MLIMBWENDE WA TAJI LA MISS ILEMELA 2016 APATIKANA.

June 04, 2016
Mlimbwende Maria Frances (katikati) ametwaa taji la MISS ILEMELA 2016. Shindano la kumsaka mlimbwende huyo lilifanyika usiku wa jana June 04,2016 katika viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza.
Katika shindano hilo, nafasi ya pili imenyakuliwa na Mwanaisha Hija (kulia) huku nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Happness Contantine (kushoto).
Imeandaliwa na BMG

WANANCHI WA KISIWANI PEMBA WATAKIWA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILILI YA TABIA NCHI.

June 04, 2016
 Pichani Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira na Idara ya Mazingira ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa ndani ya boti kuelekea mkoa wa kusini Pemba kushiriki zoezi la uzinduzi wa kupanda miti ya mikoko (leo) Juni 4
 Kushoto Naibu wa Waziri wa Wizara ya Nishati, Maji na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Juma Makungu Juma, akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina (katikati) walipokuwa wakielea kupanda miti ya mikoko kisiwa panza kusini Pemba. Kulia ni Muwakilishiwa mkuu wa Wilaya.
Walioinama (kulia) ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipanda mbegu za miti ya mikoko katika eneo la kisiwa Panza ikiwa ni siku ya uzinduzi wa upandaji miti hiyo kisiwani Pemba, kushoto ni Afisa Mazingira mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira bw. Cretus Shengena (Picha na Habari zote na Evelyn Mkokoi).

Evelyn Mkokoi,Pemba
4/6/2016

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) amewataka wananchi wa kisiwa Panza katika Mkoa wa Kusini Pemba, kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi kwa kutunza mazingira hasa kwa kupanda miti ya mikoko kwa wingi,ili kunusuru kisiwa hicho kumezwa kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari.
Mhe. Mpina ameyasema hay leo kisiwani Pemba alipozingua kampeni maalum ya kupanda miti ya mikoko ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kupanda miti.
Awali Mhe. Mpina alisemakuwa, serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  imeweza kupata kiasi cha fedha shilingi milioni 165 maalum kwa kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi kwa kujenga kuta za fukwe za Ocean Road jijini Dar es Salaam,Pangani Mjini Tanga, Kilimani mjini unguja na kisiwa Panza kisiwani Pemba.
Aliongeza kuwa, kiasi hicho cha fedha pia kimeanza kutumika katika kampeni hiyo ya kitaifa ya  kupanda miti kwa kupanda miti ya mikoko katika eneo la kisiwa Panza na ambapo miti zaidi ya milioni Moja inatarajiwa kupandwa katika eneo la hekta 238, kisiwani pemba, pamoja na zoezi hilo kuzinduliwa leo kisiwani pemba, miti hiyo aina  ya mikoko pia inatarajiwa kupandwa katika maeneo ya kilimani mjini unguja,bwawani,tovuni, micheweni na Rufiji.
Naibu Waziri Mpina aliongeza kwa kusema kuwa suala la mazingira si suala la Muungano lakini serikali hizi mbili zimeona umuhimu wa kushirikiana katika eneo hili ili kuweza kukabiliana kikamilifu na madhara na hasara zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kunusuru visiwa hivi kumezwa na bahari.
Akitolea mfano wa shule ya msigi na sekondari kisiwapanza  ambazo zipo hatarini kumezwa,  mhe Mpina aliongeza kuwa  wataalam wa masuala ya mazingira watafanya tathmini kikamilifu na kuona namna gani serikali inaweza kuongeza mbinu zaidi za kushughulikia maeneo haya hatarishi, ili maji ya bahari yasiweze kuingia katika maeneo ya makazi.
Naibu Waziri Mpina aliwasisitizia wananchi wa kisiwa panza kutunza  mazingira kwa kutokukata miti ovyo na kuchoma misitu na watunze na kuilinda miti ya mikoko iliyopandwa ili kuweza kufikia dhamira ya kukinusuru kisiwa icho kumezwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mazingira kutoka katika wizara ya Ardhi,Maji,Nishati,na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Juma makungu Juma amesema maeneo mengi ya Zanzibar yaliyopo pembezoni mwa bahari yameharibiwa na shughuli za binadamu, hivyo upandaji wa miti ya mikoko katika maeneo hayo utazuia adhari za mabadiliko ya tabia nchi kwa makazi ya watu na mashamba ambayo yamepelekea watu kuanza kuhama katika makazi yao na haya yote ni matokea ya vitendo vya wananchi.
Zoezi hilo la kupanda miti ya mikoko lililofanyika kisiwani pemba limeenda sambamba na maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo hufanyika tarehe tano Juni kila mwaka.
MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI AZINDUA MAONYESHO YA MRADI WA MJI MPYA WA ZANZIBAR

MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI AZINDUA MAONYESHO YA MRADI WA MJI MPYA WA ZANZIBAR

June 04, 2016

SAD1 
Katibu Mtendaji Kamisheni ya Ardhi Zanzibar Ahmed Abdulrahman Rashid akitoa maelezo juu ya Mpango Mkuu wa matumizi ya Ardhi wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Mradi wa Mji mpya wa Zanzibar uliofanyika Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Mjini Zanzibar.
SAD2 
Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Eugen Gies akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho ya Mradi wa Ngambo tuitakayo katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
SAD3Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Eugen Gies akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho ya Mradi wa Ngambo tuitakayo katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
SAD4 
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akitoa maelezo namna Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilivyojiandaa katika kuwapatia wananchi nyumba bora za kuishi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Ngambo Tuitakayo.
SAD5Mkurugenzi wa mipango Miji na Vijiji Dkt. Mouhammed Juma akimunyesha Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud namna ya Mji mpya utakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwake katika sherehe za uzinduzi zilizofanyika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi Mjini Zanzibar.
SAD6 
Watoto wakiangalia na kufurahia mji mpya wa Zanzibar utakavyokuwa kupitia Mradi wa Ngambo tuitakayo wakati wa uzinduzi wa maonyesho katika viwanja vya Mnara wa kumbukumbu ya Mapinduzi. Picha na Makame Mshenga /Maelezo Zanzibar.

WAZIRI WA UMMY AWAONGOZA WABUNGE WA TANGA KUWAPA POLE WAHANGA WA MAUAJI YA WATU WANANE MTAA KIBATINI JIJINI TANGA

June 04, 2016

Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani Tanga mara baada ya kutembelea eneo la Zed B ambapo wamehamia wananchi wa Mtaa wa Kibatini kulipotokea mauaji wa watu wanane kwa kuchinjwa ambapo aliongozana na wabunge wa mkoa wa Tanga kuwapa pole wahanga wa tukio hilo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso na kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga,Lucia Mwiru
Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitazama vitu vya wahanga wa tukio la mauaji lililotokea kijiji cha kibatini juzi akiwa na wabunge wa mkoa wa Tanga kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nchi za Nje na Ndani
 Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatembelea wananchi hao kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge mambo ya Ndani na Nje ,Balozi Adadi Rajabu na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM)
 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mustapha Selebosi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya wabunge wa mkoa wa Tanga kutembelea wananchi waliohamia eneo la Zed B baada ya kuhama makazi yao ya Mtaa wa Kibatini kutokana na kutoka mauaji ya watu wanane waliochinjwa juzi na watu wasiojulikana
Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) wakimpa pole mmoja wa wajane ambaye mumewe alichinjwa kwenye tukio la mauaji ya kinyama ya kuchinjwa kwa wakazi wanane wa mtaa wa kibatini na watu wasiojulikana ambao walihamia usikui wa manane

Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimuakiwapa pole mmoja wa wafiwa katika tukio hilo la mauaji
Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa na mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso wakimsikiliza mmmoja wa wajane waliwapoteza wanaume zao kwenye mauaji ya kinyama ya kuchinjwa watu wanane yaliyotokea mtaa wa kibatini jijini Tanga
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga,Lucia Mwiru akimfariji mmoja wakina mama ambaye mumewe aliuwawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana 

WABUNGE WAPATA SEMINA KUHUSU MALENGO MAPYA 17 YA DUNIA

June 04, 2016

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez  Alvaro (kulia)
akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Tulia Ackson (kulia) mara baada ya kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania , Rodriguez  Alvaro (kulia) mara baada ya mwakilishi huyo kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Rodriguez  Alvaro (kulia)
akimwonesha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (kulia) sehemu ya taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini mara baada ya kufika Ofisini kwake Bungeni Dodoma leo.

KIPINDI CHA UNYAYO WANGU: DAVID MANOTI AZUNGUMZIA ADHABU YA WABUNGE WA UPINZANI BUNGENI

June 04, 2016
Unyayo wangu ni kipindi kipya kabisa kinachokujia kupita Tone Tv, ambacho kinaletwa kwenu na Mtangazaji wetu Eddie Nyota , kinacholenga shabaha ya watu waliothubutu kufanya jambo fulani katika jamii na wanauelewa na jamii husika. Utajifunza mengina kuburudika pia kupitia kipindi hiki Kinacholenga rika zote.
 


Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail blogszamikoa@live.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.blogszamikoa.com 1458109219454_logo_blog_za_mikoi.png
RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KIONGOZI WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA LUO ZHIJUN IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KIONGOZI WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA LUO ZHIJUN IKULU

June 04, 2016

ib1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Gerson John Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson John Mdemu mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson John Mdemu mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Gerson John Mdemu wa pili kutoka kushoto. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga mara baada ya tukio la uapisho kukamilika.
ib5 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China.
ib6 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China, ikulu jijini Dar es Salaam.
ib7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini lu youqing aliyeambatana na Kiongozi huyo wa chama cha Kikomunisti cha China, Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib9 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi  wa Chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  kutoka jimbo la Jiangsu nchini China mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
ib10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa kiongozi huyo wa chama cha Kikomunisti cha China Luo Zhijun  pamoja na Balozi wa China hapa nchini lu youqing mara baada ya kumaliza Mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi pamoja na Mkuu wa mkoa wa dar es Salaam Paul Makonda. PICHA NA IKULU
WAZIRI JANUARI MAKAMBA APANDA MITI UFUKWE WA BAHARI YA HINDI

WAZIRI JANUARI MAKAMBA APANDA MITI UFUKWE WA BAHARI YA HINDI

June 04, 2016

mam1 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akitia saini kitabu cha Wageni alipotembelea Kata ya Mbweni iliyopo Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya shughuli za upandaji mikoko katika eneo hilo.
mam2 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipanda mti aina ya mkoko katika fukwe za bahari ya hindi katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam. Upandaji huo wa mikoko ni katika kuadhimisha wiki ya mazingira duniani, ambayo kilele chake ni kesho
mam3 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba  akishirikiana kupanda miti ya mikoko na wakazi wa kata ya  Mbweni jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya mazingira hapo tarehe 5 juni.
mam4 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifurahia jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbweni ambao walijumuika pamoja naye kupanda mikoko katika fukwe za Mbweni jijini Dar es salaam.
mam5 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kupanda mikoko katika fukwe za bahari ya Hindi katika kata ya Mbweni.
……………………………………………………………………………………………………………
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ametoa wito kwa Wananchi  wa Kata ya Mbweni kutunza mazingira na kutoa kipaumbele kwa mazingira. Aliyasema hayo wakati wa zoez la upandaji mikoko lilifanyika katika fukwe za bahari ya Hindi zilizoko Mbweni.
Akiongoza Wananchi wa Kata hiyo kupanda miche 5,000 ya mikoko , Waziri Mkamba alisititiza pia Wanafunzi wa shule waliopo katika eneo hilo kupenda mazingira yao na kuyatunza ili yawafae baadaye.
Wakisoma Risala yao , Wanawake wa Mbweni walimuomba Waziri awasaidie kuwapatia vitendea kazi  kwa ajili ya kuhudumia mikoko pamoja na kumuomba awasaide kuwatatulia changamoto wanazokutana nazo. Ikiwamo ya maafisa wa TRA kukata hovyo mikoko wanapokua wanafanya doria katika fukwe zaMbweni.
Mwisho Waziri aliwahukuru Wananchi wa Mbweni waliojitypkeza kujumuika naye katika zoezi hilo la upandaji mikoko. Shuhuli za upandaji mikoko ni kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira ambayo kilele chake ni tarehe 5 juni kila mwaka.

MSEMAJI WA CCM, OLE SENDEKA AFANYA ZIARA KUKAGUA NA KUIMARISHA UHAI WA CHAMA WILAYANI KILWA MKOANI LINDI LEO

June 04, 2016

Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM, Kibibi Duka akimvalisha skafu Msemaji wa CCM, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Christopher Ole Sendeka, alipowasili Ofisi ya CCM y Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama wilayani humo leo.
Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM, Ali Njonzi akitokwa na jasho jembemba wakati wa Vijana wa umoja huo walipokuwa wakimpokea msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka katika Ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa leo akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama
Msemaji wa CCM, Cheristopher Ole Sendeka akimsalimia Katibu wa CCM Wilaya ya Liwale Raphael Maumba, alipokuwa akisalimia viongozi mbalimbali wa CCM mkoa wa Lindi, baada ya kuwasili ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa leo akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa akimuongoza Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka kuingia Ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa, alipowasili akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama leo
Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa, akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarsiha uhai wa Chama wilayani humo leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa
Baadhi ya wageni waliofuatana na semaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka wakiwa ukumbi wa Ofisi ya CCM, wakati Sendeka alipokuwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Kilwa mkoani Lindi leo.
Katibu wa CCM mkoa wa Lindi Adelina Geffi akisoma taarifa ya Chama, Msemaji wa CCM alipowasili Ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa mkoani humo leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo wa Lindi Ali Mtopa.
Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka akizungumza na viongozi wa CCM, alipowasili katika Ofisi ya CCM wilaya ya Kilwa mkoani Lindi leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa.
Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiselebuka na Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM waliofika kumpokea katika Ofisi ya CCm wilaya ya Kilwa mkoani Lindi leo kukagua na kuimarisha uhai wa Chama
Wazee wa Kilwa mkoani Lindi wakimpokea kwa shamrashamra Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka, alipowasili katika ukumbi wa Hall Fair, kuzungumza nao leo akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama wilayani Kilwa mkoani Lindi
Wazee wa Kilwa mkoani Lindi wakimpokea kwa shamrashamra Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka, alipowasili katika ukumbi wa Hall Fair, kuzungumza nao leo akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa Chama wilayani Kilwa mkoani Lindi
Mwenyekiti wa Wazee wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Mohammed Msinjepi akimkaribisha Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka (katikati), kuzungumza na wazee wa wilaya ya Kilwa, katika ukumbi wa Hall Fair leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa.
Hakim Mstaafu Mzee Zuberi Liengama akisoma risala, kabla ya Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka kuzungumza na wazee wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi leo
Hakim Mstaafu Mzee Zuberi Liengama akimkabidhi risala baada ya kuisoma, kabla ya Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka kuzungumza na wazee wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi leo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ali Mtopa akimtambulisha kwa wazee wa wilaya ya Kilwa, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka, leo katika Ukumbi wa Hall Fair
Msemaji wa CCM, Cheristopher Ole Sendeka akizungumza na Wazee wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi alipokuwatana nao katika ukumbi wa Hall Fair, wilayani humo leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO