“BODI YA LIGI YAANZA MAZUNGUMZO NA AZAM MEDIA KWA AJILI YA UFADHILI WA TIMU ZINAZOSHIRIKI LIGI DARAJA LA KWANZA HAPA NCHINI”

January 04, 2015
BODI ya Ligi imesema kuwa ipo mbioni kukamilisha mchakato wa kuzipatia ufadhili klabu zinazoshiriki michuano ya ligi daraja la kwanza hapa nchini ili kuweza kuyafanya mashindano hayo kuwa na msisimuko ikiwemo ushindani kama ilivyokuwa kwenye ligi kuu.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Hamadi Yahaya wakati akizungumza na MTANDAO HUU ambapo alisema kuwa hivi sasa wapo kwenye mazungumzo na Kampuni ya Azam Media ambapo kwa asilimia kubwa mafanikio yanaweza kupatikana kutokana na hatua nzuri walioifikia.

Yahaya alisema kuwa mwaka uliopita walichagua kampuni kwa ajili ya kutafuta ufadhili lakini ilishindwa kuifanya kazi hivyo lakini wanaona kuangalia namna ya kufanya ili kufanikisha jambo hilo kwa kampuni ya Azam Media.

Kauli ya Mwenyekiti huyo inatokana na baadhi ya maombi yaliyotolewa na vilabu vinavyoshiriki michuano kuitaka bodi hiyo kuhakikisha wanavitafutia ufadhili ili kuweza kuondokana na utegemezi ambao wakati mwengine unachangia kuwepo kwa maandalizi hafifi jambo ambalo linapelekea kuikosesha ladha michuano hiyo.

Hata hivyo vilabu hivyo vilitaka pia mechi zao kuchezwa mwishoni mwa wiki badala ya katikati ya wiki kama ilivyokuwa hivi sasa ili kuweza kuzipa fursa kufanya matayarisho ya kutosha kama ilivyokuwa vilabu vya ligi kuu hapa nchini.

Akitolea ufafanuzi suala hilo, Mwenyekiti huyo alisema kuwa ligi hiyo inachezwa katikati ya wiki kutokana na  wingi wa mechi hivyo
zisipochezwa kwa staili hiyo itachukua muda mrefu kumalizika kwa
michuano hiyo .

KINAA AANZA ZIARA TANGA LEO

January 04, 2015
KATIBU MKUU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdurahamani Kinana anatarajiwa kuwasili mkoani Tanga leo kwa ajili ya kufanya ziara ya siku mbili mkoani Tanga  itakayoambatana na kuzungumza na wananachi kupitia mikutano ya hadhara katika maeneo ambayo atapita.


Akizungumza na MTANDAO HUU Ofisini kwake, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga,Shijja Othumani alisema kuwa katibu huyo atapokelewa njia ya panda ya Segera na kuelekea wilayani Lushoto kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Shija alisema kuwa ziara hiyo itafanyika kwenye Halmasahuri ya Bumbuli kwenye kiwanda cha Chai cha Mponde ikiwemo kuzungumza na wananchi wanaoishi maeneo mbalimbali kabla ya siku ya pili kuelekea wilaya ya Tanga mjini.

 Alisema kuwa siku ya pili katibu huyo atakuwa na mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye viwanja vya Tangamano jijini Tanga ambapo lengo la ziara hiyo ni kuwashukuru wakazi wa mkoa wa Tanga kwa kukipa ridhaa kwenye chaguzi wa serikali za mitaa kwenye uchaguzi uliofanyika Desemba mwaka jana.

Aidha alisema kwenye uchaguzi huo chama cha mapinduzi (CCM)
kilifanikiwa kupata ushindi wa asilimi 100 ambayo ni mafanikio makubwa ambapo kwa upande wa vijijini kilipata ushindi wa asilimia 95 na vitongoji walipata asilimia 97

Hata hiyo,Katibu huyo alitoa wito kwa viongozi waliochaguliwa kwenye chaguzi hizo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na kwa uadilifu ili kuweza kuchochea kasi ya maeneo kwa wananchi waliowap ridhaa ya kuwaongoza.

DKT. SHEIN AZINDUA MAEGESHO NA NJIA YA KUPITIA NDEGE (APRON AND TAXIWAY) ZANZIBAR LEO

January 04, 2015

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili katika uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Meneja wa Benki ya Dunia Tanzania Monthe Biyoudi wakikata utepe kuzindua maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar(kushoto0 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Meneja wa Benki ya Dunia Tanzania Monthe Biyoudi wakifungua pazia kwa pamoja kuzindua maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar
Wananchi na Viongozi mbali mbali walioalikwa katika sherehe za uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Ndege mbali mbali zikiwa katika Paki ikionesha sura halisi ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar ilivyo ambapo Ndege za mashirika mbali mbali ya ndege zinaouwezo wa kutua hapa nchini na kuweza kukuza pato la Taifa letu.
Msoma Risala Farida Rajab Yussuf akisoma risala hiyo mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Wasanii wa Ngoma ya Kibati wakitoa burudani yao wakati wa sherehe za uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) uzinduzi uliofanyika leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alikuwa mgeni rasmi wa shuhuli hiyo
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji akitoa nasaha fupi na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kutoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) uzinduzi uliofanyika leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ikulu].

