Mkinga mkoani hapa kulia ni Meneja wa NHIF mkoa wa Tanga,Ally Mwakababu na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Salum Chima na anayefuatia ni Afisa Matekelezo wa (NHIF) Miraji Msile


NA TANGA RAHA BLOG,

MKUU WA Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani hapa kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)ili kuweza kuongeza wigo mpana wa wanachama ambao wataweza kunufaika na huduma zao

Alitoa wito huo jana wakati akipokea mashuka 150 yaliyotolewa na mfuko huo vyenye thamani ya shilingi milioni tatu yaliyotolewa na Mfuko huo kwa ajili ya vituo vitatu vya afya vya Mkinga, Maramba na Lanzoni vilivyopo wilayani Mkinga ambavyo zilikuwa zikikabiliwa na changamoto ya uhaba wa mashuka.

Alisema kuwa endapo elimu itatolewa ya kutosha kwa wananchi wanaoishi maeneo mbalimbali mkoani hapa hasa wale wa vijijini itasaidia kuongeza idadi kubwa ya jamii inayoweza kunufaika na mfuko huo kwa ajili ya kupata matibabu.

  “Nisema kuwa pamoja na kazi kubwa mnayoifanya niwatake mhakikishe mnaendelea kutoa huduma nzuri kwa wanachama wenu ikiwemo kuhakikisha huduma za dawa hazikosekaniki kwenye vituo vya afya na zahanati ili kuondoa usumbufu kwa wananchi “Alisema RC Mahiza.

Hata hivyo alisema kuwa msaada huo umefika wakati muafaka ambao wagonjwa na wananchi wanaokwenda kupata huduma kwenye vituo vya afya wanakumbana na changamoto ya uhaba wa mashuka hivyo itasaidia kupunguza makali ya kutokupatikana mashuka kwenye maeneo hayo.

  “Mimi binafsi ni mdau na balozi mzuri wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na nina vijana wangu sitini ambao watajiunga na mfuko huo kwa lengo la kuhakikisha wanapata matibabu wakati wanapougua kwa sababu maradhi yanatokea wakati wowote “Alisema RC Mahiza.

Kwa upande wake,Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Ally Mwakababu alimueleza Mkuu huyo wa mkoa kuwa dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanasaidia huduma za afya kwenye maeneo yalikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa mashuka.

 “Mkuu wa mkoa sisi tumekuwa mstari wa mbele kuweza kusaidia harakati za kukabiliana na changamoto zinazopatikana kwa wananchi ambao wamejiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa kuhakikisha wanapata matibabu na dawa kwa wakati muafaka bila kuwepo vikwanzo vya aina yoyote ile “Alisema Mwakababu.

Aliongeza kuwa mikakati yao ni kuongeza ufanisi mkubwa katika
kuwahudumia wananchi waliojiunga na mfuko huo ili waweze kupata huduma za uhakika wakati wanapokuwa kwenye vituo vya afya ili kuepukana na usumbufu usiowa wa lazima

 KIBADEN KUINOA KILIMANJARO STARS

KIBADEN KUINOA KILIMANJARO STARS

November 11, 2015
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemteua Abdallah Kibadeni kuwa kocha mkuu wa timu wa Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Star’ akisaidiwa na Juma Mgunda kuelekea katika michuano ya CECAFA Chelenji itakayoanza kutimua vumbi Novemba 21 mjii Addis Ababa, Ethiopia.

Kilimanjaro Stars inashiriki michuano hiyo mikongwe kabisa barani Afrika, ambapo jumla ya nchi 12 wanachama wamedhibitisha kushiriki michuano hiyo itakayomalizika Disemba 6 mwaka huu.

Nchi zingine zinazoshiriki michuano hiyo ni tofati na Tanzania bara ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudani, Sudani Kusini, Uganda na Zanzibar.

Kibadeni mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, na timu ya Taifa Tanzania, ni kocha mwenye leseni B, ambapo ameshafundisha vilabu vingi chini kwa mafanikio ikiwemo kuifiksha klabu ya Simba katika hatua ya fainali ya kombe la Washindi mwaka 1993.

Kocha Kibadeni ni mkurugenzi wa ufundi wa kituo cha mchezo cha KISA kilichopo Chanika, amewahi pia kuzifundisha timu za Kagera Sugar, JKT Ruvu.

Kocha msaidizi wa Kilimanjaro Stars, Juma Mgunda ana leseni B ya CAF, zamani alikuwa mshambuliaji wa timu ya Coastal Union na timu ya Taifa Tanzania, pia aliweza cheza soka la kulipwa katika klabu ya Nahd nchini Oman.

