MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BANDA LA COSTECH MAONYESHO YA NANENANE KITAIFA NGONGO MKOANI LINDI

August 08, 2017
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, HusseinMansour (hayupo pichani), alipotembelea banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kwenye Maonyesho ya Nanenane viwanja vya Ngongo mkoani Lindi leo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu. Maonyesho hayo yatafungwa na Makamu wa Rais leo mchana.

COSTECH ILIVYOWANOA MAOFISA UGANI WA MKOA WA LINDI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE

August 08, 2017
 Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mafunzo ya siku moja ya kilimo chenye tija  kwa maofisa Ugani wa Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo mkoani hapa juzi.

WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA MAONESHO YA NANENANE LINDI

August 08, 2017
Na Mathias Canal, Lindi

Maonyesho ya Nanenane Kanda ya Kusini ambayo yalianza tokea tarehe 1/8/2017 katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi yanaendela kushika kasi huku kivutio kikubwa ikiwa ni baaada ya bidhaa mbalimbali zinazoonyeshwa kwenye mabanda na Halmashauri mbalimbali kutoka mikoa yote miwili inayounda kanda ya kusini ambayo ni Lindi na Mtwara.

Kwa ujumla wake maonyesho ni mazuri kwani yamehusisha shughuli nyingi za Kilimo, Uvuvi na mifugo kama kauli mbiu inavyosema “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” kauli mbiu hii ikiwa na msisitizo na hamasa zaidi kwa wananchi kutambua mbinu bora za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kuwa na kipato kikubwa kitakachopelekea wananchi kwa ujumla wao kufikia uchumi wa kati.

Pia kumekua na wajasiriamali wengi sana ambao wamefika katika Maonesho hayo wakiwa na bidhaa mbalimali zikiwemo bidhaa za ngozi, mikoba, viungo, asali, vyakula vya asili, mashine Ndogondogo na vingine vingi vya kuvutia.

WAFANYAKAZI JUMIA WAFANYA MATEMBEZI YA HISANI KUCHANGIA FEDHA KUSAIDIA JAMII

August 08, 2017

Na Jumia Travel Tanzania

Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu Jumia ianze kufanya shughuli zake barani Afrika, wafanyakazi wa kampuni wamefanya matembezi ya hisani ili kuchangisha fedha kusaidia jamii inayowazunguka.
Matembezi hayo ambayo yalifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita yaliwahusisha wafanyakazi wote wa kampuni ya Jumia nchini Tanzania kama vile Jumia Travel, Jumia Market, Jumia Food, Jumia Deals, Jumia Cars na Jumia House.

Akizungumzia juu ya tukio hilo Meneja wa Rasilimali Watu wa Jumia Tanzania, Bi. Poonam Divecha amebainisha kuwa matembezi hayo ni sehemu ya kukamilisha shamrashamra za maadhimisho ya miaka mitano tangu kampuni hiyo ianze kuwahudumia watanzania katika Nyanja ya huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao.

“Miaka mitano ni mingi katika utoaji wa huduma hususani kwenye sekta mpya ambayo ina changamoto kadhaa ndani yake. Lakini tusingefikia hapa bila ya uungwaji mkono kutoka kwa watanzania ambao ndio wateja wetu na pia kujitoa kwa wafanyakazi wa Jumia katika kuhakikisha inafanya mapinduzi ya utoaji wa huduma. Katika utoaji wa huduma hizo tunatambua kwamba tunaendesha shughuli zetu kwenye jamii ambayo imekuwa rafiki siku na kutupa moyo wa kusonga mbele zaidi,” alisema Bi. Divecha. 

“Katika kurudisha sehemu ya faida kwa jamii yetu tumeonelea ni vema tufanye matembezi ya hisani ambapo kampuni itachangia kiasi kadhaa cha fedha kwa kila umbali wa kilometa atakazozitembea mfanyakazi wa Jumia. Hivyo basi mbali na kuchangia mapato yatakayotokana na matembezi hayo lakini pia itawajenga wafanyakazi kiafya na kuwakutanisha pamoja kwani ni mara chache kukutana kwa pamoja. Tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora na kuisaidia jamii inayotuzunguka kwani ndiyo sababu ya sisi kuendelea kuwepo,” alihitimisha Meneja Rasilimali Watu wa Jumia kwa nchini Tanzania.
Kwa upande wake mmoja wa wafanyakazi wa Jumia, Mustapha Ally amesema kuwa, “Nimefurahi kwa kushiriki matembezi sio tu kwa ajili ya kusaidia watu wenye mahitaji maalum lakini pia kwa ajili ya afya yetu na pia kutuunganisha pamoja. Ningependekeza tuwe tunafanya mara kwa mara na sio mpaka kuwepo na sababu maalum.”

WAKULIMA WILAYANI KILWA MKOANI LINDI WAUFANANISHA UGONJWA WA MIHOGO NA UKIMWI

August 08, 2017
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruyaya kilichopo Kata ya Lihmalyao wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi, Hassan Amanzi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kilimo kwa wakulima wa Kijiji hicho yaliyofanyika wilayani humo jana. Wengine ni viongozi na wajumbe wa kijiji hicho. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

DKT TIZEBA: TUMEONDOA KODI ILI KUWANUFAISHA WAKULIMA WETU WA NDANI

August 08, 2017

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akiteta jambo na Waziri wa Kilimo Mifugo, Maliasili na Uvuvi Zanzibar Hamad Rashid Muhammed mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akiwasili katika banda la Ofisi ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisikiliza maelezo kuhu takwimu za hali ya chakula nchini mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Kitengo cha uratibu wa mazao na taadhari ya awali wakati wa Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOHITIMISHA ZIARA YAKE YA KIKAZI YA SIKU TANO MKOANI TANGA

August 08, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzirasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji wa Korogwe mkoani Tanga katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza madiwani na viongozi wengine baada ya kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi baada ya  kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akienda kuagana na wananchi baada ya  kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mmoja wa wa wananchi baada ya  kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
 Moja ya mabango yaliyokuwa na ujumbe wa changamoto mbalimbali za Korogwe