CCM MUHEZA WAANZA UJENZI WA JENGO JIPYA LA UTAWALA LA GHOROFA

May 15, 2023

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Like Gugu akichimba msingi jana kuashiria kuanza ujenzi wa Jengo la CCM wilaya ya Muheza la Ghorofa ambalo litajengwa eneo la Kata ya Genge wilayani humo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Like Gugu akichimba msingi kuashiria kuanza ujenzi wa Jengo la CCM wilaya ya Muheza la Ghorofa ambalo litajengwa eneo la Kata ya Genge wilayani humo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Like Gugu  akizungumza mara baada ya kumalizika halfa ya uchimbaji wa msingi kuashiria kuanza ujenzi wa Jengo la CCM wilaya ya Muheza la Ghorofa ambalo litajengwa eneo la Kata ya Genge wilayani humo
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Muheza ambaye pia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza Desderia Haule akizungumza wakati wa halfa hiyo ambapo alikipongeza chama hicho
Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Simon Leng’ese akieleza jambo katika halfa hiyo
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Muheza Herbet Mtangi akizungumza wakati wa halfa hiyo
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali




Mafundi wakiendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi huo


 Na Oscar Assenga, MUHEZA

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Muheza mkoani Tanga wameanza ujenzi wa Jengo Jipya la Utawala la Ofisi za Chama hicho la ghorofa ambalo litatumika kwenye shughuli mbalimbali.

Hatua hiyo hiyo inatokana na makubaliana waliokubaliana kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya wilaya kwamba wanajenga jengo jipya la kisasa katika eneo ambalo waliachiwa na wazee.

Akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa uchimbaji wa msingi wa ujenzi huo,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu alisema kwamba mradi huo wa ujenzi wa jengo hilo utagharimu Milioni 260

Alisema kwamba wao kama wilaya watajitahidi kutafuta fedha kwa wahisani na kushirikiana na wanachama hao ili kuweza kufanikisha malengo ya ujenzi wa ofisini hiyo ambayo wanamatumaini itakamilika kabla yam waka 2025.

“Jengo letu la zamani tutalitumia kwa ajili ya biashara na tulikubaliana kwamba wanajenga Jengo la ofisi ya CCM wilaya kwenye kikoa cha Halmashauri kuu na kwamba wanataka kujenga la kisasa kwenye uwanja tulioachiwa na wazee kabla ya kufika m waka 2025 jengo hilo lianza kutumika”Alisema Mwenyekiti huyo

Hata hivyo alisema kwamba watashirikiana na wana CCM wilayani humo kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati kabla ya muda wa kampeni kuanza ili liweze kutumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kichama.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (Das) Desderia Haule aliipongeza CCM kwa kubuni wao na kuanza ujenzi wa Jengo nzuri la kisasa ambalo hata hadhi ya wilaya itaonekana kwa viongozi watakaokuwa wakifika wilayani humo huku akihaidi kushirikiana nao. 

Katibu Tawala huyo aambaye alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Muheza alitoa wito kwa wana CCM wilaya ya Muheza kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja kwa kujitoa ili kuweza kufanikisha ujenzi huo ili kabla ya mwaka 2025 wakati wa hekaheka za uchaguzi liwe limekamilika.

‘Pale tulipo kuwa zamani hapatoshi hivyo tukiwa hapa itakuwa nzuri sana hivyo kikubwa tuendelea kushirikiana kuweza kufanikisha ujenzi huu ambao ni muhimu”Alisema

Hata hivyo alitoa wito kwa Katibu na Mwenyekiti CCM wilaya hiyo kuendelea kupambana kuhakikisha wanafanikisha jambo hilo ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya Chama na kwamba wao kama Serikali watawaunga mkono.

Naye kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Simon  Leng’ese alisema chama hicho ni kikubwa na wanapaswa kuwa na jengo nzuri la utawala na kwa bahati nzuri wilaya hiyo wazee waliowatangulia walipambana kupatikana jengo hilo la utawala ambalo pembeni yake wamejenga nyumba za makatibu  na wao CCM watabaki kwenye ujenzi huo wa ofisi ya wilaya.

Alisema wilaya ya Muheza ni tajiri katika mazao ya viungo wanajiona wana uwezo pia wamekusudia kujenga jengo nzuri na wamebuni kuchora ramani ya ghorofa moja ili angalau Jumuiya ziwe chini na chama juu na kuwepo kwa ukumbi kwa ajili ya vikao na wamekusudia hivyo.

“Leo tumefanya Halmashauri kuu maalumu na tumepata fedha ambayo itamalizia msingi na kutolea matoleo kwa ajili ya kuweka matofali tunashuruku ushirikiano wa Serikali ya wilaya na Mbunge wetu Naibu Waziri wa Michezo ,Sanaa na Utamaduni Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA kutuunga mkono kwenye jambo hili “

Mwisho.

KELELE NA MITETEMO INAUWA WATOTO NJITI 12,000 KWA MWAKA ULAYA PEKE YAKE

May 15, 2023

 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limebainisha kelele kuwa ni mojawapo ya

kisababishi cha madhara katika maisha ya binadamu. Aidha, kwa mujibu

wa “European Environmental Agency” (EEA, 2018) kelele zimeainishwa kuwa

mojawapo ya visababishi vya vifo vya mapema vya watoto “Pre-mature death”

ambapo takwimu zinaonyesha takribani watoto 12,000 hufariki kila Mwaka

katika Bara la Ulaya”.

Katika nchi yetu changamoto ya kelele zinazozidi viwango vilivyoainishwa

na TBS zinatokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo

matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia. Kwa siku za hivi karibuni, kelele

zimeongezeka kwenye maeneo ya kazi na hivyo kusababisha matatizo ya

kiafya ikiwemo kupoteza uwezo wa kusikia, matatizo ya uzazi, kupunguza

umakini katika mafunzo, ajali na kupungua uwezo wa kusikilizana.


Vyanzo vikuu vya kelele hizi ni kumbi za starehe hasa biashara za vileo (baa),

vyombo ya usafiri na usafirishaji (kama magari, ndege na treni), matumizi

ya teknolojia zilizopitwa na wakati kwenye viwanda vikubwa na vidogo

(Karakana za kuchomelea, ufyatuaji matofali, mashine za kusaga na kukoboa

nafaka), majenereta, matangazo ya biashara mitaani, shughuli za ujenzi, nyumba za ibada n.k.



SHERIA NA SERA ZINAZOONGOZA UDHIBITI WA

KELELE NA MITETEMO

Udhibiti wa kelele na mitetemo nchini unasimamiwa na Sheria mbalimbali

zikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 pamoja na

Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Udhibiti wa Kelele na Mitetemo) za

Mwaka 2015; Sheria ya Usalama Kazini ya Mwaka 2003; Sheria ya Afya ya

Jamii ya Mwaka 2009; Sheria ya Jumuiya [Sura ya 337 Marejeo ya 2002];

Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa [Sura 204 Marejeo ya 2002] na Kanuni za

Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018; Sheria ya Ardhi [sura 113 Marejeo ya

Mwaka 2019] na Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007 pamoja na Kanuni

zake za Mwaka 2018.

Sheria na Kanuni hizi zimeelekeza shughuli zote zenye madhara zifanyike

mbali na makazi ya watu na hivyo shughuli zenye kelele kufanyika mbali na

makazi ya watu ili kupunguza madhara kwa afya ya binadamu na mazingira.




BARAZA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA (NEMC)

Katika kuhakikisha kelele na mitetemo zitokanazo na shughuli mbalimbali

zinadhibitiwa, Baraza litafanya yafuatayo:

a. Kuendelea na ukaguzi wa maeneo ya biashara na kutoa

maelekezo mbalimbali ikiwemo Amri na Ilani za kudhibiti kelele.

b. Kuanisha na kutangaza maeneo ambayo kelele haziruhusiwi

(Noise Control Zone).

c. Kusimamia uanishaji wa ramani za maeneo yenye kelele

zilizopitiliza na kuandaa Mkakati wa udhibiti.

Mwongozo wa Kitaifa wa Udhibiti Kelele na Mitetemo

d. Kufanya tafiti za mara kwa mara kubaini hali ya uchafuzi wa

mazingira utokanao na kelele na mitetemo.

e. Kutoa elimu kwa jamii na maafisa mazingira kuhusu majukumu

yao katika udhibiti wa kelele na mitetemo.

f. Kupokea taarifa za malalamiko yanayohusu kelele na mitetemo.