Mgunda amewahi kuifundisha timu ya Coastal Union ya jijini Tanga, timu ya mkoa wa Tanga, kocha wa kituo cha vijana cha mkoa wa Tanga.

Aidha Mgunda ni mkufunzi wa msaidizi wa mafunzo ya makocha ngazi pevu.

VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UBAKAJI WATOTOTO WILAYA YA TEMEKE VYAONGEZEKA

November 11, 2015

 Mkuu wa Dawati la Jinsia katika Kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Chang’ombe, Thecla Kitajo.
 Mkuu wa Dawati la Jinsia katika Kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Chang’ombe, Thecla Kitajo (kulia), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana, ambao wanatembelea vituo vya polisi na masoko ya Manispaa za Ilala na Temeke kujionea jinsi vitendo hivyo vilivyo pungua baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili huo katika maeneo hayo. Kushoto ni Ofisa wa Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo hicho, Meshack Mpwage.
 Ofisa wa Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo hicho, Meshack Mpwage, akizungumza katika mkutano huo.
 Ofisa wa Jeshi la Polisi wa Kituo cha Chang’ombe, Digna Ngatena (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mwanasheria wa Shirika la EfG, Grace Mate)
Maofisa wa Jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo cha Polisi Chang’ombe. Kutoka kushoto ni Albentina Aloyce, Nuni Munisy na Rose Lukanga.
……………………………………………………………………………………
Dotto Mwaibale
 
WAKATI vitendo vya ubakaji na udhalilishaji kwa watu wakubwa vikipungua matukio ya vitendo hivyo kwa watoto wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam vimekuwa vikiongezeka kila siku.
 
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Dawati la Jinsia wa Kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Chang’ombe Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Thecla Kitajo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, ambao wanafanya ziara katika masoko ya Manispaa ya Ilala na Temeke na vituo vya polisi kujua vitendo vya ukatili wa kijinsia ulivyopungua katika maeneo hayo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG), kutoa mafunzo ya kupinga ukati huo.
 
“Vitendo vya ukatili wa kijinsia na ubakaji kwa watu wakubwa umepungua kwa kiasi fulani lakini kwa upande wa watoto bado tunachangamoto kubwa kwani kila siku tunapokea kesi ambapo kwa mwezi tunapokea matukio zaizi ya 25 na zaidi” alisema Kitajo.
 
Kitajo alisema hali hiyo inatokana na watoto hao kufanyiwa vitendo hivyo na watu wazima ambao wengi wao ni jamaa zao wa karibu na tabia ya wazazi kuwa mbali na watoto wao.
 
Alisema licha ya Jeshi la Polisi kujitahidi kufuatilia kesi hizo lakini zimekuwa zikiishia njiani baada ya wanaotakiwa kutoa ushahidi kushindwa kufika mahakamani kwa hofu ya watenda kosa ambao ni wapenzi na hao walifanyiwa vitendo kuja kungwa na sababu za kifamilia.
 
Alisema vitendo vya udhalilishaji na ubakaji vitakwisha iwapo tu jamii itavikataa kwa nguvu moja badala ya kuliachia jeshi la polisi kuvishughulikia.
 
Ofisa wa jeshi hilo  wa dawati hilo, Meshack Mpwage alisema umaskini na mambo mengine kama ya mgeni akifika nyumbani na kulazwa na watoto pia unachangia kwa kiasi kikubwa watoto kubakwa.
 
“Wazazi wamepanga vyumba viwili cha kwao na watoto mgeni akija anapangiwa kulala na watoto hukuo chumbani mgeni huyo anaamua kuwadhalilisha watoto au mtoto” alisema Mpwage
 
Mpwage alisema tabia ya ubize kwa wazazi pia ni moja ya sababu inayowawafanya watoto wakikutwa wamekwisha haribika kwa vitendo hivyo kwa sababu ya wazazi wao kuwa mbali nao na kushindwa kujua kinachoendelea dhidi yao.
 
Alisema hivi sasa changamoto kubwa ya watoto ipo kewa madereva taksi ambao wazazi wanawatumia kuwapeleka mashuleni na madereva bodaboda ambao uwashawishi watoto hao kwa kuwapa chipsi na fedha chini ya shilingi 1000 na kuanza kufanyanao mapenzi.
 
Mpwage alitoa mwito kwa kila mtu kujengea tabia ya kupiga vita vitendo hivyo vya udhalilishaji kwa kutoa taarifa polisi jambo litakalo saidia kupunguza vitendo hivyo kama sio kuvimaliza kabisa.
 
 STARS KUREJA LEO

STARS KUREJA LEO

November 11, 2015
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inarejea leo nyumbani kwa shirika la ndege la Fastjet, ambapo inatarajiwa kuwasili uwanja wa JK Nyerere majira ya saa 12 kamili jioni.

Stars iliyokuwa imeweka kambi nchini Afrika Kusini kwa takribani siku 10, inarejea nyumbani ikiwa imefanya mazoezi vizuri kujiandaa na kuwakabili Mbweha wa Jangwani Algeria siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akiongelea kuhusu kambi kocha wa Stars, Charles Mkwasa amesema anashukru kwa kambi waliyoipata Afrika Kusini, wachezaji wote wameweza kufanya mazoezi katika kiwango cha juu, hapakua na majeruhi hivyo ana imani vijana wake watafanya vizuri siku ya Jumamosi.

 Mkwasa amewaomba watanzania na wapenzi wa mpira wa miguu nchini, kujitokeza kwa wingi uwanjani kuja kuwasapoti katika mchezo dhidi ya Algeria, uwepo wa watanzania wengi uwanjani kuwashangilia utaongeza morali zaidi kwa wachezaji watakaokuwa wanapeperusha bendera ya Tanzania.

Mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam, kikosi cha Mkwasa kitafanya mazoezi kesho Alhamis jioni katika uwanja wa Taifa, na Ijumaa yakiwa ni mazoezi ya mwisho kabisa ya mchezo wenyewe unaosubiriwa kwa hamu.

Wakati huo huo wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wamewasili jijini Dar es salaam leo asubuhi , na moja moja kuingia kambini huku wakiwasubiri wachezaji wenzao wanaowasili leo na kujumuika pamoja kambini.

MFUMUKO WA BEI ZA BIDHAA MBALIMBALI WATIKISA SOKO KUU JIJINI MWANZA.

November 11, 2015
Kwa takribani Wiki mbili sasa, Mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali kupanda katika Soko Kuu la Jijini Mwanza umeendelea kuwaliza watumiaji wa soko hilo.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Mfumuko huo unalalamikiwa na pande zote mbili kwa maana ya wauzaji na wanunuaji sokoni hapo, ambapo wameomba hatua za haraka kuchukuliwa ili kiweka mambo sawa.

Bei kwa nafaka zote sokoni hapo zimepanda bei hadi shilingi 1,000 kwa kila moja tofauti na hapo awali ambapo bidhaa iliyokuwa ikiuzwa shilingi 15,000 sasa inauzwa kati ya 2,000 hadi 2,500 ambapo steki ya nyama imepanda bei kutoka shilingi 5,000 hadi shilingi 8,000 huku nyama mchanganyiko ikiuzwa shilingi 6,000 kutoka 4,000 za awali.

Mwenyekiti wa Soko hilo Hamad Nchola amesema kuwa mfumuko huo umesababisha na mazao ya wakulima kupungua katika maghala yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa mavuno kutokana na ukosefu wa mvua katika msimu uliopita, pamoja na wafanyabiashara kutoingiza sokoni bidhaa katika kipindi cha uchaguzi mkuu, ambapo amewasihi wafanyabiashara kurejea katika mzunguko wao wa biashara kama kawaida hatua ambao itasaidia kukabiliana na mfumko huo wa bei.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu Jijini Mwanza akieleza hali ya mfumuko wa bei ilivyo sokoni hapo
Mmoja wa wauzaji wa nyama katika Soko Kuu Jijini Mwanza akieleza hali ya mfumuko wa bei ilivyo sokoni hapo
Mmoja wa wauzaji wa nyama katika Soko Kuu Jijini Mwanza akieleza hali ya mfumuko wa bei ilivyo sokoni hapo
Bei ya Nyama imepanda bei maradufu
Mteja akiteta na mwanahabari juu ya mfumuko wa bei katika Soko Kuu la Jijini Mwanza
Shughuli za kibiashara katika Soko Kuu Jijini Mwanza zikiendelea
Mmoja wa akina mama wanaouza chakula Soko Kuu Jijini Mwanza anasema kuwa mfumuko huo wa bei umesababisha biashara zao kukamwa
Kushoto ni Mwenyekiti wa Soko Kuu Jijini Mwanza Hamad Ntola akizungumza na Mwanahabari ofisini kwake juu ya mfumuko wa bei katika Soko hilo
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii