TAKUKURU RAFIKI YASAIDIA KUTATUA KERO ZA ARDHI SHINYANGA

April 23, 2024

 

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy akizungumza na waandishi wa habari


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Shinyanga (TAKUKURU) kupitia Program ya TAKUKURU RAFIKI imesaidia kutatua kero za wananchi mkoani Shinyanga.

Akitoa akitoa taarifa ya utekelezaji wa kazi za TAKUKURU kwa kipindi cha robo ya tatu ya Januari hadi Machi 2024 leo Jumanne Aprili 23,2024 Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy amesema Programu ya TAKUKURU imefanya ufuatiliaji wa majibu ya kero ya kutopimwa maeneo ya makazi kwa wananchi wa kata ya Ndala Mtaa wa Ndala tangu mwaka 2018.


“Awali wananchi zaidi ya 246 walichanga kiasi cha shilingi 12,396,000/= na kulipa Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya zoezi la upimaji ardhi. Pia wananchi 1150 wa mtaa wa Mlepa waliokuwa wamechanga fedha kwa ajili ya kupimiwa na kurasimishiwa maeneo yao lakini walikuwa bado hawajapatiwa namba za upimaji wa viwanja vyao tangu mwaka 2023 walipopimiwa”,amesema Kessy.


“Wananchi wa mtaa wa Ndala walitoa keto yao kutopimiwa na kurasimishiwa maeneo yao pamoja na kuwa walikwishachangia huduma hiyo tangu mwaka 2018. Vilevile wananchi wa mtaa wa Mlepa kero yao ilikuwa kupatiwa namba za viwanja vyao tangu walipopimiwa mwaka 2023”,ameeleza.

Amesema hali hiyo ilikuwa inapelekea migogoro ya mipaka, kuwanyima fursa ya kupata mikopo katika taasisi za kifedha kwa kutumia ardhi kama dhamana lakini pia viwanja kutoongezeka thamani kwa kukosa utambuzi rasmi.


“Baada ya kupokea kero hiyo, TAKUKURU iliwasilisha Manispaa ya Shinyanga bango kitita lenye kero kusika na mikakati ya utatuzi wa kero hiyo. Halmashauri ya Manispaa Idara ya ardhi walishughulikia kero hiyo ambapo katika mtaa wa Mlepa zoezi la kugawa namba za viwanja lilianza na hadi sasa namba za viwanja 412 zimeanza kugawiwa tangu mwezi Januari na zoezi bado linaendelea”,amefafanua Kessy.

“Mwezi Februari Manispaa ya Shinyanga ilifanya zoezi la upimaji katika mtaa wa Ndala na kwa sasa Manispaa ipo kwenye mchakato wa ukamilishaji wa utengenezaji wa ramani kwa ajili ya kusajiriwa Wizarani na baada ya hapo kupata namba za viwanja hivyo 246 vya wananchi wa mtaa wa Ndala”,ameongeza.


Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga amesema TAKUKURU inaendelea kufuatilia ugawaji wa namba za viwanja vilivyopimwa katika mtaa wa Mlepa mpaka litakapokamilika lakini pia kufuatilia zoezi la ukamilishaji wa uandaaji wa namba za viwanja za mtaa wa Ndala na ugawaji wake.

Hali kadhalika TAKUKURU inaendelea kufanya vikao vya utambuzi wa kero katika kata 14 kutoka kata za Mwenge, Mwawaza, Kolandoto, Lyabukande, Puni, Nyida, Mhongoloi, Majengo, Nyasubi, Ulowa, Bulungwa, Mpunze, Bupigi na Bubiki.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy akizungumza na waandishi wa habari

BASHUNGWA KUCHUKUA HATUA KWA MAMENEJA WAZEMBE TEMESA, ATAKA MAJINA KUBAINISHWA.

BASHUNGWA KUCHUKUA HATUA KWA MAMENEJA WAZEMBE TEMESA, ATAKA MAJINA KUBAINISHWA.

April 23, 2024


zinazotolewa TEMESA, jijini Dodoma.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Lazaro Kilahala akisikiliza
kwa makini maelekezo ya Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (hayupo pichani),
alipohoji utoaji wa huduma za vivuko nchini.




Muonekano wa Kivuko cha MV Tanga ambacho kina uwezo wa kubeba abiria 100,
magari 6 sawa na tani 50.

…………………….

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA), Lazaro Kilahala kuwasilisha majina ya Mameneja wa Kanda na
Mikoa wa TEMESA ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia
wananchi ili waweze kuchukuliwa hatua.

Bashungwa ametoa agizo hilo Aprili 22, 2024 jijini Dodoma kufuatia kupokea
malalamiko mara kwa mara kuhusu huduma zinazotolewa na TEMESA ikwemo
huduma ya Kivuko cha MV.Tanga Mkoani Tanga ambapo amemuagiza Katibu Mkuu
kuingilia kati kubaini changamoto zinazokwamisha kivuko hicho.

“Mambo mengi ya kiutendaji yanaletwa kwa Waziri na Katibu Mkuu wakati Watendaji
mpo na tumewaamini kusimamia Taasisi zenu, hasa jambo hili lipo TEMESA. Mtendaji
Mkuu kama kuna mapungufu ya wasaidizi wako bora uje kwa Katibu Mkuu useme huyu
atufahi aondoke kuliko kukaa nao maana hatimaye litakuangukia wewe”, amesema
Bashungwa.

Bashungwa amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Mhandisi Aisha Amour
kuangalia namna bora ya usimamizi wa TEMESA katika huduma ya vivuko nchini ili
kuleta manufaa na uboreshaji wa huduma za usafiri na usafirishaji ziimarike.

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa bado TEMESA inaendelea kuwa na mikwamo na
kutotekeleza majukumu yake kwa uharaka pindi tatizo linapogundulika katika Vivuko na
hivyo kupelekea kuzorota kwa huduma hiyo katika baadhi ya maeneo.

“Changamoto ya marekebisho ya kivuko cha MV Tanga yanaendelea zaidi ya siku 10
sasa lakini leo naulizia vifaa bado havijafika, kama ‘parts’ ziko Dar es Salaam
inachukua masaa mangapi hadi kufika Tanga? na sio Tanga pekee yake ni maeneo
yenye vivuko”, Bashungwa akimuhoji Mtendaji Mkuu wa TEMESA.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala amekiri kuwepo kwa
changamoto hiyo katika Kivuko cha MV. Tanga na timu ya wataalam inaendelea na
marekebisho ya Kivuko hicho ili kuboresha huduma zake.

PROF. MKENDA "MGAO WA FEDHA ROMBO HAUFANYIKI KWA UPENDELEO

April 23, 2024

 NA WILLIUM PAUL, ROMBO.


MBUNGE wa Rombo ambaye ni Waziri wa Elimu Sayansi na teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema mgawanyo wa fedha zinazotolewa na serikali katika tarafa mbalimbali ndani ya wilaya ya Rombo haufanywi kwa upendeleo bali kwa kuzingatia uhitaji katika kila eneo.

Pia amesema kwa kipindi Cha miaka 3 , serikali imetenga mamilioni ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilayani hiyo ikilinganishwa na kipindi cha Miaka 10 iliyopita.

Profesa Mkenda alisema hayo wakati akifanya mkutano wa ndani na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya CCM kutoka katika Tarafa ya Mengwe kuelezea maendeleo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita wilayani Rombo kwa kipindi cha miaka mitatu chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumzia mgawanyo huo wa fedha zilizotolewa na serikali kupitia halmashauri kwa kipindi cha miaka 3 Profesa Mkenda amesema , Tarafa ya Mkuu ilipata kiasi Cha bilioni 3.8, Mengwe bilioni 3.558, Tarakea bilioni 2.3 , Useri bilioni 2.419 huku Mashati ikipata zaidi ya kiasi Cha shilingi milioni 903.



TANZANIA YAONGOZA KWA SIMBA, NYATI NA CHUI BARANI AFRIKA

April 23, 2024

 


Na John Mapepele

Serikali imesema Tanzania inaongoza kwa kuwa na Simba, Nyati na Chui wengi katika bara la Afrika huku ikishirikilia nafasi ya tatu kwa kuwa na idadi kubwa yaTembo.

Hayo yamesemwa leo Aprili 22, 2024 kwenye mkutano ambao Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki ametangaza rasmi matokeo ya Sensa ya Wanyamapori na kuzindua taarifa ya Watalii wa Kimataifa walioitembelea Tanzania mwaka 2023.

Sensa hiyo ya wanyamapori imefanywa na TAWIRI kwa kushirikiana na TANAPA, TAWA, NCAA, Idara ya Wanyamapori, na Frankfurt Zoological Society katika mifumo ya ikolojia ya Nyerere-Selous-Mikumi,Saadani-Wamimbiki na Serengeti 

Mkutano huo uliwahusisha wadau wa uhifadhi na utalii, ambapo Mhe. Kairuki amesema tayari Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kufanya sensa ya wanyamapori nchi nzima mapema hapo mwakani.

 Aidha, Mhe. Kairuki amesema matokeo ya sensa hiyo yatasaidia kwenye usimamizi wa wanyamapori nchini na kupanga mipango mbalimbali ya kuboresha  uhifadhi na  kutangaza  utalii duniani.

Mhe. Kairuki ametoa wito kwa wadau wote kushirikiana na Serikali ambapo ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori nchini (TAWIRI) kuandaa mpango kazi kwa ajili ya sensa ijayo huku pia akielekeza watendaji wa wizara yake kuchambua kwa kina  matokeo ya sensa hii  ili yaweze kuleta tija.
.

Akitoa taarifa ya sensa hiyo amesema spishi zilizoonyesha idadi kubwa ni pamoja na Nyati (59,878), Tembo (20,006), Nyumbu (19,060), Kongoni (18,361), swalapala (14,031) na Ngiri (13,806), ambapo spishi zilizoonyesha idadi ndogo ni pamoja na Twiga (1,679), Tandala mkubwa/ kudu (1,414) na puku/sheshe (496). 

Amefafanua kuwa kwa upande wa Tembo, idadi imeongezeka kutoka 15,501 (2018) hadi 20,006 (2022) na Viashiria vya ujangili wa tembo au vifo vya tembo vimepungua kwa kiasi kikubwa hadi 0.8% mwaka 2022 ikilinganishwa na 16% wakati wa sensa ya 2018. 

Akizungumzia kuhusu taarifa ya Watalii wa Kimataifa walioitembelea Tanzania mwaka 2023 amesema Sekta ya Utalii ni miongoni mwa sekta muhimu katika uchumi wa dunia na umeendelea kuimarika baada kuathiriwa na mlipuko wa janga la UVIKO-19. Mwaka 2023 sekta ya utalii duniani imeimarika kwa kiwango cha asilimia 88 ikilinganishwa na kiwango cha juu kilichofikiwa mwaka 2019.

 “Hali hii ilitokana na ukuaji endelevu wa maendeleo ya teknolojia na juhudi za kukuza na kuendeleza maeneo mengine ya utalii duniani. Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watalii duniani iliongezeka kwa asilimia 34 hadi kufikia watalii bilioni 1.3 Mwaka 2023 kutoka milioni 960 Mwaka 2022”. Ameongeza

Amesema kwa Tanzania, utalii wa Kimataifa umeimarika kwa kiwango cha asilimia 118.4 Mwaka 2023 ikilinganishwa na kiwango cha juu kabla ya janga la UVIKO-19.  Aidha, idadi ya watalii wa Kimataifa iliongezeka kutoka watalii milioni 1.4 Mwaka 2022 hadi kufikia watalii milioni 1.8 Mwaka 2023 sawa na ongezeko la asilimia 24.3. 

“Hatuna budi kutambua kazi kubwa aliyoifanya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyeitangaza Tanzania kupitia filamu ya Tanzania the Royal tour”. Amesisitiza  

Kwa kutambua umuhimu wa sekta ya utalii hapa Nchini, Serikali kwa kushirikiana na wadau ilifanya utafiti wa watalii wanaoondoka Nchini Mwaka 2023 kwa lengo la kupata taarifa zinazosaidia kutunga Sera na kuandaa mipango ya maendeleo ya utalii. Aidha, taarifa za utafiti huo zinasaidia serikali kuandaa akaunti za taifa (national accounts) na mizania ya malipo ya nje (Balance of Payments). 

Aidha amesema utafiti umebainisha kuwa mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kwa asilimia 33.5 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.4 Mwaka 2023 kutoka Dola za Marekani 2.5 bilioni zilizopatikana Mwaka 2022.  Aidha, wastani wa matumizi ya mtalii kwa siku katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliongezeka hadi kufikia Dola za Marekani 250 Mwaka 2023 kutoka wastani wa Dola za Marekani 214 Mwaka 2022. 

Kwa upande wa Zanzibar, wastani wa matumizi ya mtalii kwa siku ulikuwa Dola za Marekani 257 Mwaka 2023 ikilinganishwa na watani wa Dola za Marekani 218 Mwaka 2022.

DOZI MOJA YA CHANJO YA HPV INATOSHA KUMKINGA MSICHANA KUPATA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

April 23, 2024

 Na WAF - Mwanza


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema dozi Moja ya chanjo ya HPV inatosha kumkinga msichana kupata ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi na kuwataka wazazi/walezi kuwapeleka watoto kupata chanjo hiyo.

Waziri Ummy amesema hayo leo Aprili 22, 2024 kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Dozi moja ya chanjo ya HPV kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 iliyozinguliwa katika viwanja vya Furahisha Wilayani Ilemela Mkoa wa Mwanza.

“Wataalamu wetu ambao wanatoka kwenye Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) wametuhakikishia kuwa dozi moja ya chanjo ya HPV inatosha kumkinga msichana kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi”. Amesema Waziri Ummy

Amesema, awali dozi zilizokuwa zinatolewa mbili, ya kwanza inatolewa leo na baada ya miezi Sita inatolewa nyingine hii ilikua inapelekea mabinti wengi kutorudi kupata dozi ya pili, Sasa hivi tumeamua kutoa dozi moja ya HPV kwa kuwa inatosha kuwakinga wasichana kuja kupata maambukizi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi.

Aidha, Waziri Ummy amesema Saratani inayoongoza kuwatesa Watanzania ni Saratani ya Mlango wa Kizazi ambapo amesema katika kila wagonjwa 100 wanaougua Saratani, wagonjwa 23 ni wagonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi.

“Inafuata Saratani ya mfumo wa chakula asilimia 11, Saratani ya Matiti asilimia 10.4, Saratani ya tezi dume asilimia 8.9 kwa hiyo ukiaangalia hapo Saratani inayoongoza ni Saratani ya Mlango wa Kizazi”. Amesema Waziri Ummy

Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi na walezi wote nchini, kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote wanazopaswa kupata kwa kuwa lengo kubwa la chanjo ni kuwakinga na magonjwa yakiwemo haya ya Saratani pamoja na kuwakinga na vifo vinavyoweza kuzuilika na chanjo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. Saidi Mtanda amesema watahakikisha watoto wote wenye umri wa kuanzia miaka 9-14 wanapata chanjo hiyo ili kufikia malengo.

“Kwa mwaka 2022/23 Mkoa wa Mwanza ulifanikiwa kuchanja watoto zaidi ya laki Mbili sawa na asilimia 107 kati ya walengwa waliotarajiwa kuchanjwa ni laki 191,440 wenye umri chini ya Mwaka Mmoja, tumefikia malengo na kuyavuka”. Amesema Mhe. Makilagi








VIJIJI 52 MVOMERO KUNUFAIKA NA MRADI WA LTIP

April 23, 2024


Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bi. Judith Nguli akifungua mkutano wa wadau kujadiliutekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi tarehe 22 Aprili 2024mkoani Morogoro.

Msimamizi wa Mradi katika Wilaya ya Mvomero Bw. Sambalu Simon akitoa taarifa fupi yautekelezaji mradi wa uboreshaji wa usalama wa miliki za ardhi wilayani humo tarehe 22Aprili 2024 mkoani Morogoro.
Wadau walioshiriki katika Mkutano wa wadau kujadili utekelezaji wa Mradi wa UboreshajiUsalama wa Milki za Ardhi tarehe 22 Aprili 2024 katika Wilaya ya Mvomero, Morogoro




Vijiji takribani 52 katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro vitanufaika na Mradi waUboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) kwa kuandaliwa mipango ya matumizi yaardhi ya vijiji.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bi. Judith Nguli wakati wa kujadiliutekelezaji wa Mradi huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mvomero, tarehe 22 Aprili 2024 Mkoani Morogoro.


Alisema kupitia mradi huu lengo ni kuandaa jumla ya Mipango Shirikishi ya Matumizi yaArdhi ya Vijiji 52 katika Wilaya ya Mvomero ambapo hadi kufikia sasa tayari mipango 48 imekwishaandaliwa. 


‘‘Tarafa nne zilizopo Mvomero zitakazonufaika na mradi huu ni Tarafa ya Mgeta - vijiji 19, Tarafa ya Mvomero - vijiji 11, Tarafa ya Mlali - vijiji 11 na Tarafa ya Turiani - vijiji 11ambavyo kwa pamoja vitakuwa na jumla ya mipango ya matumizi ya ardhi 52’’ alisemaNguli.


Msimamizi wa Mradi katika Wilaya ya Mvomero Bw. Sambalu Simon amesema kuwa lengola kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji ni kuimarisha milki za ardhi na matumiziyake, kugawa ardhi na kuboresha matumizi na hifadhi ya ardhi kulingana na mapendekezo nauwezo wa Kijiji, kubaini na kutenga maeneo ya umma pamoja na kuimarisha utunzaji wamazingira kupitia sheria ndogo zinazotungwa kusimamia mpango.


Nae Bi.Sofia Lucas mkazi katika Wilaya ya Mvomero alimshukuru Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka mradi huo Wilayani kwao, kwakuwa mradi umewekeza sana katika kutoa elimu kwa jamii hususani makundi maalumu kamaushiriki wa wanawake katika kumiliki ardhi ili kuwakomboa kiuchumi.


Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unaotekelezwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi umeweka nguvu kubwa katika kutoa elimu kwa wananchikuanzia ngazi ya Kitaifa, Wilaya, Mtaa/Kijiji mpaka Kitongoji ikiwa ni pamoja na kuzingatiahaki za makundi mbalimbali yakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi, wanawake, vijana, wenye ulemavu sambamba na utoaji wa elimu ya usawa wa jinsia katika umiliki wa Ardhi ilikuhakikisha usalama kwa kila kipande cha ardhi kwa Mtanzania.