Serikali ya Norway imeihakikishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ushirikiano katika sekta za kilimo, usalama wa chakula,
nishati, biashara na uwekezaji pamoja na mabadiliko ya tabianchi.
Ahadi
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya
Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk
Nassor Mbarouk katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Balozi
Mbarouk alisema kuwa Norway imekuwa mdau mkubwa wa Tanzania katika
sekta ya afya na imekuwa ikisaidia katika masuala mbalimbali katika
sekta hiyo.
“Katika hii ziara Mhe. Naibu Waziri anatagemea
kufanya ziara ya kutembelea hospitali ya Kiluteri ya Hydom ambayo
imekuwa ikifadhiliwa na Serikali ya Norway……… madhumuni ya zaira hiyo ni
kuangalia ni kwa namna gani Norway inaweza kuongeza ushirikiano na
kuisaidia hospitali hiyo,” alisema Balozi Mbarouk.
Kwa upande
wake Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe.
Bjørg Sandkjær amesema kuwa ameitembela Tanzania kutokana na
ushirikiano imara uliopo baina yake na Serikali ya Norway uliodumu kwa
muda mrefu na ulianza kama ushirikiano wa maendeleo.
“Lengo la
ziara yangu hapa Tanzania ni kuangalia ushirikiano katika sekta ya afya
kwa sababu Norway imekuwa ikifadhili sekta, Mashirika ya Umoja wa
Mataifa, mifuko ya kimataifa, wadau wengine wanaohusika katika sekta ya
afya pamoja na asasi za kiraia zinazofanya kazi na Serikali ya Tanzania
katika kuboresha huduma za afya,” alisema Mhe. Sandkjær.
Hivyo
nitaitembelea Hospitali ya Kilutheri ya Haydom ili kujionea shughuli
zinavyofanyika na kuangalia zaidi maeneo ya ushirikiano katika sekta
hiyo.
Tanzania na Norway zimekuwa zikishirikiana katika sekta za
afya, elimu, uvuvi, nishati jadidifu, kilimo, ushafirishaji na utalii
pamoja na masuala ya bahari.
WAANDISHI WA HABARI CHUO KIKUU HURIA TZ WAPEWA MAFUNZO, WAASWA KUWA NA JICHO LA KIJINSIA
WAZIRI MKUU KIKAO CHA KIKUNDI KAZI CHA KITAIFA CHA MAWAZIRI CHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza Kikao cha Kikundi Kazi cha Kitaifa cha Mawaziri cha Nishati safi ya Kupikia, kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2023. Kushoto ni Waziri wa Nishati Januari Makamba na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) George Simbachawene. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO KUANZISHA KLINIKI ZA KIBINGWA ZA JIONI
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhan
Na Oscar Assenga, TANGA.
HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo inatajia kuanzisha huduma za Kliniki za Kibingwa wakati wa muda wa ziada wa jioni itakayoanza kuanzia Aprili 9 mwaka huu katika hospitali hiyo.
Akizungumza leo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhan amesema huduma hizo zitaaza saa tisa na nusu jioni mpaka muda ambao wagonjwa watamalizika ambao watapata fursa ya kuonana na madaktari bingwa waliopo kwenye hospitali hiyo.
Dkt Juma alisema kwamba katika kliniki hiyo huduma mbalimbali za kibingwa ikiwemo magonjwa ya ndani,magonjwa ya ya upasuaji,magonjwa ya wakina mama,magonjwa ya watoto,magonjwa wa koo,pua pamoja na sikio .
Aidha alisema kwamba huduma hizo zitatolewa kwa wagonjwa wote wenye bima bila kujalia aina gani ya bima lakini pia wale wagonjwa wanaofanya malipo ya keshi yatapokelewa.
Hata hivyo alisema huduma hiyo itatolewa siku Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa tisa na nusu mpaka pale watakapomalizika.
Dkt Juma aliwahimiza wananchi wa mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kliniki hizo ili kuweza kukutana na madaktari bingwa wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga
Hata alisema uwepo wa kliniki hiyo utasaidia kutoa fursa kwa wagonjwa kuweza kukutana na madaktari bingwa ambao wataweza kuwasaidia hivyo watumie nafasi hiyo kuweza kuonana na madaktari hao bingwa waliopo kwenye hospitali hiyo.