ASKARI WA KIKOSI CHA FFU AUAWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI VISIWANI ZANZIBAR, NI BAADA YA KUMPORA BUNDUKI AINA YA SMG NA KUVAMIA HOTELI YA KITALII.

ASKARI WA KIKOSI CHA FFU AUAWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI VISIWANI ZANZIBAR, NI BAADA YA KUMPORA BUNDUKI AINA YA SMG NA KUVAMIA HOTELI YA KITALII.

March 03, 2014
“Majambazi walifanikiwa kumpora bunduki aina ya SMG na kisha kumpiga risasi na kumjeruhi begani, tuko katika msako mkubwa hivi sasa,”Kamishna wa Polisi Zanzibar.

ZANZIBARA.
Askari wa Kikosi cha FFU, Mohamed Mjombo (Namba E 5607) ameuawa kwa kupigwa risas, huku mwingine akijeruhiwa baada ya majambazi kuvamia hoteli ya kitalii ya Pongwe Bay iliyo Pongwe mkoani Kusini Unguja.

 

Akizungumza na gazeti hili jana, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku wakati wageni wakiwa wamepumzika na askari hao wa FFU kutoka Kituo cha Polisi Machui wakiwa katika lindo kwenye hoteli hiyo.
SERIKALI ZAMWAGA AJIRA ZA WALIMU 36,000.

SERIKALI ZAMWAGA AJIRA ZA WALIMU 36,000.

March 03, 2014
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa.
 
SERIKALI imetangaza kuwajiri walimu wapya 36,071 mwaka huu ambao majina yao yanatarajia kutangazwa katikati ya mwezi huu (Machi) na watatakiwa kwenda kuripoti katika vituo vyao vya kazi Aprili mosi mwaka huu.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa, aliyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Kumepambazuka jana kinachorushwa na Radio One.
Majaliwa alisema walimu hao watapangiwa katika vituo mbalimbali vya kazi kuanzia Aprili Mosi, mwaka huu na majina yatatoka katikati ya mwezi huu.

March 03, 2014

Masheha wa Wilaya ya Micheweni katika Semina

 
MWANASHERIA wa serikali kutoka Afisi ya Mkurugnezi wa mashitaka kisiwani  Pemba Allbaghiri Yakout Juma, akiwasilisha mada juu ya utaratibu wa kushughulikia makosa ya jinai, kwenye mafunzo yaliowashirikisha masheha wa wilaya ya Micheweni, juu kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria wa majimbo ya Micheweni, mafunzo yaliofanyika Ofisi ya Kituo cha huduma za sheria Chake chake, kulia ni Mratibu wa kituo hicho, Fatma Khamis Hemed akifutiwa na Mwenyekiti wa masheha wilaya ya Micheweni Dawa Juma Mshindo (picha na Haji Nassor, Pemba)

MRATIBU wa Kituo cha huduma za sheria Pemba, Fatma Khamis Hemed, akiwasilisha mada juu ya Kazi za kituo na dhana ya wasaidizi wa sheria kwa masheha wa shehia ya Wilaya ya Micheweni mafunzo yaliofanyika afisini kwao mjini Chakechake Pemba  (picha na Haji Nassor, Pemba)
. PINDA ATULIZA HALI YA HEWA BUNGENI, UPIGAJI KURA WAWA VITA BUNGE MAALUM LA KATIBA DODOMA.

. PINDA ATULIZA HALI YA HEWA BUNGENI, UPIGAJI KURA WAWA VITA BUNGE MAALUM LA KATIBA DODOMA.

March 03, 2014
http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2013/06/pinda.jpg
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali ya papo kwa hapo Bungeni, mjini Dodoma jana.
 
DODOMA.
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda jana alifanikiwa kutuliza hali ya hewa bungeni baada ya kutoa mapendekezo yaliyoungwa mkono na pande zote zilizokuwa zinavutana kuhusu kupitisha baadhi ya vifungu vya Kanuni za Bunge la Katiba.

Katika mapendekezo yake yaliyoungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa CCM -Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Pinda alisema: “Nataka kuwaomba wenzangu wote kwenye maeneo hayo (yenye malumbano) tukiwa tunayapitia kama hatutaelewana tuyaache kwa muda na kumwomba Mwenyekiti aunde timu ya watu wazima na wenye busara wajaribu kuyatazama.

Pangua pangua Maliasili yaibua mapya

Pangua pangua Maliasili yaibua mapya

March 03, 2014
Nyalandu alikanusha tuhuma na lawama zilizorushwa kwake kuwa amewapangua wakurugenzi kinyume na taratibu, akisisitiza kuwa alichukua uamuzi huo kwa sababu ya kushindwa kutekeleza majukumu yao.PICHA|MAKTABA 
**********
Wiki moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kupangua wakurugenzi wizarani hupo, baadhi ya askari wa wanyamapori wameibuka na kupinga uamuzi huo, huku wakitishia kufanya mgomo.
Askari hao zaidi ya 10 walioomba kutotajwa majina gazetini kwa usalama wa ajira zao, wamepinga kuondolewa kwa Prof Alexander Songorwa kwenye nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori na badala yake kuteuliwa kwa Paul Sarakikya kukaimu nafasi hiyo.
March 03, 2014
*NDEREMO ZALIPUKA KAMPENI ZA CCM KALENGA KATIKA VIJIJI VYA MSENGELINDETE, MAHANZI, UFYAMBE NA UWASSA

 Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Msengelindete, Kata ya Uwassa, Iringa Vijijini alipowasili kufanya kampeni leo asubuhi.
 Wananchi wa Kijiji cha Msengelindete wakishangilia walipokuwa wakimlaki kijana wao, Godfrey Mgimwa ambaye amezaliwa katika Kata ya Uwassa.
 Karibu mwanetu karibu mwanetu, ndivyo mama huyo wa Kijiji cha Msegelindete alivyokuwa akimlaki kwa furaha mtoto wao Godfrey Mgimwa.
March 03, 2014
*MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAKUTANA NA WAANDISHI NA WADAU WA HABARI JIJINI DAR LEO
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio (kulia), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi na wadau wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo. 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absolom Kibanda, akizungumza wakati wa  mkutano na waandishi na wadau wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano ambao pia ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano uliondaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati wa  mkutano na waandishi na wadau wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo.
Meneja wa Huduma kwa wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Godfrey Mollel akisisitiza jambo wakati akitoa mada kwenye mkutano ulioandaliwa na PPF kwa waandishi na wadau wa habari katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam leo.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Janeth Ezekiel (katikati) akifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Meneja Wa Huduma Kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF , Ndg Godfrey Mollel (hayupo pichani) Ndg Godfrey Mollel wakati wa mkutano na waandishi na wadau wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo. Dokta Isaac Maro Wa AfyaCheck akizungumza wakati  wa mkutano na waandishi na wadau wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo.
 Mzee Timoth Kahoho (wa kwanza kushoto) akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ndg William Erio wakati wa mkutano na waandishi na wadau wa habari  uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ndg William Erio akibadilishana mawazo na Mwandishi wa Kituo Cha Runinga cha ITV, Bi Fatma Almas Nyangasa wakati wa mkutano na waandishi na wadau wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo.
Mzee Timoth Kahoho (katikati) akifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa na Meneja Huduma kwa Wateja wa Mfuko Wa Pensheni wa PPF, Ndg Godfrey Mollel wakati wa mkutano na waandishi na wadau wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam leo.
Washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa waandishi na wadau wa Habari uliondaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF pamoja na timu yake nzima kutoka Ofisi ya PPF Makao Makuu.
March 03, 2014

*MANGULA AWASILI KUONGEZA NGUVU IRINGA
























MANGULA ATUA RASMI KALENGA
*Asema Chadema wanalia kilio cha mamba
*Ni kwa kukimbiwa na wananchi kwa kudhuru watu.
*Asema hatapanda jukwaani, ataratibu tu kampeni
*Asisitiza anayegombea Kalenga si Mgimwa ni CCM
NA BASHIR NKOROMO, IRINGA
MRATIBU wa Kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula amesema, madai ya Chadema kwamba CCM imepeleka mamluki katika jimbo hilo ni kilio cha mamba, baada ya chama hicho kukimbiwa kutokana na vitendo vyake vya kudhuru watu ikiwemo kuwatoboa macho kwa bisibisi na kuwamwagia tindikali.
Hivi karibuni Chadema wanadaiwa kumtoboa jicho kwa bisibisi Alphonce John wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Kahama, na pia wanadaiwa kumpa ulemavu wa kudumu kwenye sura Mussa Tesha baada ya kumwagia Tindikali wakati wa uchaguzi mdogo uliofanyika Igunga 2012.
March 03, 2014

MELI INAYOZUA MASWALI MENGI YASIYO NA MAJIBU KWA KUTIA NANGA PEMBENI MWA HOTELI YA KUNDUCHI BEACH

Katika harakati za jicho la Kamera ya Sufianimafoto, ilinasa 'Image' ya picha ya Meli hii pichani isiyokuwa na jina wa kiashilio chochote cha kuonyesha mahala inapotoka meli hii, jambo ambalo lisatengeneza maswali mengi yasiyo na majibu kwa kila atakayepata fursa ya kuiona meli hii ikiwa imetia Nanga eneo hili la nyuma ya Hoteli ya Kitalii ya Kunduch Beach, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau waliozungumza na Mtandao huu, walisema kuwa meli hiyo ina muda mrefu sasa tangu walipoanza kuiona mahala hapo huku ikiwa haina shughuli yeyote zinazoendelea kwenye Meli hiyo wala mhusika.
March 03, 2014

MELI INAYOZUA MASWALI MENGI YASIYO NA MAJIBU KWA KUTIA NANGA PEMBENI MWA HOTELI YA KUNDUCHI BEACH

Katika harakati za jicho la Kamera ya Sufianimafoto, ilinasa 'Image' ya picha ya Meli hii pichani isiyokuwa na jina wa kiashilio chochote cha kuonyesha mahala inapotoka meli hii, jambo ambalo lisatengeneza maswali mengi yasiyo na majibu kwa kila atakayepata fursa ya kuiona meli hii ikiwa imetia Nanga eneo hili la nyuma ya Hoteli ya Kitalii ya Kunduch Beach, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau waliozungumza na Mtandao huu, walisema kuwa meli hiyo ina muda mrefu sasa tangu walipoanza kuiona mahala hapo huku ikiwa haina shughuli yeyote zinazoendelea kwenye Meli hiyo wala mhusika.
March 03, 2014
Release No. 036

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Machi 3, 2014



KIKOSI CHA TAIFA STARS CHATUA WINDHOEK

Kikosi cha Taifa Stars kimeondoka leo alfajiri kwenda Windhoek, Namibia kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya wenyeji itakayochezwa Machi 5 mwaka huu.



Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ina msafara wa watu 25 unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Timu imefikia hoteli ya Safari jijini humo.



Mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Sam Nujoma, na kikosi cha Taifa Stars kipo chini ya Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi ambaye ana leseni A ya ukocha inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).



Namibia (Brave Warriors) inayofundishwa na kocha Ricardo Mannetti imeingia kambini jana (Machi 2 mwaka huu) kwa ajili ya mechi hiyo ambayo tiketi zake zilianza kuuzwa Februari 28 mwaka huu.



MECHI YA YANGA, AHLY YAINGIZA MIL 488

Mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly kutoka Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki imeingiza sh. 448,414,000.



Mapato hayo yametokana na watazamaji 50,202 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 7,000, sh. 13,000, sh. 25,000 na sh. 35,000. Yanga ilishinda mechi hiyo kwa bao 1-0.



Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 68,402,135.59, gharama za kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219, waamuzi na kamishna sh. 14,665,930 na matangazo sh. 15,679,000.

Uwanja sh. 50,898,557.31, gharama za mchezo sh. 33,932,371.54, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)/Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 33,932,371.54 wakati Yanga ilipata mgawo wa sh. 220,560,415.01.
March 03, 2014
HII NDIO RIPOTI KAMILI KUHUSIANA NA MALI ZA KANUMBA

MASKINI! Stori zilizozagaa mitaani kuhusu mali za aliyekuwa mkali wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba zinasema kuwa, zimeuzwa na kampuni aliyoiacha, Kanumba The Great Film imefilisika, Ijumaa Wikienda linakupa ripoti iliyoshiba.

Marehemu Steven Kanumba.
Habari zinadai kuwa baada ya kifo cha Kanumba Aprili 7, 2012, mali alizoziacha zinafujwa, hakuna utaratibu mzuri wa kusimamia mamb
na kwamba, uzalishaji wa sinema katika kampuni yake ni mdogo tofauti na enzi za uhai wake.
Chanzo chetu cha habari ambacho ni mmoja wa wasanii wa filamu Bongo aliye na ukaribu na familia hiyo, alisema ni kweli kuna tatizo la usimamizi na uendelezaji wa mali za marehemu lakini akasema ni jambo la kawaida kwa sababu marehemu ameondoka na mbinu zake.
March 03, 2014

MAMBO YA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJI WA DODOMA KWA SASA MAGARI KUONGOZWA NA TAA ZA BARA BARANI.


Mafundi wa kampuni ya Makenga Invest LTD ya moani Tabora wakifunga taa kwa ajili ya kuongozea madereva wanaendesha vyombo mbalimbali vya
barabarani mjini Dodoma, kwa mujibu wa kampuni hiyo taa hizi zinafungwa
maeneo ya njiapanda ya Area D, na Ndasha.
March 03, 2014

*KINANA ALIPOITEKA KIBAHA KIJIJNI JANA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibaha Kijijini kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mtongani ambapo aliwaambia moja ya kazi kubwa ya viongozi wa CCM ni kutekeleza yale walioahidi kwa wananchi.
 Mbunge wa Kibaha Kijijini Ndugu Hamoud A. Jumaa akihutubia wakazi wa Kibaha Kijijini na kuwaambia mafanikio waliyoyapata ikiwa pamoja na kufungua ofisi ya kisasa ya Mbunge kugawa pikipiki tisa na baiskeli themanini na sita kwa makatibu kata na mabalozi wa shina.
 Isha Mashauzi akitumbuiza wakazi wa Kibaha Kijijini  wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM alikuwa mgeni wa Heshima.

 Viongozi wa CCM wilaya ya Kibaha wakicheza rusha roho wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani.
 Suleiman Jabir maarufu kama Msagasumu akiburudisha umati uliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani Kibaha Kijijini.
 Hamis Rashidi akirudisha kadi na makabrasha ya CUF kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mtongani Kibaha Kijijini.
 Wanachama wapya wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za uanachama wa CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani ambapo mgeni wa Heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Pikipiki tisa na Baiskeli themanini na sita zilizotolewa na Mbunge wa Kibaha Kijijini Ndugu Hamoud A. Jumaa kwa Makatibu kata na viongozi wa mashina wa Kibaha Kijijini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe Shaban Mlawa akimuambia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana waanze safari kwa pikipiki mpya zilizotolewa na Mbunge wa Kibaha Kijijini Ndugu Hamoud A.Jumaa kwa Makatibu kata na wajumbe wa mashina 86 kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani.