KINANA AKAGUA UKUMBI UTAKAOTUMIKA WAKATI WA MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM MJINI DODOMA

July 20, 2016



Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi, Nape Nnauye na Msemaji Mkuu wa CC, Christopher Ole Sendeka wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili kukagua ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center nje kidogo ya mji wa Dodoma, leo Julai 20, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akianza kukagua ukumbi huo huku akiongozana na Katibu wa NEC, ITikadi na Uenezi Nape Nnauye
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiongozwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kuingia katika ukumbi huo. Kushoto ni Msemaji Mkuu wa CCM Christopher Ole Sendeka
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokagua ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center nje kidogo ya mji wa Dodoma, leo Julai 20, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016. Wengine kutoka kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Itikadi na Uenezi Rogas Romuli, na Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka.na kushoto ni Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Itikadi na Uenezi, Kilumbea Ng'enda
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokagua ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center nje kidogo ya mji wa Dodoma, leo Julai 20, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016. ulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Itikadi na Uenezi Rogas Romuli na Msemaji Mkuu wa CCM, Ole Sendeka
Nape akionyesha eneo la meza kuu
Nape akiendelea kumpatia maelezo Kinana kuhusu hali ya ukumbi
Nape akiendelea kumpatia maelezo Kinana kuhusu hali ya ukumbi
Hali ya ukumbi sehemu ambako watakaa wajumbe na waalikwa
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya viongozi wakitazama paa la Ukumbi, Kinana alipokagua ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center nje kidogo ya mji wa Dodoma, leo Julai 20, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016.


Nape akijaribu vinasa sauti vitakavyotumika
Kinana na Nape wakikagua eneo watakakokaa viongozi katika meza kuu
Ole Sendeka akitoa mawazo yake wakati wa ukaguzi wa ukumbi huo
Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka akijaribu vinasa sauti vitakavyotumika wakati wa mkutano huo
Wakielekea kutoka ukumbini baada ya kukagua
Kinana na Nape wakiendelea kukagua maeneo mengine ya ukumbi
Eneo la mapumziko ya wageni waalikwa na viongozi
Ukumbi mdogo wa ndani
Wakienda kukagua eneo lingine la ukumbi
Wakiendelea kukagua ukumbi

Eneo la kulia chakula



Kinana, Nape na Sendeka wakitoka ukumbini


Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia baadhi ya wanachama wa CCM ambao wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali kuandaa ukumbi huo
Nape akimuonyesha eneo watakakotokea wajumbe
Geti la kutokea
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana pia alikagua banda la Uhuru Publications Limited ambalo watumishi wa kampuni hiyo wataonyesha kazi zao za uandaaji wa magazeti ya Uhuru Mzalendo na Burudani wakati wa mkutano huo

Kinana akikagua banda hilo



Kinana akiwa kwenye banda hilo



Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka kwenye banda la Uhuru Publications Ltd, Wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, alipokagua ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center nje kidogo ya mji wa Dodoma, leo Julai 20, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua ukumbi huo



Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo, baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wapili kulia), kukagua ukumbi huo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwav



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, alipokagua ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center nje kidogo ya mji wa Dodoma, leo Julai 20, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016.



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akijadili jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, alipokagua ukumbi wa mikutano wa CCM, Dodoma Conversion Center nje kidogo ya mji wa Dodoma, leo Julai 20, 2016, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika Julai 23, 2016. Katikati ni Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka



Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akijadili jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto kukagua ukumbi huo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

MAKAMU WA RAIS AZINDUA RIPOTI YA LISHE YA DUNIA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

July 20, 2016

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Ripoti ya Lishe ya Dunia kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza kwenye mkutano wa kuzindua ripoti ya lishe ya Dunia ambao mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Baadhi ya Wadau wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa uzinduzi ya ripoti ya Lishe ya Dunia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  (kulia) akikata utepe kuashiria kuzindua ripoti ya Lishe ya Dunia, katkati ni  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa PANITA ,Dkt. Tumaini Mikindo
……………………………………………………………………………………

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya awamu ya TANO itatoa msukumo mkubwa katika kukabiliana na tatizo la utapiamlo nchini kwa kuweka mipango na mikakati imara ikiwemo kuongeza bajeti ya lishe, kuongeza virutubisho kwenye vyakula na kutumia vyema wataalamu wa lishe katika kupambana na tatizo hilo hapa nchini. 
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli  hiyo jijini Dar es Salaam Trh 20-Jul-16 katika hotuba yake ya uzinduzi  wa Ripoti ya Dunia ya Utapiamlo
ambayo imetilia mkazo masuala ya lishe kama msingi wa Maendeleo hapa nchini na Duniani kwa ujumla.
Makamu wa Rais amesema viongozi wa serikali katika ngazi zote za wilaya na mikoa wanatakiwa kuunga mkono jitihada za kuondoa utapimlo nchini kwa kuweka msukuko wa kipekee katika ngazi zote za maamuzi.
Ameeleza kuwa jitihada zinazofanywa na serikali kwa ushirikiano na wadau wa Maendeleo wa Ndani na Nje ya Nchi zimesaidia kwa kiasi kikubwa kushusha kiwango cha udumavu nchini kutoka asilimia 42 mwaka 2010 hadi kufikia asilimia  34 mwaka 2015.
Amefafanua kuwa kutokana na mafanikio hayo, serikali imetoa mwongozo wa bajeti ya mwaka 2016/17 kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya masuala ya lishe kwa kila mtoto wa umri chini ya miaka MITANO hapa nchini Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na fedha hiyo kuwa kidogo lakini serikali itaendelea kuongeza kiasi cha fedha kwenye bajeti zijazo hadi kufikia kiasi cha dola 8.5 sawa na shilingi elfu 18000 kwa kila mtoto hapa nchini kama
ilivyoshauriwa na jopo la wataalamu wa Benki ya Dunia na wa masuala ya afya na uchumi duniani.
Makamu wa Rais pia ameziagiza Halmashauri zote
Nchini kupitia TAMISEMI zihakikishe zinatumia fedha hizo vizuri na kwa malengo
yaliyokusudiwa na sio vinginevyo.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA BENKI YA EXIM YA CHINA IKULU NDOGO YA CHAMWINO MKOANI DODOMA.

July 20, 2016

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang  wa kwanza kulia katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma. Wakwanza kushoto ni Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha pamoja na ujumbe wa Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang  mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika  Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang  (watatu) kutoka kulia mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing wakwanza kushoto, Waziri wa Fedha na Mipango Filipo Mpango, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Suzan Kolimba.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang watatu kutoka kulia mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwa msisitizo mara baada ya kikao chake na ujumbe wa Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana kwa furaha na Rais wa Benki ya Exim ya China Liu Liang katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU