NAIBU WAZIRI AWESO SIPO TAYARI KUONA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO ZINATUMIKA VIBAYA

March 19, 2018
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkandarasi kutoka Kampuni ya Wesers Limited ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani Kisyeri Chambiri mara baada ya kulitembelea kuona namna linavyoendelea wakati wa ziara yake ambapo alihimiza likamilike kwa wakati kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akimueleza jambo  Mkandarasi kutoka Kampuni ya Wesers Limited ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani Kisyeri Chambiri mara baada ya kulitembelea kuona namna linavyoendelea wakati wa ziara yake ambapo alihimiza likamilike kwa wakati.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akisisitiza jambo kwa umakini Mkandarasi kutoka Kampuni ya Wesers Limited ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani Kisyeri Chambiri mara baada ya kulitembelea kuona namna linavyoendelea wakati wa ziara yake ambapo alihimiza likamilike kwa wakati
 Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Abdallah akizungumza katika ziara hiyo kulia Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Sabas Chambasi

 Sehemu ya jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani ambalo ujenzi wake unaendelea

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akikagua ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea

  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akikagua ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akikagua ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akitoka kwenye eneo la ujenzi wa  Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akisalimiana na mmoja wa wakina mama wanaofanya kazi kwenye ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo kuweza kuona namna inavyoendelea

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akitembelea maeneo mbalimbali mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Halmashauri hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Seif Ally katikati ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)akisalimiana na wakazi wa Mji huo kabla ya kuvuka kivuko kuelekea upande wa pili wilayani Pangani akiwa kwenye ziara yake

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)kulia akiingia kwenye kivuko cha kuvuka mto Pangani kuelelea ng'ambo ya pili ya mji wa Pangani wakati wa ziara yake

 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)wa pili kushoto akifurahia jambo na mmoja wa wananchi wakati akiwa kwenye kivuko cha Mto Pangani kuelelea ng'ambo ya pili ya mji wa Pangani kwa ajili ya kufanya ziara kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa


Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akishuka kwenye kivuko kuelekea ng'ambo ya pili ya mto Pangani kuendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo


NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema hatakuwa tayari kuona fedha za miradi ya maendeleo zinatumika vibaya huku akimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sabasi Chambasi kuwa makini nayo.
Hatua hiyo inatokana na kuwepo kwa baadhi ya miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali kujengwa chini ya kiwango jambo ambalo linasababishwa na kutokuwa makini kwa viongozi wanaoisimamia.
Aweso aliyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Pangani ambalo limegharimu kiasi cha milioni 600 linalosimamiwa mkandarasi Kisyeri Chambiri kutoka kampuni ya Wesers Limited.
Alisema mradi huo una umuhimu mkubwa sana kwa wilaya hiyo hivyo lazima watumishi wakiwemo wale ambao wanasimamia suala hilo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ili kuweza kuongeza ufanisi wakati wakitekeleza suala hilo.
“Mkandarasi huu mradi ni muhimu sana kwa Halmashauri yetu hivyo sitopenda kuona unajengwa chini ya kiwango lakini pia hakikisheni unakamilika kwa wakati kwa lengo la kufanya kazi “Alisema.
Naibu Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) alimuagiza mkurugenzi huyo kuweka umakini mkubwa kwenye ujenzi huo ili kuepukana na utekekelezaji wake kuwa chini ya kiwango kutokana na kutumia fedha nyingi.
Hata hivyo alimwambia Mkurugenzi huyo wa Pangani kuhakikisha anamsimamia vizuri mhandisi mshauri wa mradi huo ambae ni mwajiriwa wa Halmashauri hiyo ili ukamilike kwa wakati na kuondoa adha kwa watumishi ya kutokua na Halmashauri yenye ubora.
“Si kitu cha busara kuona mhandisi mshauri ambae ni mtu muhimu katika mradi huo kutokuonekana, Mkurugenzi ninamashaka na mradi huu kama kweli utakamilika kwa muda uliopamnga ambapo ni mwezi Juni mwaka huu”Alisema.
Hata hivyo aliwatahadharisha viongozi wa Halmashauru kuwa makini na matumizi ya fedha za Serikali ambazo zinatolewa na Serikali au wadau mbalimbali wa maendeleo kwani bila kufanya hivyo wanaweza kuzorotesha maendeleo.

ULEGA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA KWA MKAKATI MZURI WA KUINUA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

March 19, 2018


Katika Picha ni chaga za kisasaa za kukaushia dagaa katika mwalo wa Muyobozi, uliyopo katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza, Mwalo ambao ulijengwa na Mradi wa kuhifadhi mazingira ya ziwa Victoria LIVEMP , chaga hizo zinatumika na wavuvi kukaushia dagaa.



Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega kushoto akizungumza na mfanyabiashara wa samaki aliyejulikana kwa jina la Bw. Ntakokola Issa katika Mwalo wa Kibirizi Mjini Kigoma kuhusu usafi wa vifaa maalum na gari la kubebea samaki, gari no T389 AZY linalotumiwa na Mfanyabiashara huyo lilipokuwa linaonekana  katika hali ya uchafu, Naibu Waziri Ulega alikagua Mwalo wa Kibirizi uliyopo Mjini Kigoma leo baada ya kumaliza Ziara yake wilayani Uvinza.


Katika Picha ni chaga za kisasaa za kukaushia dagaa katika mwalo wa Muyobozi, uliyopo katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza, Mwalo ambao ulijengwa na Mradi wa kuhifadhi mazingira ya ziwa Victoria LIVEMP , chaga hizo zinatumika na wavuvi kukaushia dagaa.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega na Ujumbe wake wakitoka kukagua gati katika mwalwo wa Muyobozi uliyopo Wilayani uvinza katika kijiji cha Mwakizega ambapo Naibu Waziri Ulega alifanya ziara leo.





Katika Picha katikati Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akipata maelezo kuhusu Mwalo wa Muyowozi toka kwa Afisa Uvuvi wa Wilaya ya uvinza Bw. Haroon Chande, wakati wa ziara yake mwalono hapo leo.


Pichani wavuvi wakiteketeza wao wenyewe nyavu haramu zilizokamatwa katika oparesheni ya kupambana na uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika Mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alipofanya ziara katika Mwalo wa Muyobozi Wilayani Uvinza leo. (Habari na Picha na Mwandishi Maalum)
NA; MWANDISHI MAALUM – UVINZA
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Uvinza kwa kuwa na mikakati thabiti ya kupambana na uvuvi haramu na kutatua kwa kiasi kikubwa migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuwekeza kwenye Ranchi za mifugo.
Ulega ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kugagua Mwalo wa Muyobosi uliyopo Wilayani uvinza ambapo alisema jitihada hizo za wilaya zitachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo na serikali kwa ujumla, kwani ina mkakati wa kutenga maeneo ya Ranchi kwa ajili ya wafugaji.
“Nataka niwahakikishie mimi na wizara yangu tutakuwa tayari kuhamia hapa kulisimamia jambo hili mtakapo tenga hayo maeneo ya kufugia, ili kuwaweka tayari wafugaji katika maeneo hayo na huo ndiyo muharobaini wa kwenda kuondoa  matatizo ya wakulima na wafugaji katika nchi yetu kwa mipango ya namna hii inawezekana kabisa, hicho ni kipaumbele chetu mimi na waziri wangu Mhe. Luhaga Mpina katika uongozi wetu tutahakikisha kama siyo kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji basi tutaindoa kabisa, kwa kushirikiana vyema na Halmashauri zetu” Alisema Ulega.
 Ulega alisisitiza suala la mapambano dhidi ya uvuvi haramu na ulinzi wa Rasilimali za uvuvi na suala zima la ufugaji wa samaki, nakuwaasa kuachana kabisa na utamaduni wa kuagiza samaki kutoka nje ya nchi.
Naibu Waziri Ulega  alisema kuwa fedha nyingi zimewekwa katika mwalo huo wa Muyobozi na kuwataka wavuvi katika eneo hilo kuutumia vizuri mwalo huo wenye hadhi ya kimataifa ambapo ameleza kwa mwaka wa fedha uliopita mwalo huo peke yake umechangia kiashi cha shilingi milioni 28 “ Ninaamini kama mtapasimamia vyema mahala hapa patachangia pato la taifa mara nne zaidi ya mwaka jana. Ninyi ndo muwe walinzi wa kwanza wa rasilimali hizi ili nchi yetu iweze kuinuka” Alisisitiza
Awali, akiongea katika ziara hiyo mwenyekiti wa kijji cha Mwakizega ambapo mwalo wa Muhyobozi umejengwa Bw. Jaffari Abdalah, alisema mwalo huo unakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na gati la mwalo huo kuwa na urefu wa mia 20 ambazo ni chache kwa boti kuegesha kupakua na kupakia kabla na baadha ya shuguli za uvuvi , hivyo ameiomba serikali kuongeza urefu wa gati hiyo ili mitumbwi mikubwa na midogo iweze kufanya shughuli za uvuvi vizuri.
Bw. Jaffar pia alisema wavuvi wa Muyobozi wanakabiliana na changamoto ya kukosa elimu kupitia mafunzo yanayoendana na wakati huu wa kisasa katika sekta ys uvuvi.