HIVI NDIVYO MGAMBO SHOOTING WALIVYOWAPIGISHA KWATA MBEYA CITY MKWAKWANI JANA.

November 04, 2014


KIKOSI CHA MGAMBO SHOOTING KILICHOIFUNGA MBEYA CITY MABAO 2-1 JUZI KWENYE UWANJA WA CCM MKWAKWANI

KOCHA MKUU WA MGAMBO SHOOTING YA TANGA,BAKARI SHIME KULIA AKIANGALIA MECHI HIYO JANA

MEYA WA JIJI LA MBEYA MZEE ATHANAS AKIFUATILIA MECHI HIYO PAMOJA NA MASHABIKI WENGINE WA TIMU HIYO JUKWAA KUU JANA


KOCHA MKUU WA MBEYA CITY JUMA MWAMBUSI AKIFUATILIA MECHI YAO NA MGAMBO SHOOTING AMBAPO MBEYA CITY ILIFUNGWA MABAO 2-1

Makamu wa Rais wa Afrika Kusini awasili nchini kwa ziara ya siku moja

November 04, 2014


Makamu wa Rais wa  Afrika Kusini, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa akiteremka katika ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere Jijini  Dar es Salaam.  Mhe. Ramaphosa yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo pamoja na mambo mengine atazungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Mahusiano , Mhe. Stephen Wasira kwa pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt.  Mahadhi Juma Maalim (Mb), na Bi. Zuhura Bundala, Kaimu Mkurugenzi   wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa mapokezi ya  Makamu wa Rais wa Afrika Kusini.  
Mhe. Ramaphosa akilakiwa na Mhe. Wasira mara baada ya kuwasili.
Mhe. Ramaphosa akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika mara baada ya kuwasili. 
Mhe. Ramaphosa akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Talha Mohammed 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Ikulu  Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa Matamela alipofika Ikulu kwa mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Ramaphosa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) kwa pamoja na Mhe. Wasira wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Rais na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Mhe. Radhia Msuya, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini 
Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazungumzo.Picha na Reginald Philip
 ZITO KABWE AWATIA RUMANDE VIGOGO WA TPDC

ZITO KABWE AWATIA RUMANDE VIGOGO WA TPDC

November 04, 2014

01
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (mbele) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (nyuma yake), wakiongozwa na Polisi kuingia kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa rumande baada ya kamati hiyo, kuwakuta na hatia ya kuidharau na kuinyima taarifa muhimu, wakati ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake hicho.
02Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, akifafanua jambo wakati akiwahoji Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Michael Mwanda na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, James Andilile wakati kamati hiyo, ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake kilichofanyika jana, Ofisi za Bunge, Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filkunjombe.

04Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC, Michael Mwanda (mbele) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, James Andilile (nyuma yake), wakiongozwa na Polisi kwenda kuingia kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa rumande baada ya kamati hiyo, kuwakuta na hatia ya kuidharau na kuinyima taarifa muhimu, wakati ilipokaa kama Mahakama katika kikao chake hicho.

JANUARI MAKAMBA AMWAGA VIATU PAIR 48600 KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI JIMBONI KWAKE.

November 04, 2014
MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO ALHAJ MAJID MWANGA AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZIDUZI WA UGAWAJI WA VIATU HIVYO KULIA NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA BUMBULI BEATRICE MSOMISI

MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO ALHAJ MAJID MWANGA AKIMVALISHA KIATU MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI SONI HALIMA BAKARI WAKATI WA UZINDUZI HUO KUSHOTO ANAYESHUHUDIA NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA BUMBULI BEATRICE MSOMISI


MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA BUMBULI BEATRICE MSOMISI AKIMVALISHA KIATU MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI SONI







NA MWANDISHI WETU,LUSHOTO.
MKUU wa wilaya ya Lushoto ,Alhaji Majid Mwanga amesifu jitihada zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Januari Makamba  kwa hatua aliyochukua kwa kuwapatia viatu wanafunzi wote waliopo kwenye shule za msingi katika Halmashauri ya Bumbuli.

Makamba alitoa viatu 48600 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi tisini na saba zilizopo kwenye maeneo mbalimbali kwenye Halmashauri ya Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga .

Lengo la kugawa viatu hivyo ni kuwasaidia kuwaepusha wanafunzi
wanaosoma kwenye shule hizo kuepukana na magonjwa mbalimbali hatarishi ikiwemo tatizo la minyoo hali ambayo inaweza kuwaathiri wakati wa usomaji wao jambo ambalo linaweza kurudisha nyuma maendeleo yao.

Mkuu huyo wa wilaya alisema jambo hilo linaonyesha jinsi gani Mbunge huyo alivyokuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wake wanapata elimu nzuri itakayowawezesha kuinua kiwango cha taaluma kwa wanafunzi waliopo kwenye shule mbalimbali kwenye halmashauri hiyo.

Alisema mbunge amafanya jambo nzuri ambalo linawatengenezea afya nzuri wanafunzi hao kitendo ambacho kitaongeza juhudi zao za ufaulu kutokana na kuepuka magonjwa ambayo yanaweza kuwakwamisha katika masomo yao ikiwa wataugua.

Aidha aliwataka wananchi wa Jimbo hilo kutumia fursa ya kuwa na mbunge huyo ili waweze kujiletea maendeleo na kuwataka viongozi wengine walipo wilayani humo kutumia njia alizopita mbunge huyo ili kuweza kuhakikisha wanafunzi wilaya nzima wanapata viatu.

     “Jambo hili alilolifanya Mbunge wetu ni kuharakisha maendeleo kwa wananchi wake kwa kuhakikisha wanapata elimu nzuri kwa kuwa katika afya nzuri hivyo juhudi hizo zinapaswa kuungwa mkono na viongozi wengine “Alisema DC Mwanga.
PAUL MAKONDA AKANUSHA KUMPIGA MZEE WARIOBA NA KULAANI WALIOANZISHA VURUGU, ASEMA ALIMSAIDIA AMON MPANJU NA MZEE WARIOBA KUTOKA SALAMA UKUMBINI

PAUL MAKONDA AKANUSHA KUMPIGA MZEE WARIOBA NA KULAANI WALIOANZISHA VURUGU, ASEMA ALIMSAIDIA AMON MPANJU NA MZEE WARIOBA KUTOKA SALAMA UKUMBINI

November 04, 2014


  M1 
Katibu wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akionesha vitu alivyokwenda navyo kwenye mdahalo huo ambavyo ni katiba ya sasa na katiba pendekezwa kwa ajili ya kutumia kujibu hoja mbalimbali wakati wa mdahalo huo, Makonda amelaani na kukanusha kuwa hakumpiga Mzee Warioba isipokuwa alikuwa na kazi moja ya kuhakikisha anamsaidia Anold Kayanda mwandishi wa BBC ambaye aliumizwa  katika vurugu hizo na  Mzee Warioba na aliyekuwa mbunge wa bunge maalum la katiba asiyeona Amon Mpanju  wakati wa vurugu zilizotokea katika  mdahalo wa kujadili rasimu ya Katiba inayopendekezwa, kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza  jana, ambapo Makonda aliyedaiwa kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu wa zamani Jaji mstaafu Joseph Warioba, amekanusha kumpiga leo katika mkutano wa waandishi wa habari, Dar es Salaam. Pia Makonda amesema kuwa hawezi kabisa kudiriki kumpiga kwani anamheshimu kama babake mzazi. Amesema kuwa hata leo asubuhi amezungumza na warioba kwenye simu kumjulia hali. Warioba naye amekanusha kupigwa na Makonda wala mtu yoyote kwenye vurugu hizo
 M3 
Makonda akisisitiza jambo katika mkutano huo ambapo pia aliwaambia kazi kubwa aliyoifanya wakati wa vurugu hizo, ni kumsaidia Warioba kutoka salama pamoja na Mwanasiasa mwenye ulemavu wa macho Amon Mpanju ambaye pia alikuwa anamuokoa ili asipatwe na dhahama hiyo.
M4 
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo wakimsikiliza kwa makini.
 MAKAMU WA RAIS AZINDUA UTOAJI WA HUDUMA KWA WALEMAVU WA USIKIVU (VIZIWI) JIJINI DAR.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA UTOAJI WA HUDUMA KWA WALEMAVU WA USIKIVU (VIZIWI) JIJINI DAR.

November 04, 2014
 unnamed 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akizindua rasmi utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Picha na OMRunnamed2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimshuhudia Mwasisi na Rais wa Taasisi ya Hearing, William Austine akimvisha mashine maalum ya kuwawezesha kusikia, mwanafunzi Amina Athuman wa darasa la tatu katika shule ya msingi Buguruni wakati wa uzinduzi utoaji wa huduma hiyo kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uliofanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Picha na OMR unnamed1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Mwasisi na Rais wa Taasisi ya Hearing, William Austine, baada ya uzinduzi wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Picha na OMRunnamed3 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimvisha Nishani, Mwanafunzi wa Darasa la tatu katika Shule ya Msingi Buguruni, mwenye ulemavu wa kusikia (kiziwi) , Amina Athuman, baada ya kuvishwa kifaa maalum kinachomwezesha kusikia, wakati wa uzinduzi rasmi wa utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi). Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Picha na OMR unnamed4 
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimvisha mwanafunzi mlemavu wa kusikia (kiziwi) Bertha Samwel wa darasa la tatu Shule ya msingi Buguruni, Kifaa maalum cha kumwezesha kusikia, wakati wa uzinduzi rasmi utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi). Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Picha na OMR
unnamed6 
Makamu wa Rais wa Jasmhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mwasisi wa Taasisi ya Starkey Hearing, William Austine, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walemavu wa kusikia, wakiopatia mashine maalum za kuwawezesha kusikia, baada ya kuvishwa mashine hizo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo. Picha na OMR
Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia, (Viziwi) wakisubiri kupatiwa huduma hiyo wakati wa uzinduzi.