DIAMOND AFUNIKA SHOW YA AMAHORO RWANDA

January 04, 2015
 Nguli wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka Tanzania, Nassib Abdul 'Diamond' akitumbuiza katika show yake iliyofanyika katika uwanja wa Amahoro mjini Kigali Rwanda wakati wa shamrashamra za siku kuu ya mwaka mpya. Diamond alikuwa Rwanda kwa mwaliko wa East Afrika Promotors.
 Diamond akiwa jukwaani
 Mashabiki wa burudani waliofurika katika uwanja wa Amahoro kumnshuhjudia mkali huyo Afrika Mashariki.
 Mwanadada wa Kiganda, Zahara Hassan anaetoka na Diamond akifuatilia show hiyo
 Diamond akifanya yake jukwaani...
 Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka nchini Rwanda, Butera Knowless anayetamba na kibao cha 'TULIA' akitumbuiza katika show hiyo kali ya kufa mtu ambapo pia vijana wa
 Mashabiki wa Knowless wakishangilia huku wakiwa na picha zake.
Mashabiki wakiwa uwanjani hapo kushuhudia burudani hiyo. SOURCE: UMUSEKE
Rais ateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya

Rais ateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya

January 04, 2015

unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM.
3 Januari, 2015
MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI AZINDUA BARABARA YA MKAPA AWAMU YA PILI

MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI AZINDUA BARABARA YA MKAPA AWAMU YA PILI

January 04, 2015


unnamed 
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Zanzibar Seif Ali Iddi akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Barabara ya Amani- Mtoni kwa awamu ya pili ya ujenzi wake katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. (kushoto alievaa kofia ya pama) Katibu Mkuu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Malik Akili. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. unnamed1 
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuzindua Barabara ya Mkapa iliopo Amani-Mtoni ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar (kushoto) Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. unnamed2 
Baandhi ya wananchi na Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Barabara ya Mkapa iliopo Amani-Mtoni Mjini Zanzibar. unnamed3 
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji akitoa nasaha fupi na kumkaribisha Balozi Seif Ali Iddi kutoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Mkapa iliopo Amani-Mtoni Mjini Zanzibar. unnamed4 
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akihutubia katika Sherehe ya uzinduzi wa Barabara ya Amani-Mtoni ikiwa ni miongoni wa shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. unnamed5 
Barabara ya Amani-Mtoni iliyozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

RIDHIWANI KIKWETE KUHARAKISHA MAENDELEO CHALINZE

January 04, 2015

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika Kijiji cha Changarikwa wakati wa ziara ya kikazi pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kuchagua viongozi wa Seikali ya Kijiji wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.CCM imepata ushindi wa Vijiji vyote katika 74 katika jimbo hilo.
 Ridhiwani akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika kijiji hicho ambapo aliwataka kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa ama sivyo vijiji vitageuka jangwa.
 Mkazi wa Kijiji cha Kwaluhongo, Dustan Sangi akiuliza swali kwa Mbunge wake Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano  uliofanyika kijijini hapo
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwaluhonbo ambapo alijibu maswali mbalimbali ya wananchi kuhusiana na kero mbaalimbali walizonazo pamoja na suluhisho
 
 Ridhiwani akizungumza jambo na Khamis Ibrahim baada ya mkutano kumalizika katika  Kijiji cha Kwaluhongo, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya Mbwewe, Chalinzi, wilayani Bagamoyo jana.
 Mama mkazi wa Kijiji cha Changarikwa akiuliza swali kwa mbunge kuhusu tatizo la kijiji hicho kutokuwa na Zahanati
 Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo,Kombo Kamote akiwafunda viongozi wapya wa Serikali ya Kijiji cha Changarikwa ambapo aliwataka kujali sana maendeleo ya wananchi badala ya maslahi yao binafsi.
 Wazee wakisikiliza kwa makini wakati Ridhiwani akihutubia katika Kijiji cha Changarikwa, Kata ya Mbwewe.
 Ridhiwani akiifariji familia ya marehemu Jangili Shaban alipokwenda kuhani msiba baada ya kumalizika kwa mkutano katika Kijiji cha Changarikwa
 Mzee Athuman Mnemwa akielezea mbele ya Mbunge wake Ridhiwani Kikwete jinsi Kijiji cha Kwang’andu kinavyoteseka na kero ya maji.
 Mwanahawa Habib akielezea mbele ya Ridhiwani jinsi wakazi wa kijiji hicho wanavyonyapaliwa na Daktari na wauguzi wa Zahanati ya kijiji hicho
 Mzee Athuman Kisuli akisisitiza umuhimu wa kupelekewa maji katika Kijiji cha Kwang’andu
 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu akiwasalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwang’andu ambapo aliahidi kusaidiana na Ridhiwani kutatua tatizo la maji linalowakabili wananachi wa kijiji hicho
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo na kuahidi kutatua kero mbalimbali ikiwemo ya maji katika kijiji hicho cha Kwang’andu, Kata ya Mbwewe
 Mwananmke aliyejitangaza kuwa anaishi na virusi vya Ukimwi Pili Mbwana akiomba mbunge Ridhiwani kusaidia kuwasaidia kupata mikopo  watu wanaoishi na VVU katika Kijiji cha Kunduchi Kata ya Mbwewe ili iwasaidie kuondokana na umasikini walio nao
 Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kijiji kipya cha Kunduchi wakati wa ziara yake atika Kata ya Mbwewe jana
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao

 Ridhiwani akizungumza na Pili Mbwana anayeishi na virusi vya Ukimwi ambapo aliahidi kumsaidia jinsi ya kupata mkopo
Ridhiwani akiteta jambo na Mzee Suleiman Kadagala baada ya kumalizika kwa mkutano huo