DARAJA LA KIGAMBONI KUFUNGULIWA RASMI JUMANNE APRILI 19, 2016

April 17, 2016 Add Comment


Viongozi Shrika la Taifa Hifadhi ya Jamii NSSF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakandarasi wa daraja la Kigamboni wakati lilipofunguliwa kwa ajili ya kupita magari kupita bure huku watembea kwa miguu na waendesha baiskeli wakipita bure. Daraja hilo litazinduliwa rasmi na Rais Dk. John Magufuli Jumanne tarehe 19.4.2016. 
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Karim Mataka akiwa katika eneo la daraja la Kigamboni mara baada ya kufunguliwa kwaajili ya kupita magari na waenda kwa miguu.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja ala Kigamboni, Karim Mataka (katikati) akionyesha barabara za kuingilia darajani upande wa Kigamboni.
Maeneo ya kuingilia darajani na kulipia tozo katika daraja la Kigamboni upande wa Kigamboni.
Ofisi mbalimbali zilizopo katika daraja la Kigamboni kikiwepo Kituo cha Polisi.
Magari yakipita kwa mara ya kwanza katika daraja la Kigamboni bila kulipa tozo.
Muonekano wa daraja la Kigamboni baada ya magari kuanza kupita.
Meya wa wa jiji la Dar es Salaam, Issa Mwita Charles akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Karim Mataka wakati alipopita katika daraja hilo siku ya kwanza baada ya kufunguliwa kwa daraja hilo.
Magari yakipita.
Meya wa wa jiji la Dar es Salaam, Issa Mwita Charles akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja ala Kigamboni, Karim Mataka.
Meya wa wa jiji la Dar es Salaam, Issa Mwita Charles akiagana na Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja ala Kigamboni, Karim Mataka walipokutana wakati akipita katika daraja hilo siku ya kwanza baada ya kufunguliwa kwa watumiaji.
Waenda kwa miguu wakipita katika daraja hilo.
Eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi wakati wa uzinduzi rasmi.
Pikipiki na magari yakipita darajani.
Magari yakielekea upande wa Kigamboni.
Waendesha baiskeli nayo wakipita.
Wengine wakishangaa darajani.
Watu wakipita darajani.
Mandhari ya darajani.
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI MDOGO KWA JESHI LA POLISI, CHUO CHA POLISI ZANZIBAR.

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI MDOGO KWA JESHI LA POLISI, CHUO CHA POLISI ZANZIBAR.

April 17, 2016 Add Comment

se1
Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akipokea salamu ya heshima kwa Maafisa na wahitimu wa mafunzo ya uongozi mdogo katika chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
se2
Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akikagua kwaride rasmin aliloandaliwa na Jeshi la Polisi alipofika kufunga mafunzo ya ungozi mdogo katika chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
se3
Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akimvisha  cheo mmoja waaskari waliofanya vizuri zaidi G.944 Makuza Azekiel Shuka kwa niaba ya wenzake katika sherehe ya kumaliza mafunzo ya uongozi mdogo kwa ngazi ya Koplo, Sajenti na Stafu Sajenti yaliyofanyika Chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
se4
Maafisa na wahitimu wa uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi wakitoa saluti kwa mgeni rasmini Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali.
se5
Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika viwanja vya Jeshi hilo Ziwani Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Habari Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Khadija Khamis /Maryam Kidiko –Maelezo Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwataka wahitimu  wa mafunzo ya uongozi mdogo kutumia mafunzo waliyoyapata ili kuleta mageuzi makubwa ya utendaji katika sehemu zao za kazi.
Balozi Seif ameeleza  hayo leo katika sherehe za ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Polisi  ngazi ya koplo, sajenti na staff sajenti yaliyofanyika katika viwanja nya Polisi Ziwani mjini Zanzibar.
Amesema kuyatumia mafunzo hayo vizuri katika utendaji wa kazi  itapelekea kupunguza uhalifu  na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.
“Nategemea mtabadilika na kuwa watendaji wazuri wanaochukia rushwa, kesi zitaendeshwa kwa haraka , haki itatendeka katika kutekeleza majukumu na haki za binaadam zitazingatiwa kwa lengo la kujenga heshima ya Serikali na kuleta uhusiano wa karibu baina yenu na Wananchi “Alisema Balozi.
Aidha alilitaka Jeshi la polisi kutopuuza uhalifu mdogo mdogo kwani uhalifu huo hatimae hupelekea uhalifu mkubwa na kusababisha uvunjifu wa amani katika nchi.
Nae Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame amewakumbusha wahitimu hao kuwa wanawajibu mkubwa wa kuwalinda raia na mali zao pamoja na kulinda sheria za nchi.
Hata hivyo amewataka kufanya kazi kwa kutumia elimu waliyoipata chuoni kwa vitendo, kuwaelimisha na kuwaongoza kwa uweledi askari huko vituoni mwao.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa chuo cha Polisi Zanzibar Deusdedit Kaizilege Nsimeki amesema Jeshi la polisi litaendelea kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi ili kuwajengea uwezo na uwelewa wa umuhimu wa utii wa sheria bila ya kushurutishwa.
Mafunzo ya uongozi mdogo wa vyeo vya Koplo, Sajenti na Staff sajenti yalifunguliwa rasmi tarehe 16/02/2016. Yakiwa na jumla ya wanafunzi 1532 kati ya hao kozi ya koplo 591, kozi ya Sajenti 706 na kozi ya Staff sajenti 235.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWASILI MKOANI MOROGORO KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWASILI MKOANI MOROGORO KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU

April 17, 2016 Add Comment

sul1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Meneja Mkuu wa Uzalishaji katika kiwanda cha Ushoni wa Nguo za aina mbalimbali Mw. Ritesh Krishandev Beesony, wakati alipowasili katika kiwanda hicho jana April 16,2016 kwa ajili ya kutembelea na kuangalia utendajia kazi zinazofanywa kiwandani hapo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
sul2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia nguo za aina mbalimbali zinazotengenezwa na kiwanda cha Ushoni cha Mazawa kiopo Msamvu Mkoani Morogoro wakati alipotembelea  kiwanda hicho jana April 16,2016 kwa ajili ya kuangalia utendajia kazi zinazofanywa kiwandani hapo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
sul4
sul6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha Ushoni wa Nguo cha Mazawa kiliopo Msamvu Mkoani Morogoro baada ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho jana April 16,2016 Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
sul7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha Ushoni wa Nguo cha Mazawa kiliopo Msamvu Mkoani Morogoro baada ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho jana April 16,2016 Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Mama wa Mhariri Mtendaji wa The New Habari Absalom Kibanda azikwa Rungwe Mbeya

Mama wa Mhariri Mtendaji wa The New Habari Absalom Kibanda azikwa Rungwe Mbeya

April 17, 2016 Add Comment


ab2
Familia ya wanahabari kutoka media mbalimbali pamoja na baadhi ya wahariri walioshiriki mazishi ya mama wa mhariri mtendaji wa The New Habari Absalom Norman Kibanda aliyesimama katikati mwenye miwani  mara baada ya maziko yaliyofanyika Rungwe mission wilayani Rungwe mkoani Mbeya jana mchana.
ab1
Kikosikazi cha Fullshangwe kinakupa pole sana kwa msiba uliokupata na kumuomba mungu akupe uvumilivu wewe pamoja na ndugu wote katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu katika familia Mungu alitoa na Mungu ametwaa jina la Bwana Lihimidiwe AMEN