KAMISHNA WA SENSA ATOA SOMO KWA WADADISI NA WAHARIRI WA MADODOSO YA UTAFITI WATU WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI 2014
Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya watu
wenye uwezo wa kufanya Kazi kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani,
Morogoro, Lindi na Mtwara wakiwa kwenye mafunzo ya siku mjini
Morogoro.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na. Veronica Kazimoto na Aron Msigwa – Morogoro.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na. Veronica Kazimoto na Aron Msigwa – Morogoro.
Wadadisi na Wahariri wa madodoso ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi mwaka 2014 wametakiwa kuzingatia maadili na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuepuka kuliletea taifa hasara kwa kutoa takwimu zisizosahihi.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Morogoro na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Hajjat Amina Mrisho Said wakati akizungumza na Wadadisi na Wahariri wa madodoso yaUtafiti wa Watu wenye uwezo wa kufanya kazi kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara walio katika mafunzo ya siku 16 mjini Morogoro.