-- Matokeo ChanyA+ chanyA+ TV chanyA+ Cloud chanyA+ Blog chanyA+ G+ chanyA+ twitter chanyA+ Facebook chanyA+ Radio Mobile

PROGRAM YA KUENDELEZA KILIMO NA UVUVI AFDP KUBORESHA MAZINGIRA YA UVUVI KILWA.

May 15, 2023
Mhandisi Erick Isack aliyesimama, akizingumzia namna ambavyo programu ya kuendeleza Kilimo na uvuvi, itakavyoboresha sekta ya uvuvi mkoani Lindi.
Wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu na Wizara ya Fedha, wakiangalia dagaa walioanikwa katika kichanja cha kienyeji, katika kata ya  KILWA Kivinje,wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea maeneo yatakayoteleza programu ya KILIMO na UVUVI (AFDP) mkoani Lindi Leo.
Picha ikionesha washiriki wa Kikao cha ugeni kutoka programu ya kuendeleza Kilimo na uvuvi (AFDP) wataalam na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya KILWA,wakati Ujumbe huo ulipotembelea maeneo yatakayoteleza programu hiyo mkoani Lindi
Mtaalamu wa masuala ya Lishe na Jinsia Bi. Irene Mbando, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu akizingumzia namna ambavyo Programu Hiyo itakavyohusisha masuala ya Lishe na jinsia.
 Picha ikionesha Dagaa walioanikwa chini, katika kata ya KILWA Kivinje mkoani Lindi.
Kulia Bw. Robert Lee mtaalam wa Uvuvi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa maendeleo ya Kilimo Duniani (IFAD) akijadili jambo na Bw. Richard Abila mtaalamu wa Ufugaji wa viumbemaji  kutoka IFAD.
Mfanya biashara wa dagaa,katika kata ya KILWA kivinje Wilayani KILWA, Mkoani Lindi akianika dagaa katika chanja ya kienyeji, ambapo programu ya kuendeleza Kilimo na uvuvi (AFDP) Itaenda kuwajengea chanja za kisasa.


Na; Mwandishi Wetu - KILWA

IMEELEZWA kuwa, Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi AFDP inategemea kwenda KUBORESHA MAZINGIRA na maisha ya wavuvi wilayani Kilwa Mkoani Lindi.

Hayo yamesemwa mapema Leo tahehe 15 Mei 2023, Mkoani Lindi na Mtaalamu wa masuala ya mazingira wa mradi huo, Mhandisi Erick Isack kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakati Ujumbe wa Programu hiyo ulipokuwa katika Ziara ya kikazi Mkoani hapo.

Mhandisi Isack amesema programu hiyo itasaidia kujenga kiwanda Cha kuchakata samaki katika maeneo ya bandari ya uvuvi KILWA Masoko na ghala la kutunzia samaki. Sambamba na hilo programu hiyo pia itaenda kujenga vichanja vya kisasa vya kukaushia dagaa katika kata ya KILWA Kivinje.

Kwa Upande wake mtaalam wa masuala ya Lishe na jinsia Bi. Irene Mmbando alisema, programu itazingatia ushiriki wa jinsia zote ikiwa wanawake watashiriki Kwa asilimia sitini (60%) na Asilimia arobaini (40%) vijana.

Aliongeza Kwa kusema kuwa Mradi huo unalenga kufika kaya laki mbili na sitini ambazo zitahusika katika kilimo, uvuvi na ufugaji wa viumbemaji.

Akizingumzia masuala ya Lishe, mtaalamu huyo Alisema programu hiyo inakwenda kuzingatia maswala ya Lishe katika kaya husika.

Awali akiongea katika mazungumzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya KILWA Bw. Eston Mngilangwa alisema, programu hii imezingatia mazingira halisi ya maeneo husika "Kwa upande wangu naona kama Lindi tumependelewa, tumeletewa miradi sita, programu hii tunaipokea Kwa mikono miwili, Tunashukuru sana, tunawahakikishia kuwa Mradi huu utaenda kuleta matokeo chanya, tumeshafanya maandalizi kwenye kila eneo,kama itatokea Kuna mahala tumekosea itakuwa ni suala la uelewa tuu." Alibainisha Mkurugenzi Huyo.

Ujumbe huo kutoka Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi, inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu,  uliohusisha wataalam kutoka IFAD, Wizara MIFUGO NA UVUVI, FEDHA na Wizara ya Kilimo itaendelea na ziara yake ya kikazi kisiwani Zanzibar wiki hii.

= MWISHO =